data:post.body HIZI NDIO CHANJO MUHIMU SANA KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO CHANJO MUHIMU SANA KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO.

                                                                       
ili mtoto akue akiwa na afya bora na isiyo na mgogoro basi anatakiwa apate chanjo zote muhimu za utotoni ambazo ndio msingi mkuu wa kuzuia vifo vingi vya watoto, ukuaji mzuri na kuzuia kudumaa.
kumekua na imani potofu kuhusu chanjo za watoto na kuna baadhi ya wazazi hawawapeleki kabisa watoto wao kupata chanjo hata kama zinapatikana karibu yao, na kitu kinachoshangaza zaidi chanjo hizi hutolewa bure kabisa bila malipo yeyote hivyo ni jukumu la mzazi kuhakikisha mwanae kapata chanjo zote kwa kukagua kadi yake ya kliniki.
zifuatazo ni chanjo ambazo mtoto anatakiwa azipate zote kwa muongozo wa hapa tanzania..
siku ya kuzaliwa; hii ni siku mtoto anatoka tumboni mwa mama yake, siku hii mtoto anatakiwa apate chanjo ya kifua kikuu kitaalamu kama bcg ambayo inachomwa kwenye bega la kulia chini kidogo ya ngozi kwa kiasi cha 0.05mils, kimsingi chanjo hii inatakiwa iache kovu..pia siku hii mtoto anapewa matone mawili mdomoni kuzuia ugonjwa wa polio ambao ni ugonjwa wa kupooza miguu yote miwili na huleta kilema cha maisha.
baada ya wiki sita;  baada ya wiki ya sita baada ya kuzaliwa mtoto anapewa chanjo ya pili ya polio matone mawili mdomoni, anachomwa chanjo ya pentavalent 1 paja la kushoto ambayo inazuia magonjwa matatu yaani tetenasi[ugonjwa wa mishipa ya fahamu], donda koo[ugonjwa wa koo] na kifaduro[ugonjwa wa mfumo wa hewa]
lakini pia siku hii mtoto huchomwa chanjo ya pcv kwenye paja la kulia kuzuia ugonjwa wa kichomi kitaalamu kama pneumonia ambao ni moja ya magonjwa yanayoua sana baada ya malaria kwa hapa tanzania na mwisho kabisa mtoto hupewa chanjo ya kunywa kitaalamu kama rotal inayozuia kuharisha ambako kunasababishwa na virusi vya rota virus.
wiki ya kumi: wiki ya kumi mtoto hupata chanjo zote ambazo nimezitaja kwenye wiki ya sita yaani kwa awamu ya pili kwa mtiririko uleule bila kuruka chanjo hata moja.
wiki ya kumi na na nne; kipindi hiki mtoto hupata chanjo za marudio lakini baadhi ya chanjo alizochoma wiki ya sita na kumi hupungua hivyo wakati huu hupata chanjo ya polio ya mdomoni, pentavalent ya kuchoma paja la kushoto na pcv ambayo huchomwa paja la kulia.[kazi zake nimezielezea kwenye wiki ya sita.
mwezi wa tisa; kwa mpangilio wa chanzo za nchini tanzania hii ndio chanjo ya mwisho kabisa ya ugonjwa wa surua ambayo inachomwa kwenye mkono wa kushoto.
mwisho;kuna watafiti wamegundua chanjo ya malaria na wanategemea kuanza kuitoa mwaka 2017 na kuisambaza chini ya jangwa la sahara, huenda ikawa ndio mwisho wa vifo vya malaria kwa nchi nyingi zilizo athirika.
                                         tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                              STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                       0653095635\0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni