data:post.body BONYEZA HAPA KUJIPIMA NA KUJIFUNZA KUHUSU IQ AU UWEZO WA AKILI.[INTELIGENT QUOTIENT] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

BONYEZA HAPA KUJIPIMA NA KUJIFUNZA KUHUSU IQ AU UWEZO WA AKILI.[INTELIGENT QUOTIENT]

inteligent quotient[IQ] ni nini?
hichi ni kipimo kinachopima uwezo wa mtu kufanya vitu fulani kulingana na umri wake, mfano mtoto mwenye miaka mitano anatakiwa aweze kufanya mambo yanayotakiwa kufanywa na mtoto wa miaka mitano kama kuongea, kusoma kama amefundishwa, kuhesabu namba na kadhalika hiyo tunaita uwezo wa kawaida na unaofaa lakini kama mtoto wa miaka mitano ana uwezo wa kufanya mambo ya mtoto wa miaka miwili au mitatu huyo uwezo wake wa kiakili ni mdogo na kama mtoto huyuhuyu wa miaka mitano anaweza kufanya mambo ya mtoto wa miaka kumi huyu uwezo wake wa akili au IQ ni kubwa sana kitaalamu tunamuita genius.
tafiti mbalimbali zilizofanyika ziligundua nchi ambazo hazijaendelea zina watu wengi sana wenye uwezo mdogo wa kiakili kulingana na sababu mbalimbali ukilinganisha na nchi zilizoendelea ambazo wana uwezo mkubwa zaidi.
                                                       
makundi ya uwezo wa kiakili[1Q]
  IQ YA 130 NA ZAIDI
hawa wana akili sana kitaalamu kama geniuses wana uwezo mkubwa sana wa kuelewa vitu haraka na kugundua jambo ambalo mtu wa kawaida hawezi kulifikiria. mwanasayansi wa karne ya 20 kwa jina la albert einstein alikua na IQ ya 160.

 IQ 120 mpaka 129
hawa ni watu wenye akili, wana uwezo wa kuelewa vitu na kufundishika, kwa nchi zilizoendelea watu hawa wapo wengi.

IQ 110 mpaka 119
hawa wana akili za kawaida zilizozidi kidogo, wanapatikana hata kwenye nchi ambazo hazijaendelea lakini hua ni wachache kwenye kikundi cha watu kadhaa.

IQ 90 mpaka 109 
hawa wana akili za kawaida, wakiweka juhudi kwenye masomo na shughuli zao huweza kufanya kazi vizuri.

IQ 80 mpaka 89 
hawa wana akili za kawaida sana na hutakiwa kuweka juhudi kubwa sana katiaka maisha yao hasa masomo ili waweze kufaulu vizuri bila hivyo ni ngumu sana.

IQ 70 mpaka 79 
hichi ni kiwango cha chini kabisa cha akili ya binadamu, watu hawa wanaongea kawaida lakini juhudi kubwa sana huhitajika kuwafanya waelewe vitu viwe vya darasani au nje ya darasa, wachache sana huweza kufika kiwango kikubwa cha juu cha elimu au kufanya kazi zao vizuri.

IQ 55 mpaka 70
hawa watu wana uwezo wa kuongea na kupata marafiki lakini wakipelekwa shule hawatafeli mitihani.

IQ 40 mpaka 55
watu hawa wanaweza kuongea, wanaweza kujisimamia mambo yao, lakini hawawezi kufaulu shuleni.

IQ 25 mpaka 40
hawa wana uwezo mdogo sana, hufundishwa jinsi ya kufanya mambo kama kuvaa na kujitunza, wanaweza kuongea kidogo sana.

IQ 20 mpaka 25
hawa wanataka uangalizi maisha yao yote, hawawezi kufanya chochote bila kusaidiwa, wana tabia za kujitenga wenyewe na maisha yao yote huishi kwa kutegemea wengine..

kumbuka; makundi yote yana uwezo wa kufanya kazi ngumu lakini hawana uwezo wa kufanya kazi za kutumia akili.
tafiti zimefanyika nchi nyingi duniani ili kujua nchi gani ina watu wenye uwezo mkubwa wa kiakil na nchi za kiafrika zimekua za mwisho kwa kipimo hicho na iq ya watanzania ni 72[average IQ]

chanzo cha IQ ndogo ni nini?
mara nyingi tatizo lolote, ugonjwa wowote au ajari yeyote inayoweza kutokea kabla binadamu hajafikisha miaka 18 huweza kumuharibia uwezo wake wa kua na akili na kumfanya awe na uwezo mdogo sana.sio rahisi mtu kupata hali hii baada ya miaka 18. dalili hizo ni kama ifuatavyo
kabla ya kuzaliwa; mtoto akiwa tumboni huweza kusababishiwa kua na uwezo mdogo wa akili sababu ya magonjwa akiwa tumboni kama kaswende, mama kutopata mlo kamili wenye virutubisho vyote, kunywa pombe na sigara kipindi cha ujauzito, kurithi kwa wazazi yaani kati ya baba au mama anaweza kua na uwezo mdogo darasani na mtoto akarithi, dawa zinazotumika na mama kipindi cha ujauzito na magonjwa ya vinasasaba vya mtoto kama down syndrome.
wakati wa kuzaliwa; siku ya mtoto kuzaliwa, mtoto huweza kukutana na changamoto nyingi sana ambazo zinaweza kumfanya awe na uwezo mdogo sana darasani mfano uchungu kuchukua muda mrefu sana, mtoto kukosa hewa wakati wa kuzaliwa, kupinda kwa kichwa wakati wa kuzaliwa sababu ya njia ndogo na hii inaweza kuchangia kichwa kukaa vibaya.
baada ya kuzaliwa; baada ya kuzaliwa mtoto huweza kupata shida mbalimbali ambazo zinaweza kuharibu uwezo wake kiakili mfano kuugua magonjwa mbalimbali mfano homa ya uti wa mgongo na magonjwa ya mishipa ya fahamu, kuugua na kulazwa kwa muda mrefu sana, kupata ajali ya kuumiza kichwa, mtoto aliyetelekezwa au kufiwa na wazazi, kukosa chakula cha kutosha wakati wa ukuaji na kadhalika.

zipi ni dalili za watu wenye uwezo mdogo wa kiakili?
wazazi wengi wamekua wakali kwa watoto wao ambao wanashindwa kufaulu au kufanya vitu fulani kwenye maisha yao bila kujua kwamba kitaalamu kuna watu hawawezi kufanya vitu fulani yaani sio kila mtoto anaweza kua daktari, injinia, rubani, au kusoma masomo magumu ya sayansi na kuna uwezekano mkubwa akili zake amezirithi kutoka kwako mzazi kama hakupata shida yeyote utotoni...kuna watu kulingana na uwezo wao hawawezi hivyo ni bora kuwakazania huku mkijua kwamba uwezekano wa yeye kua kama mnavyotaka nyinyi ni mdogo sana.
watu wenye uwezo mdogo au iq kidogo huwa na dalili hizi
 • kujifunza kuongea na kusema huchukua muda mrefu sana kuliko watoto wengine
 • uwezo wa kukaa, kutembea na kutambaa huchelewa tofauti na wenzake
 • kushindwa kupata marafiki na kua karibu na watu wengine
 • akifanyiwa kipimo cha iq test hupata maksi kidogo sana
 • kuchelewa kujifunza vitu kama kusoma,kuandika na kuhesabu namba
 • kushindwa kua na kumbukumbu nzuri
 • kushindwa kuanganisha matukio na kujua kitu fulani husababisha matatizo fulani.
 • kushindwa kupambana na matatizo yanayohitaji kufikiri.
 • kushindwa kufaulu shuleni
 • kushindwa kufanya shughuli mbalimbali za kila siku kama kuvaa na kwenda mihangaikoni.
 • kutokua mtundu wa kutaka kutatua vitu ambavyo ni tatizo kwake mfano anafeli hesabu lakini hahangaiki kujua jinsi gani afaulu.

matibabu yake ni yapi?
 • hakuna matibabu zaidi ya elimu ambayo hutakiwa kutolewa kwa wazazi au ndugu wa mtoto kwani hakuna dawa ya kutibu tatizo hili.elimu hii hutolewa kulingana na kiwango cha uwezo wa mtoto unavyomuona wewe.
 • kuwafundisha mambo ya kawaida kama kupika, kusafisha na kuosha vitu
 • kuwafundisha jinsi ya kula na kujisaidia chooni wenyewe
 • kuwapeleka kwenye shule ili wajifunze fani za kuaingizia kipato kama kushona cherehani, ujenzi wa nyumba na useremala.
 • kuwahusisha na mazoezi kwani mazoezi huupa ubongo nguvu zaidi.
 • kuwapeleka kwa wataalamu wa kuongea kwa wale ambao hawawezi kuongea kwa wakati. i.e speech therapist
 • kuwapeleka shule na kuwasaidia wale wenye uwezo kidogo ambao wnafundishika.
 • elimu kwa ndugu na jamii ili wasiwatenge watu hawa
 • kuwaelewa na kuwakubali bila kuwalazimisha kufanya vitu ambavyo hawaviwezi.

jinsi ya kuzuia kupata watu au watoto wenye uwezo mdogo sana wa kiakili
 • kama umeshazaa mtoto mwenye uwezo mdogo na mwanamke au mwanaume husika kuna uwezekano wakazaliwa wengine zaidi kama yeye ni bora kutozaa zaidi.
 • kutozaa kabla ya miaka 20 au baada ya miaka 35
 • kupima magonjwa ya hatari kabla ya kubeba mimba mfano ukimwi na kaswende
 • mama apate chanjo zote kipindi cha mimba
 • epuka sigara na pombe kipindi cha ujauzito
 • kula vizuri wakati wa ujauzito yaani mlo kamili wenye virutubusho vyote
 • kuhimiza akina mama kuzalia hospitali
 • kuwakinga watoto na magonjwa mbalimbali ya utoto kama kuharisha, malaria, polio na kadhalika.

mwisho;uwezo wa kiakili wa binadamu au IQ ndio msingi mkuu wa maisha kwamba atakuja kufanya nini au kua nani baadae, leo wazazi wengi wa kiafrika na dunia kwa ujumla huwalazimisha watoto wao kusomea mambo ambayo watoto hao hawayawezi na matokeo yake ni kuharibu pesa inaposhindikana kabisa au kufeli huko mbeleni.
watoto wenye uwezo mkubwa wa kiakili hawahitaji nguvu nyingi ili kusomea mambo magumu, hujikuta wanafaulu tu.
ifike hatua baada ya juhudi kubwa ya kujaribu kufanya mwanao awe mtu fulani kushindikana basi ukubali kwamba haiwezekani na sio kosa lake na umuache afanye anavyoweza, hapa kwetu vipimo vya uwezo wa akili hua havipo mahospitalini lakini nchi za wenzetu vipo.
lakini hata wewe msomaji unaweza kujipima uwezo wako wa kiakili kwa kubonyeza hapa na kujibu maswali kama unajua kingereza, jibu maswali haya ndani ya dakikia 15 kisha bonyeza kupata jibu lako http://www.brainmetrix.com/free-iq-test/

                                                                STAY ALIVE
                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLOND0
                                                    0653095635/0769846183
                                                            

Maoni 1 :