data:post.body Februari 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIKI NDIO CHANZO CHA KUPUNGUA UKUBWA WA UUME NA MATIBABU YAKE..

                                                                   
kupigwa na baridi au kuoga maji ya baridi husababisha uume kuaenekana mdogo na baridi ikiondoka uume hurudi kua vilevile, hii ni kawaida kwa wanume wote duniani lakini kuna baadhi ya mambo yanatokea kwa mwanume au ambayo mwanaume mwenyewe anayafanya yanaweza kumpunguzia ukubwa wa uume na kua mdogo na usirudi katika hali yake ya zamani.

je ukubwa wa uume kwa kawaida ukoje?
kwa hali ya kawaida uume unakua na vipimo vifuatavyo katika jamii nyingi duniani, vipimo hivi hutofautina wakati mwingine kutokana na nchi na nchi kwani wengine huweza kua zaidi ya hapa..
uume ukiwa umelala ni nchi 3.4 mpaka nchi 3.7 [au sentimita 8.6 mpaka 9.3]
uume ukiwa umesimama urefu wake ni nchi 5.1 mpaka nchi 5.7[ sentimita 12.9 mpaka 14.5]
uume ukiwa umesimama unene ni nchi 3.5 mpaka nchi 3.9[ sentimita 8.8 mpaka 10]

nini kinapunguza ukubwa wa uume?
wanaume wengi hawaridhiki na ukubwa wa uume wao hata kama ni mkubwa, na wengine wanaona kabisa uume umepungua ukubwa wakilinganisha na miaka iliyopita bila kujua sababu ya msingi lakini mambo yafuatayo yanaweza kufanya uume wa mtu ukapungua.
unene na kitambi; unene hufanya mafuta mengi kuongezeka tumboni na maeneo mengine ya uume, hii hufanya uume uonekane mdogo kuliko mwanzo hata ukiwa unaingia ukeni huzuiliwa na mafuta yaliyoota mwisho wa uume, lakini pia mafuta ya ndani ya mishipa ya damu ambayo yanazuia damu ya kutosha isifike kwenye uume husababisha uume usimame kwa shida sana na kua mdogo.
umri; umri wa mwanaume unavyozidi kua mkubwa uume pia huzidi kua mdogo hii husababishwa na kupungua kwa homoni za mfumo wa uzazi wa uume ambapo homoni hizi hizi ndio huufanya uume kua mkubwa kipindi mwanaume anabalehe kwa mara ya kwanza, lakini umri haupunguzi uume tu hata nyama za mwili wote kwa ujumla sababu ya kupungua kwa uwezo wa mwili kutengeneza seli mpya, ndio maana wazee wengi misuli ni midogo.
kutoshiriki tendo la ndoa kwa mara kwa mara; uume ni kama misuli mingine ya mwili, misuli inayofanya kazi mara kwa mara hua mikubwa na minene kama watu wanaofanya mazoezi ya kubeba chuma au watu wanaofanya kazi ngumu lakini misuli ikiwa haifanyishwi kazi hupungua ukubwa, hivyo kushiriki tendo la ndoa angalau mara nne kwa wiki husaidia.
ukoo; baadhi ya koo fulani unakuta familia nzima ina uume mdogo, hii husababishwa na homoni ya testesterone kwenye miili yao kushindwa kufanya kazi vizuri lakini pia baaadhi ya koo wamebarikiwa na maumbile makubwa.
upasuaji wa tezi dume; tafiti zimeonyesha kwamba upasuaji wa kuondoa tize dume husababisha uume kuingia ndani kidogo, utafiti huu ulifanyika nchini marekani kwa wanaume 126 ambao miezi kadhaa baada ya upasuaji huu walikiri kupungua kwa ukubwa wa uume.
kupiga punyeto au kujichua; uume ni kiungo laini sana ambacho hakitaki usumbufu kabisa ndio maana uke wa mwanamke una kuta laini sana ambazo haziwezi kuharibu uume, lakini unapotumia mikono yako kujichua unaumiza mishipa ya juu ya uume inayoingiza na kutoa damu lakini pia unaweza kusababisha makovu ya ndani ya misuli na kuzuia damu kufika kwa uhakika, hiki ni chanzo kikubwa cha kupungua ukubwa na nguvu za kiume kwa vijana wadogo ambao mara nyingi hujichua sana.
kuvuta sigara; kemikali ya nicotine iliyoko kwenye sigara huziba mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume, hii husababisha uume kukosa virutubisho na damu ya kutosha na kupungua ukubwa pamoja na nguvu zake.

suluhisho ni nini?
jambo la msingi sana ni kuzuia chanzo husika cha kupungua kwa uume kwa kuacha mambo ambayo yanasababisha uume wako kupungua kama ifuatavyo...
acha kupiga punyeto; najua kuacha kupiga punyeto sio swala dogo lakini naomba nikwambie kwamba kama hauchi kujichua unaendelea kujiua, soma hapa jinsi ya kuacha punyetohttp://www.sirizaafyabora.com/2014/11/hizi-ndio-njia-saba-za-kuacha-punyeto.html
punguza unene na kitambi; unene ni hali ambayo inaweza kuisha kama mtu akiamua kupungua, zipo program nyingi sana za kupungua uzito na kuisha kabisa kwa gharama za kawaida tu, soma hapa jinsi ya kupungua uzito.http://www.sirizaafyabora.com/2015/08/kama-umeshindwa-kabisa-kutoa-kitambi-na.html
acha kuvuta sigara; sigara ina addiction sana na sio rahisi kuiacha lakini kuna jinsi ya kuacha sigara ukiamua, soma hapa jinsi ya kuacha sigara kama wewe ni mvutaji.http://www.sirizaafyabora.com/2015/07/hizi-ndio-njia-kuu-kumi-za-kuacha.html
tumia virutubisho vya kuongeza homoni ya testosterone; kama wewe mwanaume uko zaidi ya miaka 40 na unaona uume wako umepungua kuliko zamani huenda homoni zako za testosterone zimeanza kushuka hivyo kuna virutubisho unaweza kutumia mara kwa mara ili kuweka kiwango cha homoni hizo kwenye kiwango cha kawaida.[tuwasiliane ukihitaji]
mazoezi ya kuongeza uuume; uume ambao hauna mazoezi au haushiriki tendo la ndoa mara kwa mara hupungua na kua mdogo kama nilivyosema hapo juu, hivyo unaweza kuufanya uume ue active kwa kufanya mazoezi ya uume ambayo yanaongeza damu kwenye uume na yamethibitika kuongeza ukubwa wa uume marudufu kwa watu ambao uume wao umepungua au ni mdogo tangu mwanzo..soma hapa kwa kujua zaidi mazoezi hayahttp://www.sirizaafyabora.com/2015/06/pata-kitabu-cha-mazoezi-ya-kuongeza.html
                                                             
                                                            STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

JE VIPIMO VYA UKIMWI VINASOMA BAADA YA MUDA GANI WA MAAMBUKIZI?

                                                                         
watu wengi hua na wasiwasi sana baada ya kulala na watu ambao tayari ni waathirika au kulala na watu ambao wanashutumiwa kwamba wameathirika...wengi wao huchangachikiwa na kutaka kupima siku hiyohiyo kujua kama wameambukizwa au vipi.
kimsingi vipimo vya ukimwi huanza kusoma positive[umeathirika] au negative[haujaathirika] kwanzia siku ya kumi mpaka miezi mitatu kulingana na kipimo kilichotumika na kinga ya mwili wa muhusika.
hivyo hata kama umeathirika tayari huwezi kujua mpaka muda fulani upite na kipindi hiki ambacho bado vipimo vitaonyesha huna, utakua na uwezo wa kuwaambukiza watu ambao sio waathirika, lakini pia kama ukitembea na mtu leo na ukaenda kupima leoleo ukajikuta ni muathirika basi virusi hivyo haukuvipata kutoka kwa mtu huyo wa siku hiyo.
vipimo mbalimbali huonyesha majibu kulingana na uwezo wake kama ifuatavyo...
rapid antibody test; hichi ni kipimo ambacho kinatumika mara nyingi kwenye vituo vyetu hapa tanzania mfano wa vipimo hivyo ni sd bioline, determine na unigold..kipimo hiki hupima askari wa mwili kitaalamu kama antibody ambao hutengenezwa na mwili kupambana na virusi vya ukimwi, mwili ambao haujaathirika hauwezi kutengeneza askari hawa.
wiki ya 4 mpaka wiki ya 6 watu wengi walioambukizwa huweza kugunduliwa kwa vipimo hivi japokua sio wote.
wiki ya 12 baada ya maambukizi zaidi ya asilimia 98 ya walioambukizwa watakua tayari wanaonyesha kwa kipimo hichi.
rapid antigen/antibody combination test; hichi ni kipimo ambacho kinagundua vimelea vya virusi vya ukimwi kitaalamu kama antigen na kugundua pia askari wanaotengenezwa na mwili kuulinda kupambana na ukimwi kitaalamu kama antibody.
siku ya 12 mpaka ya 26 vimelea hivi au antigen huweza kugundulika kwa kipimo hichi, siku ya 20 mpaka 25 askari wanaopambana na virusi hivi au antibody huweza kugundulika pia.[vipimo hivi havipatikani hapa kwetu na havipatikani kwenye hospitali zetu wala maduka ya madawa]
                                                         
rna test; vipimo hivi vinaona virusi moja kwa moja na vinatoa majibu kwa uhakika sana, kuliko nilivyotaja hapo juu...havipatikani sehemu nyingi sana duniani kwani ni gharama sana na vina uwezo wa kugundua muathirika siku ya 10 mpaka 14 baada ya kuambukizwa.
                                                           
polymerase chain reaction[pcr]; hichi kipimo pia hupima virusi moja kwa moja, hapa nchini kwetu vinatumika kupima kiasi cha virusi kwa waathirika kitaalamu kama viral load, kupima watoto waliozaliwa na mama muathirika kama wameambukizwa.
kipimo hichi husoma wiki ya 2 mpaka ya 3 baada ya maambukizi na hupatikana kwenye hospitali za rufaa tu hapa tanzania kama muhimbili, mbeya, kcmc na bugando...
                                                                     

mwisho; kujipima virusi vya ukimwi nyumbani kwa sheria za nchini kwetu ni kosa, kwani unaweza ukapata majibu mabaya bila kuandaliwa kisaikolojia kwa ushauri kwanza au unaweza ukapima vibaya ikaonekana umeathirika kumbe hujaathirika hivyo kama unataka kujua hali ya afya yako basi nenda ukapime kwenye vituo husika.

                                                            STAY ALIVE

                                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0653095635/0769846183

ZIFAHAMU FAIDA NA HASARA ZA KUTUMIA DAWA ZA MITI SHAMBA....

                                                                   

miti shamba ni nini?
huu ni utaalamu wa matibabu ya binadamu kwa kutumia mimea asilia inayopatikana sehemu mbalimbali, asilimia 25 ya dawa zinazotengenezwa viwandani hutokana na mimea asilia.
nchi zilizoendelea wataalamu wa matibabu haya wanasomea kabisa vyuoni na kupata degree za matibabu haya tofauti na hapa kwetu ambapo mtu yeyote anaweza akaibuka tu na kujiita daktari wa mitishamba, kwa mfano china kusomea udaktari huu wa mitishamba ni miaka mitano na mtu anayesomea lazima awe amaefaulu vizuri mtihani wa kidato cha sita.
miaka ya hivi karibuni watu wengi hapa nchini tanzania na duniani kwa ujumla wamegeukia dawa hizi na kupenda kuzitumia kuliko zile za hospitali ambazo nyingi hutengenezwa kiwandani.
dawa hizi zimekua zikipingwa sana na madaktari waliosemea elimu ya kisasa yaani madaktari wa kawaida japokua dawa zao nyingi zimetoka kwenye mimea kama nilivyosema hapo mwanzo..mfano kwinini za malaria, digoxin za kutibu moyo na na dawa za aspirini za maumivu ni dawa zinazotokana na magome ya miti..
leo ntaenda kuzungumzia faida na hasara za dawa hizi ili mtumiaji atumie akijua kabisa anapata nini kutoka huko na ntaanza na faida zake kama ifuatavyo...
dawa hizi hazina madhara madogo madogo wakati wa matumizi; mara nyingi dawa hizi za viwandani  zikitumika hua na madhara fulani fulani wakati wa matumizi kama kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na kadhalika lakini mitishamba watu wengi wameonyesha kuivumilia.
ni mbadala wa dawa za hospitalini; baadhi ya magonjwa ambayo wataalamu hua wanashindwa kuyapatia ufumbuzi wa moja kwa moja kuna baadhi ya mitishamba imeweza kuyatuliza japokua sio kuyatibu kabisa kama kuna dawa mbadala za presha, kisukari, pumu, kifafa na magonjwa mbalimbali yasiyotibika.
zinapatikana kwa wingi sana; dawa hizi ziko sehemu nyingi sana hasa bara la afrika na asia, na kwa mtu anayefahamu anaweza kupanda hata miche kadhaa nyumbani kwake au shambani na kuzitumia pale anapopata tatizo...nakumbuka nilipokua mdogo nilipakwa majani fulani yalikua yameota pembeni ya nyumba nikapona jipu bila hata kulipasua.
bei yake ni ya chini; tofauti na dawa za hospitali ambazo ni gharama sana kuzinunua, dawa za miti shamba ni bei nzuri kwa watu waaminifu lakini hapa kwetu tanzania wametokea watu wajanja wajanja na wanaziuza bei kali sana ambayo sio kawaida.utakuta dozi moja inauzwa laki tano mpaka milioni moja.

hebu tuone hasara za matumizi ya dawa hizi za mitishamba
hazifai kutumika kwa magonjwa mengi; kuna magonjwa mengi sana ya hatari ambayo dawa hizi haziwezi kutibu, magonjwa haya yanahitaji vipimo vya kisasa na matibabu ya kisasa ili kumpatia mgonjwa nafuu..kwa mfano mama aliyeshindwa kuzaa kwa kawaida lazima apasuliwe tu...mtaalamu wa mitishamba hawezi kufanya upasuaji wa aina yeyote, huwezi kuongeza damu wala kuongeza maji mwilini...
dawa hizi hazina dozi inayo eleweka; kuna hatari kubwa sana ya mtu kutumia zaidi ya inavyotakiwa kwani waganga wengi wa kienyeji kila mtu ana dozi yake tofauti na hospitali ambapo kuna viwango vya aina moja dunia nzima. mfano watu huchemsha na kunywa mwarobaini lakini hawajui ni kiasi gani cha kunywa...wao wanajali kunywa tu. watu wengi hawajui kwamba dawa hizi zina kemikali pia kama dawa za hospitali na kemikali zile haziko viwandani ila ziko kwenye mti wenyewe unaotibu, gome la mti wa kwinini ni kemikali hatari sana.
huingiliana na dawa za hospitali; ni vizuri kuacha mitishamba pale unapoamua kwenda hospitali au kuacha dawa za hospitali pale unapoamua kwenda kutibiwa na mganga wa miti shamba kwani dawa hizi huweza kuingiliana na kutengeneza sumu ya kuua mtu.
kukosa usimamizi wa dawa hizi; serikali haina kitengo cha kufuatilia ubora wa dawa hizi kama kweli zinafanya kazi au vipi na ukiamua kuzitumia ni kwa hatari yako mwenyewe tofauti na dawa za hospitali ambazo hukaguliwa sana ili zisidhuru watu.
kuuza vitu ambavyo si vyenyewe; tafiti nyingi zilizofanyika zilikuta chupa ya dawa ya mitishamba inayoandikwa kwamba ina dawa fulani ndani yake zilikutwa na dawa tofauti kabisa au unga ambao sio wenyewe. mfano hapa tanzania wataalamu walichukua supu ya pweza na kwenda kuipima ikakutwa imechanganywa na dawa za hospitali kwa jina la viagra.
vifo vya kuepukika; waganga wengi wa kienyeji wanaotumia dawa hizi za kienyeji hasa hapa kwetu sio waaminifu na wakweli...ukienda kwake na kansa inayoanza ambayo kimsingi ukiwahi hospitali inatibika atakuweka mpaka ufikie hali mbaya ndio akuache uende kufia hospitali lakini pia hudanganya watu kwamba wanaweza kutibu hata magonjwa yasiyotibika kama ukimwi, kisukari,kifafa,pumu na kadhalika lakini hakuna ushahidi wa mginjwa hata mmoja aliyetibiwa akapona......unaweza tembelea blog yetu ya kingereza kwa kubofya hapa  http://www.vibesinc.ga/                                    

                                                                    STAY ALIVE
                                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0653095635/0769846183

YAFAHAMU MADHARA 11 YA DAWA ZA UZAZI WA MPANGO

                                                                       
uzazi wa mpango sio kitu kibaya, wataalamu waligundua njia hizi ili kupunguza idadi kubwa ya watu hasa kwenye ngazi ya familia ambapo kuwahudumia inakua kazi sana...kwa dunia ya sasa hivi kuzaa watoto kwanzia watano kwenda mbele basi kuwasomesha na kuwatunza sio kazi rahisi.
zipo njia ambazo hazitumii dawa au kemikali zozote kwa mfano kondomu, kuchomoa uume kabla ya kufika kileleni, kalenda na kunyonyesha mtoto..hizi hazina madhara kabisa kwenye mwili wa binadamu lakini zipo zinazotumia kemikali ambazo zipo kwenye mfumo wa homoni kama za binadamu yaani oestrogen and progesteron.
homoni hizi zinapatikana kwenye mwili wa binadamu kama homoni za uzazi lakini kuna jinsi unaweza kuzitengeneza maabara ukampa mwanamke ili asipate mimba.
kwa hali ya kawaida ili upate mimba basi homoni hizi lazima ziwe kwenye kiwango maalumu..kupungua mwilini au kuongezeka mwilini kwa kiwango hichi cha homoni kunazuia mimba kabisa.
dawa hizi zinafanyaje kazi?
hufanya kazi kwa kuzuia yai la mwanaume kufika mwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke, huzuia yai kutengenezwa kutoka kwenye kiwanda cha mayai cha mwanamke[ovari], huzuia yai kushuka kutoka kwenye ovari kwenda kukutana na mbegu ya mwanaume. mfano wa dawa hizi ni zile za kumeza kila siku, kitanzi, sindano ya kila miezi mitatu na vijiti.
nini madhara ya kutumia njia hizi?
kuna madhara madogo madogo kama kichefuchefu, kutapika, kizunguzungu, matiti kuuma na kadhalika lakini kuna yale madhara makubwa ambayo ntaenda kuzungumzia leo.
kuongezeka uzito au kunenepa;  wanawake wengi wanaotumia dawa hizi ni wanene sana kuliko wale wasio tumia, tafiti zimeonyesha dawa hizi zinaongeza sana hamu ya kula na kumfanya mtumiaji ale sana kuliko kiwango cha kawaida lakini pia huzuia kiwango cha maji ya mwili kutoka nje kwa njia ya mkojo.
kuchelewa kupata uzazi; baadhi ya dawa za uzazi wa mpango huchelewesha sana mtu kubeba mimba baada ya kuziacha, mtu huweza kukaa mpaka miaka mitatu bila kubeba mimba wakati tayari ameshaacha dawa.mfano sindano
kupotea kwa hamu ya tendo la ndoa; kwasababu dawa hizi zinaenda kuvuruga mfumo wa kawaida wa homoni za mama, ambapo mfumo huo huo ndio unahusika kumpa mama hamu ya tendo la ndoa basi wanawake wengi hujikuta hawajisikii kushiriki kabisa tendo hili.
saratani ya kizazi; tafiti mpya zimeonyesha kuna mahusiano makubwa sana kati saratani ya kizazi na matumizi ya dawa hizi, wagonjwa wengi wa saratani ya kizazi walikua na historia ya kutumia dawa hizi.
chunusi; dawa za uzazi wa mpango ni msumeno unaokata mara mbili, wapo ambao wakitumia chunusi zote zinaisha kabisa na wapo ambao wakizitumia chunusi ndio zinaongezeka zaidi na hii yote ni sababu ya mabadiliko ya homoni.
saratani ya matiti; mabadiliko haya ya viwango vya homoni yanasababisha saratani ya matiti kwa watumiaji wengi wa dawa hizi japokua sio wote wataugua lakini inamuweka mtumiaji kwenye hatari hiyo.
presha, kiharusi na ugonjwa wa moyo; dawa za uzazi wa mpango zinagandisha damu ya mtumiaji, kuganda huku kunasababisha kuziba kwa baadhi ya mishipa ya damu hii huleta magonjwa ya moyo na presha.
mabadiliko ya maji maji ya uke; baadhi ya watu hujikuta wakitoa maji mengi sana kwenye uke wakati wa tendo la ndoa na wengine huweza kukaukiwa na maji hayo.
hasira; watumiaji wa dawa hizi wakati mwingine hua na mabadiliko ya maelewano na watu au mood, yaani mtu anaweza kuacha kuongea na wewe ghafla bila sababu yeyote au akapata haisira za ghafla wakati ulikua unaongea naye hapo nyuma.
maumivu ya kichwa na kushindwa kuona vizuri; baadhi ya watumiaji hujikuta wanapata maumivu makali ya kichwa na ya muda mrefu lakini pia dawa hizi huzuia maji ya mwili kutoka nje na kuongeza presha ya macho hii humfanya mtumiaji ashindwe kuona vizuri.
kukatika kwa nywele; dawa hizi zinasababisha nywele kukatika kwa baadhi ya watumiaji lakini sababu yake haifahamiki vizuri.
mwisho; makala hii hailengi kuwaambia watu waache kutumia dawa hizi, lengo ni kuwaonyesha madhara yake ili wazitumie huku wanajua au wahamie kwenye njia zingine salama zaidi, kwa waathirika wa madhara ya dawa hizi unaweza ukapata matibabu kulingana na tatizo ambalo limekupata baada ya kuzitumia...unaweza kututafuta kupata matibabu hayo.

                                                       STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 
                                               0653095635/0769846183

HIVI NDIO VYAKULA 11 VINAVYOPUNGUZA UNENE NA KUTOA KITAMBI..

                  
                                   
                                 
makala iliyopita nilizungumzia vyakula vinavyoweza kusababisha mtu kunenepa sana... kama hukuona makala hiyo soma hapa http://www.sirizaafyabora.com/2017/02/hivi-ndio-vyakula-10-vinavyonenepesha.html... katika vyakula hivyo nilivyozungumzia kuna ambavyo ni muhimu kuepuka kabisa kama soda, biskuti, ice cream na kadhalika kwani havina umuhimu kabisa mwilini na kuna vingine vya wanga kama wali,ugali,tambi,viazi,mihogo huwezi kuacha kabisa ila ni muhimu kupunguza na kula kwa kiasi kidogo sana kulingana na shughuli zako. kupunguza uzito kunataka nidhamu sana ndio maana watu wengi wameshindwa kupungua na kukata tamaa  lakini sheria kuu ni moja, mazoezi sana na kula kidogo..bila kubadilisha mfumo wako wa maisha na kula kidogo huku ukifanya mazoezi kwa nusu saa angalau mara tatu kwa wiki hata ule dawa gani unaweza ukapungua baadae ukarudi palepale. lakini pamoja na hayo kuna vyakula ambavyo ni muhimu sana kuvila wakati unapunguza uzito kwani vinasaidia kuchoma mafuta ya mwili lakini vyenyewe pia vina nguvu au calorie kidogo sana kiasi kwamba hata vikiliwa kwa kiasi kikubwa sio rahisi kunenepesha.
mayai; mayai ya protini nyingi sana ambazo zinamtosha kifaranga kutoka ndani ya yai hilo akiwa mzima. kawaida protini hujenga misuli ikiliwa kwa kiasi kinachotakiwa.utafiti unaonyesha binadamu wa kawaida anatakiwa ale mayai angalau matatu kwa siku kuondoa uwezekano wa kuongeza cholestrol ambazo ni hatari kwa moyo. ukiamka asubuhi ukala mayai kama sehemu ya kifungua kinywa chako utakaa muda mrefu bila njaa..mayai nayozungumzia hapa ni yale anayotaga kuku mwenyewe hasa ya kienyeji.
mboga za majani; hizi ni kama mchicha, bamia, nyanya chungu,kabichi, spinachi, kisamvu, msusa na zingine nyingi...mboga hizi zina vitamini nyingi, fibres au nyuzi nyingi na  wanga kidogo hivyo zinaweza kuliwa kwa kiasi kukubwa na kujaza tumbo bila kusababisha unene lakini pia zinaitwa kitaalamu kama antioxidant yaani zinaweza kuondoa sumu mwilini.
samaki; samaki wana kiasi kidogo sana cha mafuta, wana protein nyingi ambayo itakuacha muda mrefu ukiwa umeshiba na kukufanya usile sana...lakini pia samaki wana kemikali ya omega 3 ambayo ni muhimu sana kwenye mwili kwani huzuia magonjwa ya moyo na kusaidia kazi ya kuchoma mafuta.
maharage; hichi ni chakula kizuri sana cha asili ambachi kimewakuza watu wengi,  kina protini ya kutosha pamoja na fibre yaani nyuzi ambazo ni muhimu sana. lakini pia nguvu au calorie yake ni kidogo sana.
maparachichi; wakati matunda mengine yana sukari nyingi, parachichi zina mafuta na nyuzi ambazo ni muhimu sana kwa afya ya moyo na kupunguza uzito. maparachichi pia yana mafuta aina ya oleic oil ambayo yanapatikana kwenye mafuta ya mizaituni au olive oil  na hua yana maji mengi na kumfanya mlaji kutoishiwa maji mwilini.
karanga na korosho; japokua vyakula hivi vina mafuta, mafuta yake ni salama sana hayanenepeshi kama mfuta yatokanayo na wanyama...tafiti zinaonyesha kwamba mafuta haya huweza kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta mwilini.
                                                   
matunda; matunda yote unayofahamu yanapunguza uzito isipokua machache yenye sukari nyingi kama ndizi mbivu na zabibu..tafiti zimeonyesha watu wanaokula matunda mengi hua wanakula chakula kidogo sana sababu mafasi kubwa ya tumbo inachukuliwa na matunda ambayo hayaongezi uzito.                                                  
nyama ya kuku; hasa kuku wa kienyeji ambao wanakuzwa kiasilia, huwa na protein nyingi sana ambayo inajenga misuli badala ya kuongeza mafuta mwilini, kuku wa kisasa wana kemikali nyingi sana ambazo zinahusiana na magonjwa hatari kama kansa na kadhalika. kumbuka kama unakula kuku kupunguza uzito usile ngozi yake kwani ina mafuta mengi.
mafuta ya maji; mafuta yanayokuja kwa mfumo wa maji kama korie, mafuta ya nazi na alizeti ni mazuri sana kwani yakiingia mwilini hubaki kwenye mfumo ule ule lakini mafuta yanayokuja kwa mfumo wa kuganda kama kimbo, blueband na siagi sio mazuri kwani yakifika tumboni huganda vilevile.
viazi mviringo vya kuchemsha; japokua watu wengi hawataki viazi hivi na kuamua kuvikaanga kila wakati ili wale kama chips lakini ni chakula kizuri sana kama unataka kupunguza uzito..vina sukari kidogo na kiasi kikubwa cha potassium..
maziwa; tofauti na watu walivyokua wanafikiria zamani kuhusu maziwa kwamba yananenepesha sana, utafiti umeonyesha maziwa yanasaidia kupunguza uzito kwani yana kiasi kikubwa cha calcium ambacho husaidia kuchoma mafuta mwilini.
                                                                  
                                                                   
                                                              STAY ALIVE

                                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                              0653095635/0769846183

HIVI NDIO VYAKULA 10 VINAVYONENEPESHA ZAIDI NA KULETA VITAMBI...

                                                   
kumekua na tafiti nyingi zinzoonyesha vyakula vipi vinanenepesha watu zaidi duniani, japokua kila chakula kinategemea na kiasi unachokula lakini baadhi ya vyakula hunenepesha sana vinapoliwa na ni hatari kwa afya kwani huleta magonjwa kama kisukari, magonjwa ya moyo na saratani ambayo yanaongoza kuua watu wengi zaidi duniani kila mwaka. kama wewe ni mnene unataka kupungua, kama wewe ni mwembamba unataka kubaki hivyohivyo basi kaa mbali na hivi.
chipsi; hiki ni chakula kinacholiwa sana na watu duniani, kwani ni rahisi kuandaa na kukiuza na ukiwachunguza walaji wa chakula hichi  hua wana vitambi sana  au ni wanene..chips husababisha mazoea yaani addiction ambayo humfanya mlaji atamani kuzila kila siku na kunenepa zaidi kwani ukizila husikii kushiba na kula nyingi zaidi..
vinywaji vitamu; unywaji wa vinywaji vitamu sana kama soda na ice cream au kuweka sukari nyingi sana kwenye chai au juisi husababisha homoni ya insulini kutengenezwa nyingi sana, baada ya muda homoni hii inakua nyingi muda wote kwenye damu na kubadili sukari kua mafuta na kuiingiza ndani ya seli badala ya kuiacha itumike kwa kazi za kuupa nguvu mwili.
                                                       
nyama; ulaji wa nyama nyingi hasa  nyekundu yaani nyama za nguruwe, mbuzi na ngombe husababisha kuhifadhika kwa mafuta mengi sana mwilini na kuongezeka kwa lehemu au cholestrol ambayo ndio chanzo kikuu cha magonjwa ya moyo.kitaalamu mtu anatakiwa ale 70 gram ya nyama tu kwa siku sawa na finyango tatu tu ndogo lakini pia nyama hukaa masaa 20 kwenye mfumo wa chakula kabla ya kutolewa nje kama kinyesi.

viazi; viazi vitamu au viazi vya kawaida vinanenepesha sana bila kujali kwamba unavichemsha au unavikaanga kwani vina kiasi kikubwa sana cha nguvu au calories ambazo baadae hugeuka kua mafuta ndani ya mwili hivyo ulaji wake unatakiwa ue mdogo sana..
                                                               
                                                               
vyakula vya kukaangwa; vyakula vyote vya kukaangwa kama maandazi, vitumbua, chapati,sambusa, soseji,  nyama na mikaango yote unayofahamu hua na mafuta mengi ambayo mafuta hayo huingia mwilini na kumfanya muhusika awe mnene sana.
                                                       
juisi za viwandani na kuandaa nyumbani; hizi mara nyingi hua zina sukari nyingi sana ambazo kama nilivyoelezea hapo juu, sukari hii ni hatari sana na itakunenepesha tu. hakikisha unaandaa juice yako nyumbani na kuweka sukari kidogo na usinunue juice za viwandani au zinazouzwa vijiweni na mama ntilie kwani zina sukari nyingi sana.

mafuta ya kuganda; haya ni mafuta yanayoandaliwa na kua kama ya mgando...ulaji wa mafuta haya kwa mfumo wowote ule kama blue band, mayonise, kimbo au siagi hunenepesha na kuongeza kiasi cha lehemu au cholestrol  mwilini, mafuta hayo yakiingia mwilini huganda kama yalivyokua nje kabla haujayala...ni vizuri kuyaepuka na kutumia mafuta ya maji kama alizeti, korie na kadhalika..
pipi, biskuti, keki na chocolate; hivi ni vyakula ambavyo vinaonekana vina umbo dogo sana lakini vina kiasi kikubwa cha sukari na nguvu[calories] kiasi kwamba ukila inabidi ufanye mazoezi makali sana kuondoa mafuta yanayoingizwa mwilini na vyakula hivi.
                                                 
wali; wali unaopita kiwandani kurekebishwa na kuonekana mweupe zaidi, ni moja ya vyanzo vikuu vya unene na unaliwa sana dunia nzima na bei yake ni rahisi lakini hata huu wali wa kawaida tunaochukua mashambani unatakiwa uliwe kwa kiasi kidogo sana, angalau kikombe kimoja kidogo  cha wali uliopikwa kwa mlo mmoja...ukila zaidi ya hapo kitambi na unene huwezi kukwepa.
                                                         
tambi; ulaji wa tambi angalau mara moja au mbili kwa wiki hauna shida, tatizo linakuja pale mtu anapoamua kuzila kila siku..hapo unene hauwezi kukwepeka kwa mlaji huu kwani zenyewe zina wanga mwingi na pia huongezewa chumvi au sukari na kufanya vinenepeshe zaidi..
                                                               
mwisho; vyakula vya wanga ni chanzo kikuu cha unene ulipindukia duniani na ni vyakula vikuu vinavyoliwa na watu...ni vizuri kujenga tabia za kutokula wanga kila siku yaani sio lazima kila siku ule wali, ugali au viazi na mboga...unaweza ukala mboga tu kama dagaa, samaki,bamia, mboga za majani,matunda siku nzima bila kula wanga kabisa.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                               
                                                      STAY ALIVE

                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183

SABABU 10 KWANINI UACHE KUTUMIA SUKARI...

                                                                         


               
 sukari ni moja ya viungo vinavyyopendwa na kutumika sana dunia nzima, sukari inaweza kupatikana kiasilia mfano kwenye maziwa, matunda, asali, miwa, wali na kadhalika na nyingine ni  ile ambayo inatengenezwa kiwandani ili iweze kuungwa kwenye vyakula na vivywaji kama soda, biskuti, chocolate, chai, maandazi, keki, ice cream, pipi na kadhalika.
aina hii ya sukari ambayo inapatikana kwa kutengenezwa kiwandani ni hatari sana na moja ya vyanzo vikuu vya vifo duniani..
kuna aina tatu muhimu za sukari ambazo ni
glucose; hii ni sukari ambayo inatengenezwa na viumbe hai vyote vilivyoko duniani na hutupa nguvu kwa wingi lakini pia hutengenezwa viwandani.
sucrose; hii ni sukari kutoka kwenye mimea kama mahindi, ngano, miwa, uwele na kadhalika inatengenezwa na mimea lakini pia huweza kutengenezwa kiwandani au maabara.
fructose; hii ni sukari inayopatikana kwenye matunda, ni moja ya sukari hatari sana ikiliwa kwa kiasi kikubwa. kwa hali ya kawaida mtu hawezi kula matunda mpaka ikazidi mwilini lakini anaweza kula iliyotengenezwa kiwandani mpaka ikazidi mwilini.sukari tunayotumia majumbani ni mchanganyiko wa glucose na fructose.
watu wengi wamekua wakililia sukari pale inapokosekana au kupanda bei lakini naomba nikwambie kwamba kulilia sukari ni kulilia kifo kwani madhara yake yanatisha...hebu tuone hasara za sukari ile inayotengenezwa kiwandani au kuungwa kwenye vyakula...
inaharibu meno; sukari haina virutubisho au vitamini zozote, ukila sukari haupati faida yeyote kwenye mwili zaidi ya nguvu ambazo unaweza kuzipata kwenye vyakula vingine, lakini pia sukari hutengeneza mazingira mazuri mdomoni kwa bacteria kuweza kushambulia meno na kuyaharibu hivyo walaji wa kubwa wa pipi, biskuti, soda na kadhalika meno yao hutoboka sana.
ugonjwa wa maini; ugonjwa huu kitaalamu kwa jina la non alcoholic fatty liver disease unasababishwa na ulaji mwingi wa sukari ya aina ya fructuse ambayo hubadilishwa na mwili na kua mafuta...mafuta hayo hujazana kwenye maini na kusababisha magonjwa mengine ya maini kama saratani na kushindwa kazi kwa maini.
kushindwa kuacha au addiction; sukari ikitumika muda mrefu husababisha ubongo kumwaga homoni nyingi kwa jina la dopamine, homoni hii humfanya mtu azoee na kushimdwa kabisa kuacha matumizi ya aina fulani ya sukari..mfano kuna watu hawawezi kumaliza siku bila kunywa aina fulani ya soda kwani hawawezi kuvumilia ile kiu.
unene na vitambi; kama tulivyosema hapo mwanzo, sukari ikishaliwa, hubadilishwa na mwili kua mafuta na kuhifadhiwa mwilini...mwili unahifadhi sana mafuta tumboni na makalioni, mafuta haya ni hatari sana kwa afya ya mwili kiujumla..kama unataka kupunguza uzito leo, kitu cha kwanza ni kuacha kutumia sukari zote.
humfanya mtu ale sana chakula; tafiti moja zilifanyika zikagundua kwamba ulaji wa sukari ya aina ya fructose ni tofauti na ulaji wa glucose...ulaji wa vyakula vilivyoongezewa sukari ya fructose humfanya mtu asiridhike na chakula alichokula na hivyo atahitaji kula zaidi na zaidi...hii husababishwa na kuzuiliwa kwa homoni kitaalamu kwa jina la heptin, homoni huu hufanya kazi ya kutoa taarifa kwenye ubongo pale mtu anapokua ameshiba ili asiendelee kula, kushindwa kazi kwa homoni hii husababisha mtu ale sana kupitiliza...kama ni soda atakunywa nyingi zaidi, kama ni chakula atakula kingi zaidi, kama ni ice cream atakula nyingi zaidi na kadhalika...
saratani mbalimbali; tafiti zilizofanyika zimeonyesha kwamba kuna mahusiano makubwa sana kati ya kula sukari na kupata kansa...kwanza sukari husababisha homoni aina ya insulini ambayo inatumika kuvunja sukari kua juu sana muda wote na kusabababisha kansa lakini pia sukari huumiza baadhi ya mifumo ya mwili na kuleta kansa.
magonjwa ya moyo; kwa miaka mingi watu wamekua wakilaumu ulaji wa nyama nyekundu kua chanzo kikuu cha magonjwa ya moyo kwa kutengeneza aina fulani ya mafuta kitaalamu kama very low density lipoprotein ambayo huziba mishipa ya moyo..sukari aina ya fructose imegundulika  ikilika nyingi husababisha kuongezeka sana kwa mafuta haya na ni hatari sana kuliko nyama.
ugonjwa wa kisukari; ulaji wa sukari nyingi husababisha homone insulini ambayo ianahusika kuingiza sukari ndani ya seli ili tupate nguvu kushindwa kufanya kazi..hii husababisha kuwepo kiwango kikubwa sana cha sukari kwenye damu ambacho hupelekea kuanza kwa ugonjwa wa kisukari..ugonjwa huu huleta madhara makubwa kama upofu, kiharusi, na kushindwa kufanya kazi kwa moyo.
ugonjwa wa chunusi; utafiti uliofanyika mwaka 2008 uligundua kwamba ulaji wa sukari husababisha kuongezeka kwa ugonjwa wa ngozi wa chunusi sababu ya mafuta yanayopatikana sukari inapohifadhiwa mwilini..mafuta haya husiba matundu ya ngozi na kuleta chunusi.
hatari ya fangasi za mwili;
hatari ya fangasi mwilini; uwepo wa sukari nyingi mwilini husaidia fangasi kushambulia na kugawanyika haraka sana mwilini.
mwisho; mbadala mzuri wa sukari ni asali, asali ina sukari ambayo inapatikana kiasilia bila kupita mikononi mwa binadamu...lakini pia ina uwezo wa kuharibu kemikali na sumu kali za mwili ambazo zinaleta kansa..ni vizuri kuanza kutumia asali kwenye chai yako badala ya sukari lakini pia kuachana na ulaji wa sukari ambazo hazina faida mwilini mwako ambzo huongezwa kwenye vyakula mfano maandazi, keki, soda, biskuti, chocolate na vitamu vyote unavyovihamu.
unaweza tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                         STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                            0653095635/0769846183
[karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]

JE UBIKRA UNAPIMWA VIPI?

                                                          

kipimo cha ubikra ni kipi?
hichi ni kipimo kinachotumika kupima kama mwanamke bado hajawahi kushiriki ngono na mwanaume yeyote tangu azaliwe.
vipimo hivi hufanyika mara kwa mara kwenye jamii za watu fulani fulani ambazo bikra huaminika kama ndio kipimo cha usafi na tabia nzuri kabla ya ndoa, nchini south africa vipimo hivi hufanyika kabla ya kupeleka wasichana kwenda kusoma nje ya nchi lakini pia kujaribu kuzuia maambukizi ya ukimwi ambayo yako juu sana nchini humo.
nchini misri mahakama kuu ya nchi hiyo iliamuru jeshi kuwapima wasichana wote bikra kabla hawajajiunga na jeshi la nchi hiyo.
lakini vipimo hivi vimepingwa sana na watetezi wa haki za binadamu wakidai kwamba vinashusha na kuaibisha utu wa mwanamke, baadhi ya watu kama wahindi na waarabu wamejikuta wakishiriki ngono kinyume na maumbile ili kuzuia bikra isitoke kabla ya ndoa.
mara nyingi bikra hii hupimwa kwanzia miaka sita mpaka umri wa kuweza kufunga ndoa katika jamii hizo, lakini pia hapa kwetu bado jamii inawaona mabikra ni watu wenye tabia nzuri kuliko hawa wengine.

bikra inapimwa vipi?
kipimo kinachoitwa kitaalamu kama two fingers virginity test ndio kinachotumika kuwapima wanawake hawa ubikra, mara nyingi madaktari hutumika kufanya vipimo hivi.
vidole viwili huingizwa ndani ya uke kuangalia ile ngozi laini kwa jina la hymen ambayo inaaminika kutoka na kuchanika mwanamke anaposhiriki ngono kwa mara ya kwanza, wakikuta ile ngozi haipo basi mwanamke huyo sio bikra na wakikuta ngozi ile ipo basi mwanamke huyo ni bikra.
mpaka sasa hivi hakuna mashine maalumu au kifaa maalumu kinachoweza kusema kwa uhakika kwamba mtu huyu ni bikra.
lakini pia baadhi ya makabila huweka shuka nyeupe kwenye kitanda siku ya ndoa, damu ikimwagika basi huamini mtu huyo alikua bikra.
sio rahisi kupima kama mwanaume ni bikra kwani wote wako sawa kimaumbile yaani mabikra na ambao sio mabikra.

changamoto za kipimo hichi ni zipi?
ngozi laini inayopimwa kutambua ubikra inaweza kuondolewa na baiskeli, kuendesha farasi au kufanya mazoezi mazito ya kukimbia na kuruka kamba, sasa mtu huyo anaweza kupoteza ngozi ile lakini kitaalamu yeye bado ni bikra kwani hajawahi kulala na mwanaume.
wasichana wengine huzaliwa na ile ngozi ikiwa ndogo sana kiasi kwamba hata siku ya ngono kwa mara ya kwanza damu zinaweza zisitoke kabisa lakini mwanamke huyu bado ni bikra.
baadhi ya wanawake ile ngozi inaweza kua ngumu sana na ikashindwa kutoka wakati wa ngono, kumbuka ngozi ile haizibiki kabisa tundu ndio maana damu za kila mwezi zinatoka hata kama mwanamke ni bikra.

je bikra inaweza kurudi baada ya kutoka?
ndio njia pekee ya kurudisha bikra ni kufanya upasuaji wa kuishona tena ile ngozi ya ndani ambayo inatambulika kama kipimo cha bikra, ngozi ile hushwona na baada ya mwezi mmoja hupona na mwanamke hua kama bikra tena. njia hizi wamekua wakitumia wanawake wanaotaka kuolewa haraka.                                          

je bikra inaweza kutoka bila maumivu?
kama wewe ni bikra na unashindwa kutoa bikra yako sababu ya maumvu makali basi kuna mabo ya kufanya kuzuia maumivu hayo, kwanza nunua mafuta maalumu kwa jina la k gel ambazo hulainisha zaidi uke kuruhusu uume kupita, pia kuna dawa za nganzi za kupaka kwa jina la lidocaine cream ambazo zikipakwa saa moja ndani ya uke kabla ya tendo hupunguza maumivu kwa kiasi kikubwa sana.                          

     
                                                     STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                       0653095635/0769846183

karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]