data:post.body Juni 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA MTU ALIYEMEZA VITU VISIVYO KAWAIDA.


watoto wakianza kutambaa na kukua huanza kuweka kila kitu mdomoni na kukila au kukimeza, wazazi wengi wamekua wakikutana na kesi za watoto wao kumeza vitu ambavyo sio vya kawaida kama kumeza chaki,mfuniko wa soda,pini,wadudu,betri au pesa ya shilingi na kadhalika.
kwa watoto kwanzia miezi sita mpaka miaka minne watoto wa kiume humeza sana kuliko watoto wa kike.                                                      
watoto na watu wazima wenye mitimdio wa ubongo hua na hatari sana ya kumeza vitu hivi hivyo ni vizuri sana kuwapa uangalizi wa kutosha.
mara nying vitu vinavyomezwa havina madhara sana kama vinavyoenda kwenye mapafu lakini pia hivo vya kumeza pia huweza kua sumu au kutoboa utumbo na kuleta matatizo.

dalili za kumeza kitu ni zipi?
maumivu ya kifua
kushindwa kula
kutapika
kutoa mate mengi mdomoni
kukohoa
homa kali
kuvimba tumbo
kujisaidia damu
kushindwa kupata choo.

vipimo vinavyofanyika
mgonjwa aliyemeza kitu hufanyiwa kipimo cha x ray kuangalia hicho kitu kimefika wapi ili wajue jinsi ya kukitoa.

matibabu
baadhi ya vitu vilivyomezwa kama havina ncha kali vikifika tumboni huavhwa vituko vyenyewe kwenye choo kubwa lakini vile ambavyo vimekaa kwenye koo la chakula huondolewa na kifaa kinaitwa endoscopy.
mtu akimeza kitu kisichokua cha kawaida ni vizuri afikishwe hospitali kwa uangalizi na matibabu ya haraka.
                                                       STAY ALIVE

HUU NDIO MFUMO WA MAISHA UNAOKUMALIZA NGUVU ZA KIUME

dunia ya sasa ina maisha magumu sana, watu wako bize usiku na mchana wanatafuta ridhiki zao lakini ubize huu na maisha haya usipokua makini yatakuharibia maisha yako ya kijamii, hata kama unapata pesa nyingi kumbuka utajiri sio pesa tu..utajiri ni pamoja na afya yako, mahusiano yako mazuri ya mke wako na familia yako, mahusiano mazuri na majirani, na amani ya roho yako.
utajiri wa kifedha ni bure kabisa kama hauendi bega kwa bega na utajiri wa kiafya, kijamii na amani binafsi...tajiri mkubwa aliyegundua simu za iphone siku anauawa na kansa ya koo kitandani aligundua maisha yake yaliishia kwenye kazi na kusahau familia na ndugu.                                                        
kwa sasa kuna wimbi kubwa la watu ambao wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume, wengi wao matatizo yao yanatatulika kwa kubadili mfumo wa maisha tu na wachache ambao wamejiharibu kwa kujichua na magonjwa mengine ndio wanaweza kuhitaji matibabu ya muda fualani.
katika tafiti zangu nimegundua yafuatayo ni chanzo cha kuishiwa nguvu za kiume, changamoto ambayo imeletwa na mfumo wa maisha..
msongo mkubwa wa mawazo; nguvu za kiume na hamu ya kushiriki tendo hili huanzia kichwani mpaka kwenye uume wa binadamu, watu wenye misongo ya mawazo sababu ya kushindwa kutimiza wajibu wao wa kazi waliopewa kwa wakati, misongo ya mawazo sababu ya majukumu makubwa ya kifamilia ambayo yanakuja na huenda hakuna fedha za kukabiliana na hali hizo, msongo wa mawazo wa biashara zinazoyumba humfanya mwanaume asiweze kushiriki kabisa tendo la ndoa...omba msaada kama kazi zimekuzidi tafuta msaidizi kama umeajiajiri, kama waliokuajiri hawakuelewi tafuta kazi nyingine na uachane na hiyo kazi ya kufanya kazi usiku mpaka usiku lakini pia muda wa kazi ukiisha undoka kwenda nyumbani haraka kwenda nyumbani hakuna sifa ya kufanya kazi masaa mengi wakati mahusiano yako yanakufa.watu wanaofanya kazi benki ni wahanga sana wa matatizo haya.
lakini pia dawa zinazotolewa kutibu msongo wa mawazo huharibu nguvu hizi za kiume pia.
ulevi wa kupindukia; unaweza kua unapenda kunywa pombe angalau kustarehe na kuonana na ndugu na jamaa lakini unywaji wa pombe kupitiliza ni hatari sana, humaliza nguvu za kiume na kukosesha hamu. habari njema ni kwamba pombe kidogo anagalau bia moja mpaka mbili kwa siku ni nzuri kwa nguvu za kiume na afya ya moyo.
dawa mbalimbali; baadhi ya dawa zinzotumika kwa shida mbalimbali au magonjwa mbalimbali zimethibitika kupunguza nguvu za kiume hasa zile zinazomezwa mara kwa mara au kila siku mfano dawa za presha, dawa za maumivu na dawa za msongo wa mawazo.
kumbuka usiache dawa kama una ugonjwa unaohitaji dawa kila siku sababu umesoma hapa, kwa upande mwingine uhai unaweza kua muhimu kuliko nguvu za kiume.
                                                           
kufikiria sana; huwezi kupata nguvu za kiume kama unafikiria mambo mengi yanayokuathiri labda maumivu ya vifo ya wapendwa, maumivu ya kuachishwa kazi, maumivu ya kusalitiwa na mpenzi au kuachwa, na uchovu sana wa shughuli za kila siku. jaribu kurelax, kukubali matokeo, kupata usingizi wa kutosha na kushiriki mazoezi na kumbuka mazoezi yakiwa makali sana humaliza nguvu za kiume.      
                                 
hasira; hasira juu ya mwenzi wako au mtu yeyote aliyekukwaza hufanya ushindwe kushiriki tendo la ndoa, hakikisha unamwambia mpenzi wako mambo yanayokukwaza...kuyaweka moyoni haitakusaidia hata kidogo.
wasiwasi; wanaume wakishapata matukio kadhaa ya kuadhirika na kushindwa kufanya tendo la ndoa huanza kuogopa kukutana tena na mwanamke kwa hofu kwamba wataadhirika tena...tafuta chanzo ni nini na urekibishe, huenda siku hiyo haukua vizuri au ulikua na njaa...kisha jiamini kwamba sasa ntafanikisha.
vitambi na unene; vijana wengi kwanzia miaka 30 mpaka 40 hilo ndio tatizo lao kubwa, yaani kukosa nidhamu ya kupambana na ungezeko la miili yao na matokeo yake uume hua mdogo na nguvu kidogo sana lakini pia ulaji wa vyakula vya haraka kama chips na mikaango mbalimbali wakati wa kazi na kusahau vyakula asilia kama mihogo,karanga, ugali,wali, matunda na mboga za majani...asikudanganye mtu kama umeshindwa kupungua uzito nguvu za kiume utazisikia redioni.
kutojiamini; baadhi ya wanaume hushindwa kujiamini kwa kujikosoa vitu mbalimbali vilivyoko kwenye miili yao ambavyo wakati mwingine hata mwanamke mwenyewe havijali sana mfano kuhisi ana uume mdogo sana wakati uume wake ni wa kawaida, kuhisi hana mwili mzuri na kadhalika.
                                                             
                           
kukosa hamu ya tendo la ndoa; kwa maisha ya sasa hii husababishwa na kuchoka sana na kazi na kukosa muda wa kupumzika, kuna watu wanafanya kazi kila siku ya maisha yao kwa madai wana roho za kichaga...hizo pesa unazotafuta huku unaharibu afya hazitakusaidia kwa lolote hata ukizipata mwisho wa safari na utaibiwa mke na walafi wa mtaani.
                         
magonjwa; haya ni magonjwa mbalimbali ambayo hua hayaponi au huchukua muda sana kupona kwa namna moja au nyingine huharibu nguvu za kiume moja kwa moja mfano kisukari, presha, ajali za migongo na magonjwa ya mishipa ya fahamu, madonda ya tumbo, kifua kikuu, pumu na kadhalika...
                                               
mwisho; unaweza kua unaona aibu kuongea na daktari kuhusu tatizo lako lakini kimya chako hakitakusaidia, jaribu mwenyewe kufikiri chanzo ni nini ili uweze kubadili mfumo wako wa maisha kama kupunguza uzito, kupunguza kazi na kuishi kwa uwezo wako wa kifedha,kuacha kutumia dawa zinazoharibu nguvu zako, kupunguza ulevi na hata kupata matibabu kama ikionekana ni muhimu.

                                                                 STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                          0769846183/0653095635

IFAHAMU HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEPALIWA..

kupaliwa ni nini?
hii ni hali ya kukabwa na kitu kwenye koo ya hewa, inaweza kua chakula kitu chochote ambacho mtu alikua anakichezea mdomoni na hatimaye kikaenda kukwama kwenye koo la hewa.
ripoti ya shirika la afya duniani lilionyesha kwamba zaidi ya watu 162000 walifariki mwaka 2015 sababu ya kupaliwa na kukosa msaada wa haraka, idadi hiyo imetajwa kuongezeka muda unavyozidi kwenda lakini pia kupaliwa kunaweza kua hatari zaidi kwa watoto wadogo kwani anaweza kuweka kitu mdomoni na watu wakashindwa kujua kilichotokea.
mara nyingi watu hupaliwa na chakula, hela ya chuma, karanga, maharage,pini,kucha na kadhalika...                                                    

dalili za kupaliwa ni zipi?
mtu akipaliwa hua na dalili zifuatazo
kushindwa kuongea
kushindwa kupumua kawaida
kushindwa kukohoa
lips za mdomo kubadilika na kua blue sababu ya kukosa hewa
kupoteza fahamu.
                                         
utamsaidia vipi mtu aliyepaliwa?
mtu akipaliwa kama nilivyotaja hapo juu hushindwa kuongea, anaweza kuja kwako mbio bila kusema chochote akawa anakonyesha kwa vitendo tu lakini pia unaweza kua uliona wakati anapaliwa hivyo fanya vifuatavyo..
mpige ngumi au makofi matano mgongoni kwa nguvu lakini usitumie nguvu sana hasa kama ni mtoto, ukiona bado kitu hakijatoka simama nyuma yake kisha weka mikono yako kwenye tumbo la mgonjwa karibu na kifua kama picha inavyoonyesha hapo juu lisha vuta kwa ndani na kuachia mara tano kitaalamu kama heimlich manouver, lakini hii ya kuweka mikono tumboni mtoto awe na zaidi ya mwaka mmoja.
ukiona kitu kilichompalia kimetoka na mgonjwa hapumui mlaze chini kisha kandamiza kifua na kuachia kitaalamu kama cardio pulmonary resuscitation baada ya hapo mgonjwa apelekwe hospitali kuangalia kama kuna madhara yeyote ameyapata.
                                                           
                                                   
mwisho; huduma hiyo ya kumsaidia mgonjwa inatakiwa ifanyike haraka baada ya mgonjwa kukabwa kwani kukosa kwa hewa ndani ya dakika tano huweza kuleta kifo, lakini pia ukipata elimu hii wafundishe jamaa zako na ndugu zako kwani ukipaliwa wewe hutaweza kujisaidia.

                                                      STAY ALIVE 
                                                     

                 

BONYEZA HAPA KUJIPIMA NA KUJIFUNZA KUHUSU IQ AU UWEZO WA AKILI.[INTELIGENT QUOTIENT]

inteligent quotient[IQ] ni nini?
hichi ni kipimo kinachopima uwezo wa mtu kufanya vitu fulani kulingana na umri wake, mfano mtoto mwenye miaka mitano anatakiwa aweze kufanya mambo yanayotakiwa kufanywa na mtoto wa miaka mitano kama kuongea, kusoma kama amefundishwa, kuhesabu namba na kadhalika hiyo tunaita uwezo wa kawaida na unaofaa lakini kama mtoto wa miaka mitano ana uwezo wa kufanya mambo ya mtoto wa miaka miwili au mitatu huyo uwezo wake wa kiakili ni mdogo na kama mtoto huyuhuyu wa miaka mitano anaweza kufanya mambo ya mtoto wa miaka kumi huyu uwezo wake wa akili au IQ ni kubwa sana kitaalamu tunamuita genius.
tafiti mbalimbali zilizofanyika ziligundua nchi ambazo hazijaendelea zina watu wengi sana wenye uwezo mdogo wa kiakili kulingana na sababu mbalimbali ukilinganisha na nchi zilizoendelea ambazo wana uwezo mkubwa zaidi.
                                                       
makundi ya uwezo wa kiakili[1Q]
  IQ YA 130 NA ZAIDI
hawa wana akili sana kitaalamu kama geniuses wana uwezo mkubwa sana wa kuelewa vitu haraka na kugundua jambo ambalo mtu wa kawaida hawezi kulifikiria. mwanasayansi wa karne ya 20 kwa jina la albert einstein alikua na IQ ya 160.

 IQ 120 mpaka 129
hawa ni watu wenye akili, wana uwezo wa kuelewa vitu na kufundishika, kwa nchi zilizoendelea watu hawa wapo wengi.

IQ 110 mpaka 119
hawa wana akili za kawaida zilizozidi kidogo, wanapatikana hata kwenye nchi ambazo hazijaendelea lakini hua ni wachache kwenye kikundi cha watu kadhaa.

IQ 90 mpaka 109 
hawa wana akili za kawaida, wakiweka juhudi kwenye masomo na shughuli zao huweza kufanya kazi vizuri.

IQ 80 mpaka 89 
hawa wana akili za kawaida sana na hutakiwa kuweka juhudi kubwa sana katiaka maisha yao hasa masomo ili waweze kufaulu vizuri bila hivyo ni ngumu sana.

IQ 70 mpaka 79 
hichi ni kiwango cha chini kabisa cha akili ya binadamu, watu hawa wanaongea kawaida lakini juhudi kubwa sana huhitajika kuwafanya waelewe vitu viwe vya darasani au nje ya darasa, wachache sana huweza kufika kiwango kikubwa cha juu cha elimu au kufanya kazi zao vizuri.

IQ 55 mpaka 70
hawa watu wana uwezo wa kuongea na kupata marafiki lakini wakipelekwa shule hawatafeli mitihani.

IQ 40 mpaka 55
watu hawa wanaweza kuongea, wanaweza kujisimamia mambo yao, lakini hawawezi kufaulu shuleni.

IQ 25 mpaka 40
hawa wana uwezo mdogo sana, hufundishwa jinsi ya kufanya mambo kama kuvaa na kujitunza, wanaweza kuongea kidogo sana.

IQ 20 mpaka 25
hawa wanataka uangalizi maisha yao yote, hawawezi kufanya chochote bila kusaidiwa, wana tabia za kujitenga wenyewe na maisha yao yote huishi kwa kutegemea wengine..

kumbuka; makundi yote yana uwezo wa kufanya kazi ngumu lakini hawana uwezo wa kufanya kazi za kutumia akili.
tafiti zimefanyika nchi nyingi duniani ili kujua nchi gani ina watu wenye uwezo mkubwa wa kiakil na nchi za kiafrika zimekua za mwisho kwa kipimo hicho na iq ya watanzania ni 72[average IQ]

chanzo cha IQ ndogo ni nini?
mara nyingi tatizo lolote, ugonjwa wowote au ajari yeyote inayoweza kutokea kabla binadamu hajafikisha miaka 18 huweza kumuharibia uwezo wake wa kua na akili na kumfanya awe na uwezo mdogo sana.sio rahisi mtu kupata hali hii baada ya miaka 18. dalili hizo ni kama ifuatavyo
kabla ya kuzaliwa; mtoto akiwa tumboni huweza kusababishiwa kua na uwezo mdogo wa akili sababu ya magonjwa akiwa tumboni kama kaswende, mama kutopata mlo kamili wenye virutubisho vyote, kunywa pombe na sigara kipindi cha ujauzito, kurithi kwa wazazi yaani kati ya baba au mama anaweza kua na uwezo mdogo darasani na mtoto akarithi, dawa zinazotumika na mama kipindi cha ujauzito na magonjwa ya vinasasaba vya mtoto kama down syndrome.
wakati wa kuzaliwa; siku ya mtoto kuzaliwa, mtoto huweza kukutana na changamoto nyingi sana ambazo zinaweza kumfanya awe na uwezo mdogo sana darasani mfano uchungu kuchukua muda mrefu sana, mtoto kukosa hewa wakati wa kuzaliwa, kupinda kwa kichwa wakati wa kuzaliwa sababu ya njia ndogo na hii inaweza kuchangia kichwa kukaa vibaya.
baada ya kuzaliwa; baada ya kuzaliwa mtoto huweza kupata shida mbalimbali ambazo zinaweza kuharibu uwezo wake kiakili mfano kuugua magonjwa mbalimbali mfano homa ya uti wa mgongo na magonjwa ya mishipa ya fahamu, kuugua na kulazwa kwa muda mrefu sana, kupata ajali ya kuumiza kichwa, mtoto aliyetelekezwa au kufiwa na wazazi, kukosa chakula cha kutosha wakati wa ukuaji na kadhalika.

zipi ni dalili za watu wenye uwezo mdogo wa kiakili?
wazazi wengi wamekua wakali kwa watoto wao ambao wanashindwa kufaulu au kufanya vitu fulani kwenye maisha yao bila kujua kwamba kitaalamu kuna watu hawawezi kufanya vitu fulani yaani sio kila mtoto anaweza kua daktari, injinia, rubani, au kusoma masomo magumu ya sayansi na kuna uwezekano mkubwa akili zake amezirithi kutoka kwako mzazi kama hakupata shida yeyote utotoni...kuna watu kulingana na uwezo wao hawawezi hivyo ni bora kuwakazania huku mkijua kwamba uwezekano wa yeye kua kama mnavyotaka nyinyi ni mdogo sana.
watu wenye uwezo mdogo au iq kidogo huwa na dalili hizi
 • kujifunza kuongea na kusema huchukua muda mrefu sana kuliko watoto wengine
 • uwezo wa kukaa, kutembea na kutambaa huchelewa tofauti na wenzake
 • kushindwa kupata marafiki na kua karibu na watu wengine
 • akifanyiwa kipimo cha iq test hupata maksi kidogo sana
 • kuchelewa kujifunza vitu kama kusoma,kuandika na kuhesabu namba
 • kushindwa kua na kumbukumbu nzuri
 • kushindwa kuanganisha matukio na kujua kitu fulani husababisha matatizo fulani.
 • kushindwa kupambana na matatizo yanayohitaji kufikiri.
 • kushindwa kufaulu shuleni
 • kushindwa kufanya shughuli mbalimbali za kila siku kama kuvaa na kwenda mihangaikoni.
 • kutokua mtundu wa kutaka kutatua vitu ambavyo ni tatizo kwake mfano anafeli hesabu lakini hahangaiki kujua jinsi gani afaulu.

matibabu yake ni yapi?
 • hakuna matibabu zaidi ya elimu ambayo hutakiwa kutolewa kwa wazazi au ndugu wa mtoto kwani hakuna dawa ya kutibu tatizo hili.elimu hii hutolewa kulingana na kiwango cha uwezo wa mtoto unavyomuona wewe.
 • kuwafundisha mambo ya kawaida kama kupika, kusafisha na kuosha vitu
 • kuwafundisha jinsi ya kula na kujisaidia chooni wenyewe
 • kuwapeleka kwenye shule ili wajifunze fani za kuaingizia kipato kama kushona cherehani, ujenzi wa nyumba na useremala.
 • kuwahusisha na mazoezi kwani mazoezi huupa ubongo nguvu zaidi.
 • kuwapeleka kwa wataalamu wa kuongea kwa wale ambao hawawezi kuongea kwa wakati. i.e speech therapist
 • kuwapeleka shule na kuwasaidia wale wenye uwezo kidogo ambao wnafundishika.
 • elimu kwa ndugu na jamii ili wasiwatenge watu hawa
 • kuwaelewa na kuwakubali bila kuwalazimisha kufanya vitu ambavyo hawaviwezi.

jinsi ya kuzuia kupata watu au watoto wenye uwezo mdogo sana wa kiakili
 • kama umeshazaa mtoto mwenye uwezo mdogo na mwanamke au mwanaume husika kuna uwezekano wakazaliwa wengine zaidi kama yeye ni bora kutozaa zaidi.
 • kutozaa kabla ya miaka 20 au baada ya miaka 35
 • kupima magonjwa ya hatari kabla ya kubeba mimba mfano ukimwi na kaswende
 • mama apate chanjo zote kipindi cha mimba
 • epuka sigara na pombe kipindi cha ujauzito
 • kula vizuri wakati wa ujauzito yaani mlo kamili wenye virutubusho vyote
 • kuhimiza akina mama kuzalia hospitali
 • kuwakinga watoto na magonjwa mbalimbali ya utoto kama kuharisha, malaria, polio na kadhalika.

mwisho;uwezo wa kiakili wa binadamu au IQ ndio msingi mkuu wa maisha kwamba atakuja kufanya nini au kua nani baadae, leo wazazi wengi wa kiafrika na dunia kwa ujumla huwalazimisha watoto wao kusomea mambo ambayo watoto hao hawayawezi na matokeo yake ni kuharibu pesa inaposhindikana kabisa au kufeli huko mbeleni.
watoto wenye uwezo mkubwa wa kiakili hawahitaji nguvu nyingi ili kusomea mambo magumu, hujikuta wanafaulu tu.
ifike hatua baada ya juhudi kubwa ya kujaribu kufanya mwanao awe mtu fulani kushindikana basi ukubali kwamba haiwezekani na sio kosa lake na umuache afanye anavyoweza, hapa kwetu vipimo vya uwezo wa akili hua havipo mahospitalini lakini nchi za wenzetu vipo.
lakini hata wewe msomaji unaweza kujipima uwezo wako wa kiakili kwa kubonyeza hapa na kujibu maswali kama unajua kingereza, jibu maswali haya ndani ya dakikia 15 kisha bonyeza kupata jibu lako http://www.brainmetrix.com/free-iq-test/

                                                                STAY ALIVE
                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLOND0
                                                    0653095635/0769846183
                                                            

UFAHAMU UGONJWA WA FISTULA NA MATIBABU YAKE.

fistula ni nini?
kitaalamu ni tundu ambalo silo la kawaida linaloonganisha viungo viwili vya binadamu, kwa kawaida viungo vya binadamu havina matundu lakini matundu haya yanapotokea huitwa fistula, mfano tundu kati ya koo la hewa na chakula, tundu kati ya uke na njia ya choo, tundu kati ya njia ya uke na mkojo.
fistula ya uzazi hutokea pale panapokua na tundu kati ya njia ya choo kubwa, choo ndogo na uke au njia ya uzazi...hali hii husababisha kinyesi na mkojo kupita sehemu za siri.


fistula husababishwa na nini?
kwa nchi zilizoendelea kama marekani, fistula husababishwa na kutumia vifaa vya kuzalisha pale mama anaposhindwa kusukuma kwa njia ya kawaida yaani mpka asaidiwe kitaalamu kama forceps au vacuum delivery lakini kwa nchi ambazo hazijaendelea kama tanzania fistula husababishwa na uchungu wa muda mrefu ambapo mtoto anakandamiza kibofu cha mama au utumbo mkubwa na kusababisha damu kushindwa kufika eneo hilo na kuoza au kuchanika, hali hii ndio huleta tundu hilo la fistula.
sababu zingine ni kuvunjika kwa mifupa ya mapaja, saratani mbalimbali za uzazi,kubakwa,kutoa mimba au makosa wakati wa upasuaji wa kizazi, mionzi ya matibabu ya kansa, magonjwa ya zinaa kama kaswende, ugonjwa wa kichocho

dalili za fistula ni zipi?
kutokwa na mkojo au choo kubwa sehemu za siri hasa wakati wa usiku bila kujitambua au kushindwa kuzuia.
harufu kali sehemu za siri
kuugua ugonjwa wa njia ya mkojo mara kwa mara maarufu kama uti
maumivu makali ya uke na sehemu zinazozunguka
maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
msongo wa mawazo
kukosa siku za mwezi
kuharibika kwa mimba zijazo
ugonjwa wa ngozi sababu ya mkojo kumwagikia ngozi

vipimo gani hufanyika kugundua fistula?
kipimo cha picha ya utrasound hutumika sana kuangalia kama kuna tundu ambalo sio la kawaida limetokea kwenye sehemu hizo za siri.

matibabu ya fistula.
fistula ikigundulika mapema huweza kutibiwa kwa kuingiza mpira wa mkojo kitaalamu kama catheter na kuuacha hapo mpka tundu lile litakapoziba, mpira huweza kubadilishwa kulingana na na muda mgonjwa atakaotibiwa, dawa za kuua bacteria hutolewa na mgonjwa huwekewa drip za maji mengi ili kuongeza damu katika eneo husika kitu ambacho husaidia kupona haraka.
matibabu yakichelewa mgonjwa hutakiwa kufanyiwa opasuaji na daktari bingwa ili kushona tundu hilo, kwa hapa tanzania upasuaji huo ni bure kabisa katika hospitali ya CCBRT dar es laam.

madhara ya fistula ni yapi?
kibovu cha mkojo kuondoka sehemu yake
kupata ugonjwa wa njia ya mkojo mara kwa mara
ugumba
kuishiwa damu
sehemu za uke wa mwanamke kuharibika
kuvunjika kwa ndoa
kutengwa na jamii
kujiua kwa wahanga wa tatizo hili.

jinsi gani tunaweza kuzui fistula kwenye jamii zetu?
kuzuia wasichana wadogo kuzaa
hakikisha mama hakai na uchungu zaidi ya masaa 12 baada ya uchungu kuanza
hakikisha mama anazalia hospitali ili asaidiwe vizuri
kuweka miondominu mizuri kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa.

                                                STAY ALIVE

                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                     0653095635/0769846183


ZIFAHAMU FAIDA 10 ZA PILIPILI MWILINI.

                                                               
                                                                              
mara nyingi pilipili hutumika kuongeza ladha ya chakula kwenye jamii mbalimbali, watu wengi huitumia kama kiburudisho tu bila kujua kwamba pilipili hizi zina faida nyingi sana...zipo pilipili za kuwasha kama pilipili mbuzi na pilipili kichaa lakini pia zipo ambazo haziwashi kama pilipili hoho, hivyo kama wewe ni muoga wa pilipili za kuwasha basi kula hata pilipili hoho ili ufaidike na faida nyingi sana zinazopatikana kwenye vyakula hivyo.zifuatazo na faida muhimu zinazopatikana kwenye pilipili.
kiasi kikubwa cha vitamin c; utafiti umeonyesha kwamba pilipili zina kiasi kikubwa cha vitamin c kuliko hata kile kinachopatikana kwenye matunda kama machungwa na machenza, vitamin c ni nzuri kwa kinga ya mwili, na kulainisha ngozi.
husaidia kupunguza uzito; pilipili huongeza kasi ya mwili kufanya kazi na kuchoma mafuta[metabolism], kemikali ya piperin iliyoko kwenye pilipili huzuia mwili kutengeneza mafuta mapya, lakini pia zenyewe zikiwa na ujazo mdogo wa ndani kiasi kwamba hata ule nyingi kiasi gani haziwezi kukuongeza uzito, kumbuka pilipili unazowezakula nyingi ni zile ambazo haziwashi.
huzuia magonjwa yasiambukizwa; kemikali ya capsaicin inayopatikana kwenye pilipili hupunguza  lehemu mwilini au cholestrol, husaidia kupunguza sukari kwa wagonjwa wa kisukari na kupunguza maumivu ya mwili.
huzuia kansa mbalimbali; kiasi cha sulfur kinachopatikana kwenye pilipili kimethibitika kua vizuri sana katika mchakato wa kuzuia kansa za mbalimbali za mwili.
hukinga mishipa ya fahamu; pilipili za aina mbalimbali hua na vitamin b6 ambayo ni muhimu sana katika afya ya mishipa ya fahamu, ukosefu wa vitamin hii ni moja ya vyanzo vikuu vya kupata ngazi mwilini na kuhisi dalili za kuwaka moto.
hutunza macho; lutein ni enzyme inayopatikana kwenye pilipili, katika umri mkubwa wa maisha hufanya kazi ya kuzuia kutokea kwa mtoto wa jicho[cataract],huu ni weupe unaotokea kwenye lens ya jicho na kumfanya mtu apate upofu.
hupunguza kasi ya uzee; kiasi kikubwa cha vitamin e kilichopo kwenye pilipili hulainisha ngozi sana na kumfanya mtumiaji kuonekana kijana na mwenye nguvu hata katika umri mkubwa wa maisha.
huongeza virutubisho mwilini; ikipikwa na moto kidogo bila kuiva sana, pilipili ina virutubisho vingi muhimu kwa ajili ya afya ya binadamu.
hutibu mafua; mgonjwa mwenye mafua yaliyoziba kabisa akila pilipili kamasi zote zilizoganda hugeuka na kua laini sana na kumpa nafuu ya upumuaji.
husaidia mmeng'enyo wa chakula; pilipili husaida mwili kutengeneza kiasi kikubwa cha kemikali ya hydrochloric acid inayopatikana tumboni ambayo kazi yake ni kuongeza mmeng'enyo wa chakula hivyo kuupa mwili virutubisho vyote muhimu.
 
                                                           STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183
                                          UFAHAMU UGONJWA WA KANSA YA DAMU NA MATIBABU YAKE.[LEUKEMIA]

                                                                         


kansa ya damu ni nini?
kansa ya damu ni hali ambayo mwili unatengeneza seli nyingi sana nyeupe za damu kuliko kiwango ambacho kinatakiwa mwilini, seli huzi hutengenezwa na uvimbe kitaalamu kama tumour ambao unakua ndani ya mifupa ya kutengeneza damu.[bone marrow]
kuna aina mbili za kansa ya damu kama ifuatavyo
acute leukemia; hii ni aina ya kansa ya damu ambayo seli nyingi nyeupe za damu ambazo hazijakomaa hutengenezwa ndani ya mifupa[bone marrows], seli hizi hua nyingi sana na kuzuia mifupa kutengeneza seli zingine za kawaida.
mara nyingi kansa ya aina hii huwapata watoto wadogo, japokua wakubwa pia wanaweza kupata na matibabu ya haraka hutakiwa kuanza, pamoja na teknolojia ya matibabu mgonjwa mara nyingi hufariki ndani ya miezi sita.
chronic leukemia: hii ni aina ya pili ya kansa ambayo inatokea pale mifupa[bone marrows] inapotengeneza seli nyingi nyeupe ambazo zimekomaa, aina hii ya kansa huchukua miezi au miaka kusambaa mwilini na matibabu yake hucheleweshwa mpaka mgonjwa atakapoonekana anafaa kuanza matibabu.mara nyingi haina hii huwapata vijana na wazee lakini huweza kutokea kwenye umri wowote.

nini chanzo cha kansa ya damu?
mara nyingi vyanzo halisi vya kansa ya damu hua havifahamiki lakini kuna mambo ambayo yanaweza kuchangia kuanza kwa kansa hii kama ifuatavyo..

 • kupigwa na mionzi; hii inaweza kua mionzi ya jua au x ray za hospitali, mionzi hii huharibu uwezo wa mwili kuamua kwamba seli zitengenezwe nyingi au kidogo matokeo yake kansa huanza.
 • dawa zinazofanya kazi kwenye seli; mfano dawa zingine za kutibu kansa mbalimbali huweza kuleta kansa ya damu...mfano methotroxate
 • kuguswa au kuvuta hewa yakemikali ya benzene; hii ni kemikali inayopatikana sana viwandani, watu wanaofanya kazi huko hua wanakua na hatari ya kuguswa nayo mwilini lakini pia hupatikana kwa wingi kwenye sigara na kidogo kwenye mafuta tunayotumia kwenye gari, mifuko ya plastiki, gundi na rangi za kupaka mbao za viti na makabati. 
 • kushambuliwa na virusi; baadhi ya virusi huweza kushambulia mwili na kusababisha kansa mfano htlv 1 viruses
 • kuishiwa na kinga ya mwili; mara nyingi mtu akiwa mzima seli za kansa huonekana ndani ya miili yetu lakini kinga ya mwili hupambana na kua kansa hizo, kinga ikishuka uwezo wa mwili kupambana na kansa hizo huondoka na mgonjwa huugua kansa.
 • kurithi; baadhi ya koo zina vimelea ambavyo hurithishwa kutoka wazazi kwenda kwa watoto, aina za kansa za kurthi ni mbaya sana kwani huweza kumaliza ukoo mzima.
 • matumizi ya kemikali za mbolea na kuulia wadudu shambani kitaalamu kama organophosphate.


dalili za acute leukemia
kuishiwa damu
homa
kutokwa na damu sehemu mbalimbali kama puani,mdomoni,choo kubwa, machoni na matundu yote ya mwili.
mifupa na jointi kuuma
kuvimba maini
kuvimba bandama
kuugua mara kwa mara
mara nyingi seli za kansa zikifika kichwani mgonjwa huanza kuumwa kichwa, kupata kizunguzungu, kichefuchefu na kutapika.

dalili za chronic leukemia
kuchoka sana
kupungua uzito
kushindwa kupumua
maumivu ya tumbo
kutokwa jasho usiku
homa na moyo kukimbia
kuvimba kwa tezi, maini na bandama
kuishiwa damu
kinga ya mwili kushuka

vipimo ambavyo hufanyika kugundua ugonjwa huu
full blood picture; hiki ni kipimo ambacho huchukuliwa kuangalia vitu mbali mbali vya damu ikiwemo kiasi cha damu na kuongezeka kwa seli nyeupe za damu
bone marrow aspirate; kipimo hiki hufanyika kwa kuvuta seli zilizoko ndani ya mfupa kwa kutumia sindano kisha kwenda kuzipima kuangalia kama zina seli za kansa.
vipimo vingine huchukuliwa ili kuangalia kama kansa zimeshasambaa sehemu mbalimbali za mwili kama x ray ya kifua, ct scan ya kichwa na tumbo,mri ya ubongo, nyama kidogo hukatwa kwenye tezi kuangalia kama kansa imefika huko.

matibabu ya kansa ya damu
kansa hutibiwa kulingana na aina ya kansa mtu aliyonayo kama ifuatavyo...
matibabu ya acute leukemia
dawa mbalimbali hutolewa kutibu kansa hii ya damu japokua hulenga kwenye kusogeza muda tu kwani uwezekano wa kupona hua ni mdogo sana, dawa hizi za kumeza kutibu kansa kitaalamu huita chemotherapy... lakini ugonjwa huu ukigunduliwa mapema mtu huweza kupona kabisa, baada ya matibabu mgonjwa akikaa miaka mitano bila dalili zozote huhesabika amepona. dawa zinazotolewa ni kama predinisolone,vincristine,etoposide,cytarabine, and methotroxate.
kama nilivyosema mwanzo wagonjwa wa aina hii ya kansa mara nyingi hufariki ndani ya miezi sita sababu ya ukali wa aina hii ya kansa.
matibabu ya chronic leukemia
matibabu ya aina hii ya kansa hujumuisha mionzi yaani radiotherapy na dawa yaani chemotherapy, mgonjwa haanzishiwi matibabu hapo hapo mpaka vipimo vitakapoonyesha kwamba yuko tayari kwa matibabu
matumizi ya virutubisho; mara nyingi matibabu ya kansa yana madhara makubwa sana mwilini kutumia virutubisho vyenye vitamini mbalimbali huweza kumsaidia mgonjwa kupata nafuu au kupona haraka na kutopata madhara mengi, virutubisho hivyo ni vile vyenye mchanganyiko wa wa vitamin nyingi ambazo kwa kawaida huzuia kansa mfano vitamin c, vitamin e, vitamin a na kadhalika, chagua virutubisho vyovyote vya kampuni inayouza japokua baadhi ya kampuni kama forever living wana virutubisho bora zaidi ambavyo kuna watu wenye kansa hizi sehemu mbalimbali duniani wametoa ushahidi wa kupata nafuu kupitia bidhaa zao. virutubisho hivi ni muhimu sana kwa wagonjwa hawa kwani uwezo wao wa kula ni mdogo na hata wakila vyakula vyetu vingi vya kiafrika havina mchanganyiko wa mlo kamili..pichani ni dada aliyefanikiwa kwa kutumia bidhaa zao huko asia wakati anaumwa kansa ya damu.

mwisho;wagonjwa wachache sana huweza kupona kabisa ugonjwa wa kansa ya damu lakini pamoja na kupona ugonjwa huu huweza kurudi baada ya muda fulani, pamoja na teknolojia tuliyonayo kansa ya damu bado ni changamoto kubwa sana na moja ya vyanzo vya vifo vingi duniani.tembelea blog yetu ya kingereza hapa http://www.vibesinc.ga/

                                                       STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                         0653095635/0769846183[TUMA MESEJI TAFADHALI]