hizi ni dawa zinazotumika na watu kupata hali fulani ya ulevi kichwani,unapozungumzia madawa ya kulevya hatumaanishi dawa ambazo ni magendo hapana hata kutumia dawa yeyote ya duka la madawa kama valium na zingine wakati wewe sio mgonjwa hayo ni matumizi ya dawa za kulevya, kutumia pombe mpaka ukizikosa unakua mgonjwa lakini pia matumizi ya dawa marufuku kama matumizi ya bangi, matumizi ya cocaine, heroine na kadhalika.
kuingia kwenye madawa kulevya huweza kua rahisi lakini kuondoka ni ngumu sana kwani hutengeneza utegemezi kitaalamu kama addiction na kumfanya muhusika kushindwa kuacha hata kama amedhamiria kuacha kutoka moyoni.
madawa ya kulevya yana madhara mengi sana ikiwemo kupoteza uelekeo wa maisha kwa kuacha shule, kazi, biashara au shughuli yeyote ya maendeleo, kuingia kwenye wizi mpaka wa mali za nyumbani ili uweze kupata pesa ya kupata madawa zaidi, kuambukizwa magonjwa mbalimbali kama ukimwi sababu ya kuchangia sindano wakati wa kutumia madawa hayo,kudharauliwa na familia na marafiki, ajali za gari na pikipiki, kuharibika kwa viungo muhimu vya mwili kama ubongo, mapafu, maini na figo, kuzaliwa kwa watoto wenye mtindio ubongo au kasoro mbalimbali za kimwili na kadhalika.
vita ya madawa ya kulevya ukiamua kuifanya binafsi kwa moyo wako wote inawezekana kabisa kikubwa uwe umeamua.
zifuatazo ni njia unazoweza kuzitumia kuacha madawa ya kulevya.
weka mipango ya kuacha madawa ya kulevya;
andika kwa kalamu chini mpango wa kuacha madawa hayo ili ujue kabisa siku fulani ya tarehe fulani mwezi fulani ntaacha rasmi madawa ya kulevya...inaweza kua siku muhimu labda pasaka, chrsitmas, iddi, au siku yako ya kuzaliwa.
andika madhara uliyoyapata tangu umeanza madawa ya kulevya
usiandike madhara ambayo nimeyataja hapo juu hapana andika yale uliyoyapata wewe yakakugusa moja kwa moja kiasi kwamba mpaka leo ukikumbuka unaona ni aibu kubwa ambayo umeipata kwenye maisha yako.
kubali kwamba wewe ni mwizi;
watu wengi wanaotumia madawa haya wenye kipato cha chini hujikuata wakiiba chochote nyumbani kwao na kwenda kuuza ili kupata pesa ya kununua dawa zingine na wasipodhibitiwa huweza kumaliza nyumba nzima kwani ni madawa ndio yanayowatuma.
andika chini mambo utakayofanya baada ya kuacha; huenda unaona wenzako wenye umri wako wamefanya mambo makubwa kimaisha, huenda unaona kipaji chako ulichokua nacho kimekufa, huenda unafeli mitihani, huenda familia yako imesambaratika, huenda umetengwa na jamaa zako hebu andika vitu utakavyofanya kuwaonyesha kwamba umerudi na wewe sio wa kudharaulika tena.
onana na daktari; nenda ukapime magonjwa yote ambayo yanawapata sana watumiaji wa madawa ya kulevya ili ujue unaanzia wapi kupambana na afya yako hii ikiwemo ukimwi, magonjwa ya ini mfano hepatitis, figo, kaswende yaani check up ya mwili mzima.
nenda kwenye kituo cha kuacha madawa ya kulevya; kuna vituo maalumu vya watu wanaotaka kuacha madawa ya kulevya, huko utajifunza mambo mengi sana na utapewa dawa ambazo zitakusaidia kupambana na kiu kali unayoipata pale unapoaachana na madawa ya kulevya lakini pia utapata ushauri kutoka kwa wataalamu waliobobea maswala hayo.
epuka sehemu ulizokua unapata dawa hizo; kama ulikua unapata dawa kwenye kumbi za disco au sehemu fulani fulani basi usiende tena huko na marafiki ambao mlikua manatumia nao vilevi hivyo waweke mbali kabisa najua watakucheka lakini wewe unajua unataka nini maishani mwako.
jiunge na mazoezi; usifanye mazoezi mwenyewe bali nenda gym, uwanjani na kadahalika ili ukutane na watu wengine na kupata marafiki wapya, mazoezi ni moja ya njia bora sana ya kupambana na kiu ya madawa ya kulevya.
jiunge na vikundi vilivyoacha madawa; kuna watu wengi wamefankiwa kuacha madawaya kulevya hata wasanii wakubwa nchini na nje ya nchi, jiunge na vikundi hivyo na vitakujenga zaidi ili upate moyo wa kuendelea kupambana na hali yako.
tafuta kazi; kazi itakupa majukumu ambayo utalazimika kuyafanya, hii itakupa ubize sana na kusahau kabisa kuhusu madawa lakini pia kama wewe ni mwanafunzi basi rudi darasani kua makini na shule na usipoteze muda tena.
anza maisha mapya; ukishaona dawa zimekuisha mwilini na unaishi maisha ya kawaida basi jenga maisha yako upya, jenga mahusiano na ndugu na jamaa, lakini pia endelea kurudi kwenye kituo cha kuacha dawa kuonana na washauri, onana na wenzako walioacha dawa kumbuka kuacha madawa kunachukua muda mrefu sana na usione umepata nafuu ukajua tayari kwani kuna watu wengi
wanafikia hatua nzuri na kurudi tena huko.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183
Asante sana kwa kutuarifu kuhusu madhara ya sawa za kulevya na namna ya kuachana nayo.
JibuFuta