data:post.body Januari 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

JE KIPIMO CHA MIMBA KINASOMA BAADA YA MUDA GANI?

                                                                 

muda gani mzuri wa kupima mimba ni upi?
unapotaka kubeba mimba au unapokua na wasiwasi kwamba umepata mimba, mara nyingi hua ni changamoto kwa wasichana kwani wengi wao hujikuta wanapima siku hiyohoyo au kesho yake kuangalia kama mimba imeingia kitu ambacho hata kwa vipimo vya kisasa zaidi huwezi kupata majibi sahihi kwa muda mfupi hivyo.
muda mzuri wa kupima mimba kwa uhakika zaidi ni pale unapokosa siku zako za hatari za mwezi unaofuata, kipindi hiki zile homoni ambazo kitaalamu ndio zinasomwa kwenye mkojo mtu akiwa na mimba kwa jina la human chorionic gonadotrophin hormone zinakua tayari ziko za kutosha hata kwa vile vipimo ambavyo havina nguvu sana vinasoma kwa uhakika.

muda unaotumika kwa kipimo kusoma inatofautiana kwa wanawake tofauti..
wakati unataka kupima mimba unatakiwa ujue kwamba wanawake wanatofautiana sana wao kwa wao kutokana na urefu wa mizunguko yao yaani wengine mizunguko mirefu na wengine mfupi.
yai la mwanamke na mbegu ya mwanaume vinapokutana huchukua siku saba mpaka kumi kuweza kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi, baada ya hapo baada ya siku mbili mpaka tatu ndio mimba inaweza kusoma...hivyo kwa ujumla tunasema inaweza kuchukua siku 14 mpaka siku 21 kusoma kama mimba imeingia au haijaingia baada ya kulala na mwanaume. wanawake wengine hutokwa na damu kidogo mimba inapojishikisha kwenye ukuta wa uzazi kitaalamu tunaita implantation bleeding, damu hii hua inakua kidogo sana kuliko ile ya kawaida ya hedhi lakini kipindi hiki mimba inakua bado haijasoma kwenye kipimo.

unatakiwa upime saa ngapi?
kila unavyopima kipimo cha mkojo, unakua unapima homoni ya human chorionic gonadotrophin hormone ambayo nimeitaja hapo juu.
muda mzuri ambayo homoni hiyo inaonekana ni asubuhi, hivyo zingatia kupima mimba asubuhi kwa majibu mazuri zaidi, wakati mwingine ukipima mchana unaweza kuona mistari ambayo inafifia yaani haina rangi nyekundu ya kutosha.
                                                             
                                                          STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183

HUU NDIO UPASUAJI WA KUIRUDISHA BIKRA KWA MWANAWAKE[HYMENNORAPHY]

                                                             
                                                                       
                   
                                                               
bikra ni nini?
hii ni ngozi laini sana inayofunika uke kwa wanawake ambao hawajawahi kushiriki ngono kabisa, kikawaida mwanamke anaacha kuitwa bikra pale ngozi hii inapoondolewa.... ngozi hii kitaaamu inaitwa hymen.

hymenorrhaphy ni nini?
huu ni upasuaji unaofanyika kuirudisha bikra ya mwanamke ambayo imeshatoka tayari kwa sababu mbalimbali.
aina hii ya upasuaji mara nyingi hazipatikani kweye hospitali za kawaida kwani hazina umuhimu wowote kwenye matibabu na zinaweka kwenye kikundi cha plastic au cosmetic surgery,hivyo mara nyingi hufanyika kwenye hospitali au clinic binafsi na mabingwa wa magonjwa ya akina mama yaani gynacologist..
idadi ya wanawake wanaofanyiwa aina hizi za upasuaji inazidi kuongezeka miaka inavyozidi kwenda mbele kutokana na watu kuanza ngono mapema sana.
                                                             
 watu gani wanatakiwa wafanyiwe aina hizi za upasuaji?
wanawake ambao wanataka kurudisha bikra zao ambazo zimeshatoka wanatakiwa kufanya upasuaji huu kwani hakuna dawa yeyote inayoweza kurudisha bikra na ukiisikia ujue ni utapeli.
katika hali ya kawaida bikra inaweza kutoka kwa kushiriki ngono, kupata ajali na kuumia, tabia ya kujichua, mazoezi kama kuendesha baiskeli au farasi, matumizi ya aina fulani za pedi  au magonjwa fulani fulani.
wakati mwingine ngozi ila ya bikra inaweza kua ngumu sana kiasi kwamba ikakataa kuchanika hata kwa kuingiliwa kingono. hivyo mwanamke kutotoka damu wakati wa ngono kwa mara ya kwanza haimaanishi kwamba mwanamke sio bikra.

kwanini wanawake wanafanya aina hizi za upasuaji?
wanawake hua wanasababu mbalimbali kama ifuatavyo

  • kuwaonyesha wanaume zao au jamii zao kwamba wao ni mabikra kipindi cha ndoa hasa kwenye jamii fulani fulani ambazo bikra ni muhimu sana siku ya ndoa.
  • kuwasaidia wenye maumivu ya kisaikolojia baada ya kubakwa, hii inawafanye wapate amani kidogo baada ya upasuaji huu.
  • kurudisha bikra ambayo imeharibika sababu ya kuumia kwa ajari.
upasuaji huu unafanyikaje?
hii ni aina ya upasuaji mdogo ambayo inafanyika kwa kuchoma sindano ya ganzi tu na wala haihitaji kwanamke kupewa dawa za usingizi, japokua kuna wakati mwingine kutokana na mazingira ya mgonjwa daktari anaweza kulazimika kutoa dawa ya usingizi.
kuna aina tatu za upasuji za kurudisha bikra kama ifuatavyo.
  1. kuishona tena ngozi ile ya ya hymen ambayo inamfanya mwanamke aitwe bikra kwa kuirudisha pamoja na kuiacha ipone kisha kurudi kama zamani
  2. kuweka ngozi ya hymen ya bandia na kuishonea pale kisha kuweka ndani yake aina fulani ya kimiminika kinachofanana kabisa na damu ili damu ionekane ikitoka  wakati wa ngono
  3. kuikata ngozi ya hymen ambayo ilichanika mwanzoni na kuitoa nje kisha kuirudishia upya na kuishona kabisa kama mwanzo.
wanawake wanaofanya aina hii za upasuaji wanatakiwa wafahamu kwamba wanatakiwa wakae bila kushiriki ngono wiki tatu mpaka miezi mitatu ili bikra ishike vizuri hivyo ni vizuri kuifanya mapema kabla ya ndoa sio unataka ufanyiwe leo afu wiki ijayo uolewe.
nyuzi zinazotumika kushona ngozi ile ya bikra hua haziondolewi yaani baadae huyeyuka ndani kwa ndani.

madhara ya upasuaji huu
upasuaji huu ni salama kabisa ila hua una madhara madogo madogoambayo ni kawaida hata kwa uparesheni zingine kama ifuatavyo.
kutokwa damu; hii ni kawaida hata kwa uparesheni zingine lakini damu hii inatakiwa ikauke na kuondoka baada ya siku chache.
kubana sana; wakati mwingine daktari anaweza akaishona ngozi ile na kuibana sana kiasi kwamba ikawa ngumu sana siku ya kuitoa wakati wa kushiriki ngono. hua na maumivu makali ambayo huisha bila dawa yeyote baadae.
infection; hii husababishwa na kushambuliwa na bacteria baada ya upasuaji lakini huweza kuzuiliwa kwa kupewa dawa za kuzuia hali hii mfano antibiotics

mwisho; aina za upasuji hizi zinapatikana nje ya nchi kwa wingi, kwa nchini tanzania na afrika kwa ujumla zipo pia lakini ni sehemu chache sana.
dunia inakwenda kwa kasi sana hivyo mwanaume ukijikuta umeoa bikra mwenye watoto wanne usishangae...
pia unaeza tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                       STAY ALIVE

                                  DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183

                                                   





ZIFAHAMU DAWA 5 ZINAZOTUMIKA KUWAACHISHA WATU SIGARA.

                                                                         
moja ya vitu vigumu zaidi kuacha duniani ni sigara, ni watu wachache sana wenye juhudi kubwa hufanikiwa kuacha sigara kutokana na kiasi cha kemikali ya nicotine kilichoko ndani ya sigara ambacho kinamfanya mtumiaji apate kiu kali ya kutaka kuvuta sigara pale anapojaribu kuacha. ukiwa unaanza kuvuta sigara huwezi ukajua kua ipo siku utakuja kua mtumwa wa sigara lakini baada ya miaka kadhaa ndio utagundua kwamba umekua mtumwa na kuacha huwezi..
watafiti wamejitahidi kutafuta suluhisho la sigara na kugundua baadhi ya dawa , pamoja na kutumia dawa hizi mtumiaji lazima pia atumie njia kadhaa za kuacha ambazo sio za dawa kama kuamua moyoni kwamba ameamua kuacha, kukaa mbali na wavutaji sigara, kuanza mazoezi yeyote ya mwili ambayo kimsingi husaidia sana kuponya addiction, kula vizuri na kupumzika, kuepuka kutumia vilevi vyovyote ambavyo vitamrudisha huko na hata kuonana uso kwa uso na mshauri wa afya.
dawa zifuatazo zimesaidia baadhi ya watu kujikomboa na uvutaji wa sigara
bupropion; hii ni dawa ya mgandamizo wa mawazo ambayo pia hutumika kutibu watu wanaotaka kuacha sigara, hufanya kazi kwa kuondoa kiu kali ambayo huipata pale tu anapoacha sigara. mgonjwa hutumia dozi ya 100mg kutwa mara tatu huku akiendelea kuvuta sigara kisha wiki ya pili mgonjwa huacha sigara na kuendelea na dawa hizi angalau kwa muda wa wiki saba.
nicotine; hii ni kemikali inayopatikana ndani ya sigara ambayo inamfanya mtumiaji wa sigara ashindwe kuacha, hivyo wataalamu wameichukua kemikali hii na kuiweka kwenye jojo au big g ili mtumiaji aweze kuila kwa kutafuna jojo hizi kama mbadala wa sigara na baada ya muda fulani apunguze dozi ya jojo hizi mpaka pale atakapokua ameacha kabisa na mwili kuzoea kuisha bila nicotine. hutakiwi kutumia zaidi ya jojo 20 kwa ndani ya saa 24.
clonidine; hii ni dawa inayotumika kutibu presha ya kupanda lakini pia imethibitika kwamba inasaidia watu kuacha kuvuta sigara, matumizi yake ni kidonge kimoja kutwa mara mbili....unaweza kuanza kutumia dawa hii siku ya kuacha au siku tatu kabla ya kuacha na kuendelea nayo huku ukipunguza dozi kwa siku nne mpaka tano. hutakiwi kuacha dawa hii ghafla kwani huweza kupandisha presha ghafla.
varenicline; baadhi ya watafiti wanahisi dawa hii inafanya kazi kuliko dawa nyingi za kuacha sigara, hufanya kazi kwenye ubongo kwenye sehemu inayoitwa kitaalamu kama nicotine receptors kwa kumfanya mtumiaji asione raha kuvuta sigara lakini pia huondoa ile kiu mtumiajia anayoipata pale anapokosa kuvuta sigara. matumizi yake ni wiki mbili kabla ya kuacha sigara na kidonge kimoja humezwa na maji mengi baada ya kula. dawa hii huendelea kutumika mpaka wiki 12 na zaidi ili kumsaidia mtumiaje aache kabisa.
notriptyline; hii ni dawa inayotumika kutibu mgandamizo wa mawazo, ambayo pia husaidia kutuliza ile kiu mtu anayoipata anapokosa sigara. huanza kutumiaka siku 10 mpaka 28 kabla ya kuacha kuvuta sigara..dawa hii hupunguza uwezo wako wa kutumia mashine yeyote ya moto kwa kipindi hiko.. ni vizuri usitumie mashine yeyote ya moto au kuendesha gari.
mwisho; dawa hizi zina madhara madogo madogo na makubwa kama ilivyo kwa dawa zingine, ni vizuri kabla ya kuanza kuzitumia au kuzinunua uonane na daktari ili ujue kama wewe zinakufaa kwani kuna baadhi ya dawa hazifai wagonjwa fulani fulani kama wa moyo, kisukari au madonda ya tumbo. bahati mbaya hata kuzipata hapa nchini kwetu ni changamoto kidogo lakini kwa watanzania walioko nje wanaweza kuzipata hata watanzania wa ndani ya nchi wanaweza kuagiza nje kama wanaweza.
                                                         STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183
karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]

ZIFAHAMU DAWA 3 ZINAZOTUMIKA KUACHISHA WATU POMBE

                                                           
je unataka kuacha pombe lakini unashindwa? basi angalia jinsi ya kupata msaada. siku hizi kuna dawa zimeingia kwenye soko la dawa ambazo zinaweza kukusaidia kuacha pombe, dawa hizi hazikuachishi pombe lakini zinaleta hali ambayo utajikuta hupendi kunywa pombe yaani ukinywa huoni raha tena.
matibabu haya yanatakiwa yaende na nja zingine za kucha pombe kama ushauri, kuamua moyoni kuacha, kuomba msaada kwa marafiki, kukaa mbali na wanywaji, kuepuka kukutana bar na rafiki zako na kadhalika.
zifuatazo ni dawa husika za kuacha pombe
disulfiram; hii ni dawa ya kwanza kabisa iliyogunduliwa ya kuwafanywa watu kuacha pombe, inafanya kazi kwa kuzuia mwili kuondoa pombe mwilini baada ya kunywa na matokeo yake mtu huweza kukaa na hang over kwa muda wa mpaka wiki mbili.
mtu hujisikia kichwa kuuma, kutapika, kuishiwa nguvu, kuchanganyikiwa, kutokwa jasho sana, kupumua kwa shida, na kushindwa kuona vizuri kila anapokunywa. mtumiaji hutapaika sana kama mtu aliyekunywa sumu kila akigusa pombe. hali hii humfanya mtu aiogope pombe kabisa.
                                                       
naltrexone; hii ni dawa ambayo inafanya kazi kwenye ubongo, kitaalamu kuna sehemu ya ubongo ambayo hupata raha mtu anavyoendelea kunywa pombe...dawa hii huzuia sehemu hiyo ya raha na kumfanya mtu asione raha yeyote kunywa pombe.
watu wengi hunywa pombe sababu kuna raha wanaipata wakati wanakunywa pombe hivyo wakiikosa raha hii hulazimika kuacha. dawa hii haina madhara ya kutapika kama ile ya mwanzo, dawa hii huchomwa kama sindano kwa mnywaji kila baada ya muda fulani mpaka atakapoacha kabisa.
acamprosate; mtu ambaye amezoea pombe hawezi kuacha ghafla kwani anakua ameshaizoea mwilini kitaalamu kama addiction hivyo akiacha ghafla hupata matatizo ambayo yanaitwa kitaalamu kama withdraw syndrome ambayo mtu huapata dalili za wasiwasi, kutetemeka,kukosa usingizi, na kutokwa na jasho, sasa dawa hii humsaidia huyu mtumiaji arudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kuacha pombe bila kupata hayo madhara niliyotaja.

mwisho; dawa hizi hupewa kwa watu tu ambao wako tayari kuacha pombe na mgonjwa asiwekewe kwenye pombe yake au kunyweshwa bila mwenyewe kujua kwani hiatamsaidia. kabla ya kuanza dozi ni vizuri daktari aliyekaribu na mgonjwa afahamu ili kama madahara ya dawa yakiwa makubwa aweze kumsaidia muhusika.

                                                           STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183
                                                            


UFAHAMU UGONJWA WA TETE KUWANGA NA MATIBABU YAKE.

                                                                      

tete kuwanga ni nini?
huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi kwa jina la varicella zooster, ugonjwa huu hushambulia mfumo wa hewa wa upumuaji.
baadae ugonjwa huu hushambulia maini, bandama kisha huenda kwenye ngozi, kwenye ngozi ugonjwa huu huleta upele mwingi....
ugonjwa huu hushambulia watoto wenye umri wa miaka mitano mpaka kumi lakini huweza kushambulia umri wowote ule.
ukishapata ugonjwa huu huwezi kuugua tena lakini ikitokea kinga yako ikashuka sababu ya ugonjwa kama ukimwi, kisukari au mlo mbovu ugonjwa huu hurudi kama mkanda wa jeshi.

ugonjwa unaambukizwaje?
ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya hewa au kugusana na mgonjwa na baada ya siku 11 mpaka 20  baada ya kuambukizwa dalili za kwanza za ugonjwa huu hutokea.

dalili za tete kuwanga ni zipi?
mwanzoni kabisa huanza homa, kikohozi na mwili kuchoka baadae ngozi hujaa vipele vikubwa vinavyowasha ambavyo husambaa kwanzia usoni, mikononi, miguuni na tumboni

jinsi ya kugundua ugonjwa
vipimo vya maabara sio lazima kwani ugonjwa unaweza kugundulika kwa kuangalia vipele na kuvitambua kama picha inavyoonyesha.

matibabu
mgonjwa huweza kupona bila dawa yeyeote lakini kwa mgonjwa ambaye kinga yake imeshuka anaweza kupewa dawa ya acyclovir kupunguza makali ya ugonjwa. baada ya wiki moja mpaka mbili vipele huanza hukauka kabisa na kwa kutoa maji na kuacha makovu.

madhara ya kuugua ugonjwa huu.
ugonjwa huu huweza kusababisha matatizo ya moyo,figo, ini, kifua, jointi za miguu na mikono, na matatizo ya mishipa ya fahamu.

jinsi ya kuzuia ugonjwa huu
chanjo hutolewa kuzuia ugonjwa huu lakini sio sehemu ya chanjo zinazotolewa nchini tanzania kwa sasa.
mgonjwa anatakiwa atengwe mbali na watu wengine huku nguo zake na mashuka yake yakifuliwa kwa makini sana kwa kutumia gloves ili kutoambukiza watu wengine.

                                                      STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183

KWANINI NI BORA KUNYWA BIA LAINI[LIGHT BEER] KULIKO BIA YA KAWAIDA[REGULAR BEER]?

                                                                    

bia ni nini? 
bia ni kilevi cha zamani zaidi kinachotumiwa sana duniani, ni kinywaji cha tatu kunywewa na watu duniani baada ya maji na chai. kinywaji hichi hutokana na kuchachishwa kwa kwa mazao kama mahindi,mchele na ngano.
bia huangozewa aina ya maua kwa jina la hops ambayo huifanya bia kua chungu na kuitunza isiharibike ikiwa ndani ya chupa.
siku hizi kuna bia laini ambazo ni rahisi kuzitambua kwa sababu zinaitwa light mfano castle light lakini pia kuna bia za zamani ambazo hua na majina ya kawaida tu mfano castle lager, safari lager, serengeti na kadhalika.

bia ina mchanganyiko  gani?
bia ya aina yeyote hua na mchanganyiko wa maji, maua ya hops ambayo huifanya isiharibike na kuifanya chungu, ngano, mchele au mahindi ambavyo huchacha na kuleta ladha ile ya bia, uyoga ambao ndio chanzo kikuu cha kuchacha kwa bia, lakini bia huongezewa kemikali zingine ambazo huifanya kua iwe safi na kung'aa.

kwanini inashauriwa kunywa bia laini kuliko bia ya kawaida?
kwa hali ya kawaida watu wanajua bia ni bia tu lakini kitaalamu kuna utofauti, ukiwa unataka kunywa bia ni bora unywe bia laini au light beer kwasababu za tofauti zifuatazo.
kiwango cha cha nguvu au calorie; hii ni nguvu inayopatikana kwenye bia ambayo inatokana na kiasi cha ngano, mahindi au mchele kinachowekwa, bia za kawaida zina calorie nyingi kuliko bia laini mfano chupa moja ya bia ya kawaida lina calorie 150 wakati chupa moja ya bia laini ina calorie 110. hivyo mtu anayekunywa bia ya kawaida atanenepa zaidi na kuota kitambi kuliko yule anayekunywa bia laini.

kiwango cha kilevi au alcohol; bia za kawaida zina kilevi kikubwa zaidi kuliko bia laini na mnywaji hujikuta amelewa sana kwa kunywa bia chache tu hivyo kama unahitaji kunywa kiwango kidogo cha kilevi, kukaa sehemu muda mrefu bila kuchoka, kua salama bila kuibiwa, au kuweza kuendesha gari baadae na kufurahia ni bora kunywa bia laini kwani hata ukiamua kunywa maji mengi sana baada ya kuinywa inaisha haraka mwilini.

hang over au uchovu wa asubuhi; bia laini huisha mwilini haraka sana, mtu anaweza kunywa bia hizi na bado kesho yake akaamka vizuri na kwenda kazini lakini bia za kawaida ukizinywa basi kesho yake yote utaipoteza ukiwa katika hali ambayo sio ya kawaida na hana ufanisi wako wa kazi hautakua mzuri.

bei ya bia; kwa hali ya kawaida bia laini hua ina bei kidogo kuliko bia ya kawaida japokua hapa nchini kwetu ni kama zinalingana bei lakini kwa nchi zilizoendelea bia laini zina bei ndogo ila kwa sababu dunia imeanza kujua bia laini ni nzuri zaidi kiafya basi uhitaji wa bia hizi umekua mkubwa mpaka zinaanza kupanda bei. mfano nchini marekani kati ya bia 10 zinazonunuliwa basi 7 ni bia laini.

ladha ya bia; bia za kawaida zina kiwango kikubwa sana cha pombe au alcohol  hivyo ina ladha kali sana kuliko bia laini...bia laini zina ladha nyepesi sana na ni nzuri kwa watu ambao hua sio watumiaji wa pombe kama wakihitaji kunywa kwa siku hiyo.

mwisho; pamoja kua kitaalamu inashauriwa kunywa bia laini kuliko hiyo ya kawaida, bado ukinywa kupitiliza kiwango utapata matatizo hata kama ni laini hivyo kunywa kwa kujiheshimu na isiuzwe chini a miaka 18.
tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                    STAY ALIVE

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183

KAMA UNATAKA KUACHA POMBE KABISA SOMA HAPA........

                                                                 
                                                      
makala iliyopita nilizungumzia madhara ya unywaji wa pombe na kama hukuipata makala hiyo basi isome hapa........, watu wengi ambao ni walevi sana kwenye jamii hudharauliwa na kulaumiwa sana kwa kuendekeza tabia hizo, ni kweli wanaweza kua wanapaswa kulaumiwa lakini upande wa pili ni kwamba watu hawa pia hawapendi kua hivyo na wanashindwa kuacha kwasababu pombe ina kitu kinaitwa addiction yaani mazoea na sio rahisi kuacha kirahisi kwani mwili umeshazoea na unataka zaidi, ikitokea umeacha ghafla hata shughuli zako zitakushinda kwani utapata dalili kitaalamu kama withdraw syndrome ambazo ni kutetemeka, kichwa kuuma, kutapika , kushindwa kula na kua mgonjwa muda wote.
maana yangu ni kwamba mlevi aonekane kama mgonjwa kwenye jamii na kama anataka kuacha pombe basi mpeni msaada na sio kumtenga, swala la kuacha pombe linawezekana kabisa kwa walevi waliopindukia au watu wanaokunywa kawaida tu. yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa kuacha pombe..
amua kutoka moyoni; hakikisha maamuzi haya yametoka moyoni mwako kulingana na wewe unavyoona na sio kwamba unataka ili kuacha kuridhisha kikundi fulani au mtu fulani, hii itakupa nguvu ya kupambana na majaribu ya kutaka kunywa pombe tena.
wajulishe wanywaji wenzako nia yako; waambie rafiki zako kwamba umeamua kuacha pombe kwa muda fulani, wape sababu zako za msingi na kama huna waambie ni sababu binafsi za kifamilia, wajulishe kwamba inaweza kua ngumu na utaomba msaada wao iwapo ukiwaka tamaa ya kunywa pombe tena.
jiwekee malengo mafupi; anza kwa kujiwekea kwamba sitakunywa pombe mwezi huu wote wa kwanza, ukifanikisha ongeza mwezi mwingine...hii itakuapa motisha ya kuendelea kuacha kuliko kusema kwanzia leo sinywi tena kwani utajikuta unakunywa. kama mwezi ukiisha na kujikuta umesevu pesa nyingi kwa kutokunywa basi jinunulie zawadi yeyote.
pangilia starehe zako; kama starehe zako nyingi zinahusisha kunywa pombe basi pangilia starehe zingine ambazo hazitaki pombe mfano kwenda bichi, kwenda kuangalia sinema, kungalia mpira uwanjani na kadhalika. epuka kwenda disko na bar kwa kipindi hiki cha mwanzo.
jitoe nje ya raundi za pombe; kama umeacha pombe usijihusishe na kuwanunulia watu pombe kwa kuzungusha kama wanywaji wanavyofanyiana wakiwa bar, nunua kinywaji chako kimoja kama ni soda au juisi kisha kaa pembeni ukinywa. kuwanunulia watu utajikuta na wewe unanunuliwa pombe.
kama mnatoka kwenda kwenye starehe basi endesha gari; kuendesha gari ni sababu kubwa ya wewe kutokunywa pombe kama sheria inavyotaka na hata ukilazimishwa kunywa utawaambia rafiki zako kwamba mimi ni dereva leo.
kua tayari kuzungumzia swala lako; watu wengi watakua wanakuuliza kwanini umeamua kuacha pombe, basi andaa sababu za msingi za kuwaambia kama jinsi pombe inavyoharibu maisha yako ya kijamii, kiuchumi na kiafya na wakati mwingine ukiona umezidiwa waambie ni sababu za kifamilia zaidi.
badilisha sehemu za kukutana na watu; kama ulikua ukipanga kuonana na mtu, unaenda bar basi badilisha sehemu ili ue unaenda kuonana nao kwenye mgahawa au sehemu zingine za wazi ambapo pombe haziuzwi.
furahia faida za kuacha kwa muda huo; angalia ni kaisi gani cha fedha umesevu kwa kuacha pombe, unajisikiaje kukaa muda mrefu bila kupata hangover, unajisikiaje jamii iliyokudharau sasa inakuheshimu na hii itakupa nguvu zaidi a kusonga mbele.
dawa za kuacha pombe kwa walevi sana; kuna dawa maalumu ambazo zimetengenezwa kuwatibu watu ambao wanataka kuacha pombe hasa wale ambao wameshindwa kuacha kwa njia nilizotaja hapo juu, utaratibu huu hufanyika chini ya uangalizi wa daktari hasa kwa nchi zilizoendelea...dawa hizi hufanya kazi kwa kukosesha mtu hamu ya kunywa pombe, kuongeza muda wa hangover mpaka siku tatu, na kuzuia madhara mtu anayopata kwa kuacha pombe haraka mfano disulfiram.[sina uhakika kama zinapatikana nchini], pia unawea kutumia virutubisho mbalimbali vya kuondoa sumu mwilini baada ya kuacha pombe, hivyo unaweza kuvipata hapa nchini.
  pia unaeza tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                   STAY ALIVE

                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                       0653095635/0769846183
                              OFISI; UKONGA MADAFU DAR ES LAAM