data:post.body YAFAHAMU MATIBABU YA UTUMWA WA SIMU.[CELLPHONE ADDICTION] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

YAFAHAMU MATIBABU YA UTUMWA WA SIMU.[CELLPHONE ADDICTION]

makala iliyopita nilizungumzia dalili 16 zinazoonyesha kwamba mtu umekua mtumwa wa simu yako kitaalamu kama cellphone addiction kama hukusoma makala hiyo bonyeza hapa http://www.sirizaafyabora.com/2017/08/dalili-16-zinazo-onyesha-wewe-ni-mtumwa.html , lakini leo ntazungumzia ni jinsi gani unaweza kupambana na hali hiyo na kua mtu huru kama ulivyokua mwanzo, hii itakusaidia kuzalisha na kuweka mahusiano yako ya kimapenzi na kijamii katika hali nzuri, hebu tuone njia za kupambana na hali hii.
                                                                   
kua bize na mambo yako; hii ndio sababu kubwa kwanini watu wazima hawaathriki sana na simu kama vijana, ni kwasababu watu wazima wana majukumu na shughuli nyingi ambazo wanatakiwa kuzifanya tofauti na vijana ambao wengi wao hawajitumi kufanya lolote hivyo kama wewe ni kijana jishughulishe na kazi kama huna kazi jitolee sehemu, jifunze hobi mpya kama kutumia vifaa vya mziki kama gitaa, au shughulika na kazi za nyumbani ambazo siku zote hua ni nyingi sana.
                                                               
weka mipango ya matumizi ya simu; kimsingi sio lazima kutumia simu muda wote na kama mtu ana shida na wewe kama haupatikani atakutafuta hata baadae, hivyo jiwekee kwamba labda kila siku ntakua situmii simu kwanzia saa saa mbili mpaka saa nne asubuhi, au sehemu maalumu kama darasani, kanisani, kwenye mkutano au semina basi jiwekee nidhamu ya kutotumia simu kabisa.
                                                                             
anza taratibu; usianze ghafla tu kwamba kwanzia leo situmii simu muda wote hapana, nenda taratibu na ujiwekee muda kwa mfano kama simu yangu haijaita ntakua naiangalia kila baada ya nusu saa au saa moja kisha ongeza muda mpaka masaa manne na baadae utazoea.
                                                                     
ondoa baadhi ya application kwenye simu; kuna na application nyingi sana za mitandao ya kijamii ni moja ya chanzo kikubwa cha kushinda kwenye mitandao ya kijamii yaani unaangalia facebook, instagram, snapchat, tweeter, tinder, tango, you tube na kadhalika kwa muda mfupi...mara nyingi ukiangalia au usiangalie mwisho wa siku hautaingiza chochote..hivyo unaweza kuziondoa application hizo na kuziweka kwenye computer yako ya nyumbani ili jioni unaangalia tu yaliyojiri mitandaoni na kwenye simu yako ukaacha zile application muhimu kama za google,vitabu, gmail na kadhalika.
                                                           
weka simu yako mbali; usikae umeshika simu yako muda wote na ukiwa unafanya shughuli zako muhimu basi ondoa sauti ili ikiita usiisikie na fanya kazi mpaka utakapokua umemaliza ndio ukaangalie simu yako lakini pia ondoa alamu au notifications za kwenye application zako ambazo zinakupa taarifa kila kikifanyika kitu kwenye mitandao ya kijamii hizi ndio zinakufanya ukague simu ovyo. kwa mwanafunzi ambaye unataka kusoma lakini unataka google kuangalia misamiati kadhaa basi weka simu kitandani au mbali na wewe, toa sauti na tumia wi-fi ya simu kutumia google ya kompyuta yako.
                                                               
chukua likizo ya simu; nenda trip ya utalii sehemu mbalimbali za nchi kisha acha simu nyumbani, to taarifa kwa baadhi ya watu muhimu kisha izime...kipindi utakachokua huko utajifunza kufanya mambo mengine zaidi ya kutumia simu muda wote.
tembea na kitabu kidogo; watu wengi hatuna tabia ya kujisomea vitabu mbalimbali ambavyo viko nje ya fani zetu lakini vitabu vinafundisha mambo mengi sana na kuwapa watu hekima, badala ya kutoa simu kila unapokua kwenye foleni au sehemu ya kusubiri kitu toa kitabu chako usome na kwa staili hii utajikuta unasoma vitabu vingi sana, kumbuka usisome vitabu vya kwenye simu kwani utajikuta unaishia kwenye mitandao ya kijamii.
badilisha mitazamo yako kuhusu simu; usijibu kila meseji na simu zinazoingia kwenye simu yako, kabla ya kushika simu jiulize kuna ulazima wa kuitumia hii simu sasa hivi? kuna ulazima wa kujibu meseji hii sasa hivi? kama hakuna basi achana nayo mpaka ukiwa umemaliza shughuli zako ndio uanze kujibu meseji na simu zilizopigwa.
mpe mtu simu yako; wakati mwingine unashindwa kabisa kuvumilia hamu ya kutaka kutumia simu labda baada ya kula, kazi au weekend basi mpe mtu unayemuamini akushikie simu yako kisha utaenda kuichukua baadae.
zima simu yako; hii ni moja ya vitu muhimu sana kwenye maisha ya binadamu, wakati mwingine tunakua tunafanya kazi sana na kushindwa kujipa muda wa kukaa na kutafakari tuliyoyafanya siku nzima hii huleta uchovu na msongo wa mawazo...basi jiwekee muda wa kuzima simu kwa masaa kadhaa ili uweze kupata muda wa kua mwenyewe na kutafakari.. hii pia itakusaidia kwenye mahusiano kwani utakua na muda wa kuongea na wapendwa wako bila kusumbuliwa. mfano unaweza kuamua kila ikifika saa nne usiku unazima simu.
                                           
ingia kwenye mazoezi; watu hufanya mazoezi nusu saa mpaka saa moja, muda ule unakua huwezi kutumia simu lakini pia mazoezi ni moja ya njia kuu ya kuondoa utumwa au addiction yeyeote ya kitu duniani kwa kubadilisha kemia ya ubongo wako na kukufanya ujisikie vizuri.
                                                             
omba msaada na uwajulishe wengine; ongea na mshauri kuhusu shida yako lakini pia watu ambao walikua wanapenda sana kuchati na wewe waambie kwamba sasa hivi umeamua kubadili mfumo wako wa maisha hivyo hautakua unapatikana sana kwenye mitandao ya kijamii.

                                                                     STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni