data:post.body MAKOSA MAKUBWA AMBAYO HUFANYWA NA WAGONJWA WAKIWA CHUMBA CHA DAKTARI ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

MAKOSA MAKUBWA AMBAYO HUFANYWA NA WAGONJWA WAKIWA CHUMBA CHA DAKTARI

katika utoaji wa huduma za afya yapo makosa ambayo hufanywa sana na watoa huduma za afya yaani manesi, madakatari, watu wa maabara na kadhalika..hali hiii hufanya matokeo ya utoaji wa huduma hizi kutokua mazuri sana..lakini pia kuna upande ambao unasahaulika sana yaani upande wa wagonjwa, kwamba kuna makosa mengi sana ambayo mgonjwa akiyafanya huweza kufanya ugonjwa wake usionekane au asipone hata kama daktari alipatia ugonjwa wake.
                                                                     
hebu tuyaone makosa hayo.
kutotoa historia nzuri ya ugonjwa; ni vizuri kabla ya kwenda hospitali kujiandaa ili kujua unafika unasema matatizo yako yote kwa mtiririko bila kuruka kitu, baadhi ya wagonjwa huingia ghafla na kusahau matatizo yao mengine au kuyasema wakati daktari ameshamaliza kuandika..hii inaleta usumbufu na wakati mwingine daktari anaweza kupuuzia dalili hiyo kutokana na wingi wa watu wanaomsubiri.
kujifichaficha maungo yao; kuna baadhi ya sheria za udaktari ni ngumu sana kuzielewa ukiwa sio daktari lakini sheria hizo ni muhimu sana kwa manufaa ya mgonjwa, baadhi ya wagonjwa huficha maungo yao kwa kuhisi madakatari ni wadogo sana kiumri, wasichana huficha kwa kudhani madaktari wanawataka au kukataa baadhi ya ukaguzi ambao ni muhimu..mfano kitaalamu mgonjwa mwenye shida ya tumbo ni lazima aingiziwe kidole kwenye haja kubwa kuangalia shida fulani fulani, msichana au mvulana mwenye shida sehemu za siri daktari lazima azione sehemu hizo nyeti kwa macho.
kuja hospitali na ugonjwa wake; baadhi ya wagonjwa wakiugua huingia google kutafuta kwamba  ugonjwa gani wanaumwa lakini dalili za magonjwa hua zinafanana sana kiasi kwamba watu hawa huchanganywa na wakienda hospitali badala ya kumuacha daktari afanye kazi yake, wao husema kwamba wana ugonjwa fulani na wanataka vipimo fulani fulani..unaweza ukapewa huduma hii lakini tatizo muhimu lisionekane.
kubadilisha madaktari; kimsingi ukianza kutibiwa na daktari fulani au hospitali fulani endelea na matibabu hapo hapo mpaka ugonjwa wako upate suluhisho. madakatari sio wajinga kwani wakiona shida yako ni ngumu watakushauri au kukuandikia barua uende hospitali kubwa zaidi lakini kuhama hama madokta kwasababu hujapona utajikuta unaanza matibabu upya kila sehemu unayoenda kwa kupewa dawa ileile yenye sura tofauti.
kudanganya kuhusu tabia na maisha yake; dakatari anatakiwa kukuuliza maswali mengi sana ambayo wewe unaweza ukadhani anakufuatilia sana au anakutaka lakini maswali hayo ni muhimu sana ili yeye apate ugonjwa unaokusumbua..mfano kama una mchumba? kama unakunywa pombe na bia ngapi kwa siku? kuvuta sigara na sigara ngapi kwa siku?, kama una wapenzi wengi, na kadhalika lakini haya maswali hua hayaulizwi tu kukukomoa bali kuna magonjwa ambayo yanahusiana sana na hizo tabia hivyo ni vizuri kua wazi kwani madokta wamefundishwa kutunza siri.
kutofuata maelekezo ya daktari; mgonjwa anaweza kushauriwa kitu na daktari lakini baadae akifika mtaani anaambiwa vitu tofauti na watu ambavyo havina ukweli ndani yake, mfano watu wengi wamkua wakikata vimeo vya watoto kitu ambacho hakikubaliki na sheria za kitaalamu au kusema mbona fulani hafanyi hivyo na anaishi?
kutokuuliza maswali; wagonjwa wengi hawaelewi vitu baadhi wakati wanapewa maelezo lakini hawaulizi, yaani mgonjwa anaweza akaja nyumbani bila hata kujua alikua anaumwa nini au akaanza kuuliza manesi baada ya kutoka chumba cha daktari.
mavazi; hili nalo ni tatizo kubwa sana, ukienda hospitali vaa nguo ambazo ni nyepesi na rahisi kuvaa ili kuwasaidia watoa huduma kukutibu, kwa mfano ukienda umevaa shati na suruali au shati na sketi ni rahisi daktari kuangalia tumbo lako kirahisi kuliko ukienda umevaa gauni.
lakini pia ukienda na shati za mikono mifupi ni rahisi kupimwa vipimo kama presha kuliko kwenda na nguo zenye mikono mirefu kwani utalazimika kuvua shati kupimwa presha tu.
kupokea simu au kuchati akiwa na daktari; daktari mwenyewe haruhusiwi kutumia simu akiwa na mgonjwa, wewe mgonjwa unapoanza kutumia simu ujue unapoteza muda kwa wengine kutibiwa na kumchosha daktari..ukikutana na daktari mwenye hasira anaweza kukutoa nje.
kua na maneno mengi; wagonjwa wengine hua na stori nyingi ambazo hazimuhusu daktari yaani akiulizwa anaumwa nini basi ataeleza mpaka mafanikio ya shule ya mwanae, hata kama dakatari ni rafiki yako lakini huo sio muda wa kuzungumzia stori zenu.
visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/


                                                                  STAY ALIVE

0 maoni:

Chapisha Maoni