data:post.body HUU NDIO UPASUAJI WA KWANZA WA KUBADILISHA KICHWA CHA BINADAMU UTAKAOFANYIKA MWAKA 2017. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HUU NDIO UPASUAJI WA KWANZA WA KUBADILISHA KICHWA CHA BINADAMU UTAKAOFANYIKA MWAKA 2017.

                                                                         
tangu kuanza kwa karne ya 20 mpaka leo karne ya 21 yametokea mapinduzi makubwa katika fani ya utaalamu wa afya yaani magonjwa mengi ambayo yalikua hayatibiki yanatibika kwa sasa, upasuaji sasa unafanyika wakati kabla haukuepo, na upimaji wa vimelea vya ndani kabisa kitaalamu kama dna ambavyo vinaweza kutambua baba halisi wa mtoto husika, mahusiano ya ndugu na kutumika katika uhalifu kwa kuangalia alama za vidole navyo hufanyika.
sasa kwa miaka mingi madaktari wamekua wakifanya upasuaji wa kubadilisha viungo kama figo, mapafu, maini, mifupa na vingine vingi lakini upasuaji wa kubadilisha kichwa cha binadamu haujawahi kufanyika wala kujaribiwa huenda kulingana na hatari kubwa na kazi ngumu ambayo inafanywa na kichwa kiasi kwamba huwezi kukitoa kirahisi.
Dr sergio cenivero ambaye ni profesa na daktari bingwa wa upasuaji wa kichwa kutoka huko italia mwakani atafanya upasuaji wa kwanza kutoa kichwa kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
pamoja na hatari kubwa ya upasuaji huo daktari huyo amesema tayari amepata listi kubwa ya watu ambao wanahitaji sana upasuaji huo kutoka nchi mbalimbali duniani.

mgonjwa wa kwanza ni nani?
                                                         
mtu mmoja kutoka urusi kwa jina la valery spiridonov ambaye ni mrusi amejitolea kua wa kwanza kufanyiwa upasuaji huo.
kijana huyu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa mishipa ya fahamu kitaalamu kama werdinig-hoffmans amekua akiishi maisha yake yote kwenye baiskeli ya walemavu.
"leo maisha yangu ni magumu sana kwani nategemea mtu kuniweka na kunishusha kitandani angalau mara mbili kwa siku, hii inanifanya niwe mtegemezi sana hivyo kama kuna njia nyingine ya kunisaidia na kusaidia wengine ngoja ijaribiwe"

upasuaji huu utafanyika vipi?

timu ya wataalamu 150 watakuepo kwenye upasuji huu na madakatri bingwa 36 watahusika moja kwa moja kumpasua mgonjwa huyu.
kazi ya kwanza itakua kugandisha kichwa cha mgonjwa huyu kwenye barafu kuzuia seli za ubongo kufa kisha shingo litakatwa na mirija maalumu ya kupeleka damu kichwani itawekwa.
kisha itafuata sehemu ngumu zaidi ya kazi hii ambapo mfupa wa mgongo yaani spinal cord utakatwa na kisu maalumu kilichotengeneza kwa almasi na kwenda kuwekwa kwenye mwili wa mtu mwingine[huu ni mwili wa mtu aliyefariki uliohifadhiwa vizuri].
kisha kichwa kitaunganishwa na gundi maalumu kwenye mifupa ya mgongo na na misuli, mishipa ya damu na ngozi vitashonwa mahala pake.

kujaribu sayansi hii

dr conavaro anasema tutajaribu kwanza upasuaji huu kwa wagonjwa ambao ubongo wao hauna kazi tena na wanasubiri kufa[braib dead]
"tutakata mfupa wa mgongo kisha tutafuatilia maendeleo yake ndani ya masaa 6 mpaka 12, tunayo dawa maalumu ambayo tukiweka pale tunapata matokeo ya kutisha.
wakati mwingine watu wana kuja hospitali mashingo yakiwa yamekatika kwa zaidi ya asilimia tisini lakini wanapona. tumejaribu kitu hiki kwa mbwa na mbwa huyo alikua anakimbia baada ya wki mbili, narudia alikua anakimbia" aliongezea profesa huyo.

sayansi inasemaje?

madaktari bingwa kutoka sehemu zingine wamekua wanampinga profesa huyu wakidai kwamba kitu hicho hakiwezekani.
lakini profesa huyu anasisitiza mafanikio ni zaidi ya asilimia tisini.
"pale kila kitu kitakapokua sawa kuna uhakika wa mafanikio zaidi ya asilimia tisini na mgonjwa ataanza kutembea mwenyewe au kwa kusaidiwa kwa mazoezi ndani ya mwezi mmoja"
"sasa hivi tunaleta tumaini kwa watu wengi ambao wamekua wakiangushwa na mfumo wa kimagharibi wa matibabu'
"hatutaki uongo tena kwani medicine ya sasa ina uwezo wa kucheza na chembe chembe za uhai yaani genes na kuzibadilisha" alizungumza daktari huyu wakati akiongea na kipindi cha newsbeat huko ungereza.
unaweza tembelea pia blog yetu ya kingereza hapa www.secretsofgoodhealth258.blogspot.com

                                                             STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183


0 maoni:

Chapisha Maoni