data:post.body ZIFAHAMU DAWA 3 ZINAZOTUMIKA KUACHISHA WATU POMBE ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

ZIFAHAMU DAWA 3 ZINAZOTUMIKA KUACHISHA WATU POMBE

                                                           
je unataka kuacha pombe lakini unashindwa? basi angalia jinsi ya kupata msaada. siku hizi kuna dawa zimeingia kwenye soko la dawa ambazo zinaweza kukusaidia kuacha pombe, dawa hizi hazikuachishi pombe lakini zinaleta hali ambayo utajikuta hupendi kunywa pombe yaani ukinywa huoni raha tena.
matibabu haya yanatakiwa yaende na nja zingine za kucha pombe kama ushauri, kuamua moyoni kuacha, kuomba msaada kwa marafiki, kukaa mbali na wanywaji, kuepuka kukutana bar na rafiki zako na kadhalika.
zifuatazo ni dawa husika za kuacha pombe
disulfiram; hii ni dawa ya kwanza kabisa iliyogunduliwa ya kuwafanywa watu kuacha pombe, inafanya kazi kwa kuzuia mwili kuondoa pombe mwilini baada ya kunywa na matokeo yake mtu huweza kukaa na hang over kwa muda wa mpaka wiki mbili.
mtu hujisikia kichwa kuuma, kutapika, kuishiwa nguvu, kuchanganyikiwa, kutokwa jasho sana, kupumua kwa shida, na kushindwa kuona vizuri kila anapokunywa. mtumiaji hutapaika sana kama mtu aliyekunywa sumu kila akigusa pombe. hali hii humfanya mtu aiogope pombe kabisa.
                                                       
naltrexone; hii ni dawa ambayo inafanya kazi kwenye ubongo, kitaalamu kuna sehemu ya ubongo ambayo hupata raha mtu anavyoendelea kunywa pombe...dawa hii huzuia sehemu hiyo ya raha na kumfanya mtu asione raha yeyote kunywa pombe.
watu wengi hunywa pombe sababu kuna raha wanaipata wakati wanakunywa pombe hivyo wakiikosa raha hii hulazimika kuacha. dawa hii haina madhara ya kutapika kama ile ya mwanzo, dawa hii huchomwa kama sindano kwa mnywaji kila baada ya muda fulani mpaka atakapoacha kabisa.
acamprosate; mtu ambaye amezoea pombe hawezi kuacha ghafla kwani anakua ameshaizoea mwilini kitaalamu kama addiction hivyo akiacha ghafla hupata matatizo ambayo yanaitwa kitaalamu kama withdraw syndrome ambayo mtu huapata dalili za wasiwasi, kutetemeka,kukosa usingizi, na kutokwa na jasho, sasa dawa hii humsaidia huyu mtumiaji arudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kuacha pombe bila kupata hayo madhara niliyotaja.

mwisho; dawa hizi hupewa kwa watu tu ambao wako tayari kuacha pombe na mgonjwa asiwekewe kwenye pombe yake au kunyweshwa bila mwenyewe kujua kwani hiatamsaidia. kabla ya kuanza dozi ni vizuri daktari aliyekaribu na mgonjwa afahamu ili kama madahara ya dawa yakiwa makubwa aweze kumsaidia muhusika.

                                                           STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183
                                                            


0 maoni:

Chapisha Maoni