data:post.body Mei 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HATIMAYE DAWA YA UKIMWI IMEGUNDULIWA ISRAEL...

                                                               
                       
wagonjwa wa ukimwi duniani kote muda sio mrefu watapata matumaini mapya baada ya dawa ya ukimwi kwa jina la gammora kugunduliwa huko israel katika chuo kikuu cha hebrew ambacho kiko ndani ya mji wa jerusalem, dawa hii kwa sasa imehamishiwa katika kituo cha afya cha kaplan huko rehovot kwa kufanyia majaribio ya mwisho.
ugonjwa huu mpaka sasa umeua watu zaidi ya milion 35 tangu ulipogunduliwa zaidi ya mika 40 iliyopita, watafiti wamekua wakihangaika kutafuta dawa na chanjo ya ukimwi bila mafanikio, chanjo ya mwisho iliwakatisha tamaa kabisa wanasayansi baada ya kushindwa katika hatua ya tatu ya majaribio.

majaribio ya dawa
damu ya mgonjwa mwenye virusi vya ukimwi iliwekwa kwenye chupa ya maabara kwa jina la test tube na kisha dawa ya gammora ilimiminwa huko, baada ya siku 8 asilimia tisini na saba{97%] ya virusi vya ukimwi kwenye ile damu vilikua vimekufa.
huu ni ugunduzi mkubwa kuwahi kutokea kwani hakuna dawa imeshawahi kuua virusi vingi kiasi hicho ndani ya muda mfupi.

dawa inafanyaje kazi?
dawa hii ni protini ndogo sana ambazo zinalazimisha virusi vingi vya ukimwi kwenye damu kuingia ndani ya seli moja ya damu kisha seli hiyo huzidiwa nguvu na kujiua, dawa hii imegunduliwa na aabraham loyter na assaf friedler katika chuo kikuu cha hebrew.
kwa sasa hivi wagonjwa wa ukimwi wanatibiwa na dawa ambazo wanatakiwa kuzimeza kila siku kwa maisha yao yote, dawa hizi zimeshindwa kuua virusi vyote ndani ya mwili lakini pia zina changamoto ya madhara mbalimbali kwenye mwili wa binadamu kama kuharibu maini, kuharibu figo, kuharibu mishipa ya fahamu, kuleta shepu ya mwili ambayo sio ya kawaida na wakati mwingine kuzidiwa nguvu na virusi.
baadhi ya dawa za arv zimekua zikiondolewa sokoni baada ya kuonyesha madhara makubwa zaidi.
mgunduzi huyo alinukuliwa akisema "dawa yetu inaoa virusi kabisa sio kupunguza makali tu na hakuna jinsi virusi hivyo vitaishi tena"

mamlaka za israel zinasemaje?
waziri wa afya wa israel amesema muda sio mrefu wataanza kuzigawa dawa hizi kwa watu wenye hatari kubwa zaidi ya kupata virusi vya ukimwi kama wanajiuza miili yao, madaktari wanaopasua wagonjwa wa ukimwi, mashoga na kadhalika kwani dawa hii ikimezwa mara kwa mara huweza kuzuia ukimwi kabisa kama chanjo.

dawa itafikia vipi watu wote duniani
majaribio ya mwisho yakiwa tayari shirika la afya duniani yaani WHO ndio ina mamlaka rasmi ya kuitangazia dunia kwamba ukimwi kwa sasa unatibika rasmi na utaratibu wa kusambaza dawa utafuatwa.
mpaka sasa hivi ni mtu mmoja tu ndio amewahi kupona ugonjwa wa ukimwi baada ya kufanyiwa upasuaji ambao ulikua una lengo la kutibu kansa yake.
mgonjwa huyo kwa jina la timothy brown aliugua ukimwi tangu mwaka 2007 na baadae aliugua kansa iliyomfanya awekewe vimelea vipya vya kutengeneza damu kutoka kwa mtu ambaye damu yake haikubali kuambukizwa ukimwi.

je wagonjwa wa ukimwi wafanyenini?
kila ugonjwa utakuja kupata dawa yake siku za usoni kwasababu kila siku wataalamu hawalali wanatafuta dawa ya ukimwi, kikubwa kwa sasa ni kutokata tamaa ila kuendelea kumeza dawa zilizopo ili siku dawa hizo zikitoka zikukute ukiwa hai.
zamani sana hata kabla yesu hajazaliwa, ugonjwa wa ukoma ulikua tishio na uliua watu wengi sana na kwa miaka yote hiyo dawa yake haikupatikana lakini mpka kufikia karne ya 20 ukoma ulipotea kabisa duniani na sasa sio tishio tena kwani dawa za kutibu ukoma zipo kila nchi.tembelea blog yetu ya kiswahili hapa /http://www.vibesinc.ga/

                                                        STAY ALIVE

                                   DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                               0653095635/0769846183[tuma meseji tafadhali]

YAFAHAMU MADHARA YA UPASUAJI WA KUTOA MTOTO[ C SECTION]

                                                               
upasuaji wa kutoa mtoto kitaalamu kama cesarian section ni moja ya aina za upasuaji kubwa zinazofanyika sana nchini tanzania, mara nyingi upasuaji huu hufanyika baada ya mama kushindwa kabisa kuzaa kwa njia ya kawaida lakini siku hizi wanawake pia huamua tu kuzaa kwa upasuaji hata kabla ya uchungu haujaanza.
sina shida na wanawake ambao wameshindwa kusukuma mtoto kwani hao hawakua na namna lakini kwa wanawake ambao huamua kupasuliwa tu hata kabla ya uchungu haujaanza sababu ya uwezo wao wa kifedha basi nina habari mbaya kwenu sababu upasuaji ule una madhara makubwa sana ambayo kama una uwezo wa kuzaa kawaida basi achana na njia hiyo ya upasuaji.
yafuatayo ni madhara ambayo huambatana na upasuaji wa kutoa mtoto
vifo vya ghafla; upasuaji husababisha kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu, damu hizo zilizoganda huweza kusafiri mpaka kwenye mapafu na kuzuia hewa, hali hii ni moja ya chanzo kikuu cha vifo vya ghafla vya wamama waliotoka kujifungua, mazoezi ya kutembea baada ya upasuji hupunguza hatari ya damu hizi kuganda japokua sio kwa asilimia 100.
kutokwa na damu nyingi sana; mara nyingi upasuaji huu humfanya mama anapoteza damu nyingi sana ukilinganisha na yule ambaye amezaa kwa njia ya kawaida, upotevu huu mkubwa wa damu unaweza kusababisha kushindwa kwa moyo kufanya kazi na hata kama isipotokea basi itakuchukua muda mrefu sana kwa mwili kuipata ile damu tena.
kuoza kwa vidonda vya upasuaji; baada ya upasuaji kidonda kikubwa hubaki na hutakiwa kuhudumiwa mpaka kitakapofunga, wakati mwingine kidonda hushambuliwa na bacteria na kuoza au huweza kuachia na kuhitaji kushonwa tena, hali hii huambatana na homa kali na huweza kusababisha kifo cha mama.
ajali kwenye chumba cha upasuaji; mara nyingi ajali hizi hutokea kwa wamama ambao wamefanyiwa upasuaji mara nyingi, viungo ambavyo havihusiki kama kibofu cha mkojo, huweza kukatwa bahati mbaya na kusababisha taharuki kubwa zaidi kwani madaktari wanaohusika na kushona kibofu cha mkojo wanaweza wasipatikane hasa kwenye hospitali za wilaya.
madhahara ya dawa za usingizi; dawa za usingizi hua na madhara mengi ikiwepo kupata aleji ya dawa, kuchelewa kuamka au kupata maumivu makali sana ya kichwa baada ya kuamka. madhara haya yanaweza kua ya kawaida au kua makali zaidi kulingana na mgonjwa.
matatizo ya mimba zijazo; kimsingi mwanamke aliyepasuliwa anatakiwa akae angalau miaka mitatu kabla ya kubeba mimba nyingine ili kutoa nafasi kwa kizazi kupona vizuri lakini hata akikaa muda huo kujaribu kuzaa kwa njia ya kawaida ni hatari sana na huweza kupasua kizazi, kitaalamu ni vizuri kupasuliwa sio zaidi ya mara tatu na ukiendelea unaweza kupata matatizo makubwa zaidi ikiwemo ukilema wa maisha au kifo, baadhi ya hospitali hukata mirija ya uzazi wakikupasua mara ya tatu au ya nne.
kuugua kwa kizazi; ukuta wa ndani kabisa wa kizazi huweza kushambuliwa na bacteria na kusababisha homa kali, kuharibika kwa kizazi na kutokwa na harufu kali sana sehemu za siri, hali isipotibiwa vizuri huleta ugumba.
kuumia kwa mtoto; wakati mwingine mtoto aliyoko tumboni huweza kuchanwa kidogo na kisu wakati wa kuzikata zile kuta za uzazi ili kumfikia mtoto.
matatizo ya mfumo wa hewa kwa mtoto; watoto wengi wanaozaliwa kwa upasuaji hupata shida sana ya kupumua kwa siku za mwanzo, hali hii huweza kuharibu vitu muhimu kama ubongo na figo lakini pia upasuaji kabla ya wiki 39 ya ujauzito bila kua na ushahidi kama mapafu yamekomaa huweza kusababisha ugonjwa wa kushindwa kupumua kitaalamu kama respiratory distress syndrome.
makovu makubwa; hii hutegemea na aina ya mshono uatakaopata lakini baadhi ya mishono huleta makovu makubwa sana tumboni hasa unavyozidi kupasuliwa mara nyingi na hata ile aina ya mishono ambayo hukatwa chini ya kitovu huacha makovu pia japokua sio makubwa sana kama yale ya kukata juu ya kitovu.
                                                           STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     0653095635/0769846183
                                                           

NJIA 10 ZA KUJITIBU UCHOVU WA POMBE[HANGOVER]

                                                                     
hangover ni nini?
hii ni hali ya kujisikia vibaya inayowapata watu watu ambao wanakua wamekunywa pombe nyingi jana yake, dalili zake ni kuuma kichwa sana, kutapika, kuishiwa nguvu, kujisikia uvivu sana na kushindwa kufanya kazi.
hali hii huvumilika mara nyingi lakini wakati mwingine hali hua mbaya kiasi kwamba mtu huweza kulazwa hospitali kwa matibabu zaidi.
sasa wewe kama mywaji wa pombe ni vizuri ukazifahamu njia ambazo unaweza kuzitumia kutibu hangover kabla au baada kunywa pombe kama ifuatavyo.
kunywa maji mengi;maji ni matibabu makuu ya hangover kabla na baada ya kunywa pombe, kawaida pombe humfanya mtu akojoe sana na kupoteza maji mengi mwilini na hii ndio moja ya sababu kuu ya kupata hangover sasa kitaalamu ili kuzuia hangover unatakiwa unywe chupa moja ya pombe na glass moja ya maji kila wakati na ikitokea hukufanya hivo na umeamka asubuhi una hangover basi jitahidi unywa hata lita tatu mpaka nne siku hiyo.[angalizo;usinywe maji yote kwa pamoja, weka kwenye chupa unywe taratibu]
kula chakula chenye mafuta mengi kabla ya pombe; chakula kama nyama, samaki, kuku, sambusa na vingine hua na mafuta mengi...pombe ikikuta mafuta tumboni inapata tabu kufanya kazi haraka kuliko ikikuta tumbo halina kitu, hii huzuia hangover za kesho yake lakini ukishakunywa haikusaidii tena.
kunywa kahawa; kawaha kitaalamu inaitwa stimulant, hii ni nzuri kwako ambaye umeamka na hangover lakini una kazi za kufanya siku hiyo zinazohitaji umakini mkubwa hivyo kahawa itakuondolea uchovu na kukufanya uwe makini lakini kunywa na maji pia kwani kahawa hufanya mtu akojoe sana kama pombe.
meza dawa za maumivu; maumivu ya kichwa yakiwa makali kuna dawa unaruhusiwa kumeza kupunguza maumivu hayo mfano diclofenac, aspirin, ibuprofen...usinywe paracetamol au dawa yeyote yenye mchanganyiko wa paracetamol kwani ikiungana na pombe inaharibu maini
                                                             
fanya mazoezi; kama kichwa hakiumi sana fanya mazoezi yeyote kwani hii itakusaidia kupunguza pombe mwilini, na kukuletea mood ya kufanya vitu kwani ubongo hutengeneza homoni ya furaha yaani endorphine wakati wa mazoezi.
epuka kuzimua na pombe; huu msemo hutumika na walevi kwamba anaamka na pombe ili kuondoa pombe, hapana hii haifai kabisa kwani inaweza kukuletea ganzi mwilini na kukufanya uwe mtegemezi wa pombe kwenye maisha yako yaani bila kunywa pombe huwezi kufanya chochote.
                                                 
ongeza sukari mwilini;pombe hupunguza sana sukari mwilini na hii ni kwasababu maini
yanashindwa kutengeneza sukari ya ziada na kua bize kuondoa pombe mwilini hivyo unaweza kunywa juisi, soda au kula chakula. juice ni nzuri zaidi kwani hurudisha na madini yaliyopotea mwilini.
kunywa tangawizi na maji ya moto; chukua tangawizi isage kisha ichemshe na maji ya moto, hii itakuondolea kichechefu na kukuletea hamu ya kula.
rudi kulala; mara nyingi pombe huharibu mfumo wa usingizi hivyo mtu anaweza asipate usingizi wa kutosha kwa kushtuka ovyo usingizini, lala mpaka utakapoona usingizi umeisha ndio uanze shughuli zingine.
jiuepushe na mwanga mkali na sauti kubwa za kelele; mtu akiwa katika hali hii hawezi kuvumilia mwanga mkali na sauti kubwa hivyo kaa mbali navyo kupata nafuu.
                                                       



STAY ALIVE

DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183