data:post.body DALILI 10 ZINAZOONYESHA KWAMBA MWANAMKE YUKO KWENYE SIKU ZAKE ZA HATARI[OVULATION] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

DALILI 10 ZINAZOONYESHA KWAMBA MWANAMKE YUKO KWENYE SIKU ZAKE ZA HATARI[OVULATION]


dalili za mwanamke kua kwenye siku zake za hatari hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, baadhi ya wanawake hua hawapati hata hizo dalili kabisa lakini kuwepo kwa dalili hizo huweza kuwasaidia hasa wale wanaotaka kupata ujauzito.
katika maisha ya kawaida ni vizuri kila mwanamke kafahamu elimu hiyo ndogo ya uzazi kwa kujua mzunguko wake una siku ngapi, siku zake za hatari ni lini, siku za kupata hedhi ni lini na siku ya salama ni zipi.                                                    
                                                           
hii itamsaidia mwanamke husika kujua kupangilia uzazi wake mwenyewe na itakua rahisi kupata mimba hata kama ana shida ya uzazi basi daktari itakua ni rahisi kwake kujua wapi pa kaunzia kumsaidia.                                                    
siku za hatari huweza kutokea kipindi kile kile cha mwezi au zikawa zinabadilika kulingana na aina ya mizunguko, kawaida mzunguko hautakiwi uwe zaidi ya siku 35 au chini ya siku 21.kama hujui kuhesabu siku zako na mzunguko soma hapa http://www.sirizaafyabora.com/2015/04/hizi-ndizo-siku-hatari-za-kubeba-mimba.html

siku za hatari kwa mwanamke ni zipi?
hizi ni siku ambazo mwanamke anakua yupo kwenye hatari kubwa ya kupata ujauzito iwapo akishiriki tendo la ndoa na mwanaume, siku hii yai hushuka kutoka kwenye kiwanda cha mayai yani ovari na kwenda kwenye mfuko wa uzazi.
siku hizo huambatana na kupanda sana kwa kiwango cha homoni mwilini yaani oestrogen na progesterone na huambatana na dalili mbalimbali kama ifuatavyo.
kutoka ute kama maji maji kwenye uke; siku yai linashuka kitaalamu kama siku ya ovulation majimaji kama yale ya yai na ukiyagusa na kuyavuta huvutika kama kamasi kama nchi moja hivi kama picha inavyoonyesha hapo...maji haya huanza kutoka siku za hatari zikianza na siku ambayo yanakua mengi zaidi ndio siku yai limeshuka, kazi ya maji haya ni kusaidia mbegu za mwanaume kusafiri vizuri wakati wa tendo la ndoa..kuna bidhaa unaweza kutumia kuimarisha kiwango hichi cha majimaji haya ili uweze kuyaona, tuwaasiliane ukihitaji..siku zote ambazo ute huu unaonekana unaweza kubeba mimba.                                                          
kubadilika kwa hali ya mlango wa uzazi: mlango wa uzazi au cervix unaunganisha kizazi na uke, unaweza kugusa mlango wa uzazi kwa kuingiza kidole ndani ya uke na ukigusa mwisho hapo ndio kizazi kilipo.kwa hali ya kwaida kabla ya siku za hatari kizazi hua kina ugumu fulani kama pua ya binadamu ukiigusa lakini siku za hatari zikianza kizazi hua laini sana kama lips za mdomo wa binadamu.                                          
kubadilika joto la mwili: joto la mwanamke hubadilika siku zake za hatari za kupata ujauzito sababu ya mabadiliko ya homoni za uzazi, kwa hali fulani siku hizo zikikaribia joto hupungua kidogo lakini ukiona joto limepanda ghafla ujue tayari siku za hatari zimefika.jinsi ya kupima: pima joto lako la mwili kila asubuhi kabla ya kuondoka kitandani na utakua unapata joto la aina moja kama huumwi lakini siku ya hatari joto litaongezeka ghafla kwa nyuzi joto 0.5c, hivyo kama ulikua unapata 37c kila siku basi utapata 37.5 siku hiyo..kumbuka kutumia pima joto ya digitali ndio rahisi kusoma.
                                                                 
kuongezeka sana kwa hamu ya kufanya ngono:  tafiti zimeonyesha kwamba hamu ya kufanya ngono huongezeka sana kipindi hichi ambacho mwanamke anakua kwenye siku zake za hatari, hizi ndio siku ambazo mwanamke anaweza akaijikuata analala na mwanaume ambaye hakuwahi kufikiria kwamba atakuja kulala naye maishani mwake na hata msichana na mvulana ambao ni marafiki tu huweza kujikuta wanafanya ngono.
kutokwa na damu kidogo; baadhi ya wanawake homoni zao hupungua kidogo siku ya hatari na kupungua huko husababisha ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi kupungua kidogo na matokeo yake damu humwagika kidogo,...mara nyingi damu hizi hutoka siku moja tu...damu hizi zitofautishwe na damu nyepesi ambayo pia hutokea pia  baada ya mwanamke kubeba mimba pale yai linapojishikiza kwenye ukuta wa uzazi wa mwanamke na kuchubua kidogo, mara nyingi damu hizi za ujauzito hutoka siku tisa baada ya yai kushuka na kurutubishwa.
maumivu ya tumbo la chini; baadhi ya wanawake maumivu ya tumbo hutokea ule upande ambao yai linasafiri kuelekea kwenye tumbo la uzazi, maumivu haya husababishwa na yai hilo la kike kugusa kuta za mirija hiyo na kupekea hali hiyo.
maumivu ya matiti;tafiti zinaonyesha kwamba maumivu haya husababishwa na kiwango kikubwa cha homoni kilichopo mwilini kwa wakati huo ambao kinaandaa mwili kwa ajili ya kulea ujauzito iwapo kama mwanamke atabeba mimba.
kuongezeka kwa uwezo wa milango ya fahamu; kipindi hiki mwanamke huweza kusikia harufu ambayo kwa hali ya kawaida mtu hawezi kuipata, pia anaweza kuonja ladha ya kitu kwenye chakula ambayo nyinyi hamuisikii na uwezo wake wa kuona kua juu sana sababu ya homoni zake.
                                                         
kujaa kwa kutumbo kidogo; kipindi hiki utasikia kama tumbo limejaa kuliko kawaida, hii ni sababu ya kuongezeka kiwango cha homoni ambacho huzuia maji kutoka nje kitaalamu kama fluid retention.
                                                                       
kichefuchefu na kichwa kuuma; baadhi ya wanawake ambao wanakua wanaguswa sana au kua sensitive sana na mabadiliko ya kiwango cha homoni hupata maumivu dalili hizi ambazo huisha baada ya kipindi hiki kupita.
mwisho;kama nilivyosema hapo mwanzo dalili hzi sio lazima upate zote ili ugundue kwamba uko kwenye siku za hatari, lakini pia sio watu wote wanapata dalili hizi..kwa dalili ya kutoka ute kuna virutubisho unaweza kutumia kuongeza ute huo ili uonekane vizuri..
kumbuka mwanamke akimaliza mwaka mmoja anashiriki tendo la ndoa na mwanaume wake ndani bila kushika mimba tunaamini mmoja wao ana shida hivyo ni vizuri kwenda wote hospitali kwa vipimo, unaweza ukapata dalili zote na bado usishike mimba sababu ya shida mbalimbali za kizazi.visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                         STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                              MAWASILIANO 0653095635/0769846183

Maoni 14 :

  1. Mbona mi dalili zotee za kupata mimba ninazoo,lakin sipati mimba😑😑😑

    JibuFuta
  2. Mwanamke anaweza kupata ujauzito ikiwa ameweka njiti ili kuzuia mimba kutokea?

    JibuFuta
  3. Yaan jamaan hizo dalili zote Moe wangu kawa nazo,tukaamin kabisa kashika ujauzito, lakin chaajabu ,kaingia bleed Tena yasiku hizo 8 jambo jamblo mpaka Sasa limetuchanganya. Hatuelewi tufanue nn. thanks

    JibuFuta
  4. Jaman hiz dalili mm sizion ila nkilala siku za hatar sipat mimba

    JibuFuta
  5. Mwez uliopita nlikutana na mr siku ya hatar sahv zimepita siku 12 natoka ute wenye dam na nimepima sina mimba

    JibuFuta
  6. Hizi dalili zote nilizipata hasa hizo za ute uliochanganyik na damu na kuumwa kiuno juzi nimepima imo

    JibuFuta
  7. Dalili ninazo ila sipat mimba siku atari

    JibuFuta
  8. Mimi nimechoma sindano mwezinwa sita inaisha mwezi wa 9 sijaingia mwezini mpaka Leo na Nina hizo dalili zote je Nina tatizo au naweza kushika mimba

    JibuFuta
  9. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
    * upendo
    inaelezea * inaelezea kivutio
    * kama unataka ex wako nyuma
    *acha talaka
    * kuvunja obsessions
    * huponya viharusi na magonjwa yote
    * uchawi wa kinga
    *Ugumba na matatizo ya ujauzito
    * bahati nasibu
    * uchawi wa bahati
    Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp:+2349046229159

    JibuFuta
  10. Me mwezi uliopita nilianza kubleed tarehe 6 mbaka 10 ,nikaanza tena tarehe 28 mbaka tarehe 1 mwezi huu siku za hatari ni zipi na mzunguko wangu wa siku ngapi msaada?

    JibuFuta
  11. Mimi sipati Ute wa ovulation hata nikikutana na mwanaume siku za hatar sipati mimba

    JibuFuta
  12. Naomba uondoe hiyo namba ya 0712213278 inaleta usumbufu kwangu wengi wananinipigia Mimi samahani

    JibuFuta