data:post.body MFAHAMU DAKTARI ALIYEJIFANYIA UPASUAJI BAADA YA KUKOSA MSAADA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

MFAHAMU DAKTARI ALIYEJIFANYIA UPASUAJI BAADA YA KUKOSA MSAADA.


Mwezi wa tisa mwaka 1960 mpaka 1962 daktari mmoja kwa jina la Leonid Rogozov wa urusi alikua katika kituo cha utafiti na watafiti wengine 13 mbali kabisa na miji mingine ya urusi.
asubuhi ya tarehe 29 mwezi wa nne mwaka 1961 daktari huyo alisikia dalili za homa, kuishiwa nguvu, kichefuchefu na maumivu chini ya tumbo upande wa chini kulia.
                                                             
akiwa kama daktari mzoefu alijua kabisa zile zilikua dalili za kwanza kabisa za ugonjwa wa kidole tumbo kitaalamu kama appendicitis.
kituo kingine cha afya kilikua kama kilometa 1600 kutoka pale alipokua yeye na kutokana na hali ya hewa hakuna ndege ingeweza kutua huko wala usafiri wowote ambao ungemfikisha yeye kwa wakati.
alitumia dawa mbalimbali za kuweza kutibu bila upasuaji lakini ilishindika na hali ilizidi kua mbaya zaidi na zaidi.
baadae alikua hana jinsi zaidi ya kujipasua mwenyewe.

siku ya upasuaji
upasuaji ulianza saa nane kamili mchana, akisaidiwa na dereva wa gari na mtaalamu mwingine wa anga ambao walikua wanampa vifaa pamoja na kumuwekea kioo kwa tumboni ili aweze kuona vizuri wakati wa kupasua.
daktari akiwa amelala kiupandeupande alijichoma ganzi kisha akajichana urefu wa sentimita 12, wakati anaendelea kuchana chini zaidi aliukata utumbo mkubwa kwa bahati mbaya na ilibidi aushone kwanza kabla ya kuendelea.
baadae aliendelea mpaka akakutana na kidole gumba ambacho kilikua kimevimba na kubadilika sana ambapo alikadiria kwamba kingepasuka baada ya siku moja.
kidole tumbo kilikatwa na dawa za antibayotiki ziliwekwa moja kwa moja kwenye eneo ambalo lilipasuliwa na kushonwa na upasuaji ukawa umeisha saa kumi kamili mchana na hata hivyo kulingana na yeye kua na hali mbaya alikua anapumzika mara kwa mara kila baada ya muda fulani wakati upasuaji unaendelea.
baada ya upasuaji dalili za ugonjwa ziliondoka na alianza kupata nafuu kisha baada ya siku tano nyuzi ziliondolewa na alirudi kazini baada ya wiki mbili.
upasuaji huo ulishangaza sana dunia na mwaka mmoja baaadae alipewa tuzo ya heshima kwa ajili ya upasuji huo aliofanya.
lakini pia hali hiyo ilisababisha urusi kubadili sera zao na kuanza kuwafanyia uchunguzi wa kutosha madaktari kabla ya kupelekwa mbali kabisa ya mji.

miaka iliyofuata
mwaka 1962 Dr Leonid Rogozov alirudi mjini kuendelea na kazi na baadae aliandika kitabu cha jinsi ya kutibu kansa ya koo kwa njia ya upasuaji.
                                                       
mwaka 2000 alifariki akiwa na umri wa miaka 66 kutokana na maradhi ya kansa ya mapafu alipokua anatibiwa katika hospitali ya Saint Petersburg nchini urusi.....
pumzika kwa amani daktari, dunia haitakusahau kwa ushujaa uliofanya.

                                                                  STAY ALIVE


0 maoni:

Chapisha Maoni