data:post.body Aprili 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

MAMBO 10 MUHIMU YA KUZINGATIA UKIWA NA MTOTO CHINI YA MIAKA MITANO

                                                           
                                                                                             
wanaawake wengi wakishajifungua hupenda kuishi kwa mazoea au uzoefu hasa kwa kufuata bibi na mama wanasema nini kuhusu afya ya mtoto, sio vibaya lakini ni vizuri uwe makini sana kwani maisha yamebadilika sana na kuna mambo mengi yamepitwa na wakati na mengine ni hatari kiafya hivyo usikubali kila unachoambiwa na watu bila kukichuja.
kuna mambo kadhaa ya msingi sana ambayo usipokua makini nayo utampoteza mtoto kama ifuatavyo.
hakikisha anapata chanjo zote; ukiona unaambiwa mtoto anatakiwa achomwe chanjo fulani maana yake ugonjwa unaozuiliwa na chanjo hiyo umeshaua watoto wengi sana hivyo ukileta uzembe tu mtoto wako anaweza kua mmoja wa watakao uwawa na ugonjwa huo.
mpeleke hospitali akiugua; mara nyingi akina mama hunza kutibu wenyewe na wakiona mtoto amezidiwa kabisa ndio wanakimbia hospitali, mara nyingi watoto hawa wanapona kwa bahati tu lakini wengi hufariki..mtoto sio kama mtu mzima akiugua kidogo tu anafariki hivyo usilete uzembe katika hili.
tumia neti ya mbu; kama wewe neti huiwezi basi nunua kitanda maalumu cha mtoto usiku akilala alale na net, malaria inaongoza kwa kuua watu hapa afrika na watoto wakiuawa zaidi kuliko hata watu wazima.
kula vizuri mlo kamili; ili upate maziwa ya kutosha yenye virutubisho vyote hakikisha unakula vizuri kwa kufuata mlo kamili yaani mchanganyiko wa vyakula vyote, kipindi mtoto ananyonya achana na mawazo ya kupungua uzito, subiri afikishe miaka miwili ya kunyonya ndio uanze kupungua lakini pia mifupa, nyama na kila kitu cha mtoto kinatokana na wewe hivyo kula vizuri kurudishia madini yaliyopotea wakati wa ujauzito...usipozingatia hili utakutana na upungufu wa madini siku za usoni
osha matiti yako kila ukitaka kunyonyesha; akina mama wengi wana shughuli nyingi hatukatai lakini tabia ya kunyonyesha bila kuosha matiti wakati wa shughuli hizo ndio chanzo cha mtoto kuharisha mara kwa mara. ukitoka kwenye shughuli zako oga au osha matiti afu ndio umpe mtoto anyonye.
fuata ushauri wa daktari; usipende kutoa dawa hovyo bila kupata ushauri wa daktari au muhudumu wa afya, dawa hizo hutolewa kwa uzito na mara nyingi uzito wa mtoto huongezeka kila mara hivyo dozi aliyopewa miezi mitatu iliyopita huenda mwezi huu haimtoshi tena.
achana na maziwa mbadala; kama hauna jinsi labda wewe ni muathirika wa ukimwi na umekatazwa kunyonyesha au hauna maziwa ya kutosha basi unaweza kumpa mtoto maziwa ya ngombe au maziwa ya dukani lakini nikuthibitishie kwamba maziwa ya mama hayana mbadala wa 100%, yale ya mama ni bora zaidi kwa afya ya mwili na akili za darasani hapo baadae.
weka hatari zote mbali na mtoto; mtoto asipelekwe jikoni kwenye moto, usiweke dawa zozote mahali pa wazi yaani dawa za panya, dawa za binadamu na kadhalika, nyumba yako hakikisha haina shimo hata moja na hakikisha mtoto hachezi barabarani yaani hatari zote weka mbali.
simamia maendeleo ya mtoto; baadhi ya wanawake wako bize sana na maisha baada ya kujifungua hivyo kazi ya kulea huwaachia wafanyakazi wa ndani, ni hatari sana kukabidhi maisha ya mtoto wako kwa mfanyakazi..jitahidi uende clinic hata mara moja moja ujue maendeleo yakoje, jifunze jinsi ya kusoma kadi ya clinic kujua kama uzito unapanda au unashuka, rudi nyumbani ghafla ukague kama mtoto anapewa chakula kama unavyotaka.
kua makini usibebe mimba mpya kabla huyo mdogo hajakua; kunyonyesha tu kunaweza kuzuia mimba lakini kama mama ananyoshesha zaidi ya mara kumi kwa siku ndani ya miezi sita ya kwanza kama huwezi kutumia kalenda au damu hazijaanza kutoka basi chagua njia ya uzazi wa mpango ambayo ni salama kwa mtoto. tembelea blog yetu ya kingereza hapa http://www.vibesinc.ga/

                                                         STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183


HAYA NDIO MADHARA NANE YA KULA KUKU WA KISASA.

                                                           
 
kutokana na uhitaji mkubwa sana wa kuku hasa mijini ambapo kuna watu wengi sana, kuku wa kienyeji wameshindwa kabisa kutosheleza hitaji la watu hao.
teknolojia mpya ambayo iko wazi kwa watu wote imekuja na kuku wa kisasa ambao hukua ndani ya muda mfupi sana kuliko kuku wa kawaida yaani kuku wa kienyeji.
kumekua kuna elimu zikitolewa kwamba nyama nyeupe yaani kuku, samaki na ndege ni salama sana kuliko nyama nyekundu kama ngombe, mbuzi na nguruwe...ni kweli kabisa kama ukiwala wanyama hawa wakiwa kwenye asilia yao lakini ulaji wa kuku wa kisasa una madhara makubwa zaidi kuliko kula ngombe na mbuzi ambao wana nyama nyekundu.
kulingana na watu wengi kula sana kuku hawa hasa mahotelini, kwenye vyakula vya haraka kama KFC na kadhalika basi leo ntawaletea madhara ya kuku hawa kama ifuatavyo.

saratani au kansa mbalimbali; kuku za kisasa zina kemikali nyingi sana mfano kemikali phip ambazo huweza kusababisha mtu kupata kansa mbalimbali ikiwemo tezi dume na kansa ya matiti, kansa hizi zikigunduliwa mapema unaweza kupona lakini zikichelewa kugunduliwa zinakuua.

lehemu au cholestrol; kuku wa kisasa wana lehemu nyingi sana, hii ni kemikali ambayo ni moja ya vyanzo vikuu vya kuziba mishipa ya damu hasa ya moyo na kuleta magonjwa ya moyo.
tafiti zinaonyesha kuku hawa wana lehemu au cholestrol nyingi kuliko nyama za ngombe au mbuzi na mayai yao yana lehemu mara tatu zaidi ya nyama ya ngombe na mbuzi.

kuongezeka uzito; kuku wa kisasa wameonyesha kuongeza watu uzito zaidi kuliko kuku wa kienyeji kwani kuku hawa wanakua na nyama nyingi sana ambazo huwafanya watu wazile kwa uroho, hii huweza kusababisha magonjwa ya moyo, kisukari na kiharusi.kumbuka kuku hawa hawafanyi mazoezi yeyote tufauti na kuku wa kienyeji ambao hutembea sana.

huongeza sumu mwilini; kuku hawa kama nilivyosema mwanzo hukuzwa kwa kemikali nyingi sana ambazo huwakuza mara tatu zaidi haraka kuliko kuku wa kawaida, sumu hizo ni chanzo ya magonjwa kama kansa, kusahau sana uzeeni kitaalamu kama alzhaimer disease, magonjwa ya mishipa ya fahamu na kadhalika.
magonjwa haya hushambulia sana wazee hasa nchi zilizoendelea kama marekani, ujerumani, uingereza na kadhalika sababu ya mfumo wao wa kula hauna vitu asilia kabisa.

huongeza usugu wa dawa za binadamu; kuku hawa hupewa vyakula vyenye dawa za antibayotiki ambazo huwasaidia wasiugue na kufa hata kwenye mazingira magumu, sasa dawa hizi huliwa na binadamu na kumfanya azizoee sasa ikitokea anapata ugonjwa dawa nyingi atakazokula zitakataa kumtibu sababu mwili wake umeshazoea dawa.

mafua ya ndege; mafua haya yameua watu wengi sana nchi zilizoendelea na kuwaacha wengi wagonjwa kitandani, avian flu ni moja ya magonjwa tishio ambayo husababisha viungo mbalimbali mwilini kushindwa kufanya kazi.

kukua haraka kwa watoto; daktari mmoja wa mifugo  kwenye chuo kikuu cha zambia ambaye amehusika sana na tafiti za kuku hawa anasema kwamba kuku hawa wanawekewa homoni za ukuaji kitaalamu kama growth hormone ili wakue haraka na madhara yake huathiri sana watoto ambao wanakua na kujikuta wanakua na kubalehe kabla ya wakati.

kuishiwa nguvu za kiume: sababu maini ya kuku ndio yanahifadhi sumu zote za mwili wa kiumbe chochote, tafiti zinaonyesha ulaji wa maini wa kuku wa kisasa kunaweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume.tembelea group letu la kingereza hapa http://www.vibesinc.ga/

                                                           STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                          0653095635/0769846183 [tuma sms tafadhali]

                                       *karibu kwenye grupu la watsapp la siri za afya bora*

YAFAHAMU MADHARA YA KUANGALIA VIDEO ZA NGONO NA JINSI YA KUACHA.

                                                               

kuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu, kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto baada ya kuangalia video za ngono.
bahati mbaya tabia ya kuangalia video hizi watu wengi huipata wakiwa wadogo sana na usipokua makini tabia hii itakufanya vibaya sana kisaikolojia.
tabia ya kujichua sasa iko wazi kwa jinsia zote yaani wanawake na wanaume japokua imekua ikiathiri zaidi wanaume sababu ya maumbile yao.
leo tutaangalia madhara makuu ya kuangaia video hizi na jinsi ya kuachana na tabia hii.
kuishiwa hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume; kuangalia sana video za ngono hukufanya ushindwe kusisimuliwa na mwanamke au mwanaume wa kawaida, video za ngono zina wanawake na wanaume wazuri sana ambao wako vile sababu ya kufanyiwa upasuaji mbalimbali wa kuongeza makalio na matiti, hata wanaume hufanyiwa upasuaji wa kuongeza uume hivyo mwanamke anayeangalia atatamani uume mkubwa kama ule au mwanaume anayeangalia atatamani mwanamke kama yule ambaye katika mazingira ya kawaida hayupo.
sasa wanaume wanao angalia video za ngono hawawezi kusisimka au kuamsha uume hata mwanamke wa kawaida akipita uchi na hii huweza kuathiri sana mahusiano yao na kuonekana hawana nguvu za kiume kwani wao hutegemea video hizo kuamsha uume.
kujichua au kupiga punyeto sana; video za ngono zina wanawake na wanaume tofauti, kila video nzuri unayoangalia utaenda kujichua huku ukimuwaza wanaume au mwanamke husika...hii itakufanya ujichue hata mara kumi kwa siku kama unaziangalia mara kwa mara. kuishiwa nguvu za kiume, kusahau sana, kushindwa kumpa mwanamke mimba, kuchoka sana na kukojoa haraka wakati wa tendo la ndoa ni moja ya madhara makuu ya punyeto.
kushindwa kudumu kwenye mahusiano; kuangalia video za ngono hukufanya uwaze kujiridhisha mwenyewe tu na hata mwenza wako akitaka kulala na wewe unakua hutaki tena, lakini hata kwa vijana ambao hawako kwenye mahusiano hujikuta wanakua waoga sana kuwafuata wanawake au wasione sababu ya kua kwenye mahusiano, lakini pia wanaume hushindwa kuwaridhisha wenza wao na wanawake kusingizia kuchoka kila siku.
addiction; hii ni hali ya kuzoea sana video za ngono na kushindwa kuacha kuziangalia kila siku hata muda wa kazi, muhanga hujikuta akishinda mitandaoni kutafuta website mpya ili aweze kupakua au kudownload video zingine kwani alizokua nazo ameshazichoka..hii humfanya mtu kua mtumwa intaneti.
kuanza kufanya ngono ambazo sio za kawaida; hivi karibuni idadi kubwa ya wanawake wamekua wakijihusisha sana na mapenzi ya kinyume na maumbile, hii imesababishwa sana na kuangalia video za ngono na kuona ni kitu cha kawaida wakati kina madhara mengi, wanawake waliozoea kuingiliwa nyuma hata wakiolewa huendelea kufanywa na wanaume wa nje hasa kama waume zao hawajawahi kujihusisha na tabia hiyo...aina zingine za ngono amabazo zinababishwa na tabia ya kuangalia video hizi ni ushoga, usagaji, au mwanamke kulala na wanaume zaidi ya mmoja au mwanaume kulala na wanawake zaidi kwa wakati mmoja.
inawezekana wewe unayesoma hapa tayari hii tabia inakuumiza sana kwa sasa na umeshindwa kuiacha, kuna mambo ya msingi unaweza kufanya ili uweze kuacha kuangalia video hizi..
ondoa zana zote za kuangalia video hizi; kama una computer au simu futa video zote, futa website zote za video ambazo unazitumia kuangalia...kuna watu wamo kwenye magrupu ya watsapp ya kutumiana video za ngono, ondoka kabisa huko kwani unajiharibu.
jiunge na mazoezi; ni mazoezi pekee yanayoweza kumfanya mtu aweze kuachana na tabia zote ambazo sio za kawaida ambazo alikua anazifanya kipindi cha nyuma..fanya mazoezi yeyote upate uchovu wa kutoangalia tena.
badilisha tabia hii na ufanye tabia nyingine; kama una tabia ya kuangalia video hizi basi fanya mpango uwe unafanya mambo mengine muda ambao umekua ukiangalia hizi video, ikiwemo kusoma vitabu au kuongea na watu.
waambie marafiki; inawezekana unaishi na watu amabo video hizi ni kitu cha kawaida yaani inaweza kuziangalia mbele zao, waambie umeacha ili wakusaidie lakini pia waambie wasiangalie mbele yako na hata wakipata mpya wasikwambie.
pata ushauri wa kitaalamu na matibabu; unaweza kumuona mtaalamu wa saikolojia maeneo unayoishi wewe akakupa ushauri lakini pia kwa wale ambao wameshapata madhara hasa nguvu za kiume unaweza kuwasiliana na sisi kwa ushauri na dawa.
kumbuka unaweza kupata ushauri kwa simu au kwa kuja ofisi zetu zilizoko gongo la mboto dar es laam.[ huduma za ushauri sio bure kuna kiasi muhitaji huchangia kabla, kwani unatumia muda na unapata elimu mpya]
mwisho; tafiti mpya zinaonyesha kwamba ndoa nyingi sasa zinavunjika sababu ya madhara ya ngono, chukua hatua sasa kabla hujafikia hali hiyo.

                                                         STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183[TUMA MESEJI TU]
                                                    JINSI YA KUONGEZA UREFU WA MWILI WAKO KWA MAZOEZI.

                                                                 
watu wengi ambao ni wafupi hua wanakwazwa sana na maumbile ya kimo chao, wengi huathirika kiasaikolojia na kupewa majina mbalimbali,kuna sababu nyingi za kila mtu kupenda kua mrefu kama kujiamini mbele za watu, kupendeza kwenye nguo nyingi, ajira nyingine zinataka watu warefu kama ulinzi, jeshini na maonyesho ya mavazi au modelling na kadhalika...
watu wengi wana uwezo wa kuongeza urefu wa kimo chao kwa kutumia mazoezi fulani fulani ya mwili, mara nyingi urefu wa mifupa ya miguu na mapaja huacha kuongezeka mtu akifikisha miaka 20 mpaka 25 lakini urefu wa mgongo huweza kuongezeka mpaka miaka 40 na 50 kwani kuna ushahidi wa watu ambao wamefanikiwa kufanya hivyo.
sehemu zipi za mwili zinaweza kuongezeka urefu?
kama nilivyosema hapo juu, kuna sehemu kuna sehemu kuu mbili ambazo zinamfanya mtu aonekane mrefu na ndio hizo pia zinaweza kuongezwa urefu kama ifuatavyo.
miguu na mapaja; miguu na mapaja ina mifupa kitaalamu kama femur, tibia na fibula...hii ni mifupa ambayo ikiwa mirefu mtu anaonekana mrefu na ikiwa mfupi mtu anaonekana mfupi, urefu wa mifupa hii hua haupungui maisha yote ya binadamu na mara nyingi mifupa hii huacha kuongezeka urefu kwenye umri wa miaka 20 mpaka 25, hivyo kabla ya miaka 25 kuna mazoezi unaweza kufanya kurefusha mifupa hii lakini baada ya 25 haiwezekani tena.
                                                   
uti wa mgongo; uti wa mgongo ni sehemu ya pili ya mwili ambayo humfanya mtu aonekane mrefu au mfupi, eneo hili lina mifupa 33 ambayo imeungana kama pingili na kuacha nafasi katikati, hizi nafasi za katikati ndizo unaweza kuzifanyia mazoezi kuziongeza urefu kwa kuzivuta na kuonekana mrefu..kawaida umri unavyozidi kwenda pingili hizi zinazidi kubana kutokana na kusukumwa na kani ya msukumo au force of gravity ambayo inatusukuma chini na shughuli mbalimbali za kubeba vitu kichwani..hali hii humfanya mtu aliyekua mrefu wakati wa ujana kuendelea kupungua urefu umri unavyozidi kwenda isipokua yule ambaye anafanya mazoezi haya ndio anaweza asipungue.mtu mwenye umri wowote anaweza kufanya mazoezi ya kuongeza urefu wa pingili hizi.
                                                               

vitu gani vinafanya mtu awe mrefu au mfupi?
kuna sababu kuu mbili ambazo zimegawanyika kwenye vipengele mbalimbali
sababu za urithi[genetics]; 
urefu mara nyingi unafuata ukoo, japokua baba yako na mama yako kua wafupi haimaanishi na wewe lazima utakua mfupi, kama kuna ndugu wengine warefu kwenye ukoo unaweza kurithi urefu huo ukawa mrefu.
hakuna njia sahihi kabisa ya kujua utakua mrefu kiasi gani mpaka utakapofikia utu uzima lakini kuna jinsi unaweza kukadiria urefu wako kwa kuangalia urefu wa wazazi.
kanuni  iko hivi; urefu wa baba yako jumlisha urefu wa mama yako gawanya kwa mbili kisha ongeza 5 kama wewe mwanaume na punguza 5 kama wewe ni mwanamke.
mfano. baba yako ana urefu sentimita 160 na mama yako sentimita 160, ukijumlisha unapata 320 ukigawanya kwa mbili unapata 160...kama wewe ni msichana toa tano, unakadiriwa kua na urefu wa sentimita 155, na kama mvulana jumlisha tano unakadiriwa kufikisha 165.

sababu ambazo sio za urithi; hizi ni sababu ambazo zinaweza kumfanya mtu ambaye amezaliwa kwenye familia ya watu warefu awe mfupi ukubwani, mfano kukosa lishe ya kutosha kipindi cha utoto, kuugua sana utotoni, kuzaliwa na uzito mdogo sana, uvutaji wa sigara na pombe kwa mama mjamzito akiwa tumboni na kadhalika...

japokua mambo mengi sana yana amua mtu awe mrefu kiasi gani kipindi cha maisha yake lakini kuna mambo unaweza kufanya kuongeza urefu wako kidogo na kua mrefu kiasilia kama ifuatavyo..
pata usingizi wa kutosha; kama wewe ni kijana mdogo ambaye unataka kurefuka zaidi au ni mtu mzima kidogo na umeamua kuingia kwenye programu hii ya urefu basi hakikisha usiku unapata masaa yako nane ya kulala kwani mtu akilala homoni za ukuaji kitaalamu kama growth hormone hutengenezwa wa wingi sana.

kunywa maji ya kutosha; maji yanaufanya mwili uweze kufanya kazi zake za kutumia chakula kirahisi na kuondoa sumu zote mwilini, ni vizuri kunywa angalau glass nane za maji kwa siku, na hii itasaidia sana kwenye ukuaji wako.

kaa mbali na vitu vinavyozuia kuongezeka urefu; pombe na matumizi ya dawa mbalimbali huzuia ukuaji kwa vijana wengi ambao wako kwenye kipindi cha ukuaji, mfano baadhi ya dawa za pumu huweza kuchelewesha ukuaji, usinywe kahawa kwani itakunyima usingizi wa kutosha na kukufanya ushindwe kuongezeka urefu.
                                           
weka utaratibu wa kukaa na kutembea vizuri; watu wengi sana wana tabia ya kutembea wamepinda mgongo, hii ni kwasababu ya kukaa muda mrefu wakifanya kazi na kujikuta wamezoea hali hii ya kupinda mgongo...hakikisha ukiwa umekaa unanyooka na ukitembea unanyooka, siku ukizoea hali hii utashangaa kuona urefu kiasi gani ulikua umeuficha mgongoni.
                                                       

kula vizuri; achana na vyakula kama chipsi, soda, biskuti, chocolate na kadhalika kwani havina msaada kwenye ukuaji wako na jikite kwenye vyakula asilia vyenye virutubisho mbalimbali kama ifuatavyo
calcium; madini haya ni muhimu sana kwenye ukuaji wa mifupa kwani 99% ya mifupa imetengenezwa na madini haya, unaweza kuyapata kwenye maziwa, mboga za majani, soya, samaki na dagaa.
vitamin d; madini haya hufanya kazi bega kwa bega na mwili kuhakikisha madini ya calcium yanatumika na hupatikana kwenye uyoga,samaki, mayai, maziwa na unaweza kupata madini haya kwenye jua la asubuhi.
zinc; haya ni madini muhimu yanayopatikana kwenye mayai na maziwa.
                                                             

kua na ratiba nzuri ya kula; kula mara tatu kwa siku mchanganyiko wa vyakula mbalimbali vya asilia, lakini chakula cha usiku usile zaidi ya saa mbili usiku.

tumia virutubisho vya kuongeza urefu; kuna virutubisho mbalimbali vyenye madini muhimu ambayoa yanahusika moja kwa moja kuongeza urefu, tafiti zinaonyesha watu wengi hawapati madini ya kutosha kwemnye milo yao hivyo virutubisho hivi ni muhimu sana na vimesaidia watu wengi ambao wanataka kuongezeka urefu wa kimo,.(wasiliana nasi kama unavihitaji, kwasasa tunaagiza nje ya nchi)
                                               

upasuaji; nchi zilizoendelea kuna utaratibu wa kuvunja mifupa ya miguu na kuiongeza kwa upasuaji, utaratibu huu unaweza kufanikiwa kuongeza nchi 3 mpaka nne lakini kuna madhara ambayo yanaweza kutokea kwa kujaribu kufanya upasuaji huu, huku kwetu aina hizo za upasuaji hakuna.                                                

mazoezi ya kuongeza urefu; pamoja na vitu vyote ambavyo nimevitaja hapo juu, mazoezi ndio muhimu sana sana katika harakati za kuongeza urefu, sio mazoezi yote lakini kuna mazoezi muhimu ambayo yanalenga moja kwa moja kuongeza urefu wa mifupa yako na kukufanya uwe mrefu, kutokana na urefu na picha ambazo zinatumika kuonyesha mazoezi hayo kua ndefu sana nimeamua kuandika kitabu cha mazoezi makuu ya kuongeza urefu wa binadamu baada ya kufanyia majairibio njia hizo na kugundua kwamba mazoezi hayo yanafaa iwapo yakichanganywa pamoja na virutubisho na mambo niliyoyasema kwenye makala hiii.
kulingana na ukubwa wa kazi uliofanyika kwenye tafiti hizi na maandalizi ya makala hizi na kitabu, kitabu hichi kitauzwa kwa gharama ya shilingi 20000[elfu ishirini tu] za kitanzania na kitakua kwa mfumo wa soft copy yaani kitatumwa kwa email au watsapp kwa ambao watakua tayari kukitumia ili wafanikiwe kuongeza urefu.
kuongeza urefu kunataka juhudi, bidii na kutokata tamaa...kama huwezi kupambana basi usipoteze fedha zako kununua kitabu hiki.

je kuna watu ambao walifanikiwa kwa mazoezi haya?
ndio watu maarufu kabisa duniani ambao zamani walikua wafupi au walikua warefu wa kawaida baadae walifanya mazoezi haya na kufanikiwa kuwa warefu, wapo naowafahamu binafsi yaani marafiki zangu, mimi pia niliwahi kuongezeka urefu kwa mazoezi haya, watu niliosoma nao shule ya msingi na sekondari wanakumbuka ufupi wangu, ila ntazungumzia wale maarufu ambao wanafahamika dunia nzima hii imewajengea heshima na kuwaongezea kipato kama ifuatavyo..
christiano ronaldo
akiwa na umri wa miaka 18 mchezaji huyu maarufu ambaye kwa sasa anacheza soka ka kulipwa huko ulaya katika timiu ya real madrid alikua na urefu wa futi tano na nchi kumi lakini alipofikisha miaka 25 alikua na urefu wa futi sita na nchi moja kwa mazoezi hayhaya  na njia hizihiz nayozungumzia hapa.

 schwarzeniger;
huyu ni moja ya watu maarufu sana ambaye aliwahi kujihusisha na ubebaji wa vitu vizito, uigizaji wa filamu na baadae kua gavana wa jimbo la calfornia nchini marekani. yeye aliongezeka kutoka futi sita mpaka futi sita na nchi mbili.
                                                       

david robinson;
huyu alikua anapenda sana kucheza mpira wa kikapu kama basketball lakini kutokana na ufupi wake hakuweza kuruhusiwa kufanya hivyo na baadae alikata tamaa, lakini kwa mazoezi hayahaya alitoka kwenye urefu wa tano na nchi tisa mpka futi saba na nchi moja, baadae alichezea ligi kubwa                                                    

kabisa duniani ya nba na kua kati ya watu wenye mafanikioa makubwa kwenye ligi hiyo.

andy murray; huyu ni mcheza tennis ambaye hapo mwanzo alikua na urefu wa futi sita na nchi moja lakini hivi karibuni amefanikiwa kufanya mazoezi na kuongezeka mpaka futi sita na nchi tatu.
                                                               

le jingy; huyu ni muogeleaji maarufu ambaye aliongezeka kutoka futi tano na nchi saba mpaka futi sita na nchi moja kwa kufanya mazoezi hayo.
                                           

dennis rodman; akiwa na urefu wa nchi 5 na futi nane alikataliwa kwenye timu ya basketball ya shuleni kwao na kujiingiza kwenye mazoezi haya, ambayo baadae yalimpa urefu wa futi sita na nchi nane na kufanikiwa sana kwenye mchezo huu.
                                                       


STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183

ZIFAHAMU AINA YA DAWA 12 SALAMA KWA WAJAWAZITO

                                                         
makala zangu nyingi sana nimekua nikigusia swala la wajawazito na kukusisitiza kwamba watu hawa hawatakiwi watumie dawa yeyote bila kuandikiwa na daktari, niliwahi kuandika kuhusu dawa hatari kwa watu hawa kama hukuzisoma bonyeza hapa http://www.sirizaafyabora.com/2014/12/normal-0-false-false-false-en-us-x-none.html,...leo nakuja na dawa ambazo ni salama kwao, zipo nyingi sana ila ntataja zile muhimu tu ambazo zinatumika sana na zinapatikana kwenye mazingira yetu kama ifuatavyo;

penicillin; hili ni group la dawa za kuua bacteria au antibayotiki, hutumika kutibu magonjwa mbalimbali kwa mama mjamzito kama uti, kikohozi, magonjwa ya ngozi, na mengine mengi mfano ampicillin, cloxacilin, benzyl penicilin, pen v, benzathine peniciline na amoxycilline.

cephalosporins; hizi ni dawa zenye nguvu sana kuliko hizo nilizotaja hapo juu, hapa nchini hutumika kwa magonjwa ambayo mara nyingi yanakua yameshindikana kutibu magonjwa niliyotaja hapo juu mfano wa dawa hizo ni cefriaxon au powercef na cefuroxime.

macrolides; huu ni mchanganyiko wa dawa unaotibu na kuua bacteria mbalimbali wanaoshambulia mwili wa binadamu, hutumika kipindi cha ujauzito bila hofu mfano erythromycin, clarythromycin au clarinta na azithromycin au azuma.

paracetamol; hii ni dawa ya maumivu ambayo hutumika sana kipindi cha ujauzito, dawa zingine kama aspirin, diclofenac na diclopa hua hazitolewi kwa hofu ya kusababisha kuvuja sana kwa damu kwa mama huyu.

hydrocortisone cream; hii ni dawa inayotumika kutibu miwasho na aleji mbalimbali ni salama kwa mama mjamzito lakini haitakiwi kutumika kwa muda mrefu sana.

anusol; hizi ni dawa zinazotumika kutibu miwasho, maumivu au ugonjwa wowote sehemu za haja kubwa, haina madhara yeyote kipindi cha ujauzito. matatizo kama bawasiri au haemorroids huweza kutibika na dawa hii.

cotrimazole cream; hii ni dawa ya kutibu fangasi za aina mbalimbali kama za ngozi, uke na kadhalika, huweza kutumika kipindi cha ujauzito.

ducolax; hii ni dawa kwa ajili ya kutibu tatizo la kupata choo laini, kama mgonjwa anasumbukiwa na tatizo la kutoa choo ngumu sana dawa hii ni msaada mkubwa.

ranitidine; hii ni dawa ya kutibu madonda ya tumbo lakini pia hutumika kutibu gesi au kiungulia tumboni.

kwinini; hii ni dawa ya malaria ambayo ni salama kipindi chote cha ujauzito kwanzia mwanzo mpaka mwisho, dawa ya mseto ya malaria ni hatari sana miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito hivyo isitumike kipindi hicho.

cylindamycin; mara nyingi hufanya kazi zinazofanyika na fragile au metronidazole na ni mbadala mzuri kipindi hiki kwani fragile haifai kwa wazazi.

mebendazole; hii ni dawa nzuri sana kwa minyoo kipindi cha ujauzito, haina madhara yeyote, epuka matumizi ya albendazole kwani huweza kutoa mimba.

                                                  STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                           0653095635/0769846183


HIZI NDIO SABABU KUMI KWANINI KAHAWA NI SUMU KWAKO.

                                                                   
kunywa kahawa imekua moja ya ni moja ya tamaduni zetu kwenye maisha ya kila siku, kahawa inatumika na jamii nyingi duniani.
hapa kwetu tanzania kahawa inatumika majumbani na hata vijiweni utawakuta watu wanatembeza kahawa na kashata, wateja wa huduma hii ni wengi sana.

kahawa inafanya kazi vipi mwilini?
kemikali iliyopo ndani ya kahawa ya caffeine kitaalamu inaitwa 1,3,7-trimethyxanthine, kwa hali ya kawaida kahawa inakua kama unga mweusi mchungu sana lakini hupelekwa viwandani na kubadilishwa na kuongeza vionjo.
ukinywa kawaha baada ya dakika kumi huingia kwenye damu na kusafiri mpaka kwenye ubongo, huko hubadilisha hali ya mtu kutoka kwenye utulivu na kumfanya achangamke.
kahawa huzuia kemikali moja kitaalamu kwa jina la adenosine, kwa hali ya kawaida adonenosine huzuia kemikali ya uchangamfu kwa jina la acetycholine.
kahawa pia humwaga homoni za adrenaline kwenye damu, homoni hizi hua zinatengenezwa mtu akiwa na wasiwasi, uoga, hasira au akitaka kupigana.
sigara inaongeza kasi ya kazi ya kahawa mwilini hivyo wavuta sigara wakinywa kahawa inawaingia haraka kuliko watu ambao sio wavutaji.
unywaji wa kahawa huleta faida za muda tu ambazo ni kama kuondoa usingizi na kukufanya usome au ufanye kazi kwa muda mrefu, huondoa uchovu na uvivu unapoinywa, ni nzuri kwa wagonjwa wa pumu kwani hupanua mirija ya hewa, watu wengine huweza kuondoa maumivu ya kichwa kwa kunywa kawaha, kimsingi dawa nyingi za kutuliza maumivu zina kemikali ya caffeine inayopatikana kwenye kahawa.

pamoja na faida zote hizo kahawa ina madhara ambayo ni hatari kwenye mwili wa binadamu kama ifuatavyo.
huongeza sukari mwilini; kemikali ya caffeine inayopatikana kwenye kahawa huongeza sukari mwilini kwa kuongeza kiwango cha adrenaline, hii ni hatari sana kwa mgonjwa mwenye kisukari tayari.

huongeza kukojoa; kahawa hufanya mtu kukojoa mara kwa mara kitaalamu kama diuresis hii huweza kuleta usumbufu mkubwa wakati wa kulala au wakati wa kazi.

huongeza kiwango cha lehemu au cholestrol mwilini; cholestrol hatari mwilini kwa jina la lower density lipoprotein[ldl] huongezeka kwa asilimia tano kwa matumizi ya kahawa.

hupunguza kasi ya mmengenyo wa chakula; kemikali ya cafein hufunika eneo la tumbo kwa kuweka kitu kama koti na kuzuia mmengenyo mzuri wa chakula, magonjwa mbalimbali ya tumbo kama colitis huongezwa zaidi na kahawa.

kukosekana kwa vitamin b; caffeine hupotea pale kahawa inapotumika kwa wingi sana, hupunguza vitamin b ambayo ni muhimu sana kwenye kuvunja wanga na kuupa mwili nguvu.

huleta madhara kwenye moyo; kemikali ya caffaine husababisha moyo kupiga bila mpangilio maalumu, hii ni huweza kusababisha mshituko wa moyo hasa kwa wagonjwa wa moyo.

kukosa usingizi; kahawa huharibu ubora wa usingizi, hii humfanya mtu kulala kwa kuhangaika sana huku ukaimaka mara kwa mara katikati ya usingizi, mara nyingi wanafunzi wanaotaka kusoma muda mrefu usiku hunywa kawaha kupata hii kitu.

humaliza nguvu za mwili; ukinywa kahawa unaufanywa mwili ushindwe kupumzika kipindi unafanya kazi hivyo unakua una nguvu sana mwanzoni, baadae kahawa ikiisha mwilini mtu hujikuta na uchovu mkali sana.

hupunguza kiasi cha madini ya kashiamu mwilini; matumizi ya kahawa huufanya mwili kuondoa kiasi kikubwa cha kashiumu kupitia mkojo na choo kubwa na kusababisha kukosa kiasi kikubwa cha kashiumu mwilini, hii huweza kuleta magonjwa ya mifupa kama kuvunjika na matege kwa watoto.

huongeza kiasi cha tindikali tumboni; kahawa husababisha kutengeneza kwa kiasi kikubwa mno kwa tindikali ambayo hupatikana tumboni kwa ajili ya kumengenya chakula, tindikali hii ikiwa nyingi husababisha mmengenyo mbovu wa chakula na maumivu makali kwa watu wenye madonda ya tumbo

kuchosha figo na maini; sababu kemikali ya caffaine inafanyisha kazi sana viungo hivi vya mwili baadae viungo hivi huchoka sana na kupoteza ufanisi, hii ndio sababu wagonjwa wa ini na figo hushauriwa kutotumia kahawa.

madhara kwa mtoto anayenyonya; kunywa kahawa zaidi ya miligram 200 huweza kupita kwenye maziwa na kwenda kwa mtoto, kunywa kahawa kipindi cha ujauzito huweza kuleta upungufu wa damu kwa mama na mtoto.

vipi kuhusu chai ya rangi nyeusi?
japokua chai ya rangi ina kemikali ya caffaine kama kahawa ila kiasi chake ni kidogo sana kwenye chai, chai faida mbalimbali kama kuua bacteria na virusi mbalimbali mdomoni japokua chai ikitumika na chakula hapohapo huzuia mwili kupata madini kama kashiumu,madini ya chuma na zinki na pia ina madhara kama ya kahawa.
chai pai ina kemikali ya floride ambayo huimarisha meno, na husafisha mdomo.

je kitu gani ni bora kutumika mbadala wa chai nyeusi na kahawa?
chai ya kijani maarufu kama green tea ni nzuri sana kwa mwili wa binadamu...hupunguza presha ya damu,kuipa nguvu mishipa ya damu,hutibu magonjwa yasababishwayo na bacteria na kuzuia damu kuganda.
kutumia kahawa na chai nyeusi ambazo zimeondolewa kemikali ya caffeine ni vizuri lakini pia chai kwa jina la herbal tea ni nzuri sana kiafya...

                                                    STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                            MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                       karibu kwenye group la afya la siri za afya bora
                                                 

YAFAHAMU MADHARA 10 YA ULAJI MWINGI WA CHUMVI KWENYE CHAKULA

                                                       
                                         
tafiti zilizofanywa na jarida la new england journal of medicine nchini uingereza limegundua kwamba zaidi ya watu milioni moja na laki sita wanauawa na na ulaji wa chumvi kila mwaka, kifo ni hatua ya mwisho ya madhara ya chumvi lakini kuna madhara mengi sana yasababishwao na chumvi kabla ya kifo.
kitaalamu chumvi ni kompaundi au mchanganyiko wa element za sodium chloride, kemikali hii hutumika kuhifadhi chakula na kuleta ladha ya chakula, kemikali hii huweka kiwango cha maji mwilini sawa na kusaidia utumaji wa taarifa kwenye mishipa ya fahamu, husaidia kuhifadhi maji mwilini, ni muhimu kwenye damu ya mwili,kutengeneza tindikali kwa ajili ya mmengenyo wa chakula tumboni, hata dripi za maji tunazopewa mahospitalini hua zina chumvi.
maisha ya kisasa na vyakula viulivyopo vinawafanya watu kula chumvi nyingi sana kuliko zamani, hii husababisha madhara makubwa ambayo hayatibiki kirahisi.
kiafya mtu anatakiwa ale chakula chenye chumvi inayosikika kwa mbali sana na asiongeze chumvi chakula kinapokua mezani, hii ni sawa na gramu 1.5 mpaka 2.3 kwa siku, hii ni sawa na kijiko kimoja cha chakula kwa siku nzima.
ulaji mkubwa wa chumvi kwa wakati mmoja husababisha kuishiwa maji kwa seli, hii huleta kuchanganyikiwa, degedege, kupoteza fahamu na kifo lakini pia uwepo wa chumvi kidogo sana kwenye damu husababisha kuvimba kwa seli, kuchanganyikiwa,kupoteza fahamu na kufa..hii hutokana na unywaji mkubwa wa maji kupitiliza kiasi kwa wakati mmoja.
kimsingi vyakula vingi tunavyokula vina chumvi ya kutosha ambayo inatosha kabisa kuendesha mwili wetu bila kuongeza chumvi nyingine ya ziada, vyakula hivyo ni kama vitunguu,malimao,maji ya kunywa,viazi,ngano,nyanya,maboga,caroti, spinachi, kabechi,mapera, zabibu,epo,karanga,mayai, maziwa na vingine vingi
yafuatayo ni madhara ya ulaji wa chumvi nyingi ambayo yanaweza kua ya muda mrefu au ya muda mfupi.
yafuatayo ni madhara ya muda mrefu wa kula chumvi nyingi kwenye chakula...
presha ya damu; chumvi ina tabia ya kuzuia maji kutoka nje ya mwili kupitia mkojo, lakini pia kuna ushahidi kwamba kupunguza ulaji wa chumvi kwa wagonjwa wa presha hupunguza presha kwa wagonjwa wa presha.
kansa ya tumbo; utafiti umeonyesha kwamba nchi ambazo kuna ulaji mkibwa sana wa chumvi kama japani kuna wagonjwa wengi sana wa kansa ya tumbo la chakula ukilinganisha na nchi ambazo hazina ulaji mkubwa wa chumvi kama uingereza.
ugonjwa wa moyo; chumvi husababisha kuvimba kwa moyo na kuufanya kua mkubwa kitaalamu kama left ventricular hypertrophy, hii husababisha moyo kushindwa kusukuma damu kama unavyotakiwa kufanya kazi.
magonjwa ya figo; kupanda kwa presha ya damu husukuma damu nyingi sana kwenye mishipa ya damu, hii huharibu figo na kuifanya kushindwa kutoa maji mwilini lakini pia viungo muhimu kama macho na mishipa ya damu huharibika.
addiction; ulaji mkubwa wa chumvi humfanya mlaji kuendelea kupenda vyakula vyenye chumvi nyingi sana na kushindwa kabisa kuvumilia kula vyakula vyenye chumvi kidogo...hii hizidi kuathiri mwili na kuusababishia matatizo makubwa zaidi.
kiharusi; huu ni ugonjwa wa kupooza unaosababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu ya kwenye ubongo kutokana na mafuta au kuvujia kwa damu, kwa ulaji wa chumvi nyingi huongeza presha ya damu na kupasua mishipa midogo ya kichwa na kuleta kiharusi.
kuongezeka uzito; kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba chumvi huzuia maji kutoka nje ya mwili, hii huongeza uzito wa mwili na kumfanya mtu kujisikia amejaa tumbo muda mwingi, kumbuka lita moja ya maji sawasawa na kilo moja ya uzito.
kupungua kwa uwezo wa mishipa ya fahamu; katika watu wenye umri mkubwa chumvi inazidi kupunguza uwezo wao wa kufanya shughuli mbalimbali na kujikuta wakitetemeka na kushindwa kubeba hata kikombe kimoja cha chai.
magonjwa ya mifupa; mwili wa binadamu unapoteza kiwango cha calcium mwilini pale mtu anapozidi kutumia chumvi zaidi, hii huweza kusababisha mifupa kua milaini na kuvunjika kirahisi pale inapoangukua kidogo tu.
mwili kushindwa kutoa mabaki mwilini; chumvi nyingi mwilini huingilia mfumo wa mwili kuondoa mabaki ya uchafu mwilini, moja ya mabaki yanayobaki ndani ya mwili ni uric acid ambayo inaweza kusababishwa ugonjwa wa maumivu makali ya jointi kitaalamu kama gauti.
suluhisho ni nini? punguza sana kiasi cha chumvi kwenye mla wako na baada ya muda utazoea, kwa wagonjwa wa presha ambao wanatakiwa wale chumvi kidogo zaidi kuna chumvi maalumu kwa watu hao ambazo zinapatikana mijini, chumvi hizi zina kiwango kidogo sana cha sodium hivyo presha zao huweza kushuka...soma blog yetu ya kingereza hapa http://www.vibesinc.ga/

                                                    STAY ALIVE

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183
                             karibu kwenye group ya watsapp ya siri za afya bora