data:post.body MAMBO 10 WANAUME WANATAKIWA KUFAHAMU KUHUSU TENDO LA NDOA ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

MAMBO 10 WANAUME WANATAKIWA KUFAHAMU KUHUSU TENDO LA NDOA

tendo la ndoa limekua likiwapa presha wanaume wengi sana, wengi wao hawajiamini na wana wasiwasi sana kwamba huenda wapenzi wao hawaridhiki kwenye tendo hilo.
kimsingi tendo la ndoa ni pana sana na lina mambo mengi sana ambayo hakuna mtu anaweza kuandika mpaka akayamaliza.
utafiti pia unaonyesha wanaume na wanawake wengi SIKU HIZI wamekua wakidanganya kwamba wameridhika na tendo la ndoa ili waridhishe watu wao.
kuna mambo mengi sana ya kuzungumzia lakini leo ningependa nizungumzie yale machache muhimu ambayo wanaume wanatakiwa wayajue.
ukubwa wa uume sio muhimu sana; tafiti zinaonyesha kwamba 45% ya wanaume ambao wana uume wa kawaida wanahisi ni mdogo na hauwezi kuwatosheleza wanawake kitu ambacho sio kweli, uume wa kawaida una urefu wa nchi nne mpaka sita na unene wa nchi nne na nusu ukiwa umesimama, kiwango hichi kipo kwa karibia wanaume wote duniani japo wapo waliozidi.
point kubwa na kwamba wanawake pia wanatofautiana maumbile, yaani unaweza kulala na mwanamke huyu akalalamika kwamba uume ni mkubwa mno afu kesho yake ukalala na mwanamke mwingine akaona ni mdogo au akaridhika nao.
hakikisha unapata msichana ambaye anaendana na ukubwa wa uume wako yaani isiwe kubwa sana kwake wala ndogo sana kwake, watu wanafikiri ukiwa na uume mdogo sana unaachwa lakini hata ukiwa mkubwa mno unaachwa kwani mwanamke haoni raha ya tendo la ndoa zaidi ya maumivu makali.
idadi ya mabao sio muhimu sana; nimekua nikipigiwa simu na wanaume wengi wanasema kwamba wanataka kupiga mabao manne lakini wanashindwa, hivi nani aliwaambia mwanamke anataka mabao manne kuridhika? kawaida mwanaume akishamwaga bao la kwanza lazima uume ulale kwa muda fulani ndio uamke tena hivyo kama wewe unahisi uume wako unachelewa kuamka kwa mara ya pili hakikisha kabla hujatoa bao la kwanza mwanamke awe ameridhika ili kipindi unasubiri goli la pili asiwe na malalamiko yoyote kwani akiwa na malalamiko kwamba umewahi sana utapaniki na huo uume hautasimama tena, na kama una tatizo la kuwahi sana pata matibabu.
point yangu ni kwamba kuna watu wanapiga bao moja tu kwa nusu saa moja na mwanamke anaridhika kuliko hayo magoli yako manne ambayo yanakua hayana kitu.
maandalizi ni muhimu sana; sisi wanaume hata tusipoandliwa muda wote tuko tayari lakini kwa mwanamke ni tofauti, ukimuandaa vya kutosha analoana sana kiasi kwamba anaweza kufika kileleni hata kabla ya kuingiliwa au akafika kileleni dakika moja tu baada ya kumuingilia, tabia ya wanaume kuanza kusex kabla ya maandalizi huwafanya wao kua wahanga kwa kushindwa kuwaridhisha wenza wao.kwa kawaida mwanamke anatakiwa aandaliwe hata dakika 20.
mjue mwanamke wako; usihangaike sana kusoma majarida na magazeti kuhusu mwanamke, kila mwanamke ana maeneo yake ambayo yakitumiwa vizuri anapata msisimko mkali sana, hivyo usiwe muoga kumuuliza siku mkiwa mnapiga story za kawaida kujua sehemu zake muhimu kwani hii itakusaidia mwenyewe au wewe mwenyewe kufanya utafiti kwa vitendo ukiwa naye faragha.
muda mzuri ni asubuhi sana; inategemea na majukumu ya watu lakini kwa watu ambao wako bize na kazi kufanya tendo la ndoa jioni linakua halina ladha sababu ya uchovu sana hivyo kwanzia saa tisa usiku mpka asubuhi ni muda mzuri kwani mnakua mmepumzika vya kutosha na kiwango cha homoni kinakua kizuri sana wakati huo.
mazingira ya tendo hilo ni muhimu sana; kama umeshaoa wakati mwingine jitahidi kuondoka na mke wako na kwenda sehemu zingine kutembea na kushiriki tendo la ndoa huko ili kubadilisha mazingira lakini pia chumba kichafu au mashuka machafu kwa wanaume ambao hawajaoa yanaweza kumfanya mwanamke akakosa hamu ya kua pale na kujikuta anapoteza hamu ya tendo kabisa na kujilazimisha tu kua pale muda uishe aondoke lakini pia tendo la ndoa sio chumbani tu kama mazingira yanaruhusu hata bafuni na jikoni.
wanawake wanajali sana muonekano pia; wanaume wengi wanatumia pesa kuwapata wanawake ni sawa utampata lakini kumbuka kama jinsi wanaume wavyokaa na kutamani kua na mwanamke mwenye shepu nzuri vivo hivyo wanawake pia wanatamani mwanaume mwenye shapu nzuri. fanya mazoezi uwe na mwili mzuri, nukia vizuri, usinuke miguu na kua msafi na hii huchangia sana kiakili mwanamke kuridhika akiwa anashiriki tendo la ndoa.
usioe binti mdogo sana; unaweza kua unatoka na binti wadogo sana mara moja moja sio inshu kubwa lakini kama una miaka 50 halafu unamuoa mwanamke mwenye miaka 20 kwa dunia ya sasa sio rahisi kumridhisha kingono kwani bado anahitaji sana tendo la ndoa na wewe umri umeshakutuapa yaani huna nguvu kama za ujanani..kila kijana anahitaji kijana mwenzake kiakili nakimwili hivyo kama wewe unaye ni sababu ana shida tu za kifedha hivyo hata kumridhisha kingono ni ngumu sana.
tendo la ndoa lina mahusiano sana na hali ya kiakili; tendo la ndoa ni starehe, siku zote binadamu anayefanya starehe lazima awe kwenye hali tulivu na amani yaani kiakili na kimwili, usishiriki tendo la ndoa na mwanamke ambaye ana mawazo na wewe hujachangia lolote kumsaidia, ana njaa na wewe hujafanya lolote ale kwanza au kuna tatizo lolote la kimahusiano ambalo halipata ufumbuzi.weka mambo sawa kisha muandae kisaikolojia kwa tendo hilo takatifu.
usimuulize kama ameridhika; siku zote mwanamke atadanganya tu ili akuridhishe ujione kidume lakini kimsingi wewe mwenye unatakiwa ujue dalili zote za mwanamke kufika kileleni na baadhi ya wanawake watakwambia kabisa hapohapo au baadae bila hata wewe kuzungumzia hiyo maada..timiza wajibu yako na mambo yote yatakua safi.kama hujui dalili za kufika kileleni soma hapa http://www.sirizaafyabora.com/2016/04/hizi-ndio-dalili-7-muhimu-za-kuonyesha.html
tunza CV yako; hakikisha kila ukilala na mwanamke unatoa 100%, kama hujisikii kushiriki tendo la ndoa ni bora usifanye kabisa kuliko kucheza chini ya kiwango, unaweza ukakuta ndio mara ya kwanza na mara ya mwisho kulala na huyo mwanamke hivyo usipotoa utundu wako wote basi mtaa mzima utajua wewe ni mbovu kwenye hayo maswala kumbe ilitokea siku moja tu.

                                                        STAY ALIVE
                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni