data:post.body YAFAHAMU MADHARA YA UPASUAJI WA KUTOA MTOTO[ C SECTION] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

YAFAHAMU MADHARA YA UPASUAJI WA KUTOA MTOTO[ C SECTION]

                                                               
upasuaji wa kutoa mtoto kitaalamu kama cesarian section ni moja ya aina za upasuaji kubwa zinazofanyika sana nchini tanzania, mara nyingi upasuaji huu hufanyika baada ya mama kushindwa kabisa kuzaa kwa njia ya kawaida lakini siku hizi wanawake pia huamua tu kuzaa kwa upasuaji hata kabla ya uchungu haujaanza.
sina shida na wanawake ambao wameshindwa kusukuma mtoto kwani hao hawakua na namna lakini kwa wanawake ambao huamua kupasuliwa tu hata kabla ya uchungu haujaanza sababu ya uwezo wao wa kifedha basi nina habari mbaya kwenu sababu upasuaji ule una madhara makubwa sana ambayo kama una uwezo wa kuzaa kawaida basi achana na njia hiyo ya upasuaji.
yafuatayo ni madhara ambayo huambatana na upasuaji wa kutoa mtoto
vifo vya ghafla; upasuaji husababisha kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu, damu hizo zilizoganda huweza kusafiri mpaka kwenye mapafu na kuzuia hewa, hali hii ni moja ya chanzo kikuu cha vifo vya ghafla vya wamama waliotoka kujifungua, mazoezi ya kutembea baada ya upasuji hupunguza hatari ya damu hizi kuganda japokua sio kwa asilimia 100.
kutokwa na damu nyingi sana; mara nyingi upasuaji huu humfanya mama anapoteza damu nyingi sana ukilinganisha na yule ambaye amezaa kwa njia ya kawaida, upotevu huu mkubwa wa damu unaweza kusababisha kushindwa kwa moyo kufanya kazi na hata kama isipotokea basi itakuchukua muda mrefu sana kwa mwili kuipata ile damu tena.
kuoza kwa vidonda vya upasuaji; baada ya upasuaji kidonda kikubwa hubaki na hutakiwa kuhudumiwa mpaka kitakapofunga, wakati mwingine kidonda hushambuliwa na bacteria na kuoza au huweza kuachia na kuhitaji kushonwa tena, hali hii huambatana na homa kali na huweza kusababisha kifo cha mama.
ajali kwenye chumba cha upasuaji; mara nyingi ajali hizi hutokea kwa wamama ambao wamefanyiwa upasuaji mara nyingi, viungo ambavyo havihusiki kama kibofu cha mkojo, huweza kukatwa bahati mbaya na kusababisha taharuki kubwa zaidi kwani madaktari wanaohusika na kushona kibofu cha mkojo wanaweza wasipatikane hasa kwenye hospitali za wilaya.
madhahara ya dawa za usingizi; dawa za usingizi hua na madhara mengi ikiwepo kupata aleji ya dawa, kuchelewa kuamka au kupata maumivu makali sana ya kichwa baada ya kuamka. madhara haya yanaweza kua ya kawaida au kua makali zaidi kulingana na mgonjwa.
matatizo ya mimba zijazo; kimsingi mwanamke aliyepasuliwa anatakiwa akae angalau miaka mitatu kabla ya kubeba mimba nyingine ili kutoa nafasi kwa kizazi kupona vizuri lakini hata akikaa muda huo kujaribu kuzaa kwa njia ya kawaida ni hatari sana na huweza kupasua kizazi, kitaalamu ni vizuri kupasuliwa sio zaidi ya mara tatu na ukiendelea unaweza kupata matatizo makubwa zaidi ikiwemo ukilema wa maisha au kifo, baadhi ya hospitali hukata mirija ya uzazi wakikupasua mara ya tatu au ya nne.
kuugua kwa kizazi; ukuta wa ndani kabisa wa kizazi huweza kushambuliwa na bacteria na kusababisha homa kali, kuharibika kwa kizazi na kutokwa na harufu kali sana sehemu za siri, hali isipotibiwa vizuri huleta ugumba.
kuumia kwa mtoto; wakati mwingine mtoto aliyoko tumboni huweza kuchanwa kidogo na kisu wakati wa kuzikata zile kuta za uzazi ili kumfikia mtoto.
matatizo ya mfumo wa hewa kwa mtoto; watoto wengi wanaozaliwa kwa upasuaji hupata shida sana ya kupumua kwa siku za mwanzo, hali hii huweza kuharibu vitu muhimu kama ubongo na figo lakini pia upasuaji kabla ya wiki 39 ya ujauzito bila kua na ushahidi kama mapafu yamekomaa huweza kusababisha ugonjwa wa kushindwa kupumua kitaalamu kama respiratory distress syndrome.
makovu makubwa; hii hutegemea na aina ya mshono uatakaopata lakini baadhi ya mishono huleta makovu makubwa sana tumboni hasa unavyozidi kupasuliwa mara nyingi na hata ile aina ya mishono ambayo hukatwa chini ya kitovu huacha makovu pia japokua sio makubwa sana kama yale ya kukata juu ya kitovu.
                                                           STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     0653095635/0769846183
                                                           

0 maoni:

Chapisha Maoni