data:post.body Desemba 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

SABABU KUMI KWANINI UACHE KUNYWA POMBE KWANZIA LEO..

                                                                 
kila mwaka watu watu milioni mbili na laki tano wanauawa na pombe duniani, idadi hii inafanya pombe kua moja ya vyanzo vya vifo ambavyo vinazuilika duniani.. pombe huathiri mifumo mbalimbali ya mwili ikiwemo ubongo, mishipa ya fahamu, moyo, maini na hisia za mtu kiujumla.madhara ya pombe hutegemea sana na kiasi cha pombe mtu anachokunywa..
mambo yanayochangia madhara zaidi ya pombe ni jinsia, umri na historia ya familia husika kwenye unywaji wa pombe..yafuatayo ni madhara ya kutisha yanayosababishwa na unywaji wa pombe..
matatizo ya ubongo; unywaji wa pombe kwa kiasi kidogo tu husababisha mtu kushindwa kuongea, kushindwa kusikia, kushindwa kusoma na kukumbuka, na kushindwa kupata balance wakati wa kutembea.madhara madogo madogo kama haya huweza kuisha mtu akiacha kunywa pombe lakini unywaji wa pombe wa muda mrefu huleta madhara makubwa sana ya ubongo ambayo hayatibiki.
hangover za asubuhi; huu ni mkusanyiko dalili nyingi ambazo mtu huzipata asubuhi baada ya kunywa pome usiku wa jana, dalili hizi ni kama kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika, kuchoka sana, kiu, uvivu na kushindwa kufanya lolote siku nzima.
saratani; unywaji wa pombe humuweka mtumiaji katika hatari kubwa ya kupata saratani mbalimbali za mwili kama saratani ya koo ya chakula, maini, kongosho na kadhalika. unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara kwa wakati mmoja humuweka mtu kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata kansa hizi.
madhara kwa mtoto aliyeko tumboni; tafiti zinaonyesha watoto wengi wanaozaliwa na matatizo ya moyo, kuzaliwa kabla ya muda, kuzaliwa na viungo pungufu na kadhalika husababishwa na unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito.
kuumia na ajari mbalimbali; mtu akishakunywa pombe basi uwezo wake wa kutafsiri na kuamua mambo unakua mdogo, hali hii humuingiza kwenye ugomvi, kuendesha vyombo vya moto kwa uzembe hata kushiriki ngono zembe na watu mbalimbali.
utegemezi wa pombe; kuna watu wanakunywa pombe kila siku, watu hawa jamii huwashangaa sana na kuwadharau ikidhani wanafanya makusudi lakini watu hawa hawawezi kujizuia kunywa pombe sababu miili yao inataka pombe muda wote na mara nyingi watu wengi wanaoanza pombe kabla ya miaka 21 hupata addiction kubwa ya pombe.
kuongezeka uzito; pombe ina kiasi kikubwa cha nguvu kitaalamu kama calories ambayo kimsingi haina faida yeyote, mtu anayenenepa kwa kula chakula angalau anapata unene pamoja na virutubisho muhimu vya mwili vilivyomo kwenye chakula lakini kwenye pombe ni unene mtupu. ukiwaangalia wahudumu wa bar wengi ambao hunywa pombe hovyo hua ni wanene sana na wenye vitambi.
kuishi maisha mabovu ; unywaji mkubwa wa pombe huweza kuathiri uwezo wako wa kifedha, utaalamu uliosomea au kujifunza, na hisia zako. unywaji wa pombe wa muda mrefu huweza kusababisha magonjwa ya akili kama wasiwasi, mgandamizo wa mawazo na kushindwa kuelewana na watu kitaalamu kama antsocial behaviour.
vifo; unywaji wa pombe husababisha vifo vya muda mrefu kutokana na magonjwa au vifo vya ghafla, hii hutokana na kuongezeka kiasi kikubwa cha pombe kwenye damu ambacho husababisha kuchanganyikiwa, kupoteza fahamu na kufa.historia inaonyesha kwamba mashindano mengi ya kunywa pombe duniani yamesabaisha vifo vya ghafla..nakumbuka mtu mmoja aliwahi kunywa kreti nzima ya bia za guiness na akafa hapohapo.
magonjwa yasiyotibika;uywaji wa pombe unasabaisha magojwa yasiyotibika kama presha ya damu, kuharibika kwa maini na kungosho ambavyo havitibiki.
tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                           STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                            MAWASILIANO; 0653095635/0769846183
                                 OFISI; UKONGA MADAFU, DAR ES LAAM

                                                 

UFAHAMU UGONJWA WA ZIKA NA MATIBABU YAKE....

                                                     
          
utangulizi
zika ni ugonjwa unaoambukizwa na mbu uliogundulika kwa nchini uganda mwaka 1947 wakati wanasayansi wakifanya utafiti kuhusu virusi vya homa ya manjano. mwaka 1952 baadae ugonjwa huu ulikutwa tanzania na uganda kwenye damu ya binadamu. kulipuka kwa ugonjwa wa zika kumeonekana bara za marekani, asia, ulaya, na sehemu mbalimbali.
mlipuko mkubwa kabisa wa virusi hivi ulionekana visiwa vya yap mwaka 2007, baadae mwaka 2015 wanasayansi wa brazili waligundua mahusiano kati ya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo, kupooza na ugonjwa wa zika.

dalili za ugonjwa wa zika ni zipi?
dalili huanza siku kadhaa baada ya kuambukizwa kama homa kali, vipele, macho mekundu, maumivu ya misuli na mifupa, kua na kichwa kidogo na kupooza kwa watoto wanaozaliwa na  dalili hizi hua sio kali na huchukua siku mbili mpaka saba.

maambukizi
zika huambukizwa na mbu wa jamii ya aedes, mbu huyu huweza kuuma muda wowote hasa asubuhi, ni mbu yule yule anayeambukiza dengu na homa ya manjano. lakini pia unaweza kuambukizwa kwa njia ya ngono na kuongezwa damu.

jinsi ya kutambua ugonjwa
ugonjwa huweza kutambulika kwa dalili nilizotaja hapo mwanzo hasa kama mgonjwa ametoka kwenye sehemu zenye mbu ugonjwa huo lakini pia kuna njia za maabara za kuhakiki ugonjwa huu kwa kupima damu,mate,mkojo na mbegu za kiume.

matibabu
hukuna matibabu ya moja kwa moja ya ugonjwa wa zika, dalili hua sio kali na hazitaki matibabu..mgonjwa hutakiwa kunywa maji mengi, kupumzika, dawa za maumivu na homa tu. kama hali ikiwa mbaya unatakiwa umuone daktari. mpaka sasa hakuna chanjo ya ugonjwa huu.

jinsi ya kuzuia ugonjwa wa zika..
ugonjwa wa zika huzuilika kwa kuzuia kung'atwa na mbu, kuepuka ngono zembe na kupima damu kabla ya kumpa mtu sehemu zenye mlipuko wa ugonjwa huu.

                                                     STAY ALIVE
                                           0769846183/0653095635
karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]

YAFAHAMU MADHARA KUMI YA KUCHORA TATTOO MWILINI...

                                                                         
                                                                                                                       
tattoo ni nini?
hii ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani kitaalamu kama dermis kubadilisha rangi kabisa maisha yako yote au kwa muda tu, inateemea na uwekaji..
kwa dunia ya sasa kujichora tatoo ni kama fasheni fulani kwenye jamii, ukienda kuchora tattoo kuna uwezekano mkubwa sana isitoke maisha yako yote hivyo kwa usalama wako ni vizuri ukamuona mtaalamu wa tattoo ambaye ni maarufu na ana sifa kubwa katika shughuli hizo, anaweza kua ana gharama kubwa lakini binafsi itakusaidia.kwa sasa nchi ya marekani inaongoza kwa kua na watu wengi wenye tattoo duniani.
hivyo kabla hujaamua kujichora tattoo basi madhara yake haya hapa..
kansa ya ngozi; hapo mwanzoni wataalamu walikua wanasema hakuna mahusiano kati ya kansa ya ngozi na na tabia ya kujichora tattoo lakini hivi karibuni tafiti kutoka uingereza zinaonyesha kuna aina fulani za wino ambazo zinaweza kusababisha kansa zikitumika kuchora tattoo.
allergy ya ngozi; haijalishi unaweka tattoo kwa muda au ya moja kwa moja kumetokea kesi nyingi za watu wanaopata allergy baada ya kupakwa tattoo, utafiti unaonyesha rangi nyekundu ndio inaongoza kwa kusababisha allergy hizo huku rangi zingine kama nyeusi, purple na zingine hazisababishi. mara nyingi allergy hizi huonekana mtu akikaa juani.
makovu; mwili unataambua tattoo kama adui wake hivyo hujaribu kuiondoa kwa njia mbalimbali na kwa kufanya hivyo husababisha makovu ya muda mrefu ambayo yanaweza kuleta magonjwa mengine ya ngozi.
maambukizi ya ukimwi na ugonjwa wa hepatitis; tabia ya kurudia sindano zilezile wakati wa kuchora tattoo kunaweza kusababisha maambukizi ya virusi vya ukimwi na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ini kitaalamu kama hepatitis b. ugonjwa huu wa hepatitis b husababisha kansa ya ini ambayo haitibiki. ni vizuri kua makini ili uone kama sindano inayotumika kwako ni mpya.
matatizo kipindi cha kufanya kipimo cha MRI; hichi kipimo ni cha mionzi na kirefu chake ni magnetic resonance imaging, hutumika kupima viungo vya mwili ambavyo havionekani kwa macho ndani ya mwili wa binadamu kama x ray inavyofanya. tatizo ni kwamba kipimo hiki kina sumaku kali kiasi kwamba mtu hatakiwi kuingia kwenye mtambo huo akiwa amevaa chuma chochote na hata kama kiko ndani ya mwili kitavutwa nje, sasa mara nyingi tattoo nyeusi hua imetengenezwa na compound kitaalamu kama iron oxide ambayo ina chembechembe za chuma. hii inaweza ikaleta changamoto kubwa kwenye vipimo.
kubadilika kwa  rangi ya ngozi; sehemu inayochorwa tattoo hubadilika moja kwa moja na kua na rangi tofauti, hakuna jinsi unaweza ukaitoa hiyo rangi tena, hata baada ya muda mrefu tattoo ikipungua nguvu lakini ngozi haiwezi kua kama zamani.
hutoruhusiwa kuchangia damu; mara nyingi watu wenye tattoo hawaruhusiwi kuchangia damu kwani wana hatari ya kusambaza ugonjwa kwenda kwa mtu mwingine, kimsingi mtu aliyechora ndani ya muda mfupi ndio haruhusiwi lakini kwasababu wakati mwingine sio rahisi kutofautisha tattoo mpya na ya zamani basi hawa watu huwa hawaruhusiwi kabisa.mchezaji wa kimataifa christian ronaldo hachori tattoo kwa sababu ya hili.
unaweza kukosa fursa mbalimbali; kuna kampuni mbalimbali duniani haziwapi watu kazi kwasababu wamechora tattoo kulingana na imani za kampuni husika lakini pia kazi yeyote ya jeshi duniani hairuhusu tattoo hivyo kama wewe unayesoma hapa umeshachora tattoo ujue kazi ya jeshi huna tena.
tattoo huingiliana na matumizi ya dawa fulani; kama wewe unatumia dawa za kuzuia damu isingane mwilini ukichora tattoo inaweza kufanya utoke damu nyingi sana kwani dawa hizo huzuia uwezo wa mwili kukausha damu na kuponyesha vidonda.
magonjwa ya ngozi; wakati mwingine bacteria huweza kuvamia sehemu zenye vidonda vya tattoo na kusababisha kutopona haraka, dalili huweza kua homa kali, maunivu makali na sehemu ya tattoo kuvimba.
damu kuganda juu ya ngozi[haematoma]; hii husababishwa na kuvuja kwa damu nyingi chini ya ngozi, huonekana sana pembeni pembeni ya sehemu ambapo rangi ya tatoo imepita na huchelewesha kupona kwa kidonda.
nini kifanyike kwa wanaopenda tattoo?
siku hizi kuna tattoo zinachorwa juu ya ngozi kama hina na kuondoka baada ya muda fulani, hizi hazina madhara kabisa, huchorwa kwa bei ndogo na hukupa nafasi ya wewe kubadilisha tatoo za aina mbalimbali kwenye sehemu moja ya mwili.
je tattoo inafutika?
ni ngumu sana kuifuta tattoo na hii ni changamoto kwa watu ambao wamechora tattoo za majina au sura za wapenzi wao wa zamani. kuna kikaa kinaitwa laser ambacho kinaweza kutumika kufuta tattoo yote au sehemu ndogo tu ya tattoo. mara nyingi rangi nyeusi zinaweza kutoka ukilinganisha na rangi zingine. maumivu yanayotumiaka kuiondoa tattoo ni makali kuliko maumivu ya kuiweka na hapa kwetu tanzania siana uhakika kama huduma hii ya kuondoa tattoo ipo.
                         
 tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                                           

                             
                                                           STAY ALIVE

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183
                                     
                                                 

YAFAHAMU MAGONJWA KUMI YALIONGOZA KUUA WATU WENGI ZAIDI DUNIANI MWAKA 2016

                                                                 
                                                       
tukiwa mwishoni mwa mwaka 2016, kuna mambo mengi tumeyashuhudia kama ajari, vifo vya wapendwa wetu, milipoku ya magonjwa mbalimbali, vita na taabu nyingi sana ambavyo vimechukua maisha ya watu wengi sana..ukiwa umekaa nyumbani mbele ya tv yako unaweza ukaona jinsi watu wanavyolalamika sana kuhusu magonjwa kama kipindupindu, ebola, kansa ya matiti na kadhalika lakini utapigwa na butwaa utakapojua hayo magonjwa yanaua watu wachache sana. shirika la afya la umoja wa mataifa[WHO] linaonyesha riport ya magonjwa nguli ambayo yanaua sana  na yanategemea kuua zaidi miaka ijayo kulingana na uhalisi wa maisha ya sasa.
magonjwa haya kwa nchi za afrika zamani yalikua hayapo kabisa lakini sababu ya sisi watu weusi kuanza kuiga mifumo ya kimaisha ya nchi zilizoendelea yaani kwa kuiga vyakula vyao, madawa yao, na mfumo mzima wa maisha. kwa sasa tafiti zinaonyesha afrika kuna ongezeko kubwa la magonjwa haya kuliko nchi zilizoendelea. magonjwa hayo ni kama ifuatavyo..........
magonjwa ya moyo[coronary heart disease]; huu ndio ugonjwa ambao unaongoza kwa kuua watu wengi sana dunia ni kwa sasa, ugonjwa huu unatokana na mishipa mikubwa inayopeleka damu kwenye moyo kitaalamu kama coronary artery kua myembamba sana na kuziba.ripoti la shirika la afya duniani inaonyesha kwamba watu milion saba na laki nne wanauawa na ugonjwa huu  kila mwaka sawa 13.2% ya vifo vyote duniani. nchini marekani tu kila mwaka watu laki sita wanauawa na ugonjwa huu hivyo kuufanya ugonjwa hatari zaidi nchini humo na duniani kwa ujumla.
hatari ya kupata ugonjwa huu ni uzito mkubwa, uvutaji wa sigara na kiasi kukubwa cha lehemu[cholestrol] kwenye damu, hivyo mazoezi ya mara kwa mara, kula vizuri na kupunguza uzito huweza kukukinga na magonjwa haya.
kiharusi[stroke]; huu ni ugonjwa uliomuua waziri mkuu wa zamani wa israel ariel sharon mwaka 2014, ugonjwa huu husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye ubongo na hii husababisha kufa kwa seli za ubongo na mtu kupooza nusu ya mwili wake.
ugonjwa wakiharusi umeua watu milioni sita na laki saba ikiwa ni 11.2% ya vifo vyote duniani kulingana na repoti ya shirika la afya duniani.
nchini marekani watu 130000 hufa kila mwaka kutoka na na kiharusi yaani kila baada ya dakika nne mtu mmoja anapata kiharusi. ugonjwa huu unazuilika kwa kufuata kanuni za afya kama nilivyoongelea kwenye point ya kwanza hapo juu.
magonjwa ya kubana kifua[chronic obstructive pulmonary diseases]; haya ni magonjwa yanayosababisha mgonjwa kushindwa kupumua vizuri mfano asthma,bronchitis,empysema na kadhalika.
ugonjwa huu unasabishwa na uchafuzi wa hali ya hewa na uvutaji wa sigara. watu milion 3.1 hufa kila mwaka kutoka na ugonjwa huu na hii ni asilimia 5.6% ya vifo vyote duniani. ugonjwa huu hautibiki lakini kuna dawa za kupunguza makali kusogeza muda mbele.
magonjwa ya yanayoshambulia kifua[lower respiratory tract infections]; magonjwa ya kifua yanayosabishwa na bakteria na virusi mbalimbali, magonjwa haya ni kama pneumonia na mafua makali kitaalamu kama influenza. kwa hapa tanzania magonjwa haya yanaua watoto wengi sana walioko chini ya miaka mitano. duniani kiujumla ugonjwa huu unaua zaidi ya watu milion 3 kila mwaka na hii ni asilimia 5.5% ya vifo vyote duniani...
kansa ya koo na kifua; hizi ni kansa zinazoongoza kwa kuua watu wengi zaidi, chanzo chake ni uvutaji wa sigara, kuishi na wavuta sigara, uchafuzi wa hali ya hewa na sumu zingine za mazingira.kansa hizi zinaua watu milioni 1.6 kila mwaka ni sawa na asilimia 2.9 vifo vyote duniani.
ugonjwa wa ukimwi; huu ni ugonjwa unaoshambulia kinga ya mwili na kumuacha mtu akiwa hawezi kupambana na magonjwa nyemelezi ya mwili. ripoti za shirika la utafiti wa ugonjwa wa ukimwi linaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 40 wameuawa na ukimwi tangu ulipingia duniani, zaidi ya watu milioni mbili hufa kila mwaka, na watu 5700 huambukizwa kila siku. kwa sasa watu zaidi ya milioni 60 duniani wanaumwa ugonjwa huu na bara la afrika likiwa limeathirika zaidi kwani asilimia 91% ya watoto wenye virusi vya ukimwi wanaishi afrika.
magonjwa ya kuharisha; mtu anaharisha pale anapotoa choo laini sana mara tatu kwa siku, hali hii hupunguza madini muhimu mwilini na kumfanya mgoonjwa kudhoofu sana. kuharisha husababishwa na minyoo, virusi na bakteria ambao hushambulia utumbo mkubwa wa chakula.
zaidi ya watu milioni moja na laki tano hufa kila mwaka na ugonjwa huu na hii kuweka asilimia 2.7% ya vifo vyote duniani. kwa upande wa watoto tu, wanaougua ni bilioni mbili na laki tano kila mwaka na kati ya hao laki saba na elfu sitini hufariki kila mwaka.
ugonjwa huu unazuilika sana kwa kuongeza jitihada za usafi na mara nyingi nchi ambazo hazijaendelea zinathirika zaidi.
ugonjwa wa kisukari; huu ni ugonjwa uanosababishwa na kushindwa kwa kongosho kutoa homoni ya insulini kwa ajili ya kuchukua sukari kwenye damu ili iingie ndani ya seli kufanya kazi. mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na uzito mkubwa, kutofanya mazoezi na kula vibaya.
watu milioni moja na laki tano hufa kila mwaka kwa ugonjwa huu lakini pia nchi ambazo hazijaendelea hutoa vifo vingi kutokana na kua na teknolojia ndogo ya matibabu.
watoto wanaozaliwa kabla ya muda; zaidi ya watoto milioni moja na laki moja hufa kila mwaka sababu ya kuzaliwa kabla ya mwezi wa tisa wa mimba, vifo hivi ni vingi nchi ambazo hazijaendelea sababu ya teknolojia ndogo ya kuhudumia watoto hawa.
ugonjwa wa kifua kikuu; huu ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya hewa na bakteria wanaoitwa kitaalamu kama mayobacterium tuberculae, bacteria huyu ndio anaongoza kwa kuua watu wengi zaidi kuliko bakteria wote duniani. bakteria hawa wameanza kukataa matibabu ya dawa zilizopo na kuleta changamoto kubwa. zaidi ya watu laki tisa duniani hufa kila mwaka kwa ugonjwa huu.
mwisho; ugonjwa wa malaria japokua haupo kwenye listi hii ndio ugonjwa unaongoza kwa kuua watu wengi zaidi hapa tanzania na afrika kwa ujumla, ugonjwa huu unaua zaidi ya watu milioni sita na laki saba kila mwaka huku asilimia tisini ya wagonjwa hao wako afrika.
                         tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                             STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

HAYA NDIO MADHARA 12 YA KUJICHUBUA NGOZI.

                                                           
                                               
                                                             
                                         
tabia ya kujichubua ilianza kupata umaarufu kwanzia mika ya 1980 mpaka miaka ya hivi karibuni, hii hasa kwenye nchi za watu ambao hawana ngozi nyeupe kabisa kama waarabu, wahindi na waafrika. biashara hii imewafanya watu wanaotengeneza bidhaa hizi kua matajiri sana huku zikiacha madhara makubwa kwa watumiaji.
kitaalamu  matibabu dawa kujichubua yalitakiwa yatolewe kitaalamu kwa ajili ya kuondoa mabaka ya ngozi na kuondoa makunyazi ya uzee lakini chini ya usimamizi maalumu wa daktari na matumizi yake yawe ya muda fulani tu kama dozi ya dawa lakini hali hii imekua tofauti kwani kemikali hizi zimekua zikitumika bila usimamizi na kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji.
kwa hapa tanzania tafiti zinaonyesha zaidi ya asilimia 70 ya wanawake hutumia dawa za kujichubua na huku asilimia mbili mpaka tano ya wanaume hutumia pia.
kuna aina tatu ya madawa hayo, dawa za kumeza, dawa za kupaka, dawaza kuchoma sindano na njia ya upasuaji lakini kwa hapa kwetu wengi hutumia za kupaka na wachache za kunywa.
watu wengi wamekua wakiiga wasanii wa nje kama marekani huku wakishindwa kujua kwamba wale pale wanafanya vile kwa usimamizi wa madaktari bingwa wa ngozi na kwa  dozi maalumu ili wasipate madhara yeyote.
serikali imekua ikijitahidi kuyapiga marufuku madawa hayo bila mafanikio kwani watu wengi huyapitisha na kuyatumia kwa magendo wakidhani wanaikomoa serikali bila kujua wanajiua wenyewe.
yafuatayo ni madhara yatokanayo na kujichubua ngozi..
kansa ya ngozi;dawa za kujichubua zina kemikali kuu mbili yaani hydroquinone na mercury, lakini dawa nyingi zinazopatikana mtaani zina mchanganyiko wa steroids, tretinion, na hydroquinone. kemikali hizi ni moja ya vyanzo vikuu vya kansa ya ngozi na kuharibu maini.

kuongezeka kwa weusi wa ngozi; matumizi ya kemikali kama hydroquinone 2% kwa muda wa miezi mitatu mfululizo huweza kusababisha ngozi kua nyeusi zaidi na kukataa matibabu yeyote ya kuirudisha kwenye hali yake ya kawaida. lakini pia matumizi makubwa ya vipodozi hivi husababisha sehemu kama za vidole, miguu na masikio kua nyeusi zaidi kuliko sehemu zingine.
                                                     
ngozi kua nyembamba sana; hii husababishwa na kemikali ambazo hupunguza sana unene wa ngozi, ngozi hii honyesha mishipa ya ndani ya damu na ni rahisi sana kuumia na kuvuja damu kirahisi.                                
vidonda visivyopona; kawaida ngozi ya mtu wa kawaida huweza kupona yenyewe ikiumia bila kutumia dawa yeyote lakini matumizi ya kemikali za kujichubua husababisha ngozi kupoteza uwezo wake wa kupona wenyewe.
kuungua na mapele ya ngozi;kemikali hizi huweza kuunguza ngozi na kufanya iwe na mabaka baka, chunusi, harara na ngozi isiyokua na afya. kemikali ya hydroquinone hufanya kazi ya kuzuia ngozi kutengeneza kitu kinachoitwa melanin ambacho ni muhimu kwa ajili ya kuleta rangi ya ngozi.
                                         
magonjwa ya ngozi; tafiti nyingi zilizofanywa na madaktari wa ngozi zimegundua kwamba watu wengi wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali ya ngozi kama upele, miwasho, fangasi na aleji ni watu wanaotumia kemikali hizi hatari za kujichubua.
                                         
huingiza sumu za ndani ya mwili; moja ya madhara makubwa ya kutumia kemikali za kuchubua rangi ya ngozi ni kuingiza sumu mwilini. sumu hizi huingia ndani ya mwili kupitia ndani ya ngozi, kwa vidonge vya kujichubua au sindano zinazotumika kwa kazi hii. madhara yake ni kuharibika kwa figo, kuharibika kwa ngozi, kinga ya mwili kushuka, kupata ngazi sehemu mbalimbali za mwili.
                                                     
kubadilika kwa ngozi ya uso; hali hii hutokea pale ngozi ya uso inakua nyembamba sana kuliko sehemu zingine za mwili na husababisha kubadilika kwa ngozi ya uso na kua na hali tofauti kabisa.
                                                   
kuathirika kisaikolijia; watu wengi waliojichubua na kupata madhara wanakosa amani wakiwa mbele za watu kwa kuhisi kwamba wanasemwa sana kulingana na hali yao ya sasa ilivyo, hii huwanyima uhuru na kuwafanya wawe watu wa kukaa ndani tu au kuvaa nguo za kuficha sura zao muda mwingi.
                                           
kuharibu watoto tumboni; kemikali za kujichubua zina uwezo wa kuingia mpaka kwenye kizazi cha mama mjamzito, hali hii huweza kusababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye upungufu wa viungo fulani vya mwili kama mkono mmoja au mguu mmoja.


upofu; kemikali za kuchubua ngozi ambazo hupakwa usoni zina uwezo wa kuharibu macho na kumfanya mtu awe kipofu kabisa, mimi binafsi nimeshuhudia watu waliopata upofu sababu ya kujichubua ngozi.
michirizi ya ngozi; kwasasa kuna wanawake wengi sana wanasumbuliwa na tatizo la michirizi ya ngozi, japokua michirizi hii huletwa na unene auujauzito lakini kujichubua pia moja ya vyanzo vikuu vya hali hii.
mwisho; kama wewe ndio unaanza kujichubua basi ujue uko kwenye hatari kubwa, inawezekana kwa sasa mambo yako ni safi kwamba umeshakua mweupe na kila mtu anakusifia lakini naomba nikwambie mbio zako za sakafuni zina ukingo..... kama umeshaathirika tayari basi ni wakati wa kuacha na kuomba msaada wa matibabu ili urudi kwenye hali yako ya kawaida. sasa hivi kuna kampuni nyingi za nje zinauza dawa kwa ajili ya matibabu ya waathirika wa hali hii.pia unaweza ukawasilaina na sisi na ukapata matibabu popote ulipo.

                  tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                   STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                         O653095635/0769846183


HAYA NDIO MAMBO 10 YA KUZINGATIA KWENYE MATUNZO WA UUME.....

                                                               
kuhifadhi uume wako kwa usafi, mvuto na afya ni swala la kipaumbele kwa wanaume, kiungo hichi cha uzazi ni muhimu sana kwani ndio tofauti kubwa kati ya mwanaume na mwanamke, hata ukiwa baunsa na nguvu sana kama uume wako hauutunzi vizuri wewe ni bure tu. mambo yafuatayo ni muhimu kwenye kutunza uume wako.

 1. safisha uume wako na maji ya uvuguvugu angalau mara mbili kwa wiki, safisha korodani, safisha shingo la uume, kichwa cha uume na shingo lake kisha sugua taratibu korodani zako bila kutumia nguvu.
 2. kuacha nywele nyingi sio vizuri, zinaweza kukata ngozi ya uume au uke wakati wa tendo la ndoa, huweza kukata na kupasua kondomu, huleta harufu mbaya na hua chanzo kikuu cha majipu ya sehemu za siri.
 3. usiapuuzie ugonjwa wa uume wako, ukiona upele, jipu, mabadiliko ya rangi au hali  yeyote ambayo sio ya kawaida nenda ukaonane na daktari haraka sana ili upate suluhisho la tatizo linalokusumbua.
 4. wanaume wengi wana tabia ya kuvaa boksa moja wiki nzima au hata mwezi mmoja kabisa, hii inasababisha harufu kali sehemu za siri ambayo haitoki kirahisi. hebu nunua boksa mpya za jumla sokoni uwe nazo hata kumi ila kila siku unavaa boxer safi.[epuka boksa za mtumba ni hatari sana]
 5. chakula unachokula kina madhara kwenye ubora wa mbegu zako, epuka matumizi makubwa ya vitunguu swaumu, pombe, kahawa, vitunguu na viungo vya chakula. kula matunda yenye sukari ya asili kama maembe, maepo,machungwa na kula asali pia.zinafanya mbegu zako ziwe vizuri na kutoa mtoto mwenye afya.
 6. usitumie urembo wowote kwenye uume kama pafyumu, poda au manukato yeyote ya kufanya panukie. uume hautakiwi unukie, hiyo ni sehemu ya kazi tu. unaweza kusababisha michubuko na magonjwa ya ajabu.
 7. epuka kutumia dawa za kunyoa nywele kwenye sehemu zako za siri, zile dawa zina kemikali nyingi ambazo zinaweza kuharibu utengenezaji wa mbegu zako na kukuletea kansa na magonjwa mengine ya ajabu.tumia mkasi au mashine kunyoa.
 8. kama mwanaume vaa boksa ambazo zinakuachia hewa na ubaridi wa kutosha sehemu za siri, boksa zinazobana sana au uvaaji wa nguo nyingi huleta joto sana kwenye korodani na kuzuia utengenezaji wa mbegu za kiume.
 9. chagua kuvaa boksa zaidi kuliko chupi kwani boksa huacha uume wako ukiwa huru na hata ukuaji wa uume wako unakua mwepesi. watu wengi wanaovaa chupi wana uume uliopinda sababu ya kuulazimisha kulala upande fulani kila siku na hata ukuaji wa uume unazuiliwa.
 10. hakikisha umetailiwa ili uweze kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi, kama hujatailiwa basi vuta ngozi kwa nyuma na uoshe uchafu wa ndani ya uume kila siku.
     kumbuka; uume ni mtukufu kuliko hata upanga wa goliati yule aliyepambana na daudi, lakini mwisho kabisa hakikisha unajifunza kugundua mabadiliko yeyote ya uume wako...inaweza kua ni kansa ya tezi dume ambayo inashika wanaume wengi zaidi ya miaka 50. kansa ya tezi dume ni halisi na inaua watu wengi sana duniani.
kumbuka hii makala sio matusi ila ni elimu, shea kwa rafiki zako wa kike na wa kiume waweze kusoma makala hii na kujifunza.
                                tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                            STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183