data:post.body Septemba 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

ZIFAHAMU NJIA 10 ZINAZOWEZA KUKUPA WATOTO MAPACHAwatoto mapacha hupendwa sana na wanawake wengi wanaotaka kujifungua siku za usoni, lakini ni mara chache sana mwanamke kubeba mimba za mapacha.
                                                                     
tafiti zinaonyesha kwamba uwezekano wa mwanamke mmoja kubeba mimba ya mapacha ni 3% na kuna njia mbalimbali zinaweza kuongeza uwezekano huu mpaka asilimia tano au kumi na tutaziona hapo chini.
 kwenye ulimwengu huu wa maisha magumu wanawake wengi hupenda kuzaa mapacha mara moja tu wa jinsia tofauti au jinsia moja na kufunga kizazi.
japokua watoto mapacha wanapendeza sana na kufurahisha nyumba sio wanawake wote wanapenda watoto mapacha na mapacha hubeba hatari kubwa kipindi cha ujauzito kwani sio rahisi kuwazaa kwa njia ya kawiada huku wakiongeza dalili za ujauzito kua kali zaidi kama kutapika sana, kuchoka sana na kadhalika.

watoto mapacha wanatokea vipi kwenye kizazi?
kuna aina mbili za watoto mapacha..
mapacha wa kufanana au identical twin; hawa ni mapacha ambao hutokea pale yai la mwanamke lililorutubishwa na na mbegu ya mwanaume linapogawanyika na kutengeneza watoto wawili, watoto hawa hufanana kwa kila kitu yaani sura,tabia mpaka jinsia na hua ni vigumu sana kuwatofautisha kwa macho.
mapacha wasiofanana au non identical twin; mapacha hawa hutokea pale mayai mawili ya mama yanavyorutubishwa na kujishikiza tofauti kwenye mfuko wa uzazi, mapacha hawa hua wako tofauti kwa sura, jinsia na hata tabia..hawa ni kama ndugu waliofuatana tu.

je unawezaje kupata watoto mapacha?
kiukweli hakuna njia ya moja kwa moja ya kupata watoto mapacha lakini kuna baadhi ya sababu zinaongeza nafasi kubwa ya kubeba mimba ya watoto mapacha na tafiti nyingi zimeonyesha kwamba matumizi ya njia hizo yanaongeza nafasi kubwa sana ya kubeba watoto mapacha.
chagua mpenzi wa aina hiyo; kama unatoka familia ambayo mapacha wanazaliwa mara kwa mara uko kwenye uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha na kama ukizaa na mtu ambaye kwao kuna mapacha wa mara kwa mara basi na wewe una nafasi kubwa ya kuzaa mapacha..hii ni njia ngumu kidogo kwani sio rahisi kujua utampenda nani maishani mwako..kumbuka ni mwanamke tu, aliyetoka kwenye ukoo wa mapacha anaweza kuongeza nafasi ya kuzaa mapacha, mwanaume wa mapacha hawezi kuongeza nafasi ya kumpa mwanamke mimba ya mapacha.
zaa umri ukiwa umeenda kidogo; mwanamke akifkisha umri wa miaka 35 na kuendelea kunatokea mabadiliko ya mfumo wake wa uzazi kiasi kwamba mwili wake huanza kuachia mayai mawili kila mwezi badala ya yai moja kama ilivyokawaida, na hii huongeza nafasi kubwa sana ya yeye kubeba mimba ya watoto mapacha.
matumizi ya dawa za uzazi; kuna dawa ambazo hutumiwa na wanawake ambao wanashindwa kubeba mimba, dawa hizi hufanya yai zaidi ya moja kuachiwa kutoka kwenye mirija ya uzazi na hii huongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mapacha, na wanawake wanaotumia dawa hizi hujikuta wanabeba mapacha.mfano dawa za clomiphene citrate.
kua na watoto tayari; wanawake ambao wamezaa mtoto mmoja au wawili kabla wana nafasi kubwa sana ya kuzaa mapacha kuliko wale ambao hawajawahi kuzaa kabisa, ukifuatilia mapacha wengi hua hawazaliwi mimba ya kwanza ila kwanzia mimba ya pili kwenda mbele.
kupata mimba ukiwa kwenye dawa za majira; japokua sio rahisi sana lakini tafiti zinaonyesha kwamba mimba zinazoingia kwa bahati mbaya mwanamke akiwa anatumia dawa za uzazi wa mpango hutengeneza mapacha lakini pia mimba zinazoingia muda mfupi baada ya kuacha dawa za uzazi wa mpango hua zinaleta watoto mapacha.
urefu na unene; tafiti zinzonyesha kwamba wanawake warefu wana nafasi kubwa sana ya kubeba mimba za mapacha kuliko wanawake wafupi, lakini pia wanawake wanaobeba mimba wakiwa wanene wanakua na nafasi kubwa sana ya kupata mapacha.
chakula; jamii ambazo chakula chao kikuu ni viazi vikuu, zimeonyesha kua na mapacha wengi kuliko jamii zingine, tafiti zinasema kwamba viazi hivyo vina kiasi kikubwa sana cha homoni za oestrogen ambazo zinasababisha mama kutoa mayai mengi kitaalamu kama hyperovulation.
endelea kunyonyesha mtoto wako kwa muda mrefu; kuna homoni moja inaitwa prolactin ambayo inahusika na kutoa maziwa kipindi mama ananyonyesha, sasa kuendelea kuwepo kwa homoni hii kwa kiasi kikubwa wakati mama ameanza kushiriki tendo la ndoa kuna muongezea nafasi kubwa ya kupata mapacha akibeba mimba.
matumizi ya dawa za folic acid; dawa za folic acid hutumika na wajawazito wote ili kuzuia uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile hasa kwenye mishipa ya fahamu, lakini matumizi ya dawa hizi mwezi mmoja kabla ya kubeba mimba yanaongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mimba za mapacha.
kua pacha mwenyewe; kama wewe mwenyewe ulizaliwa kama mapacha basi uwezekano wa kubeba mimba ya mapacha ni mkubwa sana kuliko wale wengine ambao walizaliwa kawaida. visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                                       STAY ALIVE

                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183

SABABU TANO KWANINI UACHE KULA UGALI WA SEMBE

ugali wa sembe ni upi?
huu ni ule ugali ambao unakua mweupe sana baada ya kupikwa, hii ni sababu ya kukobolewa kwa mahindi au  kuondoa sehemu ya juu kabisa ya ya mahindi na kutengeneza pumba kisha kiini cha ndani cha mahindi kutengeneza unga.
                                                               
sehemu za mijini kama dar es laam na mwanza watu hupendelea sana kula ugali wa  sembe sababu ya muonekano wake mzuri tofauti na mikoani ambapo watu wengi hupendelea zaidi unga wa dona yaani ule ambao mahindi yake hayajakobolewa.
pamoja na makundi yote ya walaji kuona wanakula ugali wa aina moja lakini sio kama wanavyofikiria kwani chakula wanachokula ni tofauti kabisa.
ugali wa sembe una madhara makubwa kuliko dona kama ifuatavyo
ukosefu wa vitamini muhimu; unga wa sembe hauna vitamin b1 ambayo inapatikana kwenye ugali wa dona, vitamin hii ni muhimu sana kwa ajili ya kazi mbalimbali za mwili ikiwemo kusaidia mwili kutengeneza nguvu za mwili, kuchoma mafuta mwilini,kazi za ubongo,moyo,mishipa ya fahamu, na misuli...ukosefu wa vitamin hii husababisha kushindwa kazi kwa moyo, akili kidogo darasani, ganzi ya mwili, msongo wa mawazo na shida ya tumbo na utumbo.
kuongezeka unene; ugali wa sembe kitaalamu uko highly viscous hali ambayo inaongeza mzigo kwa mfumo wa chakula na kusababisha watu kuongezeka lakini pia mlaji wa dona anakua anakula sehemu ya wanga na sehemu ya vitamini na madini tofauti na huyu wa sembe ambayo mlaji anakula wanga tupu na wanga ndio moja ya vyanzo vikuu vya unene.
chanzo cha magonjwa ya kisasa; ugali wa sembe una tindikali nyingi sana kitaalamu kama highly acidic, tindikali hii ndio chanzo cha kuharibu viungo mbalimbali vya mwili na kuleta magonjwa ya kisasa kama kisukari, magonjwa ya moyo, presha, na kansa....vyakula kama mboga za majani na matunda hua na tindikali kidogo hivyo hufanya kazi ya kuzuia magonjwa haya.
ukosefu wa madini muhimu; madini muhimu kama phosphorus,magnesium,zinc,calcium,manganese,zinc, na selenium ni muhimu sana kwa kazi za kimwili lakini hupatikana kwenye mahindi kabla hayajakobolewa na baada ya kukobolewa hubaki bila madini kabisa.
kiasi kidogo sana cha nyuzinyuzi; nyunzinyuzi au fibres kwenye chakula ni muhimu sana kwa ajili ya kusafisha utumbo, kuondoa sumu mwilini na kuzuia mtu kupata choo ngumu lakini nyunyuzi hizi hazipatikani kwenye ugali wa sembe na matokeo yake mlaji hukosa faida zote hizo kwa kupata choo ngumu, sumu mwilini na kua na mfumo wa chakula ambao sio msafi.visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                               STAY ALIVE


KWANINI WANAWAKE WAFUPI HAWAWEZI KUZAA KWA NJIA YA KAWAIDA.[CPD]

mwanamke akienda kliniki kwa mara ya kwanza baada ya kupata ujauzito, moja ya vitu muhumu ambavyo vinapimwa ni urefu wake, ikionekana mwanamke yuko chini ya sentimita 150 basi hupewa ushauri wa kwenda hospitali kubwa kuzalia huko muda wa kuzaa ukikaribia, kwani uwezekano wa kuzaa kwa njia ya kawaida ni mdogo sana.

kwanini hili hutokea?
katika maswala ya uzazi kuna kitu kinaitwa cephalopelvic disproportion, hii ni kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya nyonga na mtoto anayetarajiwa kuzaliwa yaani kwa hali ya kawaida ili mtoto azaliwe kwa njia ya kawaida inabidi asiwe mkubwa kuliko nyonga ya mama sasa katika hali isiyo ya kawaida wanawake wafupi sana hua na nyonga ndogo kiasi kwamba hata mtoto akiwa na ukubwa wa kawaida yaani kilo mbili na nusu mpaka tatu na nusu bado atashindwa kupita kwenye nyonga yake.

nini matibabu yake?
hakuna dawa inayoweza kumfanya mwanamke mwenye nyonga ndogo kua na nyonga kubwa hivyo, wewe mwanamke ukiona kwamba una urefu chini ya sentimita 150 hakikisha unazaa kwenye hospitali yenye uwezo wa kufanya upasuaji ili ikishindikana kuzaa kawaida ufanyiwe upasuaji haraka.
lakini pia sio wanawake wote wafupi wana nyonga ndogo lakini wengi wao wana nyonga ndogo ndio maana hushauriwa kufanya hivyo.

unatakiwa kwenda hospitali lini?
usisubiri mpaka uchungu uanze, tarehe za matarajio zikikaribia nenda mwenyewe hospitali na huko utapewa kitanda na kuanza kusubiri siku ya kujifungua.visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                            STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0653095635/0769846183

ZIFAHAMU SABABU, DALILI NA MATIBABU YA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI.

kwa kawaida yai la mwanamke likisha rutubishwa na mbegu za kiume husafiri kwenye mirija ya uzazi kitaaalamu kama fallopian tubes mpaka kwenye kizazi, huko hujishikiza na na mtoto huanza kukua hapo lakini katika hali ambayo sio ya yai lilorutubishwa hushindwa kusafiri kwenda kwenye kizazi na kukwama kwenye mirija hiyo na mimba kuanza kukua hapo.
                                                                             
mimba inaweza kutungwa nje ya kizazi sehemu mbalimbali kama kwenye mlango wa uzazi, tumboni, na sehemu mbalimbali lakini mara nyingi hutunga kwenye mirija ya kizazi.
mimba ikishatunga nje ya kizazi, hakuna jinsi inaweza kua mimba ya kawaida tena hivyo mama mjamzito anatakiwa apate matibabu haraka kutibu tatizo hilo.

nini chanzo cha mimba kutunga nje ya kizazi?
mimba hutunga nje ya kizazi sababu ya mirija inayotumika kusafirisha yai la mama lililorutubishwa kwenda kwenye kizazi kuharibiwa, lakini hakuna sababu za moja kwa moja za kutungwa mimba nje ya kizazi lakini zifuatazo ni sababu zinazomuweka mtu kwenye hatari ya kupata ujauzito nje ya kizazi.

 • kuvuta sigara; kemikali ya nikotini ambayo inapatikana kwenye sigara huharibu ulaini ambao uko kwenye mirija ya kizazi hivyo kusababisha yai kukwama wakati wa kusafiri.
 • magonjwa ya kizazi; magonjwa yanayoshambulia kizazi kama kisonono na chylamidia huweza kuleta makovu kwenye mirija ya uzazi.
 • endomitriosis; huu ni ugonjwa wa kuzaliwa nao ambao unasababisha kuwepo kwa makovu kwenye mirija ya uzazi.
 • kuathiriwa na baadhi ya kemikali ukiwa tumboni kabla hujazaliwa
 • upasuaji ambao unahusisha kizazi na mirija ya kizazi.
 • kupandikizwa kwa mbegu za kiume ili kushika mimba kwa wanawake ambao wanafanyiwa huduma hizo.
dalili za mimba kutunga nje ya kizazi ni zipi?
mimba ikitungwa nje ya kizazi mwanzoni hua na dalili za kawaida za mimba kama watu wenye mimba zingine, mfano kutopata hedhi, maumivu ya chuchu, kichefuchefu na kutapika lakini dalili muhimu za mimba kuharibika hutokea pale ambapo mirija inapopasuka ambapo mwanamke hupata maumivu makali ya ghafla ya tumbo la chini ambayo huanzia upande mmoja na kusambaa tumbo zima pia kutokwa na damu nyingi sana sehemu za siri.

vipimo gani hutumika kuhakikisha kama mimba imetungwa nje ya kizazi?
mara nyingi kipimo cha utrasound hutumika kuhakikisha kama kweli mimba imetungwa nje ya kizazi na kwa sehemu ambazo vipimo hivi havipatikani daktari anaweza kutumia utaalamu wake mwingine kujua hilo. mfano mirija ikishapasuka damu nyingi humwagika kwenye eneo la nje la tumbo na utumbo kitaalamu kama abdominal cavity hivyo akichoma sindano kwenye tumbo atavuta damu.

matibabu gani hutumika.
mimba ikigunduliwa mapema kama imetungwa nje ya kizazi yaani kabla yaijapasua mirija mama hupewa dawa aina ya  methotroxate kuitoa mimba lliyo haribika  kabla hijaleta madhara ya kupasua mirija ya kizazi lakini kama mirija imeshapasuka, upasuaji wa haraka utafanyika ili kuondoa mrija mmoja uliopasuka na kuushona ili usimwage damu mpaka kusababisha kifo.

jinsi ya kuzuia tatizo hili.
hakuna jinsi unaweza kuzuia mimba kutunga mimba nje ya kizazi lakini njia bora ya kuzuia madhara ya kufanyiwa upasuaji ni kupima picha ya utrasound kwa mapema unapogundua una mimba hasa kama uko kwenye hatari ya kupata shida hiyo kulingana na sababu nilizotaja mwanzoni lakini hata kama huna hatari ya kupata hali kama hiyo kama una uwezo pima kwani wakati mwingine hata watu ambao hawako kwenye hatari ya kupata mimba nje ya kizazi hupata hali hiyo.visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                         STAY ALIVE

                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183

UFAHAMU UGONJWA WA KIDOLE TUMBO NA MATIBABU YAKE[appendicitis]

appendicitis ni nini?
ni mashambulizi au maradhi yanayotokana na kuugua kwa kidole tumbo, kidole tumbo ni eneo ambalo linapatikana kwenye utumbo mkubwa wa binadamu upande wa kulia kwa chini.
kidole tumbo au appendicitis ni ugonjwa ambao ni hatari sana na unahitaji matibabu ya haraka kabla mtu hajapoteza maisha.              

nini kinasababisha ugonjwa wa kidole tumbo?
kidole tumbo husababishwa na vitu vifuatavyo.

 • minyoo kuingia ndani ya kidole tumbo
 • vitu vya nje ya mwili kama mchanga.
 • kinyesi kujaa na kuingia hapo
 • kuvimba kwa tezi za tumboni.
dalili za ugonjwa huu ni zipi?
 • maumivu makali ya tumbo yanayoanzia kwenye tumbo la chini kushoto kwenda kwenye kitovu.
 • maumivu makali ya tumbo kwa kuligusa.
 • maumivu makali ya tumbo la chini kulia wakati wa kukohoa.
 • homa kali
 • kichefuchefu na kutapika.
dalili muhimu.
rovsing sign; ukikandamiza upande wa kushoto chini, maumivu yanahamia upande wa tumbo chini kushoto

psoas sign; mgonjwa atakutwa amelala huku amekunja mguu wa kulia na akiuunyosha anasikia maumivu.

obtrurator sign; ukiuchukua mguu wa kuume wa mgonjwa na kuukunja na kuuzungusha kwa ndani unasikia maumivu.
                                                                 
vipimo vinavyofanyika


 • kipimo cha picha ya utrasound ni muhimu sana kwani kitaonyesha kidole tumbo chenye tatizo.
 • kipimo cha damu cha full blood picture kitaonyesha kuongezeka sana kwa chembechembe nyeupe za damu.


   matibabu; 
matibabu pekee ya kidole tumbo ni upasuaji wa haraka na kukiondoa, huduma hizi hutolewa kwenye hospitali zote za wilaya nchini tanzania.

                                                                    STAY ALIVE
                        visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/


                                            DR.  KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183