data:post.body Julai 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA PRESHA YA MACHO NA MATIBABU YAKE [GLAUCOMA]

glaucoma ni nini?
hili ni ongezeko la presha ya macho, kimsingi macho hua yana presha ya 10mmhg mpaka 21mmhg lakini inapozidi hapo mgonjwa hutambulika kama mgonjwa wa presha ya macho.
mara nyingi ugonjwa huu hurithiwa na hauonyeshi dalili zozote mpaka baadae sana mtu anapokua mtu mzima.                                                  

ugonjwa huu huathiri mishipa ya fahamu inayohusika na kuona kitaalamu kama optic nerve na mgonjwa asipokua makini na matibabu yake basi huweza kupata upofu wa moja kwa moja na asione tena.

nini chanzo cha presha ya macho?
kitaalamu upande wa mbele ya jicho kuna maji maji kitaalamu tunaita aquous homour ambayo kazi yake ni kuleta virutubisho kwenye sehemu za jicho kama iris, lenzi na cornea pia kuondoa mabaki ya matumizi ya virutubisho hivyo lakini pia hutunza shepu ya jicho sasa maji maji haya yanapozidi ndio presha ya macho inapanda.
kwa kawaida hali hii hurithiwa kutoka kwenye kizazi kimoja mpaka kingine na sababu zingine zinazoweza kuongeza presha hii ni magonjwa ya macho, kuumia jicho kwa kupigwa na kitu au kumwagikiwa na kemikali au baada ya upasuaji wa macho wa kutibu tatizo lingine la macho.

watu gani wako kwenye hatari ya kuugua ugonjwa huu?

 • watu ambao ukoo wao una wagonjwa wa hivyo
 • watu wenye kisukari
 • watu wenye umri zaidi ya miaka 40
 • watu walioumia macho
 • watu wanaotumia dawa fulani fulani kama predinisolone
 • watu waliopata ajali na kuumia macho
 • watu wasioona vizuri
dalili za ugonjwa huu ni zipi?
mara nyingi ugonjwa huu dalili zake haziji moja kwa moja na huja kwa kujificha sana bila muhusika kujua na kuja kugunduliwa kwenye hatua mbaya kabisa. moja ya dalili ni 
 • kushindwa kuona mbali na pembeni 
 • kua na macho mekundu
 • maumivu makali ya macho
 • kichefuchefu na kutapika
 • kuona kama mawingu mawingu
je inagunduliwa vipi hospitali?
daktari atatumia vipimo maalumu kupima presha yako ya macho kisha atapima kuangalia kama mishipa ya fahamu inayohusika na kuona imeathirika kiasi gani...kipimo cha tenometry hutumika kupima presha ya macho.

matibabu yakoje?
hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu kabisa lakini kuna dawa za kutumia kwa muda wote wa maisha yako ambazo zitakua zinapunguza presha ya macho yako yaani zile za matone mfano timolol lakini pia wakati mwingine kuna aina za upasuaji hufanyika kuweka matundu kwenye iris ili kuachia maji haya kupita na kupunguza presha.

je unaweza kuzuia ugonjwa huu? 
huwezi kuzuia ugonjwa huu lakini unaweza kuzuia upofu kwa kuanza matibabu mapema na kuyafuatilia matibabu kwa umakini. kama kwenye ukoo wenu kuna ugonjwa huu na uko zaidi ya miaka 40 fanya vipimo kila baada ya mwaka mmoja au miwili lakini pia kama una kisukari pia fanya hivyo.
                                                                 STAY ALIVE

NJIA KUMI ZA KUMTAMBUA MTU ANAYESEMA UONGO WAKATI UNAONGEA NAYE.[SAIKOLOJIA]


kuna msemo unasema kwamba kila mtu ni muongo hapa duniani yaani , hakuna mtu ambaye ameshawahi kuishi bila kusema uongo kabisa..
kitaalamu mtu akiulizwa swali akajibu uongo, hali ya mwili hubadilika yaani mapigo ya moyo hukimbia, presha hupanda na anaweza hata kutokwa jasho.
                                                                 
kipimo cha polygraphy hutumia njia hii kufahamu kama mtu anadanganya au vipi kwa kuangalia mabadiliko ya mfumo wa mwili pale anapokua anaulizwa maswali, mara nyingi kipimo cha polygraphy hutumika na askari polisi kwenye nchi zilizoendelea kuwagundua wahalifu lakini pia baadhi ya vipindi vya mahusiano kwenye tv huweza kuwapima wapenzi au wanandoa kujua kama mmoja wao sio muaminifu.
sasa katika njia za kijasusi, inawezekana kujua mtu, rafiki yako, ndugu yako, mpenzi wako au mke wako anakudanganya kwa kuangalia vitu muhimu wakati wa kumohoji muhusika bila kua na mashine na kujua kwamba anakudanganya kama ifuatavyo.
kuchelewa kujibu swali; ukimuuliza mtu swali akachelewa kujibu kuna uwezekano mkubwa anadanganya lakini inategemea na aina ya swali ulilolo muuliza, kwa mfano ukimuuliza sikukuu ya christmas mwaka 2005 ulikua wapi? kwa hali ya kawaida lazima atafikiria kabla ya kutoa jibu na hatatoa jibu la uhakika sana lakini ukimuuliza miaka mitano iliyopita ulinisaliti na mwanaume mwingine kama hakukusali atajibu haraka kwa mshangao kwamba sio kweli lakini kama ni kweli alikusaliti akili yake itaanza kuwaza huyu mtu kajuaje na atachelewa kujibu kisha baada ya muda atatoa jibu la kukana au  atadanganya.
kukosekana mahusiano ya maneno na vitendo; kwa hali ya kawaida mtu akiulizwa swali na akatakiwa kujibu ndio au hapana kama ni ndio atatikisa kichwa kwenda juu na kama sio kweli atatikisa kichwa kwa pembeni sasa mtu akiulizwa swali akadanganya ataenda tofauti na hali ya kawaida mfano ukimuuliza kwamba ulienda kazini? atajibu ndio huku anatikisa kichwa kwenda pembeni bila yeye kutambua kwamba ulimi wake ndio unakubali lakini mwili wake umekataa.
kukohoa kidogo au kumeza kabla ya kujibu; mtu akipata wasiwasi baada ya kuulizwa kitu ambacho kimemkosesha amani kitaalamu mfumo wa mishipa ya fahamu kama sympathetic pathway unakua umefanya kazi hivyo mate yatakauka mdomoni na kwenye koo hivyo kuondoa hiyo hali atakohoa kidogo au kumeza mate kabla hajajibu ili kupata muda zaidi wa kutafuta cha kudanganya.
kuficha macho au mdomo kwa kutumia mikono; hii hutokea bila yeye kufahamu kitaalamu kama subconcious level yaani kibinadamu anashindwa kuuvumilia ule uongo anaosema hivyo atajikuta mwenyewe anaweka mikono sehemu hizo bila kujua ila wewe unayemuuliza maswali ndio utagundua kwamba anadanganya.
kushika shika sana sehemu za kichwa chake; kama nilivyosema hapo juu, mfumo wa sympathetic system ukianza kufanya kazi mishipa ya damu huanza kujikunja hasa na sehemu zinazokosa damu hasa usoni huanza kuwasha kwa mbali na kua tofauti hivyo muongo atajikuta anakuna pua, anakuna sikio na hata viganja vya mikono.
kuhangaika mazingira yanayomzunguka; mtu anayedanganya akiulizwa swali anaweza kuanza kuanza kurekebisha vitu ambavyo viko sahihi kwa mfano kurekebisha tai,miwani, kuchomekea vizuri...kama ni mwanamke muongo ataanza kuweka nywele vizuri na kurekebisha sketi yake kabla ya kujibu kumbuka kama akifanya vitu hivyo baada ya kujibu sio muongo au unamuuliza mtu swali amekaa mezani ghafla kila kitu kimebadilika sehemu kilipokuwepo yaani kahamisha glass ya maji, funguo zake, simu na kadhalika.
kushindwa kukuangalia usoni; unaweza ukaanza kumuuliza vitu vya kweli kabisa huku mnaangaliana lakini ghafla chomeka swali la tofauti ambalo unataka kujua kama ni kweli au sio kweli basi utaona anaanza kungalia pembeni na kushidwa kuangalia usoni na wakati mwingine kijasho chembamba kitamtoka.
kua na maneno mengi sana; unaweza ukampigia simu ukamuuliza mtu kwamba yuko wapi akakujibu nilienda hospitali kuona mgonjwa njiani kidogo ningatwe na mbwa afu nimechoka sana ntajitahidi leo nilale mapema na kadhalika...huyu anaweza kua medanganya kitu sasa anajaribu kukificha na maneno mengi ili usimjue lakini ukute kwa hali ya kawaida angesema niko hospitali kisha akakaa kimya.
kupunguza sauti; mtu kama huyu unaweza kaunza kumuuliza mambo anayofahamu kwa uhakika mfano jina lake, miaka yake, anaishi wapi au kama ni mchumba wako unaweza kumuuliza rafiki yake anaitwa nani, anafanya kazi gani na hapo atakua mchangamfu na kujibu vizuri kisha ghafla ukamuuliza nasikia umelala na mwanaume fulani hapo sauti itakua ndogo na atakataa kwa sauti ya chini.
kuapa mara nyingi; mtu muongo hujitahidi sana kujitetea aonekane hana kosa yaani kila baada ya muda ata apa kwa mungu, atakua na kauli kama 'ukweli kutoka moyoni", atasema hichi nachokisema hapa ni kweli kabisa lakini mtu mkweli anaweza kusema kitu mara moja hata usipomuamini hatajali sana na ataendelea na mambo yake.

                                                           STAY ALIVE
                               

HAYA NDIO MADHARA KUMI YA SIMU KIAFYA..


ulimwengu wa teknolojia unakua kwa kasi sana, mwaka 2005 na kurudi nyuma simu za mkononi zilikua chache sana lakini pia kabla ya mwaka 2000 simu hizi zilikua hazipo kabisa na watu wengi walikua wanatumia simu za mezani,barua au simu za posta kufanya mawasiliano...
lakini leo hii mfumo wa maisha umebadilika kabisa kiasi kwamba simu imekua moja ya vitu vya msingi sana vya binadamu ukiachana na chakula, nguo na maradhi yaani ukiwa huna simu kwa sasa mambo mengi na huduma nyingi huwezi kupata kirahisi ikiwemo huduma za kifedha na malipo ya huduma mbalimbali ka luku, maji, na kadhalika..
                                                       
lakini kama ilivyo ada kila kizuri kinachokuja au kila teknolojia mpya huambatana na madhara yake, tafiti zinaonyesha kuna magonjwa au matatizo hayakuwahi kuwepo kabisa kabla ya teknolojia kuanza lakini leo ndio yamezidi zaidi baada ya teknolojia kushika kasi.
hebu tuone madhara makubwa yaliyojificha nyuma ya simu za mkononi
saratani za ubongo; kitaalamu simu hutumia mionzi ya radio frequency au non ionizing radiations ambazo kimsingi hazina madhara makubwa sana kama ionizing radiation kama x ray na wenzake lakini mionzi hii ambayo hutolewa na simu kwenye antena zake tafiti zimeonyesha kwamba matumizi yake hasa yakiwa makubwa sana hasa kwa wale waongeaji wakubwa wa simu husababisha baadhi ya kansa za ubongo.
ugumba na utasa; tafiti moja iliwahi kufanyika na kugundua kwamba matumizi ya mionzi ya simu maarufu kama wi-fi yanashusha sana kiwango cha mbegu za kiume kwenye korodani ukilinganisha na wanaume ambao hawatumii wi-fi kwenye kazi zao, tafiti hizi zilifanyika baada ya kuona ongezeko kubwa la wanaume tasa kwenye jamii yetu na moja ya majibu ilikua ni matumizi ya wi-fi.
magonjwa ya kuambukiza; daktari mmmoja bingwa mtaalamu wa wadudu kitaalamu kama microbiologist alifanya tafiti na kugundua kwamba simu tunazotembea nazo sababu ya shughuli mbalimbali tuzazofanya tukiwa nazo huwa zina wadudu wengi wa maradhi kuliko wadudu wanaopatikana pembeni ya choo, tafiti iliongeza kwamba moja ya bacteria waliopatikana ni wale wasiosikia dawa kabisa mfano e.coli na kutoa ushauri watu kusafisha simu zao na dawa za kuua wadudu yaani antseptic angalau mara moja kwa siku kwani kutumia simu na baadae kula bila kunawa vizuri unakula uchafu mwingi sana.
aleji mbalimbali; kuna watu wengi wamekua wakiugua magonjwa ya ngozi kwa kuvimba na kuwashwa bila kujua chanzo ni nini lakini wataalamu wamegundua kwamba madini ya nickel yanayopatikana kwenye simu ni moja ya vyanzo vikuu vya aleji na mtu anaweza kuteseka miaka mingi bila kujua chanzo.
kukosa usingizi na msongo wa mawazo; watu wengi wamekua wakitumia simu mpaka usiku sana wakiwa kwenye mitandao ya kijamii hii huharibu mfumo wa usingizi na kujikuta mtu analala masaa machache sana na kuamka kwa kuchelewa sana au kuamka mapema kuwahi kwenye shughuli zake, na huko kazini hujikuta akilala muda mwingi na kupoteza ufanisi na kupelekea msongo wa mawazo.
mazoea au addiction; huko china wameanzisha clinic za kutibu wagonjwa ambao wamepata addiction ya kutumia internet ya simu na kushinda kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kua unaona msihara lakini siku hizi watu hawawezi kukaa nusu saa bila kuangalia kwenye simu na mtu simu yake ikikosa intaneti masaa kadhaa hukosa raha hata kama hakuna kitu cha msingi anafuatilia huko, kifupi ni kwamba watu hawa huko china wanatibiwa kama wahanga wa madawa ya kulevya.
matatizo ya macho; simu ina kioo kidogo sana ukilinganisha na kile cha komputa hivyo mtu hulazimika kukaza macho sana ili aweze kuona vizuri na mara nyingi watu wakitaka kulala baada ya kuzima taa huendelea kutumia simu na kupata mwanga wa moja kwa moja kutoka kwenye simu na hii huharibu uwezo wa macho kufanya kazi na baadae mtu atalazimika kuvaa miwani.
maumivu makali ya mgongo; matumizi ya simu huhitaji muhusika kuinama muda mwingi hasa kama anatuma meseji ili aweze kuona vizuri, lakini aina hii ya mkao humafanya mtumiaji kupindisha mgongo na kuanzisha maumivu makala sana ya mgongo hapo baadae.
kuvunjika kwa mahusiano; simu zimekua zikivunja mahusiano ya kijamii na mahusiano ya kimapenzi yaani watu wawili wanaweza kusafiri mkoa mmoja mpaka mwingine bila kufahamiana kiundani na hii inaweza kukunyima fursa kwani hujui unasafiri na nani huenda akikusaidia kuboresha maisha yako  lakini pia simu ndio zimekua chachu ya watu kutembea nje ya ndoa zao au nje ya mahusiano yao na kuficha siri huko.
ajali mbalimbali;tafiti zimeonyesha kupungua sana kwa umakini kwa madereva wanaotumia vyombo vya moto huku wanatumia simu lakini pia hata watembea kwa mguu wanaotembea huku wanatuama meseji wanakua kwenye hatari kubwa ya kuumia na kupata majeraha...hii imesababisha ajali nyingi sehemu mbalimbali na baadhi ya miili iliokotwa simu zao zikionyesha walikua wanatuma meseji, naomba nikazie hapa...unaweza kua unafikiri unatuma meseji mara moja tu lakini sekunde moja tu inaweza kukuokoa au kukuua ukiwa barabarani.
mwisho; kwa madhara niliyotaja hapo juu nafikiri ni wakati wa wewe ndugu msomaji kuanza kuchukua hatua na kutumia simu hizi pale unapokua unahitaji kweli hii itakusaidia kukulinda na majanga mbalimbali yatokanayo na simu.

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                   0653095635/0769846183
                                                           STAY ALIVE

FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA NDOTO NYEVU [WET DREAMS]

ndoto nyevu ni nini?
hii hali ya kuamka asubuhi na kujikuta umemwaga mbegu au manii kitandani, mara nyingi mtu humwaga mbegu hizi kwa kuota kwamba amefanya ngono wakati wa usiku na wakati mwingine unaweza kuamka asubuhi bila kukumbuka ndoto husika, hii inaweza kukuletea aibu kubwa hasa kama umelala ugenini na mbegu zimemwagika mpaka kwenye shuka lakini kitaalamu ni hali ya kawaida.
huhitaji kushika uume au kujichua kumwaga mbegu ila utaamka asubuhi na kujikuta tayari umemwaga mbegu kitandani.                                  

chanzo chake ni nini?
mwanaume yeyote anapoanza balehe kitaalamu homoni za testosterone huongezeka mwilini na kusababisha kuzaliwa kwa mbegu za kiume, kipindi hiki mwanaume husimamisha uume mara kwa mara bila hata kupenda yaani akiwa shule, kanisani, akiwa amelala, akiwa anaangalia tv na kadhalika, kwa sababu hii mbegu hujazana ndani ya korodani na njia pekaa ya kuzitoa ni kuota ndoto nyevu.

je kila mtu anapata ndoto nyevu?
hapana sio kweli kuna baadhi ya watu hawapati kabisa ndoto nyevu na kuna wengine wanapata zaidi ya mara tatu kwa wiki hivyo kama unazipata au hauzipati isikupe hofu kabisa kwamba unaweza kua una matatizo bali hiyo ni hali ya kawaida kabisa.

je wasichana wanapata ndoto nyevu?
watu wengi hufikiri ndoto hizi ni za wanaume tu lakini ndoto hizi huweza kuwapata hata wanawake japokua wao hawamwagi mbegu ila huweza kufika kileleni wakati wa usiku na kuamka asubuhi huku uke umeleoa sana lakini ni wachache sana ukilinganisha na wanaume.

je nifanyeje kuzui ndoto nyevu?
kama nilivyosema hapo mwanzo hakuna tatizo lolote linalotokana na kupata ndoto hizi hivyo unaweza kuachana nazo na kuzipuuzia au kuchukua hatua kama unataka kama ifuatavyo
ingia kwenye mahusiano; kama nilivyosema hapo mwanzo hamu kali ya ngono na kujaa kwa mbegu nyingi kwenye korodani ndio chanzo kikuu cha ndoto hizi hivyo tafuta mtu wa kushiriki naye tendo la ndoa kama umri wako na tamaduni zako zinakuruhusu kufanya hivyo kwa wakati huu, kumbuka korodani ni kama chupa ya maji yaani ikijaa lazima imwagike lakini pia watu wanaopiga punyeto hawapati ndoto nyevu.
usilale kwa tumbo; mara nyingi ukilalia tumbo, uume unakua unasugua shuka hivyo inaweza ikakuletea mazingira ya kuanza kuota umelala na mwanamke na kumwaga ndevu hivyo lala kwa mgongo au kwa upande.
usilale uchi; kulala uchi hasa kwa wanaume kunafanya uume wako uwe huru sana na kuguswa na mashuka muda wote hii itakufanya usimamishe uume muda mwingi usiku na kupata ndoto nyevu bila kutarajia.
fanya mazoezi mara kwa mara; mazoezi hupunguza sana mawazo ya ngono, hivyo hukufanya urelax usiku na kulala bila kuwaza ngono.
epuka kuangalia video za ngono au kuwaza ngono wakati wa kulala; kufanya hivi hukufanya ulale ukiwa na hamu sana ya kushiriki tendo la ndoa na matokeo yake utajikuta unamwaga mbegu wakati wa usiku.
epuka vyakula vinavyo ongenza mbegu kwa wingi; vyakula kama karanga, korosho na maparachichi sio vizuri kwa mtu anayetaka kupambana na ndoto nyevu kwani vyenyewe pia vinachangia hali hii.
amka mapema asubuhi; mara nyingi watu huota ndoto hizi baada ya saa 11 alfajiri hivyo ukijiwekea nidhamu ya kuamka mapema saa 11 asubuhi na kwenda mazoezini au kwenye shughuli zako ndoto hizi hazitakusumbua.

                                                             STAY ALIVE

JINSI YA KUJIPIMA MATITI YAKO KAMA KUNA KANSA...

shirika la afya duniani linasema kwamba zaidi ya wanawake laki tano waliuawa na kansa ya matiti mwaka 2011, idadi ya vifo hii hitegemewi kupungua zaidi ya kuongezeka miaka inavyozidi kwenda mbele... kutokana na hali hii njia mbalimbali zimekua zikitumika kujaribu kugundua kansa hizi mapema na kuzitibu kabla hazijafika hali mbaya zaidi.
unaweza kufika kwenye hospitali mbalimbali ukafanyiwa kipimo cha kuangalia uvimbe kwa kupapasa kwa kutumia mikono ya daktari au vipimo maalumu vya mionzi.
kama wewe ni msichana au mwanamke basi ni vizuri ukaweka utarativu wa kwenda kupima kansa ya matiti anagalau kila baada ya miezi sita na kama huwez kwenda hospitali basi leo ntaenda kufundisha jinsi ya kujikagua ili ukigundua uwahi hospitali, kumbuka katika hatua za mwanzo kabisa za kansa mgonjwa anaweza kutibiwa na kupona kabisa lakini ikishasambaa mwili mzima inakua ngumu kidogo kumsaidia mgonjwa kama huyo..

zifuatazo ni hatua tano za kujikagua matiti yako
hatua ya kwanza;
ukiwa kifua wazi simama mbele ya kioo huku umeweka mikono kiunoni kisha angalia kama kuna vitu vifuatavyo

 • angalia kama matiti yako yamebadilika rangi, shepu au ukubwa...kwa hali ya kawaida matiti hufanana kwa kila kitu bila uvimbe au chochote.
 • ukiona mabadiliko ya ngozi kwa hali yeyote ile, chuchu kuvimba au kutumbukia ndani, wekundu au upele basi nenda hospitali upesi..
hatua ya pili..
inua mikono kwenda juu na uangalie tena, hapa angalia kama kuna majimaji yeyote yanayotoka kwenye matiti...inaweza kua maziwa, maji au damu na ukiona maji ya aina yeyote na rangi yeyote vinatoka nenda hospitali haraka.

hatua ya tatu;
 sasa lala kitandani na uanze kuyatomasa maziwa yako kwa kutumia mikono na kwa ziwa la kushoto tumia mkono wa kulia na ziwa la kulia tumia mkono wa kushoto..
hapa unaweza kutumia njia tatu kuu, kwanza unaweza kuanzia kwenye chuchu na kutomasa kwa duara kwenda nyuma mpaka ufike mwisho wa titi, pili unaweza kutomasa kama unapanda na kushuka mwinuko wa ziwa tatu unaweza kutomasa kwanzia ndani kwenda nje moja kwa moja kama picha zinavyoonyesha hapo...hakikisha unakandamiza vizuri mpaka ndani kabisa ya ziwa na ukihisi vitu kama vya duara ndani ya ziw, ugumu kwenye ngozi au kitu chochote ambacho mwanzoni hukua nacho wahi hospitali..

hatua ya nne;
simama na uyakague matiti kama jinsi nilivyoelekeza kwenye hatua ya tatu, wanawake wengi hupendelea kufanya hivi wakiwa wameloa maji kwenye matiti hasa kwenye hatua hii ya kusimama hivyo unaweza kufanya hivi ukiwa bafuni tu.

mwisho; maelekezo niliyotoa hapo ni mepesi sana na muda mchache sana unaweza kutumika kufanya kazi hii lakini ukipuuzia unaweza kupoteza maisha, kumbuka unaweza kujipima angalau mara mbili au mara nne kwa mwaka yaani kila baaada ya miezi mitatu mpaka sita na kila mwanamke yuko hatarini kupata kansa ya matiti.

                                                                   STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                          0653095635/0769846183

HIZI NDIO NJIA 10 MUHIMU ZA KUACHA MADAWA YA KULEVYA

madawa ya kulevya ni nini?
hizi ni dawa zinazotumika na watu kupata hali fulani ya ulevi kichwani,unapozungumzia madawa ya kulevya hatumaanishi dawa ambazo ni magendo hapana hata kutumia dawa yeyote ya duka la madawa kama valium na zingine wakati wewe sio mgonjwa hayo ni matumizi ya dawa za kulevya, kutumia pombe mpaka ukizikosa unakua mgonjwa lakini pia matumizi ya dawa marufuku kama  matumizi ya bangi, matumizi ya cocaine, heroine na kadhalika.
                                                 

madawa ya kulevya ni moja ya majanga makubwa ambayo yanatingisha afya na uchumi wa nchi mbalimbali duniani kwani huathiri vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa, kama wewe hujawahi kutumia dawa za kulevya usishawishike hata kuonjwa kwani hauta acha kirahisi, serikali mbalimbali ikiwemo serikali ya tanzania zimekua mstari wa mbele kujaribu kupambana na madawa ya kulevya lakini pia kuanzisha vituo kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya.
kuingia kwenye madawa kulevya huweza kua rahisi lakini kuondoka ni ngumu sana kwani hutengeneza utegemezi kitaalamu kama addiction na kumfanya muhusika kushindwa kuacha hata kama amedhamiria kuacha kutoka moyoni.
madawa ya kulevya yana madhara mengi sana ikiwemo kupoteza uelekeo wa maisha kwa kuacha shule, kazi, biashara au shughuli yeyote ya maendeleo, kuingia kwenye wizi mpaka wa mali za nyumbani ili uweze kupata pesa ya kupata madawa zaidi, kuambukizwa magonjwa mbalimbali kama ukimwi sababu ya kuchangia sindano wakati wa kutumia madawa hayo,kudharauliwa na familia na marafiki, ajali za gari na pikipiki, kuharibika kwa viungo muhimu vya mwili kama ubongo, mapafu, maini na figo, kuzaliwa kwa watoto wenye mtindio ubongo au kasoro mbalimbali za kimwili na kadhalika.
vita ya madawa ya kulevya ukiamua kuifanya binafsi kwa moyo wako wote inawezekana kabisa kikubwa uwe umeamua.
zifuatazo ni njia unazoweza kuzitumia kuacha madawa ya kulevya.
weka mipango ya kuacha madawa ya kulevya;
andika kwa kalamu chini mpango wa kuacha madawa hayo ili ujue kabisa siku fulani ya tarehe fulani mwezi fulani ntaacha rasmi madawa ya kulevya...inaweza kua siku muhimu labda pasaka, chrsitmas, iddi, au siku yako ya kuzaliwa.
andika madhara uliyoyapata tangu umeanza madawa ya kulevya
usiandike madhara ambayo nimeyataja hapo juu hapana andika yale uliyoyapata wewe yakakugusa moja kwa moja kiasi kwamba mpaka leo ukikumbuka unaona ni aibu kubwa ambayo umeipata kwenye maisha yako.
kubali kwamba wewe ni mwizi;
watu wengi wanaotumia madawa haya wenye kipato cha chini hujikuata wakiiba chochote nyumbani kwao na kwenda kuuza ili kupata pesa ya kununua dawa zingine na wasipodhibitiwa huweza kumaliza nyumba nzima kwani ni madawa ndio yanayowatuma.
andika chini mambo utakayofanya baada ya kuacha; huenda unaona wenzako wenye umri wako wamefanya mambo makubwa kimaisha, huenda unaona kipaji chako ulichokua nacho kimekufa, huenda unafeli mitihani, huenda familia yako imesambaratika, huenda umetengwa na jamaa zako hebu andika vitu utakavyofanya kuwaonyesha kwamba umerudi na wewe sio wa kudharaulika tena.
onana na daktari; nenda ukapime magonjwa yote ambayo yanawapata sana watumiaji wa madawa ya kulevya ili ujue unaanzia wapi kupambana na afya yako hii ikiwemo ukimwi, magonjwa ya ini mfano hepatitis, figo, kaswende yaani check up ya mwili mzima.
nenda kwenye kituo cha kuacha madawa ya kulevya; kuna vituo maalumu vya watu wanaotaka kuacha madawa ya kulevya, huko utajifunza mambo mengi sana na utapewa dawa ambazo zitakusaidia kupambana na kiu kali unayoipata pale unapoaachana na madawa ya kulevya lakini pia utapata ushauri kutoka kwa wataalamu waliobobea maswala hayo.
epuka sehemu ulizokua unapata dawa hizo; kama ulikua unapata dawa kwenye kumbi za disco au sehemu fulani fulani basi usiende tena huko na marafiki ambao mlikua manatumia nao vilevi hivyo waweke mbali kabisa najua watakucheka lakini wewe unajua unataka nini maishani mwako.
jiunge na mazoezi; usifanye mazoezi mwenyewe bali nenda gym, uwanjani na kadahalika ili ukutane na watu wengine na kupata marafiki wapya, mazoezi ni moja ya njia bora sana ya kupambana na kiu ya madawa ya kulevya.
jiunge na vikundi vilivyoacha madawa; kuna watu wengi wamefankiwa kuacha madawaya kulevya hata wasanii wakubwa nchini na nje ya nchi, jiunge na vikundi hivyo na vitakujenga zaidi ili upate moyo wa kuendelea kupambana na hali yako.
tafuta kazi; kazi itakupa majukumu ambayo utalazimika kuyafanya, hii itakupa ubize sana na kusahau kabisa kuhusu madawa lakini pia kama wewe ni mwanafunzi basi rudi darasani kua makini na shule na usipoteze muda tena.
anza maisha mapya; ukishaona dawa zimekuisha mwilini na unaishi maisha ya kawaida basi jenga maisha yako upya, jenga mahusiano na ndugu na jamaa, lakini pia endelea kurudi kwenye kituo cha kuacha dawa kuonana na washauri, onana na wenzako walioacha dawa kumbuka kuacha madawa kunachukua muda mrefu sana na usione umepata nafuu ukajua tayari kwani kuna watu wengi
wanafikia hatua nzuri na kurudi tena huko.

                                                                STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                       0653095635/0769846183