kansa ya damu ni nini?
kansa ya damu ni hali ambayo mwili unatengeneza seli nyingi sana nyeupe za damu kuliko kiwango ambacho kinatakiwa mwilini, seli huzi hutengenezwa na uvimbe kitaalamu kama tumour ambao unakua ndani ya mifupa ya kutengeneza damu.[bone marrow]
kuna aina mbili za kansa ya damu kama ifuatavyo
acute leukemia; hii ni aina ya kansa ya damu ambayo seli nyingi nyeupe za damu ambazo hazijakomaa hutengenezwa ndani ya mifupa[bone marrows], seli hizi hua nyingi sana na kuzuia mifupa kutengeneza seli zingine za kawaida.
mara nyingi kansa ya aina hii huwapata watoto wadogo, japokua wakubwa pia wanaweza kupata na matibabu ya haraka hutakiwa kuanza, pamoja na teknolojia ya matibabu mgonjwa mara nyingi hufariki ndani ya miezi sita.
chronic leukemia: hii ni aina ya pili ya kansa ambayo inatokea pale mifupa[bone marrows] inapotengeneza seli nyingi nyeupe ambazo zimekomaa, aina hii ya kansa huchukua miezi au miaka kusambaa mwilini na matibabu yake hucheleweshwa mpaka mgonjwa atakapoonekana anafaa kuanza matibabu.mara nyingi haina hii huwapata vijana na wazee lakini huweza kutokea kwenye umri wowote.
nini chanzo cha kansa ya damu?
mara nyingi vyanzo halisi vya kansa ya damu hua havifahamiki lakini kuna mambo ambayo yanaweza kuchangia kuanza kwa kansa hii kama ifuatavyo..
- kupigwa na mionzi; hii inaweza kua mionzi ya jua au x ray za hospitali, mionzi hii huharibu uwezo wa mwili kuamua kwamba seli zitengenezwe nyingi au kidogo matokeo yake kansa huanza.
- dawa zinazofanya kazi kwenye seli; mfano dawa zingine za kutibu kansa mbalimbali huweza kuleta kansa ya damu...mfano methotroxate
- kuguswa au kuvuta hewa yakemikali ya benzene; hii ni kemikali inayopatikana sana viwandani, watu wanaofanya kazi huko hua wanakua na hatari ya kuguswa nayo mwilini lakini pia hupatikana kwa wingi kwenye sigara na kidogo kwenye mafuta tunayotumia kwenye gari, mifuko ya plastiki, gundi na rangi za kupaka mbao za viti na makabati.
- kushambuliwa na virusi; baadhi ya virusi huweza kushambulia mwili na kusababisha kansa mfano htlv 1 viruses
- kuishiwa na kinga ya mwili; mara nyingi mtu akiwa mzima seli za kansa huonekana ndani ya miili yetu lakini kinga ya mwili hupambana na kua kansa hizo, kinga ikishuka uwezo wa mwili kupambana na kansa hizo huondoka na mgonjwa huugua kansa.
- kurithi; baadhi ya koo zina vimelea ambavyo hurithishwa kutoka wazazi kwenda kwa watoto, aina za kansa za kurthi ni mbaya sana kwani huweza kumaliza ukoo mzima.
- matumizi ya kemikali za mbolea na kuulia wadudu shambani kitaalamu kama organophosphate.
dalili za acute leukemia
kuishiwa damu
homa
kutokwa na damu sehemu mbalimbali kama puani,mdomoni,choo kubwa, machoni na matundu yote ya mwili.
mifupa na jointi kuuma
kuvimba maini
kuvimba bandama
kuugua mara kwa mara
mara nyingi seli za kansa zikifika kichwani mgonjwa huanza kuumwa kichwa, kupata kizunguzungu, kichefuchefu na kutapika.
dalili za chronic leukemia
kuchoka sana
kupungua uzito
kushindwa kupumua
maumivu ya tumbo
kutokwa jasho usiku
homa na moyo kukimbia
kuvimba kwa tezi, maini na bandama
kuishiwa damu
kinga ya mwili kushuka
vipimo ambavyo hufanyika kugundua ugonjwa huu
full blood picture; hiki ni kipimo ambacho huchukuliwa kuangalia vitu mbali mbali vya damu ikiwemo kiasi cha damu na kuongezeka kwa seli nyeupe za damu
bone marrow aspirate; kipimo hiki hufanyika kwa kuvuta seli zilizoko ndani ya mfupa kwa kutumia sindano kisha kwenda kuzipima kuangalia kama zina seli za kansa.
vipimo vingine huchukuliwa ili kuangalia kama kansa zimeshasambaa sehemu mbalimbali za mwili kama x ray ya kifua, ct scan ya kichwa na tumbo,mri ya ubongo, nyama kidogo hukatwa kwenye tezi kuangalia kama kansa imefika huko.
matibabu ya kansa ya damu
kansa hutibiwa kulingana na aina ya kansa mtu aliyonayo kama ifuatavyo...
matibabu ya acute leukemia
dawa mbalimbali hutolewa kutibu kansa hii ya damu japokua hulenga kwenye kusogeza muda tu kwani uwezekano wa kupona hua ni mdogo sana, dawa hizi za kumeza kutibu kansa kitaalamu huita chemotherapy... lakini ugonjwa huu ukigunduliwa mapema mtu huweza kupona kabisa, baada ya matibabu mgonjwa akikaa miaka mitano bila dalili zozote huhesabika amepona. dawa zinazotolewa ni kama predinisolone,vincristine,etoposide,cytarabine, and methotroxate.
kama nilivyosema mwanzo wagonjwa wa aina hii ya kansa mara nyingi hufariki ndani ya miezi sita sababu ya ukali wa aina hii ya kansa.
matibabu ya chronic leukemia
matibabu ya aina hii ya kansa hujumuisha mionzi yaani radiotherapy na dawa yaani chemotherapy, mgonjwa haanzishiwi matibabu hapo hapo mpaka vipimo vitakapoonyesha kwamba yuko tayari kwa matibabu
matumizi ya virutubisho; mara nyingi matibabu ya kansa yana madhara makubwa sana mwilini kutumia virutubisho vyenye vitamini mbalimbali huweza kumsaidia mgonjwa kupata nafuu au kupona haraka na kutopata madhara mengi, virutubisho hivyo ni vile vyenye mchanganyiko wa wa vitamin nyingi ambazo kwa kawaida huzuia kansa mfano vitamin c, vitamin e, vitamin a na kadhalika, chagua virutubisho vyovyote vya kampuni inayouza japokua baadhi ya kampuni kama forever living wana virutubisho bora zaidi ambavyo kuna watu wenye kansa hizi sehemu mbalimbali duniani wametoa ushahidi wa kupata nafuu kupitia bidhaa zao. virutubisho hivi ni muhimu sana kwa wagonjwa hawa kwani uwezo wao wa kula ni mdogo na hata wakila vyakula vyetu vingi vya kiafrika havina mchanganyiko wa mlo kamili..pichani ni dada aliyefanikiwa kwa kutumia bidhaa zao huko asia wakati anaumwa kansa ya damu.
mwisho;wagonjwa wachache sana huweza kupona kabisa ugonjwa wa kansa ya damu lakini pamoja na kupona ugonjwa huu huweza kurudi baada ya muda fulani, pamoja na teknolojia tuliyonayo kansa ya damu bado ni changamoto kubwa sana na moja ya vyanzo vya vifo vingi duniani.tembelea blog yetu ya kingereza hapa http://www.vibesinc.ga/
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183[TUMA MESEJI TAFADHALI]
0 maoni:
Chapisha Maoni