unaweza kua unamfahamu mtu ambaye kwa sasa ni mtumwa wa simu ukadhani labda anafanya makusudi, hapana huyo ni mgonjwa na anataka msaada.
kwa tafiti ndogo tu wahanga na watumwa wa simu ni vijana zaidi kuliko watu wenye umri mkubwa, yaani zaidi ya 58% ya vijana wana utumwa huu.
sasa kama umebahatika kuingia kwenye makala hii na kusoma basi hizi ndio dalili kwamba wewe ni mtumwa wa simu na unahitaji matibabu ili uweze kurudi katika hali yako ya kawaida.
ukikaa sehemu unasubiri kitu lazima utoe simu; hii inaweza kua kwenye foleni ya benki, darasani unasubiri mwalimu aje, kwenye dalalala au basi unaenda sehemu, kikao kinakaribia kuanza, na kadhalika lakini kabla simu hazijaja watu walikua wanatumia nafasi hizo kufahamiana, kuangalia mazingira ya nje kama utaona fursa, kuongea na wafanyakazi wenzao, kuongea na wanafunzi wenzako kuhusu somo husika na kadhalika lakini kwa sasa hali ni mbaya kiasi kwamba hata kama kikao kinaendelea, mwalimu anafundisha watu bado wanaangalia simu zao.
unapoteza muda mwingi kuangalia post kwenye intaneti; umekaa sehemu unatoa simu yako unaingia facebook au instagram na kuanza kuperuzi kwa muda mrefu kwenda chini bila kungalia chochote cha maana na kila baada ya dakika kadhaa unafungua kuangalia kama kuna post mpya na wewe uwahi kutoa maoni yako..lakini pia ukiona hakuna jipya unahamia kwenye mitandao mingine ya kijamii kutafuta jipya na ukikosa kabisa unaweza kuingia you tube na kupotelea huko.
kuisha kwa chaji ya simu yako kunakukosesha raha; simu kuisha chaji sio mwisho wa dunia hasa kama hutegemei simu yeyote muhimu kwa siku hiyo, badala ya kuchanganyikiwa na kuanza kutafuta chaja iko wapi basi achana nayo upate muda wa kufanya mambo mengine na kupumzisha macho yako.
unalala na kuamka na simu; mpaka usiku wa manane umeshazima na taa ya chumbani bado macho yako yako kwenye simu na muda mwingine unasinzia bila kujua simu uliiacha wapi lakini ukiamka asubuhi saa moja ya kwanza lazima upitie kila kitu kwenye simu yako kabla ya kuamka na kwenda kuoga na kujiandaa.
simu yako inakusumbua wakati wa kuendesha gari; ukiwa unaendesha gari meseji zinazoingia zinakupa muwasho wa kutaka kujua ni nani matokeo yake unajikuta unachati huku unaendesha gari lakini pia ukiwa kwenye foleni lazima uchukue simu uangalie wakati kuna mambo mengi unaweza kufanya kama kusikiliza radio ya gari au kuzungumza na watu ambao uko nao. angalizo; hii ni hatari na imeua watu wengi sana.
watu wanaokuzunguka huenda wanakwambia; wazazi wako wanakwazwa sana na kukuona muda mwingi uko kwenye simu, rafiki zako na mchumba wako pia wanakwambia kwamba hupati muda wa kuongea nao sababu ya simu, muda wa kula au kuangalia tv wewe umeshika simu unajibu sms.
simu yako inafanya ushindwe kusoma; kama wewe ni mwanafunzi na unajikuta muda wote unasoma huku unaangalia na kujibu meseji za kwenye simu basi ujue umeshageuka mtumwa na utajikuta unasoma vitu vichache sana yaani kama ukipanga kusoma masaa mawili basi nusu saa tu ndio umesoma na saa moja na nusu umeitumia kwenye simu.
hisia kwamba simu yako inaita zinakundama; kama kuna muda unasikia simu yako inaita au unapata hisia kwamba simu yako inatoa vibrations halafu ukiangalia hakuna kitu basi ujue imeshakukamata mpaka kwenye mishipa ya fahamu na ndio maana unapata hizo hisia za uongo kwamba simu inaita.
unaishi maisha ya kwenye mitandao ya kijamii; unahisi kwamba idadi ya likes unazopata na comment unahisi zinafanya kazi kwenye maisha ya kiuhalisia yaani ukipost ukapata likes nyingi sana unahisi maisha umeyamaliza kabisa kumbe una mambo mengi sana ya muhimu hujayafanya maishani mwako.
muda mwingi unaangalia kama kuna ujumbe mpya au notifications; simu yako haijaita lakini kila baada ya dakika tano unatoa kuangalia kama kuna kitu kimekupita kwenye mitandao ya kijamii na usingependwa kuachwa nyuma kabisa lakini pia meseji ambazo hajizajibiwa zinakuwasha kiasi kwamba uko radhi uwahi google kutafuta jibu uweje kukoment mapema.
kujibu meseji kunakupotezea muda wako; huenda ungekua unawahi zaidi huko unapotaka kwenda
kama ungekua hujibu kila kitu kinachotumwa kwenye mitandao ya kijamii, yaani msanii mkubwa akipost kitu uko tayari usimame sehemu ukomenti ndio undelee na shughuli zako au unapoteza muda mwingi kuwaambia watu uko unafanya nini.
unatumia simu na computer kwa wakati mmoja; yaani unaweza kukuta mtu ameingia facebook kwa computer yake lakini bado atachukua na simu yake aingie hukohuko facebook lakini pia hata akiangalia movie au video yeyote kwenye computer basi simu yake pia iko pembeni anaangalia huku na huku.
unaenda na simu mpaka chooni au bafuni; ule muda ambao utakua chooni unajisaidia unahisi kama utapitwa matokeo yake simu unaingia nayo mpaka huko na kuiwekea bakteria wengi ambao ni hatari kwa afya yako.
unatembea na simu yako mkononi sio mfukoni kwako; ukiwa njiani unahisi ukiweka simu mfukoni utachelewa kuitumia pale meseji zitakapoingia hivyo unaishika mkononi kama gazeti lakini pia unatembea uko unasoma ujumbe na kujibu kiasi kwamba umeshawahi kujikwaa au kushindwa kuangalia mbele sababu ya simu.
sherehe zenu au kukutana kwenu kunaharibiwa na simu; yaani mnaweza kua mmeandaa sherehe kama marafiki, au umepanga kuonana na mtu, au nyinyi wote mko kwenye meza moja ya sherehe lakini kila mtu yuko bize na simu kiasi kwamba maana ya nyinyi kuoanana au kukaa pamoja haipo tena.
mwisho; makala ijayo nitazungumzia ni vitu gani muhimu vya kuzingatia ili uweze kuachana na utumwa huu wa simu na kuishi maisha yenye mchango kwenye shughuli zako za kila siku.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni