data:post.body Machi 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA KUKOSA USINGIZI NA SULUHISHO LAKE.

                                                               
tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 9 mpaka 15 ya binadamu duniani wanasumbuliwa na matatizo ya kukosa usingizi, tatizo hili ni moja ya matatizo mabaya sana ambayo huweza kumfanya mtu ashindwe kutambua anaishi ulimwengu wa aina gani kwani muda mwingi anakua ni mchovu na hawezi kufanya kitu chochote kwa umakini.
ugonjwa wa kukosa usingizi huwasumbua zaidi watu wazima kwanzia miaka 40 kwenda mbele hasa wanawake kuliko wanaume japokua unaweza pia kuwashambulia vijana wadogo kulingana na matatizo mbalimbali lakini watu wazima sana ndio waathirika wakuu wa shida hii.

kuna aina tatu za matatizo ya kukosa usingizi
kukosa usingizi kunaweza kuja kwa aina tatu yaani kukosa usingizi ghafla, kukosa usingizi mara moja moja au kukosa usingizi kwa muda mrefu sana.
hali hii ya kukosa usingizi husababisha matatizo mbalimbali kama kunenepa,kupoteza kumbukumbu, kushindwa kufaulu darasani, kushindwa kua makini na kazi, kuchoka sana,wasiwasi, mgandamizo wa mawazo, na hatari ya kupata magonjwa yasiyotibika kama ugonjwa wa presha na kisukari.

nini husababisha kukosa usingizi?
watu sababu mbalimbali huweza kukosa usingizi kama ifuatavyo
mabadiliko ya mfumo wa maisha; hii inaweza kusababishwa na kazi unayofanya kama kuanza kufanya kazi usiku...kazi za ulinzi, kazi za uuguzi, na kadhalika lakini pia kuishi sehemu yenye kelele sana,kusoma sana usiku, baridi sana au joto sana.
matatizo ya kisaikolojia; watu wenye msongo wa mawazo unaosababishwa na matatizo mbalimbali kama kukosa ajira, matatizo ya kiuchumi, kuvunjika kwa mahusiano, magonjwa ya akili, kua na wasiwasi sana wa mambo yanayokuja, wasiwasi wa kuibiwa mali zako ukiwa ndani umelala hasa wamiliki wa magari na mali zinazolala nje.
magonjwa mbalimbali; kuugua magonjwa fulani fulani huweza kumfanya muhusika kukosa usingizi kabisa wakati wa kulala mfano pumu au asthma, magonjwa ya moyo, maumivu makali ya sehumu ya mwili,kiharusi, madonda ya tumbo, maumivu ya jino, na kansa mbalimbali.
mabadiliko ya kiwango cha homoni; hii hutokea wakati wa kipindi cha hedhi ambapo kunakua na mabadiliko madogo ya homoni za uzazi, kipindi cha ujauzito na ugonjwa wowote unaobadilisha kiwango hicho.
teknolojia; kulala na simu na kuendelea kuchati, tv au komputa chumba cha kulala,michezo ya gemu na kadhalika..hii imeathiri sana watu wengi kwani siku hizi kabla ya kulala utamkuta kila mtu anachezea simu angalau saa moja.
dawa mbalimbali; kuna dawa nyingi sana ambazo zimetajwa kunyima watu usingizi kama ifuatavyo
dawa za presha mfano propanolol,metoprol,losartan,atenolol,metoprol, captopril,enapril na solatol,lisinopril
dawa za msongo wa mawazo mfano fluoxetine na paroxetine
dawa za kushusha kiwango cha lehemu mwilini mfano simvastatin,rosuvastatin,lovastatin.
dawa za kupunguza maumivu ya mifupa mfano chrondotin na glucosamine
dawa za kutibu aleji mfano cetrizine
sababu zingine mfano kulala sehemu yenye kelele nyingi, kulala na mtu anayekoroma usiku, kulala sehemu yenye wadudu kama mbu na chawa

watu gani hasa wanasumbuliwa na shida hii?

  • watu wanaosafiri sana
  • watu wanaofanya kazi za usiku
  • wazee sana
  • wanaotumia dawa mbalimbali
  • vijana wadogo ambao mahusiano na ajira ni tatizo kubwa kwao.
  • wanawake waliofika mwisho kuona siku zao za hatari
  • watu wenye magonjwa ya akili
dalili za kukosa usingizi ni kama ifuatavyo..
  • kushindwa kulala kabisa
  • kuamka usiku sana na kukosa usingizi
  • kuamka mapema sana kuliko kawaida
  • kusikia usingizi baada ya kuamka asubuhi
  • kuchoka sana mchana wakati wa kazi
  • mgandamizo wa mawazo na kua na wasiwasi sana
  • kukosa umakini wakati wa kazi
  • kupata ajari za wakati wa kutumia vyombo vya usafiri.
  • kuumwa kichwa sana
  • kuharisha, kichefuchefu na kukosa hamu ya chakula
  • kushindwa kuongeza na watu
vipimo vinavyofanyika
daktari humuuliza mgonjwa mbalimbali kuhusu tatizo lake la kukosa usingizi, vipimo mbalimbali pia huweza kuchukuliwa pia kutafuta magonjwa ambayo yanaweza kumkosesha mtu usingizi.
kwa mtu kugunduliwa na tatizo hili lazima awe amemaliza mwezi mmoja bila kupata usingizi unaoeleweka
vipimo vya kisasa zaidi kama polysmonography huweza kutumika kwa mgonjwa aliyelazwa kupima usingizi wake wakati wa usiku

matibabu;
mara nyingi matatizo ya kukosa usingizi hua yanaaisha pale chanzo cha tatizo kinapotibiwa kwa mgonjwa husika, hivyo mara nyingi matibabu yanalenga kuondoa chanzo cha tatizo hili.
matibbu yamegawanyika katika matibabu yasiyohusu dawa yaani non pharmacological treatment na matibabu yanayohusu dawa yaani pharmacological treatment kama ifuatavyo

matibabu yasiyohusu dawa[ non pharmacological treatment]
ongeza nidhamu ya usingizi; epuka kulala sana au kidogo sana, epuka kulala na njaa, epuka kunywa kahawa na kuvuta sigara wakati wa kulala, hakikisha ratiba yako ya kulala haibadiliki, hakikisha unalala kwenye mazingira rafiki ya usingizi yaani bila kelele au usumbufu wowote.
muone mtalaamu wa ushauri; unaweza kuonana na mshauri akakusaidia kutatua tatizo lako la kisaikolojia linalokusumbua, huduma hiyo tunatoa pia.
epuka vitu mambo ya teknolojia yanayozuia usingizi; tabia ya kua na tv chumba cha kulala, laptop kitandani au kutumia simu usiku kabla ya kulala huweza kukunyima usingizi.
epuka kulala mchana; tabia ya kulala mchana huweza kukunyima kabisa usingizi wakati wa usiku, hivyo kaa mbali kabisa na kitanda wakati wa mchana.
pata matibabu ya tatizo lolote la kiafya linalokusumbua; kama kuna ugonjwa wowote unakusumbua hakikisha unatibiwa, kama ni ugonjwa usiotibika basi hakikisha unafuata matibabu ya kupunguza makali yake.
pata suluhisho la tatizo la kisaikolojia;kama una msongo wa mawazo sababu ya kuachwa kwenye mahusiano huwezi kulala kabisa, kama una matatizo ya kiuchumi, umefiwa, au msongo wowote wa mawazo basi hakikisha unapata suluhisho lake.

matibabu ya dawa[pharmacological treatment]
wakati mwingine chanzo cha kukosa usingizi kinaweza kua nje ya uwezo wa muhusika yaani hawezi kutatua tatizo linalomsumbua hivyo anahitaji matibabu ya dawa ambazo angalau zitampa usingizi alale kama ifuatavyo
ant depressant; mfano fluoxetine na paroxetine
anthistamine
ramelteon
melatonin

                                                  STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                          0653095635/0769846183









ZIFAHAMU HATUA MUHMU ZA UKUAJI WA MTOTO ANAPOZALIWA MPAKA MIAKA MITANO.

                                                                     
kila mtoto mwenye afya njema hufuata ukuaji maalumu ambao umefanyiwa utafiti kwamba unafuatwa na watoto wote kitaalamu kama developmental milestone, mtoto ambaye anayekua chini ya ukuuaji huu au zaidi sana ya ukuaji huu anaweza kua na tatizo hivyo anatakiwa achunguzwe haraka. magonjwa mbalimbali kama utapiamlo, upungufu wa homoni za ukuaji, kisukari, kifua kikuu, magonjwa ya moyo, kuharisha na kuugua mara kwa mara huweza kucheleaesha ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili lakini pia uzalishwaji wa homoni nyingi kitaalamu kama growth homone huweza kumfanya mtoto kukua kuliko kawaida na hii mara nyingi husababishwa na uvimbe wa kansa kwenye ubongo, lakini hii ni mara chache saana..watoto wengi walioko tanzania na afrika kwa ujumla huchelewa kukua na hii huwafanya kuwa wafupi ukubwani na kua na uelewa mdogo darasani.zifuatazo ni hatu muhimu za ukuaji..

wakati wa kuzaliwa;mtoto hupungua uzito kwa 5% mpaka 10% ndani ya siku saba mpaka kumi za kuzaliwa, baadae mtoto huongezeka kilo mbili kila mwaka mpaka atakapofikisha miaka mitano, mtoto huzaliwa na urefu wa sentimita 50, baada ya mwaka mmoja hufikisha sentimita 75 na na baada ya miaka minne hufikisha urefu wa sentimita 100.
mtoto huzaliwa na kichwa chenye mzunguko au diameter au mzunguko  wa sentimita 35 na kuongezeka sentimita moja kila mwezi na baada ya miezi 12 kichwa hufikisha sentimita 46

wiki ya sita; katika umri huu mtoto huanza kutabasamu bila kuongea chochote.

mwezi wa pili; mtoto huanza kukunja na kunyoosha mikono huku akivuta nguo zake na za mtu anayembeba.

mwezi wa nne; kipindi hiki mtoto huanza kushika vitu na kuviweka mdomoni na kuanza kugeuka pale anaposikia sauti ya mtu inaita na kuweza kutumia shingo lake japokua wakati mwingine huweza kushika shingo akiwa na miezi mitatu tu.

mwezi wa sita; kipindi hiki mtoto huota meno, huanza kutambaa, huanza kukaa mwenyewe na hupata wasiwasi akimuona mtu ambaye hamfahamu.

mwezi wa tisa; mtoto huanza kusimama, kuita majina kama dada, mama, kaka na kuanza kucheza michezo ya kitoto.

mwezi wa 12; mtoto huanza kutembea kwa sapoti ya kushikwa au kutumia vifaa maalumu vya kusukuma, huanza kuongeza maneno zaidi ya kaka na dada na pia huweza kushika kikombe na kunywa mwenyewe.

mwezi wa 15; mtoto huanza kutembea mwenyewe, huweza kuchora mstari na kuonyesha kitu anachokihitaji kwa kidole.

mwezi wa 18; mtoto huweza kupanda ngazi, huongeza idadi ya maneno na hufuata akiagizwa kufanya au kutofanya kitu fulani, hapa huanza kutumia kijiko na kujishika sehemu za mwili wake.

miaka miwili; hapa mtoto huweza kukimbia na kupiga mpira, huweza kuvua nguo na kuanza kutamka maneno kama mimi, wewe yule na kadhalika.

miaka mitatu; hapa mtoto anazidi kua mkubwa na kuanza kusimama kwa mguu mmoja, kukimbia zaidi, kujua jinsia na umri wake, huweza kuvaa na kuvua nguo lakini hawezi kufunga vifungo, anaweza kuhesabu moja mpaka kumi kama akifundishwa, anaweza kuruka na kuchora duara.

miaka minne; mtoto anaweza kusimulia kitu kilichomtokea, kutumia choo na kufunga vifungo, huweza kucheza michezo mingi zaidi, huweza kuruka kwa mguu moja bila kuanguka.

miaka mitano; mtoto anaweza kuzitambua rangi nne za msingi, anaweza kuendesha baiskeli, anaongea kama watu wengine bila kuchanganya wakati uliopo na ujao.

mwisho; utaratibu wa kwenda kliniki kwa muda wa miaka mitano uliwekwa ili kuhakikisha mtoto anafuatiliwa na hachelewi kukua na kama kuna tatizo lolote basi lifanyiwe kazi kwa wakati hivyo ni muhimu kuendelea kwenda kliniki hata kama unaona mtoto amekua.
hatua hizo za ukuaji zinatofautiana kulingana na mataifa mbalimbali lakini mtoto wako akiwahi kufanya vitu sio dhambi ila ukiona anachelewa kupita kiasi basi ni dalili mbaya ya ukuaji na kliniki watakwambia.tembelea blog yetu ya kingereza hapa http://www.vibesinc.ga/

                                                               STAY ALIVE

                                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     0653095635/0769846183

HIZI NDIO FAIDA KUMI ZA TENDO LA NDOA KIPINDI CHA UJAUZITO

                                                         
kuna watu wamekua wakiuliza mara kwa mara kama inaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka umri gani wa mimba au ni sahihi kufanya tendo la ndoa kipindi cha ujauzito? maswali yalikua mengi sana hivyo leo nimeamua nijibu maswali hayo na makala hii.
mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama anatarajia kuzaa kesho yake, hakuna tatizo lolote linalomzuia kufanya hivyo, baadhi ya wanawake wamekua wazito sana kufanya hivyo kwa kua na sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanazikosa faida hizi ambazo ni muhumu kiafya.faida zenyewe ni kama zifuatazo
husaidia uchungu mzuri na kupona mapema; kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.
hupunguza kwenda ovyo kukojoa au kujikojolea; wakati wa ujauzito mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.
huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba; tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinaua wanawake wengi sana.
hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida; kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.
huwapa uwezo wa kujiamini; kipindi cha ujauzito mwanamke hua anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.
hupunguza msongo wa mawazo; kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao...je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu utakuaje? je ntapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin, homoni hii hupunguza mawazo na kumpa amani mjamzito.
huongeza upendo na mshikamano  kati ya wapenzi; katika hali ya kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la ndoa tu, amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana kwani kuna mtoto anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakiwa wanapatana.
hukuandaa na uchungu; ukishiriki ndoa wakati wa tarehe zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za  mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.
hutibu tatizo la kukosa usingizi; wanawake wengi wajawazito hua na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri.
hupunguza presha ya damu; kipindi cha tendo la ndoa presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.
mwisho; hakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mtoto na mama yaani hakikisha haulilalii tumbo hasa mimba ikiwa kubwa, kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande mmoja, mwanamke kuja juu, au mwanamke kuinama.tembelea blog yetu ya kingereza hapa http://www.vibesinc.ga/
                                         

                                                                  STAY ALIVE

                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0653095635/0769846183


MAMBO MATANO YA KUTISHA YANAYOTOKEA KWENYE UUME UNAVYOZIDI KUKUA KIUMRI.

                                                     
             
umri wa binadamu unabadilisha kila kitu mwilini, mifumo yote ya mwili hupungua uwezo wa kufanya kazi pale mtu anapoanza kukaribia miaka hamsini, hii huwafanya watu wa umri kushindwa kujikubali na kupambana sana kurudi ujanani lakini sote tunajua uzee hauzuiliki, wakati ukifika lazima yakutokea yatokee..mfumo wa kuona, moyo, upumuaji, figo, mfumo wa chakula, ngozi na kadhalika vyote huishiwa nguvu.
uume wa mwanaume huanza kazi rasmi anavyofikisha miaka 14, hapo hufanya kazi kwa nguvu zote lakini miaka ya mbele baadae mabadiliko huanza kuonekana kama ifuatavyo.
kupungua ukubwa wa uume moja kwa moja; hali hii husababishwa na kubadilika kwa seli nene ambazo zinapatikana kwenye uume na kubadilishwa nyuzi nyuzi za nyama kitaalama kama collagen fibres ambazo ni nyembamba sana lakini hali hii huchangiwa pia na mafuta yanayoziba uume usipate damu ya kutosha, kupungua kiasi cha hormone ya mwanaume ya testosterone na hali hii hufanywa kua mbaya zaidi na uotaji wa kitambi ambao huficha uume ndani kabisa
kupinda kwa uume; shughuli za kushiriki ngono na mazoezi mbalimbali ambayo huumiza uume bila kujijua huleta makovu mengi ndani kwa ndani kwenye uume ambapo baadae uume ukishakua na makovu mengi hupinda kuelekea chini hata wakati ukiwa umesimama, yaani kama uume wako ujanani ulikua kama mshale sasa utakua kama upinde.
kuishiwa nguvu za kiume; tatizo hili linaathiri zaidi ya wanaume milioni 30 dunia nzima, katika hali ya ukuaji hali hii husababishwa na kupungua kwa kiasi cha damu ambacho kinaingia kwenye uume kila siku ukihitaji kuusimamisha sababu ya kuziba kwa mishipa ya damu na mafuta kama nilivyoeleza hapo juu, usitegemee nguvu zako za kiume ulizokua nazo ukiwa na miaka 18 utakuja kuzipata tena kwenye miaka 40.
saratani za sehemu hizo za siri; saratani mbalimbali kama saratani ya uume hasa kwa watu ambao hawajatailiwa, saratani ya korodani na saratani ya tezi dume. utafiti mpya unaonyesha kutoshiriki ngono kwa wanaume mara kwa mara kunaongeza nafasi ya kupata saratani ya tezi dume.baada ya miaka 30 ni vizuri kupima angalau mara moja kwa mwaka kuangalia kama kuna kansa imeanza.
kuchelewa kufika kileleni; mishipa ya fahamu ambayo inatoa taarifa kutoka kwenye uume kwenda kwenye ubongo huishiwa nguvu umri unavyozidi kwenda na hii humfanya muhanga kuchukua muda mrefu sana kufika kileleni swala ambalo linaweza kua baya au zuri kulingana na muhusika na hata akifika kileleni hutoa mbegu kidogo sana.
suluhisho; kuna mambo unaweza kufanya kuchelewesha au kupunguza kasi ya madhara haya ya ukuaji kwa kumeza vichochoe vya kutengeneza hormone ya testosterone mwilini mara kwa mara ambavyo huongeza nguvu za kiume,stamina, mbegu na kupunguza kasi yaa uume kua mwembamba, kufanya mazoezi na kula vizuri kuepusha kitambi na kushiriki mazoezi ya uume ambayo kwa watu wanaozidisha miaka 30 ni muhimu kua sehemu ya maisha yao ili kubaki na uume bora wenye afya..soma hapa kuona mazoezi ya uume http://www.sirizaafyabora.com/2015/06/pata-kitabu-cha-mazoezi-ya-kuongeza.html
                         
                                                         STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183