data:post.body JE KIPIMO CHA MIMBA KINASOMA BAADA YA MUDA GANI? ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JE KIPIMO CHA MIMBA KINASOMA BAADA YA MUDA GANI?

                                                                 

muda gani mzuri wa kupima mimba ni upi?
unapotaka kubeba mimba au unapokua na wasiwasi kwamba umepata mimba, mara nyingi hua ni changamoto kwa wasichana kwani wengi wao hujikuta wanapima siku hiyohoyo au kesho yake kuangalia kama mimba imeingia kitu ambacho hata kwa vipimo vya kisasa zaidi huwezi kupata majibi sahihi kwa muda mfupi hivyo.
muda mzuri wa kupima mimba kwa uhakika zaidi ni pale unapokosa siku zako za hatari za mwezi unaofuata, kipindi hiki zile homoni ambazo kitaalamu ndio zinasomwa kwenye mkojo mtu akiwa na mimba kwa jina la human chorionic gonadotrophin hormone zinakua tayari ziko za kutosha hata kwa vile vipimo ambavyo havina nguvu sana vinasoma kwa uhakika.

muda unaotumika kwa kipimo kusoma inatofautiana kwa wanawake tofauti..
wakati unataka kupima mimba unatakiwa ujue kwamba wanawake wanatofautiana sana wao kwa wao kutokana na urefu wa mizunguko yao yaani wengine mizunguko mirefu na wengine mfupi.
yai la mwanamke na mbegu ya mwanaume vinapokutana huchukua siku saba mpaka kumi kuweza kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi, baada ya hapo baada ya siku mbili mpaka tatu ndio mimba inaweza kusoma...hivyo kwa ujumla tunasema inaweza kuchukua siku 14 mpaka siku 21 kusoma kama mimba imeingia au haijaingia baada ya kulala na mwanaume. wanawake wengine hutokwa na damu kidogo mimba inapojishikisha kwenye ukuta wa uzazi kitaalamu tunaita implantation bleeding, damu hii hua inakua kidogo sana kuliko ile ya kawaida ya hedhi lakini kipindi hiki mimba inakua bado haijasoma kwenye kipimo.

unatakiwa upime saa ngapi?
kila unavyopima kipimo cha mkojo, unakua unapima homoni ya human chorionic gonadotrophin hormone ambayo nimeitaja hapo juu.
muda mzuri ambayo homoni hiyo inaonekana ni asubuhi, hivyo zingatia kupima mimba asubuhi kwa majibu mazuri zaidi, wakati mwingine ukipima mchana unaweza kuona mistari ambayo inafifia yaani haina rangi nyekundu ya kutosha.
                                                             
                                                          STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183

Maoni 13 :

 1. Mimi tumbo linauma hasa kwenye nyonga

  JibuFuta
 2. Habari mimi ni lienda hospital nilikua sipati period na pia nimeolewa nilikua natamani kupata mtoto miezi ya nyuma nilienda hospital nilipata matibabu na period yangu nilipata mwenzi wa kwanza vinzuri hila niliandikiwa dawa zinaitwa clomid mwenzi wa pili nilitumia hizo dawa kawaida period yangu ni siku 5 hila nilipo tumia nilipata siku 3 nilikaa mpaka siku ya hatali nikakutana na mme wangu, hilipita wiki 2 nikaaza kuisi kichefu chefu, kuchoka, usingizi, kuchagua chakula, pia naona mabadiliko ya mwili haswa tumbo chini ya kitovu linakua gumu nilienda kununua kipimo cha mimba kikaja kimstali kimoja roho hiliniuma nikakata tamaa hila mpaka sasa Nina wiki 5period sijapata nakua mchovu2,na tumbo chini nigumu kiasi hila kuna mdaa siuisi hila nikitembea nasikia maumivu chini ya kitovu je nimimba?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Nimimba lakini mbona ikipimwa kipimo hakisomi positive?

   Futa
 3. Habari mimi ni lienda hospital nilikua sipati period na pia nimeolewa nilikua natamani kupata mtoto miezi ya nyuma nilienda hospital nilipata matibabu na period yangu nilipata mwenzi wa kwanza vinzuri hila niliandikiwa dawa zinaitwa clomid mwenzi wa pili nilitumia hizo dawa kawaida period yangu ni siku 5 hila nilipo tumia nilipata siku 3 nilikaa mpaka siku ya hatali nikakutana na mme wangu, hilipita wiki 2 nikaaza kuisi kichefu chefu, kuchoka, usingizi, kuchagua chakula, pia naona mabadiliko ya mwili haswa tumbo chini ya kitovu linakua gumu nilienda kununua kipimo cha mimba kikaja kimstali kimoja roho hiliniuma nikakata tamaa hila mpaka sasa Nina wiki 5period sijapata nakua mchovu2,na tumbo chini nigumu kiasi hila kuna mdaa siuisi hila nikitembea nasikia maumivu chini ya kitovu je nimimba?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Samahani ulipata majibu au utatuzi maana hilo swala ndio ninalo japo mm nina watoto

   Futa
 4. habari...me naomba kuulza et km una uti alaf ukatumia kipimo cha UPT kupima ujazito kinaweza kuonesha unaujazito hata km huna??

  JibuFuta
 5. Nilitakiwa niingie p tarehe 8 ILa app ya my tracker inaonesha tarehe 6 cjaingia je naweza pima na hcho kipimo ikaonekana?

  JibuFuta
 6. Mm tumb linan uma chin ykitovu naxkia kit kinan chezsch

  JibuFuta
 7. Je unaweza kupima mimba Ina siku 21 na isionekane ?

  JibuFuta