data:post.body ZIFAHAMU SABABU, DALILI NA MATIBABU YA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

ZIFAHAMU SABABU, DALILI NA MATIBABU YA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI.

kwa kawaida yai la mwanamke likisha rutubishwa na mbegu za kiume husafiri kwenye mirija ya uzazi kitaaalamu kama fallopian tubes mpaka kwenye kizazi, huko hujishikiza na na mtoto huanza kukua hapo lakini katika hali ambayo sio ya yai lilorutubishwa hushindwa kusafiri kwenda kwenye kizazi na kukwama kwenye mirija hiyo na mimba kuanza kukua hapo.
                                                                             
mimba inaweza kutungwa nje ya kizazi sehemu mbalimbali kama kwenye mlango wa uzazi, tumboni, na sehemu mbalimbali lakini mara nyingi hutunga kwenye mirija ya kizazi.
mimba ikishatunga nje ya kizazi, hakuna jinsi inaweza kua mimba ya kawaida tena hivyo mama mjamzito anatakiwa apate matibabu haraka kutibu tatizo hilo.

nini chanzo cha mimba kutunga nje ya kizazi?
mimba hutunga nje ya kizazi sababu ya mirija inayotumika kusafirisha yai la mama lililorutubishwa kwenda kwenye kizazi kuharibiwa, lakini hakuna sababu za moja kwa moja za kutungwa mimba nje ya kizazi lakini zifuatazo ni sababu zinazomuweka mtu kwenye hatari ya kupata ujauzito nje ya kizazi.

  • kuvuta sigara; kemikali ya nikotini ambayo inapatikana kwenye sigara huharibu ulaini ambao uko kwenye mirija ya kizazi hivyo kusababisha yai kukwama wakati wa kusafiri.
  • magonjwa ya kizazi; magonjwa yanayoshambulia kizazi kama kisonono na chylamidia huweza kuleta makovu kwenye mirija ya uzazi.
  • endomitriosis; huu ni ugonjwa wa kuzaliwa nao ambao unasababisha kuwepo kwa makovu kwenye mirija ya uzazi.
  • kuathiriwa na baadhi ya kemikali ukiwa tumboni kabla hujazaliwa
  • upasuaji ambao unahusisha kizazi na mirija ya kizazi.
  • kupandikizwa kwa mbegu za kiume ili kushika mimba kwa wanawake ambao wanafanyiwa huduma hizo.
dalili za mimba kutunga nje ya kizazi ni zipi?
mimba ikitungwa nje ya kizazi mwanzoni hua na dalili za kawaida za mimba kama watu wenye mimba zingine, mfano kutopata hedhi, maumivu ya chuchu, kichefuchefu na kutapika lakini dalili muhimu za mimba kuharibika hutokea pale ambapo mirija inapopasuka ambapo mwanamke hupata maumivu makali ya ghafla ya tumbo la chini ambayo huanzia upande mmoja na kusambaa tumbo zima pia kutokwa na damu nyingi sana sehemu za siri.

vipimo gani hutumika kuhakikisha kama mimba imetungwa nje ya kizazi?
mara nyingi kipimo cha utrasound hutumika kuhakikisha kama kweli mimba imetungwa nje ya kizazi na kwa sehemu ambazo vipimo hivi havipatikani daktari anaweza kutumia utaalamu wake mwingine kujua hilo. mfano mirija ikishapasuka damu nyingi humwagika kwenye eneo la nje la tumbo na utumbo kitaalamu kama abdominal cavity hivyo akichoma sindano kwenye tumbo atavuta damu.

matibabu gani hutumika.
mimba ikigunduliwa mapema kama imetungwa nje ya kizazi yaani kabla yaijapasua mirija mama hupewa dawa aina ya  methotroxate kuitoa mimba lliyo haribika  kabla hijaleta madhara ya kupasua mirija ya kizazi lakini kama mirija imeshapasuka, upasuaji wa haraka utafanyika ili kuondoa mrija mmoja uliopasuka na kuushona ili usimwage damu mpaka kusababisha kifo.

jinsi ya kuzuia tatizo hili.
hakuna jinsi unaweza kuzuia mimba kutunga mimba nje ya kizazi lakini njia bora ya kuzuia madhara ya kufanyiwa upasuaji ni kupima picha ya utrasound kwa mapema unapogundua una mimba hasa kama uko kwenye hatari ya kupata shida hiyo kulingana na sababu nilizotaja mwanzoni lakini hata kama huna hatari ya kupata hali kama hiyo kama una uwezo pima kwani wakati mwingine hata watu ambao hawako kwenye hatari ya kupata mimba nje ya kizazi hupata hali hiyo.visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                         STAY ALIVE

                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni