data:post.body ZIFAHAMU FAIDA NA HASARA ZA KUTUMIA DAWA ZA MITI SHAMBA.... ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

ZIFAHAMU FAIDA NA HASARA ZA KUTUMIA DAWA ZA MITI SHAMBA....

                                                                   

miti shamba ni nini?
huu ni utaalamu wa matibabu ya binadamu kwa kutumia mimea asilia inayopatikana sehemu mbalimbali, asilimia 25 ya dawa zinazotengenezwa viwandani hutokana na mimea asilia.
nchi zilizoendelea wataalamu wa matibabu haya wanasomea kabisa vyuoni na kupata degree za matibabu haya tofauti na hapa kwetu ambapo mtu yeyote anaweza akaibuka tu na kujiita daktari wa mitishamba, kwa mfano china kusomea udaktari huu wa mitishamba ni miaka mitano na mtu anayesomea lazima awe amaefaulu vizuri mtihani wa kidato cha sita.
miaka ya hivi karibuni watu wengi hapa nchini tanzania na duniani kwa ujumla wamegeukia dawa hizi na kupenda kuzitumia kuliko zile za hospitali ambazo nyingi hutengenezwa kiwandani.
dawa hizi zimekua zikipingwa sana na madaktari waliosemea elimu ya kisasa yaani madaktari wa kawaida japokua dawa zao nyingi zimetoka kwenye mimea kama nilivyosema hapo mwanzo..mfano kwinini za malaria, digoxin za kutibu moyo na na dawa za aspirini za maumivu ni dawa zinazotokana na magome ya miti..
leo ntaenda kuzungumzia faida na hasara za dawa hizi ili mtumiaji atumie akijua kabisa anapata nini kutoka huko na ntaanza na faida zake kama ifuatavyo...
dawa hizi hazina madhara madogo madogo wakati wa matumizi; mara nyingi dawa hizi za viwandani  zikitumika hua na madhara fulani fulani wakati wa matumizi kama kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na kadhalika lakini mitishamba watu wengi wameonyesha kuivumilia.
ni mbadala wa dawa za hospitalini; baadhi ya magonjwa ambayo wataalamu hua wanashindwa kuyapatia ufumbuzi wa moja kwa moja kuna baadhi ya mitishamba imeweza kuyatuliza japokua sio kuyatibu kabisa kama kuna dawa mbadala za presha, kisukari, pumu, kifafa na magonjwa mbalimbali yasiyotibika.
zinapatikana kwa wingi sana; dawa hizi ziko sehemu nyingi sana hasa bara la afrika na asia, na kwa mtu anayefahamu anaweza kupanda hata miche kadhaa nyumbani kwake au shambani na kuzitumia pale anapopata tatizo...nakumbuka nilipokua mdogo nilipakwa majani fulani yalikua yameota pembeni ya nyumba nikapona jipu bila hata kulipasua.
bei yake ni ya chini; tofauti na dawa za hospitali ambazo ni gharama sana kuzinunua, dawa za miti shamba ni bei nzuri kwa watu waaminifu lakini hapa kwetu tanzania wametokea watu wajanja wajanja na wanaziuza bei kali sana ambayo sio kawaida.utakuta dozi moja inauzwa laki tano mpaka milioni moja.

hebu tuone hasara za matumizi ya dawa hizi za mitishamba
hazifai kutumika kwa magonjwa mengi; kuna magonjwa mengi sana ya hatari ambayo dawa hizi haziwezi kutibu, magonjwa haya yanahitaji vipimo vya kisasa na matibabu ya kisasa ili kumpatia mgonjwa nafuu..kwa mfano mama aliyeshindwa kuzaa kwa kawaida lazima apasuliwe tu...mtaalamu wa mitishamba hawezi kufanya upasuaji wa aina yeyote, huwezi kuongeza damu wala kuongeza maji mwilini...
dawa hizi hazina dozi inayo eleweka; kuna hatari kubwa sana ya mtu kutumia zaidi ya inavyotakiwa kwani waganga wengi wa kienyeji kila mtu ana dozi yake tofauti na hospitali ambapo kuna viwango vya aina moja dunia nzima. mfano watu huchemsha na kunywa mwarobaini lakini hawajui ni kiasi gani cha kunywa...wao wanajali kunywa tu. watu wengi hawajui kwamba dawa hizi zina kemikali pia kama dawa za hospitali na kemikali zile haziko viwandani ila ziko kwenye mti wenyewe unaotibu, gome la mti wa kwinini ni kemikali hatari sana.
huingiliana na dawa za hospitali; ni vizuri kuacha mitishamba pale unapoamua kwenda hospitali au kuacha dawa za hospitali pale unapoamua kwenda kutibiwa na mganga wa miti shamba kwani dawa hizi huweza kuingiliana na kutengeneza sumu ya kuua mtu.
kukosa usimamizi wa dawa hizi; serikali haina kitengo cha kufuatilia ubora wa dawa hizi kama kweli zinafanya kazi au vipi na ukiamua kuzitumia ni kwa hatari yako mwenyewe tofauti na dawa za hospitali ambazo hukaguliwa sana ili zisidhuru watu.
kuuza vitu ambavyo si vyenyewe; tafiti nyingi zilizofanyika zilikuta chupa ya dawa ya mitishamba inayoandikwa kwamba ina dawa fulani ndani yake zilikutwa na dawa tofauti kabisa au unga ambao sio wenyewe. mfano hapa tanzania wataalamu walichukua supu ya pweza na kwenda kuipima ikakutwa imechanganywa na dawa za hospitali kwa jina la viagra.
vifo vya kuepukika; waganga wengi wa kienyeji wanaotumia dawa hizi za kienyeji hasa hapa kwetu sio waaminifu na wakweli...ukienda kwake na kansa inayoanza ambayo kimsingi ukiwahi hospitali inatibika atakuweka mpaka ufikie hali mbaya ndio akuache uende kufia hospitali lakini pia hudanganya watu kwamba wanaweza kutibu hata magonjwa yasiyotibika kama ukimwi, kisukari,kifafa,pumu na kadhalika lakini hakuna ushahidi wa mginjwa hata mmoja aliyetibiwa akapona......unaweza tembelea blog yetu ya kingereza kwa kubofya hapa  http://www.vibesinc.ga/                                    

                                                                    STAY ALIVE
                                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni