data:post.body HIZI NDIO CHANJO KUMI MUHIMU ZA MAGONJWA HATARI ZA KUCHOMWA BAADA YA MIAKA 14 NA KUENDELEA ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO CHANJO KUMI MUHIMU ZA MAGONJWA HATARI ZA KUCHOMWA BAADA YA MIAKA 14 NA KUENDELEA

                                                      

chanjo ni nini?
chanjo ni mchanganyiko wa aina fulani ya kemikali inayochomwa kuzuia maambukizi ya magonjwa fulani fulani, mara nyingi zimekua zikionekana zinachomwa sana kwa watoto na watu wengi hapa tanzania na afrika kwa ujumla wanadhani chanjo ni kwa ajili ya watoto tu.
kuna magonjwa yanayoua watu mara kwa mara lakini yanazuilika kwa chanjo tu, bahati mbaya sio chanjo zote zinapatikana nchini hapana, zipo chanjo ambazo hapa kwetu hazipo lakini kama wewe ni mtanzania unaishi nje ya nchi au hua unasafiri kwenda nje unaweza ukazipata, kwa wale ambao wanaishi hapahapa na hua hawasafiri basi ni vizuri kupata hata hizi ambazo tunazo hapa kwetu kwa ajili ya usalama wa maisha yetu.zifuatazo ni chanjo muhimu kwa watu wazima yaani kwanzia miaka 18 na kuendelea.
chanjo ya hepatitis b; hii ni chanjo inayotolewa kuzuia ugonjwa wa maini kitaalamu kwa jina la hepatitis, ugonjwa huu huambukizwa na virusi kitaalamu kwa jina la hepatitis b virus ambavyo hushambulia maini. ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya kugusa virusi hivi kwa njia ya kugusa virusi hivyo vikiwa kwenye damu, mate, kushiriki tendo la ndoa na kadhalika. ugonjwa huu unaambukia na kuua kirahisi sana kuliko hata ukimwi. tafiti zilizofanywa hapa kwetu tanzania zimeonyesha kuwepo kwa wagonjwa wengi wa hepatitis ambao hata hajawajui kama wanaumwa kwani ugonjwa huu unaweza kukaa bila dalili. ugonjwa huu husabaisha kansa ya maini au makovu ya maini[liver cirrhosis] ambavyo ndio vyanzo vikuu vya vifo kwa wagonjwa hawa. chanjo hii inapatikana japokua sio kirahisi sana na wanafunzi wote wanaosoma afya au watumishi ni lazima wachome hii kwani wao wana hatari kubwa ya maambukizi kutokana na kazi zao.
chanjo ya human papiloma virus; kirusi cha human papiloma mara nyingi huambukizwa kwa ngono kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine na watu wanashiriki ngono na wapenzi wengi ndio wako kwenye hatari kubwa ya kupata kirusi hichi. tafiti nchini marekani zinasema kwenye watu wanne basi mmoja wao ana kirusi hicho. kirusi hichi husababisha kansa ya mlango wa uzazi[cervix] ambayo ianua mamilioni ya watu kila mwaka duniani.
chanjo ya yellow fever ; yellow fever ni ugonjwa unaosabaishwa na kirusi kwa jina la flavivirus, ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya mbu na mara nyingi hushambulia sehemu moja ghafla kwa wakati mmoja. ugonjwa huu hauna dawa na mara nyingi huua watu ndani ya muda mfupi sana.dalili yake kuu ni kutokwa na damu kwenye matundu yote ya mwili kama macho, masikio, mdomoni, sehemu za siri na kadhalika.chanjo yake inapatikana tanzania na sheria ya nchi kwa sasa huwezi kusafiri kwenda nje ya nchi bila kupata chanjo hii.
chanjo ya tetenasi; tetenasi ni ugonjwa unasababishwa na bacteria kitaaalamu kwa jina clostridium perfringens, hushambulia mtu mara nyingi baada ya kupata kidonda ambacho wadudu hawa huingia baada ya kidonda kutohudumiwa vizuri. ugonjwa huu hushambulia mishipa ya fahamu na kuleta degedege kali na baadae kifo.chanjo ya kuzuia tetenasi kabisa inapatikana mahospitalini ukiachana na ile moja ambayo watu huchomwa mara moja baada ya kuumia unaweza ukachomwa hata sasa hivi na usichome tena.
chanjo ya homa ya uti wa mgongo; ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis ni hatari sana na huua watu wengi hasa unaposhambulia eneo fulani kwa wakati mmoja..wanaobahatika kupona ugonjwa huu mara nyingi hawana akili nzuri. ugonjwa huu hushambulia sana maeneo watu wanaishi kwenye mikusanyiko mikubwa na hewa kidogo kama watoto wanaokaa bweni na wafungwa lakini hata watu wa kawaida hupata.
chanjo ya kichaa cha mbwa; hii ni chanjo ambayo hutolewa mara moja baada ya mgonjwa kungatwa na mbwa ambaye amesadikika ana kichaa tayari. chanjo hii ni muhimu sana kwani ukishonyesha dalili za kichaa cha mbwa kama kubweka kama mbwa na kuogopa maji huwezi kupona kwenye hospitali yeyote ile duniani.
chanjo ya kipindupindu; hii ni aina ya chanjo ambayo hutolewa pale tu ugonjwa huu unapozuka hivyo kama ugonjwa haujaanza hutakiwi kupewa. inazuia ugonjwa huu kwa zaidi ya 98% miezi sita ya kwanza, 50 mpaka 75% miezi sita inayofuata na chini ya 50% mwaka wa pili na kuendelea. kwa hapa nchini haitolewi hata ugonjwa huu ukianza huenda sababu ya bajeti  au sera lakini kuna mashirika kama ya wakimbizi huchoma wafanyakazi wao ugonjwa unapoanza hapa nchini.
chanjo ya mkanda wa jeshi; huu ugonjwa kitaalamu unaitwa herpes zooster, huambukizwa na virusi kwa jina la herpes zooster...mara nyingi ugonjwa huu huwapata watu ambao kinga zao zimeshuka kwasababu ya magonjwa kama ukimwi, kansa, kisukari na lishe mbaya. ni ugonjwa unaosababisha maumivu makali ya sehemu zinazoathirika na kuacha makovu ya kudumu kama umeungua na moto vile.watu walioko kwenye hatari na hata ambao hawapo kwenye hatari ni vizuri kupata chanjo hii.. hapa kwetu haipo.
chanjo ya ugonjwa wa typoid; ugonjwa huu unafamika kama homa ya matumbo, ni ugonjwa unaoshambulia watu wengi hasa maeneo ya afrika, usipogundulika mapema huweza kuua kwa kutoboa utumbo wa binadamu na kusababisha bacteria kuingia ndani ya damu kusambaa mwili mzima. hapa nchini chanjo hii haipo.
chanjo ya ugonjwa wa kimeta; huu ni ugonjwa kitaalamu kwa jina la anthrax, ni ugonjwa hatari sana unaoambukizwa kutoka kwa wanyama au mifugo inayoumwa ugonjwa huu. mgonjwa huambukizwa kwa kugusa ngozi au nyama ya mnyama aliyeathirika. ugonjwa hushambulia ngozi, tumbo au mapafu. uwezekano wa kufa kwa kimeta ambaye anasababishwa na bacteria kwa jina kwa bacillus anthracis ni zaidi ya 80%. kwa nchi zilizoendelea chanjo ya ugonjwa huu hutolewa kwa watu wote wanaomiliki mifugo au waliko hatarini lakini pia nchi nyingi duniani zimetengeneza silaha za kijeshi kwa kutumia bacteria ili zitumike vitani.
 
                                                              STAY ALIVE
                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni