data:post.body IFAHAMU TEKNOLOJIA YA KUFUFUA WAFU AMBAYO IMEANZA KUTUMIKA[CYRONICS] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

IFAHAMU TEKNOLOJIA YA KUFUFUA WAFU AMBAYO IMEANZA KUTUMIKA[CYRONICS]

                                                                           
cyronics ni nini?
hii ni tekinolojia ya kuhifadhi miili ya watu waliokufa kwa magonjwa ambayo kwa sasa hayatibiki kwa matumaini kwamba ipo siku moja watafufuliwa tiba ya magonjwa yao itakapopatikana, utaalamu huu unahifadhi mwili kwenye kiwango cha baridi kali sana kwenye nyuzi joto -196. kwa tekinolojia ya sasa uwezo wa kuamsha wafu hao bado haupo lakini wataalamu wanaamini miaka ijayo kitu hicho kitawezekana.
tekinolojia hii sio mfumo wa matibabu ya kawaida yaliyozoeleka, lakini pia tekinolojia hii inaamini kwamba kifo ni hatua ya fulani ya maisha mtu anapitia kabla ya kufika mwisho wa maisha hivyo hatua hii inaweza kuzuiliwa.
hatua za kuhifadhi mwili kwa ajili ya kuufufua baadae huanza ndani ya dakika chache baada ya moyo kusimama kwa kuuhifadhi kwenye baridi kali na kutumia kemikali ambazo zinazuia mwili huo kutoharibiwa na barafu.
dr.james bedford alikua binadamu wa kwanza kuhifadhiwa mwaka 1967,  na mpaka mwaka 2014 miili 250 ilikua imehifadhiwa nchini marekani huku zaidi ya watu 1500 wakijiandikisha kuhifadhiwa siku wakifa pia.

kwanini watu wameamua kuhifadhiwa?
watu wengi waliojiandikisha kwa ajili ya huduma hii wamedai kwamba hawakupenda kufa mapema, wengine wanasema wanataka kuona dunia itakuaje baada ya miaka mingi ijayo, wengine ni wazee ambao wanasema walitamani kuishi zaidi lakini umri umewatupa mkono lakini wanaamini huenda miaka ijayo wanaweza kurudishwa kwenye ujana, wengine wanaamini huenda siku moja dawa ya kuzuia kifo itapatikana na wataishi milele duniani na wapendwa wao. lakini wataalamu wa saikolojia wamesema kwamba kifo hakijawahi kuzoeleka tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia, ile hali ya mtu kujua kwamba ipo siku atakufa na kuoza na kupotea kabisa duniani imekua ikiwatesa wengi sana ndio maana wataalamu wamelazimika kufanya utafiti huu wa maisha mengine.

sayansi inasemaje?
kitaalamu wakati wa upasuaji wa moyo, ubongo wa binadamu unahifadhiwa kwenye joto la chini kama nyuzi choto 18 ili uweze kutoharibika na kuhifadhi kumbukumbu vizuri, kwa kufanya hivi mahitaji ya ubongo ya hewa ya oksijeni, sukari na shughuli zingine hupungua, sasa kwenye cyronics binadamu huwekwa kwenye baridi kali zaidi ya hii kiasi kwamba ubongo unasimama kabisa kufanya kazi na viungo vingine. mtu anayehifadhiwa na miaka 15 baada ya miaka 100 au miak 200 atakua na umri ulele wa miaka 15 yaani bado kijana.
cyronics inaamini kwamba mtu hajafa mpaka pale ubongo wake unavyoharibika au kufa kitaalamu kama 'brain dead' lakini kama moyo wa mtu ukisimama na mkashindwa kumuasha kwa teknolojia ya sasa na ubongo wake bado mzima basi huyo mtu hajafa ila yuko kwenye hatua ya kufa.

gharama yake ikoje?
kwa sasa tekinolojia hii ipo  nchi mbalimbali zilizoendelea kama marekani,urusi,canada, ufaransa na kadhalika... mpaka mwaka 2014 gharama ya kuhifadhi mwili wa mtu anayehitaji ilikua milion 400 za kitanzania kwa kipindi chote utakachohifadhiwa pamoja na ghrama ya kufufuliwa na mara nyingi gharama hizi hulipwa na bima ya afya ambayo ulikua unatumia kipindi cha uhai wako.baadhi ya nchi ambazo hazitoi huduma hii kuna makampuni yanayotoa huduma ya kuusafirisha mwili mpaka nchi inayohifadhi, kwa mfano mwaka huu[2016] binti wa miaka 14 nchini uingereza alipelekwa marekani kwa ajili ya huduma hii. kuna watu wengine waliomba kuhifadhiwa vichwa tu kwani kwani ni wazee sana na wangependa kupata miili mipya na gharama kwao ni chini kidogo.

uhifadhi unafanywaje?
dakika moja baada ya kifo mwili wa mgonjwa huanza kuandaliwa kwa huduma hii, kwanza damu yote hutolewa na kuhifadhiwa sehemu yake, kisha kifua hufunguliwa ili kuufikia moyo, kisha kemikali maalumu ambayo hufanya kazi ya kuzuia kuharibika kwa seli ambapo kunasababishwa na barafu inawekwa kwenye moyo na kusambaa kwenye mishipa yote ya damu, baada ya hapo mwili hutumbukizwa na kuhifadhiwa kwemye hewa ya nitrogen na baridi kali kama tulivyoona mwanzo, na kisha mwili huwekwa kwenye mashine maalumu na kuhifadhiwa huko. wataalamu wanaamini mtu anaweza kukaa humo miaka milioni 24 bila kuharibika, lakini pia umakini unahitajika sana hasa kwenye uhifadhi wa ubongo kwani ndio kumbukumbu zinapohifadhiwa.
"nina kansa ya ubongo, kansa ya maini, kansa ya miguu, kansa ya mapafu na kansa ya damu, najua nitakufa muda sio mrefu lakini naumia sana kumuacha mume wangu na familia yangu lakini pia ninapenda sana kua hai ndio maana nimeamua nihifadhiwe baada ya kufa kwa matumaini ipo siku nitaishi tena" aliongea mama mmoja wa kimarekani kwa uchungu sana alipokua kitandani anasubiri kifo na baadae alifariki na kuhifadhiwa.

ufufuo
wataalamu wa cyronics wanaamini watu waliohifadhiwa watakuja kufufuliwa na tekinolojia ya hali ya juu miaka 100 mpaka 500 ijayo kutokana na kukua kwa fani za bioengeneering,nanotechnology, na nanomedicine.
ufufuo utahitaji kurekebisha viungo vilivyoharibiwa kidogo na barafu, kukosa hewa ya oksijeni kwa muda mrefu na sumu za tekinojia hii ya kuhifadhi lakini pia chanzo cha kifo cha muhusika itabidi kitibiwe kabla ya mtu huyu kurudishiwa uhai.
wataalamu wanaamini miaka ijayo huenda watu hawa wakafufuliwa kirahisi sana kuliko tunavyodhani na wataohifadhiwa miaka ijayo watapata bahati kwani hata tekinolojia ya kuwahifadhi itakua juu sana kuliko sasa hivi.

historia
mwaka 1962 mwalimu wa physics chuo kikuu cha michigan kwa jina la robert ettinger aliandiaka kitabu alichokiita prospect of immortality na kueleza kwamba kuwagandisha watu wanaokufa kwa barafu ni njia rahisi ya kufikia tekinolojia ya matibabu ya miaka ijayo. mwalimu huyo aliongeza kwamba japokua ukigandishwa kwenye barafu ni kifo na huwezi kuamka tena lakini yeye alisema kinachoshindikana mwaka huu kinawezekana baada ya miaka kadhaa ijayo.kama jinsi ukoma ulivyoitesa dunia miaka ya zamani lakini sasa hivi sio tatizo tena.
kuongezea msumari katika hilo mwaka 1955 james lavelock aliwafufua panya waliokua wamegandishwa na kufa  kwenye nyozi joto sifuri na hii ilitoa mwanga mkubwa ya uwezekano wa kuamsha wafu wa kibinadamu.

mapokeo ya jamii..
kumekua na upinzani mkubwa sana katika swala hili kutoka kwa watu wenye imani tofauti, watu wanaoamini dini wamepinga sana hili lakini watu wasioamini dini wameikubali kwa kiasi kikubwa lakini pia baadhi ya wataalamu wa afya bado hawaamini kama kazi hii itawezekana.

watu maarufu waliohifadhiwa
baadhi ya watu maarufu wanaoamini katika hili wamehifadhiwa kusubiri siku ufufuo wao mfano dick clair,hal finney,jerry leaf,tedy william, na james bedford.
                                 
                                            tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                               STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                       0769846183/0653095635

                                                            

0 maoni:

Chapisha Maoni