data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA FISTULA NA MATIBABU YAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA FISTULA NA MATIBABU YAKE.

fistula ni nini?
kitaalamu ni tundu ambalo silo la kawaida linaloonganisha viungo viwili vya binadamu, kwa kawaida viungo vya binadamu havina matundu lakini matundu haya yanapotokea huitwa fistula, mfano tundu kati ya koo la hewa na chakula, tundu kati ya uke na njia ya choo, tundu kati ya njia ya uke na mkojo.
fistula ya uzazi hutokea pale panapokua na tundu kati ya njia ya choo kubwa, choo ndogo na uke au njia ya uzazi...hali hii husababisha kinyesi na mkojo kupita sehemu za siri.


fistula husababishwa na nini?
kwa nchi zilizoendelea kama marekani, fistula husababishwa na kutumia vifaa vya kuzalisha pale mama anaposhindwa kusukuma kwa njia ya kawaida yaani mpka asaidiwe kitaalamu kama forceps au vacuum delivery lakini kwa nchi ambazo hazijaendelea kama tanzania fistula husababishwa na uchungu wa muda mrefu ambapo mtoto anakandamiza kibofu cha mama au utumbo mkubwa na kusababisha damu kushindwa kufika eneo hilo na kuoza au kuchanika, hali hii ndio huleta tundu hilo la fistula.
sababu zingine ni kuvunjika kwa mifupa ya mapaja, saratani mbalimbali za uzazi,kubakwa,kutoa mimba au makosa wakati wa upasuaji wa kizazi, mionzi ya matibabu ya kansa, magonjwa ya zinaa kama kaswende, ugonjwa wa kichocho

dalili za fistula ni zipi?
kutokwa na mkojo au choo kubwa sehemu za siri hasa wakati wa usiku bila kujitambua au kushindwa kuzuia.
harufu kali sehemu za siri
kuugua ugonjwa wa njia ya mkojo mara kwa mara maarufu kama uti
maumivu makali ya uke na sehemu zinazozunguka
maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
msongo wa mawazo
kukosa siku za mwezi
kuharibika kwa mimba zijazo
ugonjwa wa ngozi sababu ya mkojo kumwagikia ngozi

vipimo gani hufanyika kugundua fistula?
kipimo cha picha ya utrasound hutumika sana kuangalia kama kuna tundu ambalo sio la kawaida limetokea kwenye sehemu hizo za siri.

matibabu ya fistula.
fistula ikigundulika mapema huweza kutibiwa kwa kuingiza mpira wa mkojo kitaalamu kama catheter na kuuacha hapo mpka tundu lile litakapoziba, mpira huweza kubadilishwa kulingana na na muda mgonjwa atakaotibiwa, dawa za kuua bacteria hutolewa na mgonjwa huwekewa drip za maji mengi ili kuongeza damu katika eneo husika kitu ambacho husaidia kupona haraka.
matibabu yakichelewa mgonjwa hutakiwa kufanyiwa opasuaji na daktari bingwa ili kushona tundu hilo, kwa hapa tanzania upasuaji huo ni bure kabisa katika hospitali ya CCBRT dar es laam.

madhara ya fistula ni yapi?
kibovu cha mkojo kuondoka sehemu yake
kupata ugonjwa wa njia ya mkojo mara kwa mara
ugumba
kuishiwa damu
sehemu za uke wa mwanamke kuharibika
kuvunjika kwa ndoa
kutengwa na jamii
kujiua kwa wahanga wa tatizo hili.

jinsi gani tunaweza kuzui fistula kwenye jamii zetu?
kuzuia wasichana wadogo kuzaa
hakikisha mama hakai na uchungu zaidi ya masaa 12 baada ya uchungu kuanza
hakikisha mama anazalia hospitali ili asaidiwe vizuri
kuweka miondominu mizuri kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa.

                                                STAY ALIVE

                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                     0653095635/0769846183






Maoni 1 :

  1. Ahsante sana dr. Ila nnauliza je kuna madhara gani yanayoweza tokea endapo utafanya tendo la ndoa na mgonjwa wa fistula

    JibuFuta