data:post.body LIFAHAMU TATIZO LA KUKOROMA USIKU NA MATIBABU YAKE ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA KUKOROMA USIKU NA MATIBABU YAKE

kukoroma ni nini?
hii ni hali ya mtu kutoa kelele kama za kuunguruma wakati wote akiwa amelala, hali hii huwapata sana watu wazima na huweza kua usumbufu sana kwa watu ambao wamelala karibu yao na kama ni mchumba wako au mke wako ambaye unaishi naye unaweza kukosa raha kabisa ya usingizi.
                                       

nini chanzo cha kukoroma?
umbile la ndani la mdomo wako; mtu mwenye kimeo kirefu ambacho kinazuia mpaka njia ya chakula huweza kukoroma sana lakini pia mtu akinenepa, nyama za kooni huweza kuongezeka ukubwa na kumfanya aanze kukoroma sana.
unywaji wa pombe sana; pombe hufanya koo la chakula kulegea na kushindwa kuzuia kinga yako halisi ya mwili kupambana na vitu ambavyo vina uwezo wa kuziba koo.
matatizo ya pua; mafua makali, nyama za puani na matundu madogo sana ya puani huweza kuzuia hewa ya kutosha kuingia kwenye mapafu na hii humfanya mgonjwa akorome kupita kawaida.
ugonjwa wa kushindwa kupumua; hali hii huitwa kitaalamu kama obstructive sleep apnoea yaani koo la hewa linakua linaziba kabisa koo la hewa na mtu kushindwa kupumua...hali hii ni hatari sana na huweza kuleta kifo cha ghafla.
kulala chali; kukoroma huongezaka sana mtu anapolala chali kwani kwani kani ya mgandamizo au force of gravity inakandamiza koo lake.

dalili za mtu anayekoroma sana ni zipi?

 • kutoa sauti kali usiku na kufanya wengine washindwe kulala.
 • maumivu ya koo
 • presha ya damu kua juu.
 • maumivu ya kifua 
 • maumivu ya kichwa asubuhi
 • kulala sana mchana
 • kupaliwa usiku.
vipimo gani hufanyika?
daktari huweza kuagiza vipimo kama ct scan, mri, au x ray kuangalia eneo lako la koo kama liko sahini na hakuna shida yeyote na kwa nchi zilizoendelea mgonjwa hutakiwa kulala katika kituo cha afya ili wakati amelala afanyiwe vipimo mbalimbali ambavyo huchunguza usingizi wake.


matibabu gani hutolewa?
matibabu mbalimbali huweza kutolewa kulingana na teknolojia ya nchi husika lakini kabla ya matibabu kuna vitu mbalimbali ambavyo utashauriwa kufanya ambavyo vinaweza kukusaidia kupona bila matibabu yeyote mfano;
 • acha pombe
 • kunywa maji ya kutosha
 • pata usingizi wa kutosha
 • epuka kulala chali
 • badilisha mto mara kwa mara kukwepa aleji.
 • punguza uzito.
matibabu mengine ni kama 
vifaa ya mdomo: kitaalamu kama oral appliances huwekwa na madaktari wa meno kusaidia kuongeza nafasi ya taya na ulimi ili hewa iweze kupita vizuri.
kukata kimeo; hii kitaalamu kama uvulectomy ni upasuaji mdogo wa kukata nyama fulani inayoonekana mtu akifungua mdomo nyuma kabisa ya ulimi, upasuaji huu ufanyike hospitali tu na sio vichochoroni.

                                                              STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0769846183/0653095635

                                                                 

0 maoni:

Chapisha Maoni