tukiwa mwishoni mwa mwaka 2016, kuna mambo mengi tumeyashuhudia kama ajari, vifo vya wapendwa wetu, milipoku ya magonjwa mbalimbali, vita na taabu nyingi sana ambavyo vimechukua maisha ya watu wengi sana..ukiwa umekaa nyumbani mbele ya tv yako unaweza ukaona jinsi watu wanavyolalamika sana kuhusu magonjwa kama kipindupindu, ebola, kansa ya matiti na kadhalika lakini utapigwa na butwaa utakapojua hayo magonjwa yanaua watu wachache sana. shirika la afya la umoja wa mataifa[WHO] linaonyesha riport ya magonjwa nguli ambayo yanaua sana na yanategemea kuua zaidi miaka ijayo kulingana na uhalisi wa maisha ya sasa.
magonjwa haya kwa nchi za afrika zamani yalikua hayapo kabisa lakini sababu ya sisi watu weusi kuanza kuiga mifumo ya kimaisha ya nchi zilizoendelea yaani kwa kuiga vyakula vyao, madawa yao, na mfumo mzima wa maisha. kwa sasa tafiti zinaonyesha afrika kuna ongezeko kubwa la magonjwa haya kuliko nchi zilizoendelea. magonjwa hayo ni kama ifuatavyo..........
magonjwa ya moyo[coronary heart disease]; huu ndio ugonjwa ambao unaongoza kwa kuua watu wengi sana dunia ni kwa sasa, ugonjwa huu unatokana na mishipa mikubwa inayopeleka damu kwenye moyo kitaalamu kama coronary artery kua myembamba sana na kuziba.ripoti la shirika la afya duniani inaonyesha kwamba watu milion saba na laki nne wanauawa na ugonjwa huu kila mwaka sawa 13.2% ya vifo vyote duniani. nchini marekani tu kila mwaka watu laki sita wanauawa na ugonjwa huu hivyo kuufanya ugonjwa hatari zaidi nchini humo na duniani kwa ujumla.
hatari ya kupata ugonjwa huu ni uzito mkubwa, uvutaji wa sigara na kiasi kukubwa cha lehemu[cholestrol] kwenye damu, hivyo mazoezi ya mara kwa mara, kula vizuri na kupunguza uzito huweza kukukinga na magonjwa haya.
kiharusi[stroke]; huu ni ugonjwa uliomuua waziri mkuu wa zamani wa israel ariel sharon mwaka 2014, ugonjwa huu husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye ubongo na hii husababisha kufa kwa seli za ubongo na mtu kupooza nusu ya mwili wake.
ugonjwa wakiharusi umeua watu milioni sita na laki saba ikiwa ni 11.2% ya vifo vyote duniani kulingana na repoti ya shirika la afya duniani.
nchini marekani watu 130000 hufa kila mwaka kutoka na na kiharusi yaani kila baada ya dakika nne mtu mmoja anapata kiharusi. ugonjwa huu unazuilika kwa kufuata kanuni za afya kama nilivyoongelea kwenye point ya kwanza hapo juu.
magonjwa ya kubana kifua[chronic obstructive pulmonary diseases]; haya ni magonjwa yanayosababisha mgonjwa kushindwa kupumua vizuri mfano asthma,bronchitis,empysema na kadhalika.
ugonjwa huu unasabishwa na uchafuzi wa hali ya hewa na uvutaji wa sigara. watu milion 3.1 hufa kila mwaka kutoka na ugonjwa huu na hii ni asilimia 5.6% ya vifo vyote duniani. ugonjwa huu hautibiki lakini kuna dawa za kupunguza makali kusogeza muda mbele.
magonjwa ya yanayoshambulia kifua[lower respiratory tract infections]; magonjwa ya kifua yanayosabishwa na bakteria na virusi mbalimbali, magonjwa haya ni kama pneumonia na mafua makali kitaalamu kama influenza. kwa hapa tanzania magonjwa haya yanaua watoto wengi sana walioko chini ya miaka mitano. duniani kiujumla ugonjwa huu unaua zaidi ya watu milion 3 kila mwaka na hii ni asilimia 5.5% ya vifo vyote duniani...
kansa ya koo na kifua; hizi ni kansa zinazoongoza kwa kuua watu wengi zaidi, chanzo chake ni uvutaji wa sigara, kuishi na wavuta sigara, uchafuzi wa hali ya hewa na sumu zingine za mazingira.kansa hizi zinaua watu milioni 1.6 kila mwaka ni sawa na asilimia 2.9 vifo vyote duniani.
ugonjwa wa ukimwi; huu ni ugonjwa unaoshambulia kinga ya mwili na kumuacha mtu akiwa hawezi kupambana na magonjwa nyemelezi ya mwili. ripoti za shirika la utafiti wa ugonjwa wa ukimwi linaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 40 wameuawa na ukimwi tangu ulipingia duniani, zaidi ya watu milioni mbili hufa kila mwaka, na watu 5700 huambukizwa kila siku. kwa sasa watu zaidi ya milioni 60 duniani wanaumwa ugonjwa huu na bara la afrika likiwa limeathirika zaidi kwani asilimia 91% ya watoto wenye virusi vya ukimwi wanaishi afrika.
magonjwa ya kuharisha; mtu anaharisha pale anapotoa choo laini sana mara tatu kwa siku, hali hii hupunguza madini muhimu mwilini na kumfanya mgoonjwa kudhoofu sana. kuharisha husababishwa na minyoo, virusi na bakteria ambao hushambulia utumbo mkubwa wa chakula.
zaidi ya watu milioni moja na laki tano hufa kila mwaka na ugonjwa huu na hii kuweka asilimia 2.7% ya vifo vyote duniani. kwa upande wa watoto tu, wanaougua ni bilioni mbili na laki tano kila mwaka na kati ya hao laki saba na elfu sitini hufariki kila mwaka.
ugonjwa huu unazuilika sana kwa kuongeza jitihada za usafi na mara nyingi nchi ambazo hazijaendelea zinathirika zaidi.
ugonjwa wa kisukari; huu ni ugonjwa uanosababishwa na kushindwa kwa kongosho kutoa homoni ya insulini kwa ajili ya kuchukua sukari kwenye damu ili iingie ndani ya seli kufanya kazi. mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na uzito mkubwa, kutofanya mazoezi na kula vibaya.
watu milioni moja na laki tano hufa kila mwaka kwa ugonjwa huu lakini pia nchi ambazo hazijaendelea hutoa vifo vingi kutokana na kua na teknolojia ndogo ya matibabu.
watoto wanaozaliwa kabla ya muda; zaidi ya watoto milioni moja na laki moja hufa kila mwaka sababu ya kuzaliwa kabla ya mwezi wa tisa wa mimba, vifo hivi ni vingi nchi ambazo hazijaendelea sababu ya teknolojia ndogo ya kuhudumia watoto hawa.
ugonjwa wa kifua kikuu; huu ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya hewa na bakteria wanaoitwa kitaalamu kama mayobacterium tuberculae, bacteria huyu ndio anaongoza kwa kuua watu wengi zaidi kuliko bakteria wote duniani. bakteria hawa wameanza kukataa matibabu ya dawa zilizopo na kuleta changamoto kubwa. zaidi ya watu laki tisa duniani hufa kila mwaka kwa ugonjwa huu.
mwisho; ugonjwa wa malaria japokua haupo kwenye listi hii ndio ugonjwa unaongoza kwa kuua watu wengi zaidi hapa tanzania na afrika kwa ujumla, ugonjwa huu unaua zaidi ya watu milioni sita na laki saba kila mwaka huku asilimia tisini ya wagonjwa hao wako afrika.
tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni