data:post.body Agosti 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

KIFAHAMU KIPIMO KINACHO ONYESHA SIKU ZA HATARI ZA KUBEBA MIMBA.

pamoja na elimu mbalimbali ambazo zimekua zikitolewa na wachapishaji mbalimbali wa makala za afya hapa nchini kuhusu siku za hatari za kubeba mimba bado ni changamoto kwa watu wengi kuelewa hesabu hizo zinavyonda lakini pia baadhi ya watu mizunguko yao inabadilika sana mpaka inawachanganya hawajui nini cha kufanya.
                                                                     
ovulation prediction kit ni nini?
hiki ni kipimo kilichogunduliwa kwa ajili ya kumuonyesha mwanamke anayetaka kupata ujauzito kwamba siku zake za hatari sasa zimefika, kipimo hichi hupima kiasi cha homoni inayoitwa lutenising hormone ambayo huongezeka masaa 12 mpaka 36 kabla ya siku za hatari kuanza hivyo kwa uhakika zaidi mwanamke anaweza kuanza kushiriki tendo la ndoa siku zote hizo mfululizo ili kuongeza nafasi ya kupata mimba.
                                                       
kipimo hichi hutumika kupima mkojo kama vile mtu anavyopima mimba lakini pia vipo vya kupima mate, kwenye mate hupima kiasi cha chumvi ambacho huongezeka wakati homoni hizi zimeongezeka mwilini.

ovulation kit zinafanya kazi vipi?
kipimo hichi hupima kuongezeka kwa homoni kwa jina la lutenising hormone ambayo kwa hali ya kawaida hua ipo kwenye mwili wa binadamu kwa kiasi kidogo lakini siku za hatari zikikaribia homoni hiyo huongezeka ghafla kwenye mkojo na damu.
unakua kwenye uwezekano mkubwa sana wa kupata mimba kwanzia masaa 12 mpaka 36 baada ya kipimo hicho kusoma positive yaani homoni zako zimepanda hivyo siku zako za hatari karibia zinaanza..ni vema kushiriki tendo la ndoa angalau siku tatu mpaka tano mfululizo ili kujihakikishia zaidi uwezekano wa kubeba mimba.

je zinawafaa watu wa aina gani hizi ovulation kit?
hizi huwafaa wanawake ambao wanataka kupata mimba ambao

  • mizunguko yao haieleweki yaani sio rahisi kupiga hesabu na kujua siku zao za hatari ni zipi.
  • umetafuta mimba muda mrefu hupati na hata ukipimwa unaambiwa huna shida yeyote.
  • uko bize sana na kazi kiasi kwamba huwez kutulia na kufuatilia siku zako.
  • mme wako au mpenzi wako muda mwingi hauko naye hivyo sio rahisi kulala naye mara kwa mara
  • unataka mtoto haraka.

ovulation kit inatumikaje?
ulimaliza kuona siku zako za hedhi, chukua kipimo kimoja kila siku kisha kikojolee au chukua mkojo kwenye chupa ndogo kisha tumbukiza kama vile unavyopima mimba kisha angalia majibu, endelea kupima kila siku mpaka uone hedhi nyingine, kama siku zako za hatari zifika kipimo kitaonyesha mistari miwili kama siku zako hazijafika kipimo kitaonyesha mstari mmoja, kutokana na matatizo mbalimbali ya uzazi unaweza usione siku zako za hatari mwezi huo hivyo unaweza kuendelea kujaribu miezi mingine lakini asilimia kubwa siku zao huziona baada ya kutumia kwa mzunguko mmoja tu.
kumbuka, kipimo hichi kinatakiwa kisomwe ndani ya dakika kumi, na  muda wa kupima ni saa nne asubuhi mpaka saa mbili usiku, usipime haraka baada ya kuamka kwani homoni hizi huchelewa kuongezeka mwilini baada ya kuamka, usinywe maji mengi sana kabla ya kipimo kwani mkojo utakua mwepesi sana na kushindwa kusoma majibu.

uhakika ni kiasi gani?
vipimo hivi vina uhakika zaidi ya asilimia mia moja kwamba siku zako za hatari zimeanza na unaweza kupata ujauzito muda wowote kwanzia siku hiyo.
                                                                         
changamoto ni zipi?
kipimo hiki kinaweza kusoma majibu ya uongo kama una magonjwa ya kizazi ambayo yanaongeza kiasi cha homoni hiyo mwilini, kama una miaka zaidi ya 40, kama unameza dawa za kutafuta kubeba ujauzito hivyo inabidi uache kwanza kumeza, matatizo ya uzazi ambayo kipimo kinaweza kuonyesha yai limeshuka lakini njia imeziba na yai halijatoka.

faida ni zipi?
hii ni moja ya njia ya haraka sana ya kubeba mimba kwa watu ambao wametafuta mtoto muda mrefu kwani mwanaume hupata nafasi ya kujiandaa na kusubiri siku ya hatari ili kumwaga mbegu zilizokomaa ndani ya mwanamke tofauti na kujaribu kila siku ambapo kunamfanya mwanaume amwage mbegu ambazo hazijakomaa.


naweza kuzipata wapi kipimo hichi cha ovulation kit?
vipimo hivi ni adimu kidogo hasa nchini kwetu tanzania lakini kama unaishi nje ya nchi unaweza kuvipata kirahisi lakini pia wewe unayeishi hapa nchini unaweza kuwasiliana nasi kwa ajili ya kuvipata.visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                                    STAY ALIVE

                                           DR  KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                               0653095635/0769846183


          

DALILI 10 ZINAZOONYESHA KWAMBA MWANAMKE YUKO KWENYE SIKU ZAKE ZA HATARI[OVULATION]


dalili za mwanamke kua kwenye siku zake za hatari hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, baadhi ya wanawake hua hawapati hata hizo dalili kabisa lakini kuwepo kwa dalili hizo huweza kuwasaidia hasa wale wanaotaka kupata ujauzito.
katika maisha ya kawaida ni vizuri kila mwanamke kafahamu elimu hiyo ndogo ya uzazi kwa kujua mzunguko wake una siku ngapi, siku zake za hatari ni lini, siku za kupata hedhi ni lini na siku ya salama ni zipi.                                                    
                                                           
hii itamsaidia mwanamke husika kujua kupangilia uzazi wake mwenyewe na itakua rahisi kupata mimba hata kama ana shida ya uzazi basi daktari itakua ni rahisi kwake kujua wapi pa kaunzia kumsaidia.                                                    
siku za hatari huweza kutokea kipindi kile kile cha mwezi au zikawa zinabadilika kulingana na aina ya mizunguko, kawaida mzunguko hautakiwi uwe zaidi ya siku 35 au chini ya siku 21.kama hujui kuhesabu siku zako na mzunguko soma hapa http://www.sirizaafyabora.com/2015/04/hizi-ndizo-siku-hatari-za-kubeba-mimba.html

siku za hatari kwa mwanamke ni zipi?
hizi ni siku ambazo mwanamke anakua yupo kwenye hatari kubwa ya kupata ujauzito iwapo akishiriki tendo la ndoa na mwanaume, siku hii yai hushuka kutoka kwenye kiwanda cha mayai yani ovari na kwenda kwenye mfuko wa uzazi.
siku hizo huambatana na kupanda sana kwa kiwango cha homoni mwilini yaani oestrogen na progesterone na huambatana na dalili mbalimbali kama ifuatavyo.
kutoka ute kama maji maji kwenye uke; siku yai linashuka kitaalamu kama siku ya ovulation majimaji kama yale ya yai na ukiyagusa na kuyavuta huvutika kama kamasi kama nchi moja hivi kama picha inavyoonyesha hapo...maji haya huanza kutoka siku za hatari zikianza na siku ambayo yanakua mengi zaidi ndio siku yai limeshuka, kazi ya maji haya ni kusaidia mbegu za mwanaume kusafiri vizuri wakati wa tendo la ndoa..kuna bidhaa unaweza kutumia kuimarisha kiwango hichi cha majimaji haya ili uweze kuyaona, tuwaasiliane ukihitaji..siku zote ambazo ute huu unaonekana unaweza kubeba mimba.                                                          
kubadilika kwa hali ya mlango wa uzazi: mlango wa uzazi au cervix unaunganisha kizazi na uke, unaweza kugusa mlango wa uzazi kwa kuingiza kidole ndani ya uke na ukigusa mwisho hapo ndio kizazi kilipo.kwa hali ya kwaida kabla ya siku za hatari kizazi hua kina ugumu fulani kama pua ya binadamu ukiigusa lakini siku za hatari zikianza kizazi hua laini sana kama lips za mdomo wa binadamu.                                          
kubadilika joto la mwili: joto la mwanamke hubadilika siku zake za hatari za kupata ujauzito sababu ya mabadiliko ya homoni za uzazi, kwa hali fulani siku hizo zikikaribia joto hupungua kidogo lakini ukiona joto limepanda ghafla ujue tayari siku za hatari zimefika.jinsi ya kupima: pima joto lako la mwili kila asubuhi kabla ya kuondoka kitandani na utakua unapata joto la aina moja kama huumwi lakini siku ya hatari joto litaongezeka ghafla kwa nyuzi joto 0.5c, hivyo kama ulikua unapata 37c kila siku basi utapata 37.5 siku hiyo..kumbuka kutumia pima joto ya digitali ndio rahisi kusoma.
                                                                 
kuongezeka sana kwa hamu ya kufanya ngono:  tafiti zimeonyesha kwamba hamu ya kufanya ngono huongezeka sana kipindi hichi ambacho mwanamke anakua kwenye siku zake za hatari, hizi ndio siku ambazo mwanamke anaweza akaijikuata analala na mwanaume ambaye hakuwahi kufikiria kwamba atakuja kulala naye maishani mwake na hata msichana na mvulana ambao ni marafiki tu huweza kujikuta wanafanya ngono.
kutokwa na damu kidogo; baadhi ya wanawake homoni zao hupungua kidogo siku ya hatari na kupungua huko husababisha ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi kupungua kidogo na matokeo yake damu humwagika kidogo,...mara nyingi damu hizi hutoka siku moja tu...damu hizi zitofautishwe na damu nyepesi ambayo pia hutokea pia  baada ya mwanamke kubeba mimba pale yai linapojishikiza kwenye ukuta wa uzazi wa mwanamke na kuchubua kidogo, mara nyingi damu hizi za ujauzito hutoka siku tisa baada ya yai kushuka na kurutubishwa.
maumivu ya tumbo la chini; baadhi ya wanawake maumivu ya tumbo hutokea ule upande ambao yai linasafiri kuelekea kwenye tumbo la uzazi, maumivu haya husababishwa na yai hilo la kike kugusa kuta za mirija hiyo na kupekea hali hiyo.
maumivu ya matiti;tafiti zinaonyesha kwamba maumivu haya husababishwa na kiwango kikubwa cha homoni kilichopo mwilini kwa wakati huo ambao kinaandaa mwili kwa ajili ya kulea ujauzito iwapo kama mwanamke atabeba mimba.
kuongezeka kwa uwezo wa milango ya fahamu; kipindi hiki mwanamke huweza kusikia harufu ambayo kwa hali ya kawaida mtu hawezi kuipata, pia anaweza kuonja ladha ya kitu kwenye chakula ambayo nyinyi hamuisikii na uwezo wake wa kuona kua juu sana sababu ya homoni zake.
                                                         
kujaa kwa kutumbo kidogo; kipindi hiki utasikia kama tumbo limejaa kuliko kawaida, hii ni sababu ya kuongezeka kiwango cha homoni ambacho huzuia maji kutoka nje kitaalamu kama fluid retention.
                                                                       
kichefuchefu na kichwa kuuma; baadhi ya wanawake ambao wanakua wanaguswa sana au kua sensitive sana na mabadiliko ya kiwango cha homoni hupata maumivu dalili hizi ambazo huisha baada ya kipindi hiki kupita.
mwisho;kama nilivyosema hapo mwanzo dalili hzi sio lazima upate zote ili ugundue kwamba uko kwenye siku za hatari, lakini pia sio watu wote wanapata dalili hizi..kwa dalili ya kutoka ute kuna virutubisho unaweza kutumia kuongeza ute huo ili uonekane vizuri..
kumbuka mwanamke akimaliza mwaka mmoja anashiriki tendo la ndoa na mwanaume wake ndani bila kushika mimba tunaamini mmoja wao ana shida hivyo ni vizuri kwenda wote hospitali kwa vipimo, unaweza ukapata dalili zote na bado usishike mimba sababu ya shida mbalimbali za kizazi.visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                         STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                              MAWASILIANO 0653095635/0769846183

HIZI NDIO FAIDA SABA ZA KULALA BILA NGUO KABISA

katika swala la kulala kila mtu hua ana utamaduni wake wa kulala, wengine hua wana mavazi maalumu ya kulalia, na wengine hulala na nguo yeyote tu ambayo hujikuta ameivaa siku hiyo...kitaalamu kulala na nguo sio kuzuri kiafya na kisaikolojia kwani kuna mambo unayakosa kwa kulala na nguo zako ambayo kimsingi ni mambo mazuri na ya bure kabisa.
leo ntaenda kuzungumzia faida za kulala bila nguo yeyote kabisa ambazo huenda ulikua huzijui na ukizijua leo zitakusaidia kuimarisha afya yako.
                                                             
kupata usingizi wa kutosha; ukilala bila nguo kabisa mwili wako unakua huru sana, nguo hua na tabia ya kukubana sana na kukunyima usingizi wa kutosha kitu ambacho wewe kama mlalaji unaweza usigundue...wakati mwingine huenda umeshawahi kulala umevaa shati lakini asubuhi ukajikuta huna, hii ni kwasababu ukiwa katika nje ya fahamu yaani usingizini uliamka ukavua mwenyewe bila kujua sababu usingizi ulikua haupatikani vizuri.

huzuia magonjwa ya ngozi; ukilala bila nguo, joto lako la mwili hushuka kidogo na katika hali ya kawaida wadudu nyemelezi wa mwili hutaka sehemu yenye joto au unyevunyevu ili kuweza kushambulia hivyo ukilala bila nguo wadudu hawa hawatapata nafasi ya kuushambulia mwili wako na kukuletea magonjwa,,,hata kipindi cha baridi ni vizuri kujifunika na blanketi nyingi kuliko kuvaa nguo.

husaidia kupunguza uzito; ukilala na nguo, sababu ya ule usumbufu mtu hupata msongo wa mawazo na hali hiyo husababisha wewe kujisikia njaa na kutaka kula zaidi wakati wa usiku lakini mtu anayelala bila nguo anarelax sana na kusinzia bila hata kusikia dalili za njaa.

hulinda sehemu za siri; kwa mwanaume kulala bila nguo huweka korodani zako katika hali ya ubaridi na kusaidia kutengeneza mbegu nyingi za kutosha, lakini pia kwa mwanamke huupa uke hewa ya kutosha ya oksijeni na kuzuia magonjwa ya fangasi yanayopenda kushambulia huko.

hunogesha tendo la ndoa na mahusiano; utafiti unaonyesha kwamba wanandoa wanaolala bila nguo kila siku hushiriki tendo la ndoa mara nyingi zaidi kuliko wale wanaolala na nguo na hii huongeza chachu ya mahusiano na kufanya wajione wapya kila siku sababu ya miili yao kutengeneza homoni ya oxytocin ambayo ni homoni ya upendo.

hupunguza kasi ya kuzeeka; ukilala bila nguo unatengeneza mazingira mazuri sana ya homoni za mwili wako kufanya kazi sana kuliko kipindi ukilala na nguo ambapo homoni zako zinafanya kazi kwenye mazingira magumu...kifupi ni kwamba kulala na nguo kunakufanya uzeeke haraka.

hukupa furaha na uhuru; kwa hali ya kawaida tu mwanamke anapotoka kazini au mizungukoni na kufika nyumbani kitu cha kwanza kabisa kufanya ni kuvua sidiria na kuitupa huko sababu ya kubanwa sana kwa siku nzima,  kuvua humpa  uhuru sawa sawa na mtu ambaye analala bila nguo ambaye hupata faida hiyo.

mwisho; chukua hatua sasa, kama ulikua unalala na nguo ni muda wa kuanza kufanya mabadiliko na kumuhusisha mwenzako pia.visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/

                                                              STAY ALIVE

DALILI SABA ZA MTU ANAYETAKA KUJIUA.[SUICIDE]

shirika la afya duniani yaani who linatoa taarifa kwamba kila mwaka zaidi ya watu milioni moja hujiua kwa sababu mbalimbali... nchini marekani ni chanzo cha tatu cha vifo cha vijana kati ya miaka 15 mpaka 24 na ni chanzo cha 11 cha vifo kwa watu wote nchini humo.
taarifa hiyo inaongeza kua watu wenye umri wa miaka 15 mpaka 44 hujiua zaidi kuliko makundi yote ya umri, wanaume huongoza kwa kujiua kuliko wanawake lakini wanawake huongoza kwa kujaribu kujiua kuliko wanaume.
                                                               
kimsingi kujiua sio ugonjwa wa akili lakini ni matokeo ya msongo wa mawazo na magonjwa ya akili yanayosababishwa na  matatizo mbalimbali ya kiafya, kiuchumi, kimahusiano, msongo wa mawazo, matumizi ya dawa fulani za kulevya,kukoza kazi na kufiwa na wapendwa wetu.
vijana ndio moja ya kundi kubwa ambalo haliwezi kuvumilia matatizo ya kimaisha yaani mtu akiachwa na mpenzi, akikosa kazi, akifilisika, akigunduliwa na ugonjwa hatari kama ukimwi, kansa au kisukari basi haoni sababu za kuendelea kuishi.
kwa miaka 45 iliyopita tatizo la kujiua limeongezeka kwa 60% na kwa sasa kila baada ya sekunde 40 mtu mmoja hujiua, na inakadiriwa kwamba mpaka mwaka 2020 kila baada ya sekunde 20 mtu mmoja atajiua, baadhi ya data za kujiua hukosekana sababu ya watu kuonekana wamepotea kumbe wamejiua na miili yao haikupatikana.
tatizo la kujiua au kujaribu kujiua nchini tanzania pia ni kubwa sana kuliko linavyofikiriwa kulingana na kukosekana kwa huduma za ushauri hasa kwa watu wenye shida zinazotaka ushauri wa kina na pia kuhisi watu hawa wamekufa ghafla kulingana na njia walizotumia kujiua.

makundi  gani wako kwenye hatari ya kujiua?
  • wazee ambao wamepoteza mme au mke kwa vifo au talaka.
  • watu ambao wamejaribu kujiua kipindi cha nyuma
  • watu ambao kuna historia za kujiua kwenye ukoo wao
  • watu wenye historia ya kuumizwa kihisia au kulazimishwa kingono
  • watu ambao hawajaolewa au kuoa, hawana ujuzi au hawana kazi
  • watu wanaotumia madawa ya kulevya
  • watu ambao ni wakorofi sana kwenye jamii
  • watu waliowahi kuugua magonjwa ya akili.
katika mazingira yetu watu hushtuka kusikia fulani kajiua lakini ukifuatilia kwa makini mtu huyu alionyesha dalili zote za kutaka kujiua lakini watu hawakuzitambua na dalili hizo ni kama ifuatavyo.
kukosa raha kwa muda mrefu; mtu anakaa miezi sita mpaka mwaka akiwa hana raha huku akilalamikia jambo moja ambalo linamsumbua, kwa kawaida binadamu tuna matatizo mengi lakini mtu kuganda na tatizo moja kwa muda mrefu na kukosa msaada basi ujue anaelekea kubaya.
kua mpole ghafla; mtu ambaye kwa muda mrefu amekua akililia jambo fulani bila msaada kisha akakaa kimya ghafla na kuonekana kawaida na wakati jambo lililokua linamkwaza bado halijapata suluhisho huenda amejkata shauri sasa anajiua.
kukosa tumaini la siku zijazo; huenda huenda mtu ana madeni makubwa ya kifedha, biashara yake imekufa, amekutwa na ugonjwa hatari, kafiwa na wazazi, mume,mke au watoto na vitu hivyo vilikua nguzo yake kuu na haoni tena maisha yake ya baadae..
kujitenga na watu; mtu anaanza kujitenga na ndugu, jamaa na marafiki yaani anapenda kukaa peke yake bila kujichanganya na watu na hata mambo aliyokua akiyapenda kuyafanya zamani katika sehemu za starehe sasa hana raha tena akiyafanya.
kukosa usingizi; mtu anayeelekea kujiua hukosa usingizi kutokana na matatizo yanayomkabili, usku mzima hua macho na kitu kidogo kikipita nje lazima atakisikia...muda huu huwaza na kuwazua kuhusu matatizo yake ambayo kwa muda mrefu sasa yamekosa suluhisho na yeye haoni sababu ya kuendelea kuishi.
kubadilika ghafla kimtazamo; mtu aliyekua mchangamfu ghafla anakua mpole, mtu aliyekua mtanashati ghafla anaanza kuvaa hovyo na kutembea kwa haraka sana huku akiongea peke yake, vitu vya kawaida sasa vinamchukiza na kua mkali kwa chochote anachoambiwa.
kutishia kujiua; zaidi ya 75% ya watu wanaotaka kujiua watatoa vitisho kwamba siku moja nitajiua, katika hali ya kawaida mtu unaweza ukapuuza ukidhani ni masihara lakini nakwambia ukioana mtu anatishia kujiua basi usipuuze kauli zake kitaalamu inaitwa 'call for help' kwamba anaomba msaada ili asijiue na hii ndio dalili kuu muhimu kuliko zote.
kuanza kujiaandaa; mtu anayetaka kujiua ataanza maandalizi kwa kugawa baadhi ya mali zake, kuwatembelea ndugu na jamaa, kuandika usia wa mali zake, kuandika barua ya chanzo cha yeye kujiua, na huweza kunua vitu vya kujiua kama dawa, sumu, bunduki au kamba.

je kujiua kunaweza kuzuilika?
ndio mtu anayetaka kujiua mara nyingi anakua anataka msaada, jaribu kukaa na kumuuliza kitu gani kinamsumbua na kama amefikiria kujiua..
mshauri kwamba matatizo hayapo kwa ajili yake tu kwani kuna watu wengi wenye matatizo zaidi yake na kikubwa ni kuvumilia kipindi hiki kigumu lakini pia msaidie kwenda hospitali au kituo chochote akaonane na mshauri, kama una nafasi ya kumsaidia basi msaidie kulingana na tatizo lake..

nifanye nini kumsaidia mtu anayetaka kujiua?
ukishagundua mtu anataka kujiua kuna mambo ya msingi sana unatakiwa kuyafanya ili kumsaidia asijiue kama ifuatavyo.
usimuache peke yake; hakikisha unakaa naye muda wote na ikiwezekana piga simu kwa ndugu na jamaa na marafiki ili wakusaidie.
weka mbali vitu vya hatari; kama kuna kamba, au silaha yeyote basi ficha mbali lakini pia mwambie muhusika kwamba kama kuna kitu chochote ameshenunua kujidhuru basi mwambie akukabidhi uviweke mbali,
wasiliana na daktari ; kama ni mgonjwa wa akili ambaye anafahamika siku nyingi basi mpigie simu daktari wake ili aweze kurudishwa hospitali na kulazwa kabisa na kama hua sio mgonjwa wa akili basi apelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi.

mwisho; huenda wewe msomaji ndio muhusika ambaye umekata tamaa na unataka kujiua, nikupe moyo kwamba matatizo hayakuumbwa kwa ajili yako tu...kuna watu wengi wana matatizo makubwa zaidi yako na wengine waliwahi kua kwenye matatizo kama hayo na sasa wana mafanikio makubwa..usijiue hata kama umepata aibu au tatizo kubwa kiasi gani maishani mwako. kama ni mpenzi utapata mwingine, kama ni mtaji utapata mwingine, kama ni ugonjwa wewe sio wa kwanza kuugua hivyo jifunze kupambana nao...kumbuka muda ndio daktari mkuu yaani wazungu wanasema time will heal you,visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/
                                                        STAY ALIVE   
       
                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183
           

ZIFAHAMU DAWA ZINAZOTUMIKA KAMA CHANJO YA UKIMWI KWA SASA[PREP]

katika ukimwengu wa ukimwi mpaka sasa hivi shirika la afya duniani halijatoa tamko rasmi kwamba kuna dawa ya ukimwi inayoweza kutibu kabisa japokua baadhi ya nchi kama israel zimegundua dawa ambazo zimethibitika kuua zaidi ya asilimia 90% ya virusi lakini dawa hizo pia hazijaanza kutumika.
                                                                 

pre exposure prophylaxis ni nini?
katika mpango wa kutoa ARV kuna dawa ambazo zimethibitika zinaweza kufanya kazi kama chanjo ya ukimwi iwapo zikitumika kwa ufasaha bila kuruka, dawa hizi ni mchnagnyiko wa tenofovir na emtricitabine maarufu kama truvada, changamoto ya dawa hizi ni kwamba hazitumiki mara moja kama chanjo zingine yaani kama unataka usiugue ukimwi maisha yako yote unatakiwa uwe unazimeza kila siku na hapo unaweza kushiriki tendo la ndoa bila kuathirika hata kama ukilala na muathirika.

uwezekano wa kuzuia ukimwi ni asilimia ngapi?
tafiti zilizofanywa zimegundua kua dawa hizo zikitumika kila siku kama inavyotakiwa zinaweza kuzuia ugonjwa wa ukimwi kwa zaidi ya 99% kwa njia ya ngono na zaidi ya 70% kwa watu wanaochangia sindano za madawa ya kulevya.

watu gani wanatakiwa kumeza dawa hizi?
dawa hizi mara nyingi hupewa kwa makundi maalumu ya watu ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi kama ifuatavyo.

  • wanawake wanaouza miili yao ili kupata fedha.
  • walevi sana ambao hujisahau na kulala na mtu yeyote bila kinga.
  • wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujichoma sindano na kuzichangia.
  • kama una mpenzi, mke au mme ambaye ni muathirika na unataka kuzaa naye.
  • mashoga ambao wanajiuza na hata wale ambao hawajiuzi.
  • wanaume wenye wanawake wengi ambao hua watumii kondom.
  • watu wawili wanaoshiriki  ngono bila kondom wakati hawajui afya zao.
  • watu wanaoshiriki ngono ya watu wengi kwa wakati mmoja bila kinga maarufu kama threesome au foursome.
  • wanaohudumia wagonjwa wa ukimwi majumbani.
  • watu wenye magonjwa ya zinaa yanaowahatarisha kuugua ukimwi.
  • watu wenye wapenzi au wana ndoa ambao mmoja wao ni muathirika.

dawa hizi zinafanya kazi vipi?
dawa hizi huzuia virusi vilivyoingia kwenye mwili wa binadamu na kuvifanya vishndwe kusambaa mwilini, baada ya muda virusi hivyo hushindwa kuishi kwa kukosa chakula na kufa.

watu gani hawaruhusiwi kutumia dawa hizi?

  • watu ambao ni waathirika wa ukimwi hawatakiwi kutumia tena dawa hizi sababu hazitawasaidia kitu
  • watu wenye matatizo ya figo.
  • watu wenye matatizo ya maini.
  • wanawake wajawazito na wanaonyoshesha.
madhara gani hupatikana kwa kutumia dawa hizi?
madhara mdogo madogo kama kichefuchefu na kukosa hamu ya kula huweza kutokea mwanzoni lakini baadae huisha lakini ukiona mkojo unabadilikia rangi, tumbo kuuma sana na kupata msongo mkubwa wa mawazo to taarifa kwa daktari.

dawa hizi hutumika vipi?
kwa kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi truvada humezwa kidonge kimoja kila siku na muda uleule....ukisahau kumeza dawa usimeze viwili ila meza kilekile kimoja na kutumia kondom kwa angalau wiki moja.

ninaweza kuanzishiwa vipi dawa hizi?
kwa hapa tanzania dawa hizi zipo kwenye vituo vyote vya wagonjwa wa ukimwi na kabla hujaanzishiwa unatakiwa upimwe ili uanzishiwe kama wewe sio muathirika lakini pia utahitajika kwenda kituoni kila baada ya miezi mitatu kuangalia afya yako na kuongezewa dawa zingine, kumbuka kama wewe unafanya biashara ya kujiuza kondom bado ni muhimu kuzuia magonjwa mengine ya zinaa.

vipi kama nimeshalala na muathirika?
kama umeshalala na muathirika dawa hizi hazitumiki kuzuia ukimwi lakini kuna dawa zingine kitaalamu kama PEP ambazo humezwa ndani ya masaa 72 baada ya kukutana na muathirika na kwa maelezo zaidi kuhusu dawa hizo soma hapa http://www.sirizaafyabora.com/2015/05/jinsi-ya-kuzuia-vya-virusi-ukimwi-ndani.html

visit our english language blog here http://secretsofgoodhealth258.blogspot.com/
                                                                  STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.
                                                      0653095635/0769846183





YAFAHAMU MATIBABU YA UTUMWA WA SIMU.[CELLPHONE ADDICTION]

makala iliyopita nilizungumzia dalili 16 zinazoonyesha kwamba mtu umekua mtumwa wa simu yako kitaalamu kama cellphone addiction kama hukusoma makala hiyo bonyeza hapa http://www.sirizaafyabora.com/2017/08/dalili-16-zinazo-onyesha-wewe-ni-mtumwa.html , lakini leo ntazungumzia ni jinsi gani unaweza kupambana na hali hiyo na kua mtu huru kama ulivyokua mwanzo, hii itakusaidia kuzalisha na kuweka mahusiano yako ya kimapenzi na kijamii katika hali nzuri, hebu tuone njia za kupambana na hali hii.
                                                                   
kua bize na mambo yako; hii ndio sababu kubwa kwanini watu wazima hawaathriki sana na simu kama vijana, ni kwasababu watu wazima wana majukumu na shughuli nyingi ambazo wanatakiwa kuzifanya tofauti na vijana ambao wengi wao hawajitumi kufanya lolote hivyo kama wewe ni kijana jishughulishe na kazi kama huna kazi jitolee sehemu, jifunze hobi mpya kama kutumia vifaa vya mziki kama gitaa, au shughulika na kazi za nyumbani ambazo siku zote hua ni nyingi sana.
                                                               
weka mipango ya matumizi ya simu; kimsingi sio lazima kutumia simu muda wote na kama mtu ana shida na wewe kama haupatikani atakutafuta hata baadae, hivyo jiwekee kwamba labda kila siku ntakua situmii simu kwanzia saa saa mbili mpaka saa nne asubuhi, au sehemu maalumu kama darasani, kanisani, kwenye mkutano au semina basi jiwekee nidhamu ya kutotumia simu kabisa.
                                                                             
anza taratibu; usianze ghafla tu kwamba kwanzia leo situmii simu muda wote hapana, nenda taratibu na ujiwekee muda kwa mfano kama simu yangu haijaita ntakua naiangalia kila baada ya nusu saa au saa moja kisha ongeza muda mpaka masaa manne na baadae utazoea.
                                                                     
ondoa baadhi ya application kwenye simu; kuna na application nyingi sana za mitandao ya kijamii ni moja ya chanzo kikubwa cha kushinda kwenye mitandao ya kijamii yaani unaangalia facebook, instagram, snapchat, tweeter, tinder, tango, you tube na kadhalika kwa muda mfupi...mara nyingi ukiangalia au usiangalie mwisho wa siku hautaingiza chochote..hivyo unaweza kuziondoa application hizo na kuziweka kwenye computer yako ya nyumbani ili jioni unaangalia tu yaliyojiri mitandaoni na kwenye simu yako ukaacha zile application muhimu kama za google,vitabu, gmail na kadhalika.
                                                           
weka simu yako mbali; usikae umeshika simu yako muda wote na ukiwa unafanya shughuli zako muhimu basi ondoa sauti ili ikiita usiisikie na fanya kazi mpaka utakapokua umemaliza ndio ukaangalie simu yako lakini pia ondoa alamu au notifications za kwenye application zako ambazo zinakupa taarifa kila kikifanyika kitu kwenye mitandao ya kijamii hizi ndio zinakufanya ukague simu ovyo. kwa mwanafunzi ambaye unataka kusoma lakini unataka google kuangalia misamiati kadhaa basi weka simu kitandani au mbali na wewe, toa sauti na tumia wi-fi ya simu kutumia google ya kompyuta yako.
                                                               
chukua likizo ya simu; nenda trip ya utalii sehemu mbalimbali za nchi kisha acha simu nyumbani, to taarifa kwa baadhi ya watu muhimu kisha izime...kipindi utakachokua huko utajifunza kufanya mambo mengine zaidi ya kutumia simu muda wote.
tembea na kitabu kidogo; watu wengi hatuna tabia ya kujisomea vitabu mbalimbali ambavyo viko nje ya fani zetu lakini vitabu vinafundisha mambo mengi sana na kuwapa watu hekima, badala ya kutoa simu kila unapokua kwenye foleni au sehemu ya kusubiri kitu toa kitabu chako usome na kwa staili hii utajikuta unasoma vitabu vingi sana, kumbuka usisome vitabu vya kwenye simu kwani utajikuta unaishia kwenye mitandao ya kijamii.
badilisha mitazamo yako kuhusu simu; usijibu kila meseji na simu zinazoingia kwenye simu yako, kabla ya kushika simu jiulize kuna ulazima wa kuitumia hii simu sasa hivi? kuna ulazima wa kujibu meseji hii sasa hivi? kama hakuna basi achana nayo mpaka ukiwa umemaliza shughuli zako ndio uanze kujibu meseji na simu zilizopigwa.
mpe mtu simu yako; wakati mwingine unashindwa kabisa kuvumilia hamu ya kutaka kutumia simu labda baada ya kula, kazi au weekend basi mpe mtu unayemuamini akushikie simu yako kisha utaenda kuichukua baadae.
zima simu yako; hii ni moja ya vitu muhimu sana kwenye maisha ya binadamu, wakati mwingine tunakua tunafanya kazi sana na kushindwa kujipa muda wa kukaa na kutafakari tuliyoyafanya siku nzima hii huleta uchovu na msongo wa mawazo...basi jiwekee muda wa kuzima simu kwa masaa kadhaa ili uweze kupata muda wa kua mwenyewe na kutafakari.. hii pia itakusaidia kwenye mahusiano kwani utakua na muda wa kuongea na wapendwa wako bila kusumbuliwa. mfano unaweza kuamua kila ikifika saa nne usiku unazima simu.
                                           
ingia kwenye mazoezi; watu hufanya mazoezi nusu saa mpaka saa moja, muda ule unakua huwezi kutumia simu lakini pia mazoezi ni moja ya njia kuu ya kuondoa utumwa au addiction yeyeote ya kitu duniani kwa kubadilisha kemia ya ubongo wako na kukufanya ujisikie vizuri.
                                                             
omba msaada na uwajulishe wengine; ongea na mshauri kuhusu shida yako lakini pia watu ambao walikua wanapenda sana kuchati na wewe waambie kwamba sasa hivi umeamua kubadili mfumo wako wa maisha hivyo hautakua unapatikana sana kwenye mitandao ya kijamii.

                                                                     STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183

DALILI 16 ZINAZO ONYESHA WEWE NI MTUMWA WA SIMU YAKO.[CELLPHONE ADDICTION]

Ni miaka michache tu tangu kuingia kwa simu za mikononi duniani lakini tayari zimeleta utumwa mkubwa wa kimaisha na kifikra kiasi kwamba baadhi ya serikali duniani na kampuni binafsi zimeingilia kwa kuweka sheria kwamba matumizi ya simu hayatakiwi kazini kwani yanasababisha kazi zisiende, huko china tayari wamefungua vituo vingi vya kuwasaidai watu ambao wamepata addiction hizi sa simu na intanet... lakini pia mahusiano ya kimapenzi kuharibika sababu ya mtu kukaa kwenye simu muda wote bila kuzungumza na mwenza, kushindwa kuendela binafsi kwa shughuli zako za kiuchumi na kijamii kwa kupoteza muda mwingi sana kwenye simu badala ya kushughulika na maisha, kukosa fursa kwa kushindwa kuwasiliana na watu kwenye usafiri kama mabasi au daladala, uvivu wa kupitiliza kwa kushindwa kufanya kazi za nyumbani kama kupika, kufua, kufanya usafi na kadhalika.
unaweza kua unamfahamu mtu ambaye kwa sasa ni mtumwa wa simu ukadhani labda anafanya makusudi, hapana huyo ni mgonjwa na anataka msaada.
                                                       
         
kwa tafiti ndogo tu wahanga na watumwa wa simu ni vijana zaidi kuliko watu wenye umri mkubwa, yaani zaidi ya 58% ya vijana wana utumwa huu.
sasa kama umebahatika kuingia kwenye makala hii na kusoma basi hizi ndio dalili kwamba wewe ni mtumwa wa simu na unahitaji matibabu ili uweze kurudi katika hali yako ya kawaida.
ukikaa sehemu unasubiri kitu lazima utoe simu; hii inaweza kua kwenye foleni ya benki, darasani unasubiri mwalimu aje, kwenye dalalala au basi unaenda sehemu, kikao kinakaribia kuanza, na kadhalika lakini kabla simu hazijaja watu walikua wanatumia nafasi hizo kufahamiana, kuangalia mazingira ya nje kama utaona fursa, kuongea na wafanyakazi wenzao, kuongea na wanafunzi wenzako kuhusu somo husika na kadhalika lakini kwa sasa hali ni mbaya kiasi kwamba hata kama kikao kinaendelea, mwalimu anafundisha watu bado wanaangalia simu zao.
                                                                   
unapoteza muda mwingi kuangalia post kwenye intaneti; umekaa sehemu unatoa simu yako unaingia facebook au instagram na kuanza kuperuzi kwa muda mrefu kwenda chini bila kungalia chochote cha maana na kila baada ya dakika kadhaa unafungua kuangalia kama kuna post mpya na wewe uwahi kutoa maoni yako..lakini pia ukiona hakuna jipya unahamia kwenye mitandao mingine ya kijamii kutafuta jipya na ukikosa kabisa unaweza kuingia you tube na kupotelea huko.
                                                                 

unabeba chaja ya simu popote unapoenda; usisingizie kuisha kwa betri hapana wewe ndio unamaliza moto wa simu kwa zaidi ya 50% ya moto wote ndani ya saa moja ya siku inapoanza kwa kufungua vitu vingi sana ambavyo vinakula moto..kwa hali ya kawaida ukiamka na simu asubuhi ukawa bize na shughuli zako na kuitumia kupokea simu na kujibu meseji muhimu itafika jioni bado simu itakua ina moto lakini kama muda wote unayo simu  lazima itazima mapema lakini pia jiulize kwanini ukiwa na simu ndogo pembeni isiyo na intaneti huimalizi chaji?.
                                                                   
kuisha kwa chaji ya simu yako kunakukosesha raha; simu kuisha chaji sio mwisho wa dunia hasa kama hutegemei simu yeyote muhimu kwa siku hiyo, badala ya kuchanganyikiwa na kuanza kutafuta chaja iko wapi basi achana nayo upate muda wa kufanya mambo mengine na kupumzisha macho yako.
                                                             
unalala na kuamka na simu; mpaka usiku wa manane umeshazima na taa ya chumbani bado macho yako yako kwenye simu na muda mwingine unasinzia bila kujua simu uliiacha wapi lakini ukiamka asubuhi saa moja ya kwanza lazima upitie kila kitu kwenye simu yako kabla ya kuamka na kwenda kuoga na kujiandaa.
simu yako inakusumbua wakati wa kuendesha gari; ukiwa unaendesha gari meseji zinazoingia zinakupa muwasho wa kutaka kujua ni nani matokeo yake unajikuta unachati huku unaendesha gari lakini pia ukiwa kwenye foleni lazima uchukue simu uangalie wakati kuna mambo mengi unaweza kufanya kama kusikiliza radio ya gari au kuzungumza na watu ambao uko nao. angalizo; hii ni hatari na imeua watu wengi sana.
watu wanaokuzunguka huenda wanakwambia; wazazi wako wanakwazwa sana na kukuona muda mwingi uko kwenye simu, rafiki zako na mchumba wako pia wanakwambia kwamba hupati muda wa kuongea nao sababu ya simu, muda wa kula au kuangalia tv wewe umeshika simu unajibu sms.
                                                         
simu yako inafanya ushindwe kusoma; kama wewe ni mwanafunzi na unajikuta muda wote unasoma huku unaangalia na kujibu meseji za kwenye simu basi ujue umeshageuka mtumwa na utajikuta unasoma vitu vichache sana yaani kama ukipanga kusoma masaa mawili basi nusu saa tu ndio umesoma na saa moja na nusu umeitumia kwenye simu.
                                                             
hisia kwamba simu yako inaita zinakundama; kama kuna muda unasikia simu yako inaita au unapata hisia kwamba simu yako inatoa vibrations halafu ukiangalia hakuna kitu basi ujue imeshakukamata mpaka kwenye mishipa ya fahamu na ndio maana unapata hizo hisia za uongo kwamba simu inaita.
unaishi maisha ya kwenye mitandao ya kijamii; unahisi kwamba idadi ya likes unazopata na comment unahisi zinafanya kazi kwenye maisha ya kiuhalisia yaani ukipost ukapata likes nyingi sana unahisi maisha umeyamaliza kabisa kumbe una mambo mengi sana ya muhimu hujayafanya maishani mwako.                                                
muda mwingi unaangalia kama kuna ujumbe mpya au notifications; simu yako haijaita lakini kila baada ya dakika tano unatoa kuangalia kama kuna kitu kimekupita kwenye mitandao ya kijamii na usingependwa kuachwa nyuma kabisa lakini pia meseji ambazo hajizajibiwa zinakuwasha kiasi kwamba uko radhi uwahi google kutafuta jibu uweje kukoment mapema.
                                                                       
kujibu meseji kunakupotezea muda wako; huenda ungekua unawahi zaidi huko unapotaka kwenda
kama ungekua hujibu kila kitu kinachotumwa kwenye mitandao ya kijamii, yaani msanii mkubwa akipost kitu uko tayari usimame sehemu ukomenti ndio undelee na shughuli zako au unapoteza muda mwingi kuwaambia watu uko unafanya nini.
                                                       
unatumia simu na computer kwa wakati mmoja; yaani unaweza kukuta mtu ameingia facebook kwa computer yake lakini bado atachukua na simu yake aingie hukohuko facebook lakini pia hata akiangalia movie au video yeyote kwenye computer basi simu yake pia iko pembeni anaangalia huku na huku.                                              
unaenda na simu mpaka chooni au bafuni; ule muda ambao utakua chooni unajisaidia unahisi kama utapitwa matokeo yake simu unaingia nayo mpaka huko na kuiwekea bakteria wengi ambao ni hatari kwa afya yako.
unatembea na simu yako mkononi sio mfukoni kwako; ukiwa njiani unahisi ukiweka simu mfukoni utachelewa kuitumia pale meseji zitakapoingia hivyo unaishika mkononi kama gazeti lakini pia unatembea uko unasoma ujumbe na kujibu kiasi kwamba umeshawahi kujikwaa au kushindwa kuangalia mbele sababu ya simu.
unaangalia saa kwemye simu halafu unasahau; hii imeshawakuta wengi yaani unatoa simu kuangalia saa lakini ikishazima mwanga wake unakua tayari umesahau ni saa ngapi hiyo unaangalia tena kuhakikisha.
sherehe zenu au kukutana kwenu kunaharibiwa na simu; yaani mnaweza kua mmeandaa sherehe kama marafiki, au umepanga kuonana na mtu, au nyinyi wote mko kwenye meza moja ya sherehe lakini kila mtu yuko bize na simu kiasi kwamba maana ya nyinyi kuoanana au kukaa pamoja haipo tena.                                                          
mwisho; makala ijayo nitazungumzia ni vitu gani muhimu vya kuzingatia ili uweze kuachana na utumwa huu wa simu na kuishi maisha yenye mchango kwenye  shughuli zako za kila siku.

                                                                   STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183