data:post.body Novemba 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

IFAHAMU TEKNOLOJIA YA KUFUFUA WAFU AMBAYO IMEANZA KUTUMIKA[CYRONICS]

                                                                           
cyronics ni nini?
hii ni tekinolojia ya kuhifadhi miili ya watu waliokufa kwa magonjwa ambayo kwa sasa hayatibiki kwa matumaini kwamba ipo siku moja watafufuliwa tiba ya magonjwa yao itakapopatikana, utaalamu huu unahifadhi mwili kwenye kiwango cha baridi kali sana kwenye nyuzi joto -196. kwa tekinolojia ya sasa uwezo wa kuamsha wafu hao bado haupo lakini wataalamu wanaamini miaka ijayo kitu hicho kitawezekana.
tekinolojia hii sio mfumo wa matibabu ya kawaida yaliyozoeleka, lakini pia tekinolojia hii inaamini kwamba kifo ni hatua ya fulani ya maisha mtu anapitia kabla ya kufika mwisho wa maisha hivyo hatua hii inaweza kuzuiliwa.
hatua za kuhifadhi mwili kwa ajili ya kuufufua baadae huanza ndani ya dakika chache baada ya moyo kusimama kwa kuuhifadhi kwenye baridi kali na kutumia kemikali ambazo zinazuia mwili huo kutoharibiwa na barafu.
dr.james bedford alikua binadamu wa kwanza kuhifadhiwa mwaka 1967,  na mpaka mwaka 2014 miili 250 ilikua imehifadhiwa nchini marekani huku zaidi ya watu 1500 wakijiandikisha kuhifadhiwa siku wakifa pia.

kwanini watu wameamua kuhifadhiwa?
watu wengi waliojiandikisha kwa ajili ya huduma hii wamedai kwamba hawakupenda kufa mapema, wengine wanasema wanataka kuona dunia itakuaje baada ya miaka mingi ijayo, wengine ni wazee ambao wanasema walitamani kuishi zaidi lakini umri umewatupa mkono lakini wanaamini huenda miaka ijayo wanaweza kurudishwa kwenye ujana, wengine wanaamini huenda siku moja dawa ya kuzuia kifo itapatikana na wataishi milele duniani na wapendwa wao. lakini wataalamu wa saikolojia wamesema kwamba kifo hakijawahi kuzoeleka tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia, ile hali ya mtu kujua kwamba ipo siku atakufa na kuoza na kupotea kabisa duniani imekua ikiwatesa wengi sana ndio maana wataalamu wamelazimika kufanya utafiti huu wa maisha mengine.

sayansi inasemaje?
kitaalamu wakati wa upasuaji wa moyo, ubongo wa binadamu unahifadhiwa kwenye joto la chini kama nyuzi choto 18 ili uweze kutoharibika na kuhifadhi kumbukumbu vizuri, kwa kufanya hivi mahitaji ya ubongo ya hewa ya oksijeni, sukari na shughuli zingine hupungua, sasa kwenye cyronics binadamu huwekwa kwenye baridi kali zaidi ya hii kiasi kwamba ubongo unasimama kabisa kufanya kazi na viungo vingine. mtu anayehifadhiwa na miaka 15 baada ya miaka 100 au miak 200 atakua na umri ulele wa miaka 15 yaani bado kijana.
cyronics inaamini kwamba mtu hajafa mpaka pale ubongo wake unavyoharibika au kufa kitaalamu kama 'brain dead' lakini kama moyo wa mtu ukisimama na mkashindwa kumuasha kwa teknolojia ya sasa na ubongo wake bado mzima basi huyo mtu hajafa ila yuko kwenye hatua ya kufa.

gharama yake ikoje?
kwa sasa tekinolojia hii ipo  nchi mbalimbali zilizoendelea kama marekani,urusi,canada, ufaransa na kadhalika... mpaka mwaka 2014 gharama ya kuhifadhi mwili wa mtu anayehitaji ilikua milion 400 za kitanzania kwa kipindi chote utakachohifadhiwa pamoja na ghrama ya kufufuliwa na mara nyingi gharama hizi hulipwa na bima ya afya ambayo ulikua unatumia kipindi cha uhai wako.baadhi ya nchi ambazo hazitoi huduma hii kuna makampuni yanayotoa huduma ya kuusafirisha mwili mpaka nchi inayohifadhi, kwa mfano mwaka huu[2016] binti wa miaka 14 nchini uingereza alipelekwa marekani kwa ajili ya huduma hii. kuna watu wengine waliomba kuhifadhiwa vichwa tu kwani kwani ni wazee sana na wangependa kupata miili mipya na gharama kwao ni chini kidogo.

uhifadhi unafanywaje?
dakika moja baada ya kifo mwili wa mgonjwa huanza kuandaliwa kwa huduma hii, kwanza damu yote hutolewa na kuhifadhiwa sehemu yake, kisha kifua hufunguliwa ili kuufikia moyo, kisha kemikali maalumu ambayo hufanya kazi ya kuzuia kuharibika kwa seli ambapo kunasababishwa na barafu inawekwa kwenye moyo na kusambaa kwenye mishipa yote ya damu, baada ya hapo mwili hutumbukizwa na kuhifadhiwa kwemye hewa ya nitrogen na baridi kali kama tulivyoona mwanzo, na kisha mwili huwekwa kwenye mashine maalumu na kuhifadhiwa huko. wataalamu wanaamini mtu anaweza kukaa humo miaka milioni 24 bila kuharibika, lakini pia umakini unahitajika sana hasa kwenye uhifadhi wa ubongo kwani ndio kumbukumbu zinapohifadhiwa.
"nina kansa ya ubongo, kansa ya maini, kansa ya miguu, kansa ya mapafu na kansa ya damu, najua nitakufa muda sio mrefu lakini naumia sana kumuacha mume wangu na familia yangu lakini pia ninapenda sana kua hai ndio maana nimeamua nihifadhiwe baada ya kufa kwa matumaini ipo siku nitaishi tena" aliongea mama mmoja wa kimarekani kwa uchungu sana alipokua kitandani anasubiri kifo na baadae alifariki na kuhifadhiwa.

ufufuo
wataalamu wa cyronics wanaamini watu waliohifadhiwa watakuja kufufuliwa na tekinolojia ya hali ya juu miaka 100 mpaka 500 ijayo kutokana na kukua kwa fani za bioengeneering,nanotechnology, na nanomedicine.
ufufuo utahitaji kurekebisha viungo vilivyoharibiwa kidogo na barafu, kukosa hewa ya oksijeni kwa muda mrefu na sumu za tekinojia hii ya kuhifadhi lakini pia chanzo cha kifo cha muhusika itabidi kitibiwe kabla ya mtu huyu kurudishiwa uhai.
wataalamu wanaamini miaka ijayo huenda watu hawa wakafufuliwa kirahisi sana kuliko tunavyodhani na wataohifadhiwa miaka ijayo watapata bahati kwani hata tekinolojia ya kuwahifadhi itakua juu sana kuliko sasa hivi.

historia
mwaka 1962 mwalimu wa physics chuo kikuu cha michigan kwa jina la robert ettinger aliandiaka kitabu alichokiita prospect of immortality na kueleza kwamba kuwagandisha watu wanaokufa kwa barafu ni njia rahisi ya kufikia tekinolojia ya matibabu ya miaka ijayo. mwalimu huyo aliongeza kwamba japokua ukigandishwa kwenye barafu ni kifo na huwezi kuamka tena lakini yeye alisema kinachoshindikana mwaka huu kinawezekana baada ya miaka kadhaa ijayo.kama jinsi ukoma ulivyoitesa dunia miaka ya zamani lakini sasa hivi sio tatizo tena.
kuongezea msumari katika hilo mwaka 1955 james lavelock aliwafufua panya waliokua wamegandishwa na kufa  kwenye nyozi joto sifuri na hii ilitoa mwanga mkubwa ya uwezekano wa kuamsha wafu wa kibinadamu.

mapokeo ya jamii..
kumekua na upinzani mkubwa sana katika swala hili kutoka kwa watu wenye imani tofauti, watu wanaoamini dini wamepinga sana hili lakini watu wasioamini dini wameikubali kwa kiasi kikubwa lakini pia baadhi ya wataalamu wa afya bado hawaamini kama kazi hii itawezekana.

watu maarufu waliohifadhiwa
baadhi ya watu maarufu wanaoamini katika hili wamehifadhiwa kusubiri siku ufufuo wao mfano dick clair,hal finney,jerry leaf,tedy william, na james bedford.
                                 
                                            tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                               STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                       0769846183/0653095635

                                                            

JE NI LINI UNATAKIWA UANZE KUSHIRIKI TENDO LA NDOA BAADA YA KUJIFUNGUA?

                                                               
hili ni swali wanawake wengi hujiuliza baada ya kujifungua, lakini kitaalamu ni kwamba uwe umezaa kwa upasuaji au kwa njia ya kawaida hutakiwi kushiriki tendo la ndoa mpaka wiki sita ziishe na wiki sita sikishaisha wewe mwanamke unaweza kujitafakari kama uko tayari au bado kwa ajili ya tendo hilo yaani kwa sababu za kisaikolojia zaidi yaani uchovu na msongo wa mawazo.
je kwanini sio vizuri kushiriki tendo la ndoa kabla ya wiki ya sita?
maumivu kipindi cha tendo la ndoa; hii husababishwa na mabadiliko makubwa ya viwango vya homoni mwilini hasa kupanda kwa homoni ya kutoa maziwa ya mama kitaalamu kama prolactin na kushuka kwa homoni za uzazi yaani progesterone na eostrogen, hii inaweza kusababisha uke kuwa mkavu sana na kuleta maumivu wakati wa tendo.
nini cha kufanya? muuleze kistaarabu mpenzi wako kuhusu hili na aelewe kwamba ukavu wako hausababishwi na kupungua kwa mapenzi yako kwake, lakini hata baada ya wiki ya sita ukavu huu unaweza kuendelea hivyo mnaweza kutumia vilainishi kama ky gel kusaidia hili.
ladha ya tendo la ndoa haitakua kama mwanzo; hii ni sababu ya kupanuka sana kwa misuli ya uke hivyo mwanamke anakua hausikii vizuri uume kama mwanzo na unaweza kuona kama hakuna ladha tena.
nini cha kufanya?
fanya mazoezi ya kegel, mazoezi haya yaligunduliwa na doctor arnord kegel mwaka 1948 ambaye alikua bingwa wa magonjwa ya kina mama yaani obstretic and gynacology specialist..mazoezi haya hufanywa kwa kubana msuli ambao unautumia kuzuia mkojo wakati wa kukojoa, sasa bana msuli huu wakati hauna mkojo kwa sekunde kumi na kuachia kwa sekunde kumi...fanya mara tatu asubuhi mchana na jioni na uke wako utarudi kua mdogo kama zamani.
matiti baada yanatoa maziwa mengi; hii inaweza ikafanya tendo la ndoa lisiwe la furaha sana hasa wakati mwanamke anafika kileleni maziwa yanaweza kumwagika mengi sana na hii pia inaweza kuendelea mpaka zaidi ya wiki ya sita sababu mtoto anakua bado anaendelea kunyonya na hata usipompa titi maziwa yataendelea kutoka.
nini cha kufanya? jitahidi kuvaa sidiria nzito wakati wa tendo la ndoa kuzuia hali hii ambayo inaweza isiwe nzuri hasa kwa mwenzi wako.
huna amani na mwili wako; huchukua mpaka miezi miwili kwa tumbo la uzazi kurudi kwenye hali yake ya zamani. yaani mtu akizaa anakua bado anamuonekano wa mtu mwenye ujauzito wa miezi sita, na kurudi kwenye uzito wa zamani inaweza kuchukua mpaka mwaka mmoja kama ukifanya mazoezi na usipofanya unaweza kubaki vilevile au kuongezeka.[watanzania wengi hawafanyi mazozi baada ya kuzaa na hunenepa zaidi]
nini cha kufanya?
usiwe na wasiwasi sana kwani mume wako anaelewa mabadiliko ya mwili wako yanasababishwa na uzazi, lakini pia penda ulichokipata kwani mpaka umepata huyo mtoto umepitia mateso makubwa ya jasho na damu. kikubwa anza mazoezi pale utakapokua tayari.
kuna hatari ya kubeba mimba nyingine; japokua uwezekano wa kubeba mimba nyingine baada ya kujifungua hua ni mdogo sana lakini sio kwamba haiwezekani kabisa kwani mimi binafsi nimekutana na watu waliobeba mimba kipindi hiki. hii ni sababu ya kuchelewa kuanza kuona siku zako za hedhi na kutoona siku zako kunaweza kukufanya ushindwe kuhesabu siku zako za  hatari.
vidonda bado havijapona; kama ulizaa kwa upasuaji au njia ya kawaida bado kuna vidonda ndani ya uke na uzazi ambavyo vilisababishwa na mtoto kupita ukiachilia mbali kidonda cha upasuaji ambacho mara nyingi hua hakina hali nzuri kabla ya wiki ya 6. hivyo ukishiriki tendo la ndoa unaweza kusababisha magonjwa yaani infection na kuugua, kusabaisha kuachia kwa mshono wa upasuaji au kuhatarisha afya ya kizazi kwa ajili ya watoto wajao.
nini cha kufanya?
mueleweshe mume wako kuhusu uwezekano wa kupata magonjwa na atakuelewa.
mwisho;hali hii ni ya muda tu, wewe kama mwanamke kua mstari wa mbele kuhakikisha unapona mapema na kurudi katika hali yako ya zamani, ndoa nyingi huanza kuharibika hapa kwani wanawake hutumia nafasi hii kuwanyima unyumba waume zao kwa muda mrefu sana kwa kisingizio cha uzazi huku wakisahau kwamba huko nje kuna wakware wanasubiri ushindwe huku ndani wambebe mumeo.
                                       tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                             STAY ALIVE
                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183
                                        
                         karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]
                                               

HIZI NDIO CHANJO MUHIMU SANA KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO.

                                                                       
ili mtoto akue akiwa na afya bora na isiyo na mgogoro basi anatakiwa apate chanjo zote muhimu za utotoni ambazo ndio msingi mkuu wa kuzuia vifo vingi vya watoto, ukuaji mzuri na kuzuia kudumaa.
kumekua na imani potofu kuhusu chanjo za watoto na kuna baadhi ya wazazi hawawapeleki kabisa watoto wao kupata chanjo hata kama zinapatikana karibu yao, na kitu kinachoshangaza zaidi chanjo hizi hutolewa bure kabisa bila malipo yeyote hivyo ni jukumu la mzazi kuhakikisha mwanae kapata chanjo zote kwa kukagua kadi yake ya kliniki.
zifuatazo ni chanjo ambazo mtoto anatakiwa azipate zote kwa muongozo wa hapa tanzania..
siku ya kuzaliwa; hii ni siku mtoto anatoka tumboni mwa mama yake, siku hii mtoto anatakiwa apate chanjo ya kifua kikuu kitaalamu kama bcg ambayo inachomwa kwenye bega la kulia chini kidogo ya ngozi kwa kiasi cha 0.05mils, kimsingi chanjo hii inatakiwa iache kovu..pia siku hii mtoto anapewa matone mawili mdomoni kuzuia ugonjwa wa polio ambao ni ugonjwa wa kupooza miguu yote miwili na huleta kilema cha maisha.
baada ya wiki sita;  baada ya wiki ya sita baada ya kuzaliwa mtoto anapewa chanjo ya pili ya polio matone mawili mdomoni, anachomwa chanjo ya pentavalent 1 paja la kushoto ambayo inazuia magonjwa matatu yaani tetenasi[ugonjwa wa mishipa ya fahamu], donda koo[ugonjwa wa koo] na kifaduro[ugonjwa wa mfumo wa hewa]
lakini pia siku hii mtoto huchomwa chanjo ya pcv kwenye paja la kulia kuzuia ugonjwa wa kichomi kitaalamu kama pneumonia ambao ni moja ya magonjwa yanayoua sana baada ya malaria kwa hapa tanzania na mwisho kabisa mtoto hupewa chanjo ya kunywa kitaalamu kama rotal inayozuia kuharisha ambako kunasababishwa na virusi vya rota virus.
wiki ya kumi: wiki ya kumi mtoto hupata chanjo zote ambazo nimezitaja kwenye wiki ya sita yaani kwa awamu ya pili kwa mtiririko uleule bila kuruka chanjo hata moja.
wiki ya kumi na na nne; kipindi hiki mtoto hupata chanjo za marudio lakini baadhi ya chanjo alizochoma wiki ya sita na kumi hupungua hivyo wakati huu hupata chanjo ya polio ya mdomoni, pentavalent ya kuchoma paja la kushoto na pcv ambayo huchomwa paja la kulia.[kazi zake nimezielezea kwenye wiki ya sita.
mwezi wa tisa; kwa mpangilio wa chanzo za nchini tanzania hii ndio chanjo ya mwisho kabisa ya ugonjwa wa surua ambayo inachomwa kwenye mkono wa kushoto.
mwisho;kuna watafiti wamegundua chanjo ya malaria na wanategemea kuanza kuitoa mwaka 2017 na kuisambaza chini ya jangwa la sahara, huenda ikawa ndio mwisho wa vifo vya malaria kwa nchi nyingi zilizo athirika.
                                         tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                              STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                       0653095635\0769846183

HIZI NDIO CHANJO KUMI MUHIMU ZA MAGONJWA HATARI ZA KUCHOMWA BAADA YA MIAKA 14 NA KUENDELEA

                                                      

chanjo ni nini?
chanjo ni mchanganyiko wa aina fulani ya kemikali inayochomwa kuzuia maambukizi ya magonjwa fulani fulani, mara nyingi zimekua zikionekana zinachomwa sana kwa watoto na watu wengi hapa tanzania na afrika kwa ujumla wanadhani chanjo ni kwa ajili ya watoto tu.
kuna magonjwa yanayoua watu mara kwa mara lakini yanazuilika kwa chanjo tu, bahati mbaya sio chanjo zote zinapatikana nchini hapana, zipo chanjo ambazo hapa kwetu hazipo lakini kama wewe ni mtanzania unaishi nje ya nchi au hua unasafiri kwenda nje unaweza ukazipata, kwa wale ambao wanaishi hapahapa na hua hawasafiri basi ni vizuri kupata hata hizi ambazo tunazo hapa kwetu kwa ajili ya usalama wa maisha yetu.zifuatazo ni chanjo muhimu kwa watu wazima yaani kwanzia miaka 18 na kuendelea.
chanjo ya hepatitis b; hii ni chanjo inayotolewa kuzuia ugonjwa wa maini kitaalamu kwa jina la hepatitis, ugonjwa huu huambukizwa na virusi kitaalamu kwa jina la hepatitis b virus ambavyo hushambulia maini. ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya kugusa virusi hivi kwa njia ya kugusa virusi hivyo vikiwa kwenye damu, mate, kushiriki tendo la ndoa na kadhalika. ugonjwa huu unaambukia na kuua kirahisi sana kuliko hata ukimwi. tafiti zilizofanywa hapa kwetu tanzania zimeonyesha kuwepo kwa wagonjwa wengi wa hepatitis ambao hata hajawajui kama wanaumwa kwani ugonjwa huu unaweza kukaa bila dalili. ugonjwa huu husabaisha kansa ya maini au makovu ya maini[liver cirrhosis] ambavyo ndio vyanzo vikuu vya vifo kwa wagonjwa hawa. chanjo hii inapatikana japokua sio kirahisi sana na wanafunzi wote wanaosoma afya au watumishi ni lazima wachome hii kwani wao wana hatari kubwa ya maambukizi kutokana na kazi zao.
chanjo ya human papiloma virus; kirusi cha human papiloma mara nyingi huambukizwa kwa ngono kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine na watu wanashiriki ngono na wapenzi wengi ndio wako kwenye hatari kubwa ya kupata kirusi hichi. tafiti nchini marekani zinasema kwenye watu wanne basi mmoja wao ana kirusi hicho. kirusi hichi husababisha kansa ya mlango wa uzazi[cervix] ambayo ianua mamilioni ya watu kila mwaka duniani.
chanjo ya yellow fever ; yellow fever ni ugonjwa unaosabaishwa na kirusi kwa jina la flavivirus, ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya mbu na mara nyingi hushambulia sehemu moja ghafla kwa wakati mmoja. ugonjwa huu hauna dawa na mara nyingi huua watu ndani ya muda mfupi sana.dalili yake kuu ni kutokwa na damu kwenye matundu yote ya mwili kama macho, masikio, mdomoni, sehemu za siri na kadhalika.chanjo yake inapatikana tanzania na sheria ya nchi kwa sasa huwezi kusafiri kwenda nje ya nchi bila kupata chanjo hii.
chanjo ya tetenasi; tetenasi ni ugonjwa unasababishwa na bacteria kitaaalamu kwa jina clostridium perfringens, hushambulia mtu mara nyingi baada ya kupata kidonda ambacho wadudu hawa huingia baada ya kidonda kutohudumiwa vizuri. ugonjwa huu hushambulia mishipa ya fahamu na kuleta degedege kali na baadae kifo.chanjo ya kuzuia tetenasi kabisa inapatikana mahospitalini ukiachana na ile moja ambayo watu huchomwa mara moja baada ya kuumia unaweza ukachomwa hata sasa hivi na usichome tena.
chanjo ya homa ya uti wa mgongo; ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis ni hatari sana na huua watu wengi hasa unaposhambulia eneo fulani kwa wakati mmoja..wanaobahatika kupona ugonjwa huu mara nyingi hawana akili nzuri. ugonjwa huu hushambulia sana maeneo watu wanaishi kwenye mikusanyiko mikubwa na hewa kidogo kama watoto wanaokaa bweni na wafungwa lakini hata watu wa kawaida hupata.
chanjo ya kichaa cha mbwa; hii ni chanjo ambayo hutolewa mara moja baada ya mgonjwa kungatwa na mbwa ambaye amesadikika ana kichaa tayari. chanjo hii ni muhimu sana kwani ukishonyesha dalili za kichaa cha mbwa kama kubweka kama mbwa na kuogopa maji huwezi kupona kwenye hospitali yeyote ile duniani.
chanjo ya kipindupindu; hii ni aina ya chanjo ambayo hutolewa pale tu ugonjwa huu unapozuka hivyo kama ugonjwa haujaanza hutakiwi kupewa. inazuia ugonjwa huu kwa zaidi ya 98% miezi sita ya kwanza, 50 mpaka 75% miezi sita inayofuata na chini ya 50% mwaka wa pili na kuendelea. kwa hapa nchini haitolewi hata ugonjwa huu ukianza huenda sababu ya bajeti  au sera lakini kuna mashirika kama ya wakimbizi huchoma wafanyakazi wao ugonjwa unapoanza hapa nchini.
chanjo ya mkanda wa jeshi; huu ugonjwa kitaalamu unaitwa herpes zooster, huambukizwa na virusi kwa jina la herpes zooster...mara nyingi ugonjwa huu huwapata watu ambao kinga zao zimeshuka kwasababu ya magonjwa kama ukimwi, kansa, kisukari na lishe mbaya. ni ugonjwa unaosababisha maumivu makali ya sehemu zinazoathirika na kuacha makovu ya kudumu kama umeungua na moto vile.watu walioko kwenye hatari na hata ambao hawapo kwenye hatari ni vizuri kupata chanjo hii.. hapa kwetu haipo.
chanjo ya ugonjwa wa typoid; ugonjwa huu unafamika kama homa ya matumbo, ni ugonjwa unaoshambulia watu wengi hasa maeneo ya afrika, usipogundulika mapema huweza kuua kwa kutoboa utumbo wa binadamu na kusababisha bacteria kuingia ndani ya damu kusambaa mwili mzima. hapa nchini chanjo hii haipo.
chanjo ya ugonjwa wa kimeta; huu ni ugonjwa kitaalamu kwa jina la anthrax, ni ugonjwa hatari sana unaoambukizwa kutoka kwa wanyama au mifugo inayoumwa ugonjwa huu. mgonjwa huambukizwa kwa kugusa ngozi au nyama ya mnyama aliyeathirika. ugonjwa hushambulia ngozi, tumbo au mapafu. uwezekano wa kufa kwa kimeta ambaye anasababishwa na bacteria kwa jina kwa bacillus anthracis ni zaidi ya 80%. kwa nchi zilizoendelea chanjo ya ugonjwa huu hutolewa kwa watu wote wanaomiliki mifugo au waliko hatarini lakini pia nchi nyingi duniani zimetengeneza silaha za kijeshi kwa kutumia bacteria ili zitumike vitani.
 
                                                              STAY ALIVE
                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

MFAHAMU DAKTARI WA KWANZA KUFANYA UPASUAJI WA KUBADILISHA MOYO DUNIANI, MZALIWA WA SOUTH AFRIKA.

                                                             
hospitali ya groote schuur ilitazamwa kwa jicho la pili na kupata heshima kubwa duniani kote pale ambapo doctor christiaan barnard alipofanya upasuaji wa kwanza wa kubadilisha moyo katika mji wa western cape huko south africa mwaka 1967.
bahati mbaya mgonjwa alifariki baada ya siku 18 baada ya kuugua ugonjwa mwingine wa mapafu kwa jina la pneumoni lakini mpaka anafariki moyo wake ulikua unafanya kazi vizuri

historia yake.
doctor christiaan benard alizaliwa mwaka 1922 katika mji wa beufort west katika eneo lenye ukame kidogo huko south afrika, baba yake alikua na watoto wanne na familia yake haikua na uwezo huku baba yake akifanya kazi kama pasta.
alicheza mpira na kujifunza muziki lakini baadae aliamua kwenda kusoma udaktari katika chuo kikuu cha cape town hukohuko south africa.
alibahatika kupata ufadhili wa miaka mitatu na akawa anaishi kwa kaka yake huku akitembea kwenda chuoni, fedha ilikua ngumu kwake na hakua na nafasi au uwezo wa kustarehe na maisha yake. tatizo lake lingine lilikua kingereza kwani yeye alikua anajua lugha ya afrikaan ambayo ndio lugha ya nyumbani hivyo ilibidi ajifunze kujieleza kwa kingereza. baada ya miaka sita alimaliza chuo cha udaktari na kufanya internship yaani mwaka wa mazoezi ya kidaktari. baadae alihama kwenda kwenye mji mwingine mdogo na kumuoa mwanamke kwa jina la louwjie.
ndoto zake zilianza baada  moja ya wagonjwa wake kuzaa mtoto ambaye alikua na shida ya moyo na baadae yule mtoto alifariki, ndipo alipoanza kuwaza kwanini moyo usibadilishwe kwenye hali kama hiyo.
baadae aliendelea na masomo katika chuo kikuu cha capetown  na kua daktari bingwa katika fani ya upasuaji wa moyo kitaalamu kama cardiac surgeon,.
baada ya masomo haya alipata nafasi ya kwenda kufanya kazi marekani chini ya dakatri bingwa kwa jina la professor wagensteen aliyekua mtaalamu sana wa mambo ya upasuaji  na hivyo alizidi kukokomaa zaidi kwenye fani hiyo. lakini aliendelea kua na dukuduku kama figo inaweza kubadilishwa kwa nini moyo usibadilishwe? hivyo aliendelea kufanya tafiti mbalimbali.
mwaka 1958 doctor christiaan barnard alirejea south africa huku akiwa anasubiriwa kwa hamu sana katika hospitali aliyokua anafanyia kazi mwanzoni.

upasuaji wa kubadilisha moyo
aliporudi south afrika alifanya maandalizi muhimu na kufanya upasuaji wa kwanza wa kubadilisha figo kwa mafanikio makubwa na kuleta sifa kubwa kwenye hospitali hiyo lakini baadae alimwambia daktari mmoja ambaye alikua mmiliki wa hospitali hiyo kua amefanya maandalizi yote na anaamini upasuaji wa kubadilisha moyo unawezekana kwa kiasi kikubwa.
mwezi wa 11 mwaka 1967 mmiliki wa hospitali hiyo kwa jina la proffesor schirire alimuita doctor chriss na kumwambia kua kuna mgonjwa alikua anashida ya moyo na angekufa muda sio mrefu na alikua tayari kufanyiwa upasuaji huo wa kwanza, mgonjwa huyo kwa jina la washkansky alikua ameugua moyo kwa muda mrefu sana.

binti mmoja kwa jina la denise darvall alikua amepata ajari ya gari na kufariki, baba yake aliombwa moyo wa binti yake uwekwe kwa mgonjwa huyo aliyekua anasumbuliwa na moyo akakubali,  na hapo ndipo historia ya dunia ilipoandikwa yaani kwa mara ya kwanza mwaka tarehe 3 desemba mwaka 1967 upasuaji wa kwanza wa kubadilisha moyo ulifanyika ndani ya masaa tisa ukiwa unashuhudiwa na kusimamiwa na madaktari bingwa wa moyo, bingwa wa usingizi, madaktari bingwa wa mionzi, manesi na wengine wengi walihusika na kuimaliza kwa mafanikio makubwa.
chumba cha upasuaji kilichotumika kufanya upasuaji huu  kwa sasa kimegeuzwa kama makumbusho kwa ajili ya heshima ya wataalamu hawa waliofanya hii kazi.
proffesor barnard christiaan alifariki katika mji wa cyprus huko ugiriki tarehe mbili mwezi wa tisa mwaka 2001 baada ya kupata shambulio la ghafla la ugojwa wa pumu.
doctor barnard christiaan anakumbukwa mpaka leo kwa mchango wake mkubwa uliobadili fikra za watu wengi na miaka iliyofuata upasuaji huo ukiendelea katika hospitali mbalimbali duniani na kuwasaidia wagonjwa wengi.
                                                         STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183

HUU NDIO UPASUAJI WA KWANZA WA KUBADILISHA KICHWA CHA BINADAMU UTAKAOFANYIKA MWAKA 2017.

                                                                         
tangu kuanza kwa karne ya 20 mpaka leo karne ya 21 yametokea mapinduzi makubwa katika fani ya utaalamu wa afya yaani magonjwa mengi ambayo yalikua hayatibiki yanatibika kwa sasa, upasuaji sasa unafanyika wakati kabla haukuepo, na upimaji wa vimelea vya ndani kabisa kitaalamu kama dna ambavyo vinaweza kutambua baba halisi wa mtoto husika, mahusiano ya ndugu na kutumika katika uhalifu kwa kuangalia alama za vidole navyo hufanyika.
sasa kwa miaka mingi madaktari wamekua wakifanya upasuaji wa kubadilisha viungo kama figo, mapafu, maini, mifupa na vingine vingi lakini upasuaji wa kubadilisha kichwa cha binadamu haujawahi kufanyika wala kujaribiwa huenda kulingana na hatari kubwa na kazi ngumu ambayo inafanywa na kichwa kiasi kwamba huwezi kukitoa kirahisi.
Dr sergio cenivero ambaye ni profesa na daktari bingwa wa upasuaji wa kichwa kutoka huko italia mwakani atafanya upasuaji wa kwanza kutoa kichwa kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
pamoja na hatari kubwa ya upasuaji huo daktari huyo amesema tayari amepata listi kubwa ya watu ambao wanahitaji sana upasuaji huo kutoka nchi mbalimbali duniani.

mgonjwa wa kwanza ni nani?
                                                         
mtu mmoja kutoka urusi kwa jina la valery spiridonov ambaye ni mrusi amejitolea kua wa kwanza kufanyiwa upasuaji huo.
kijana huyu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa mishipa ya fahamu kitaalamu kama werdinig-hoffmans amekua akiishi maisha yake yote kwenye baiskeli ya walemavu.
"leo maisha yangu ni magumu sana kwani nategemea mtu kuniweka na kunishusha kitandani angalau mara mbili kwa siku, hii inanifanya niwe mtegemezi sana hivyo kama kuna njia nyingine ya kunisaidia na kusaidia wengine ngoja ijaribiwe"

upasuaji huu utafanyika vipi?

timu ya wataalamu 150 watakuepo kwenye upasuji huu na madakatri bingwa 36 watahusika moja kwa moja kumpasua mgonjwa huyu.
kazi ya kwanza itakua kugandisha kichwa cha mgonjwa huyu kwenye barafu kuzuia seli za ubongo kufa kisha shingo litakatwa na mirija maalumu ya kupeleka damu kichwani itawekwa.
kisha itafuata sehemu ngumu zaidi ya kazi hii ambapo mfupa wa mgongo yaani spinal cord utakatwa na kisu maalumu kilichotengeneza kwa almasi na kwenda kuwekwa kwenye mwili wa mtu mwingine[huu ni mwili wa mtu aliyefariki uliohifadhiwa vizuri].
kisha kichwa kitaunganishwa na gundi maalumu kwenye mifupa ya mgongo na na misuli, mishipa ya damu na ngozi vitashonwa mahala pake.

kujaribu sayansi hii

dr conavaro anasema tutajaribu kwanza upasuaji huu kwa wagonjwa ambao ubongo wao hauna kazi tena na wanasubiri kufa[braib dead]
"tutakata mfupa wa mgongo kisha tutafuatilia maendeleo yake ndani ya masaa 6 mpaka 12, tunayo dawa maalumu ambayo tukiweka pale tunapata matokeo ya kutisha.
wakati mwingine watu wana kuja hospitali mashingo yakiwa yamekatika kwa zaidi ya asilimia tisini lakini wanapona. tumejaribu kitu hiki kwa mbwa na mbwa huyo alikua anakimbia baada ya wki mbili, narudia alikua anakimbia" aliongezea profesa huyo.

sayansi inasemaje?

madaktari bingwa kutoka sehemu zingine wamekua wanampinga profesa huyu wakidai kwamba kitu hicho hakiwezekani.
lakini profesa huyu anasisitiza mafanikio ni zaidi ya asilimia tisini.
"pale kila kitu kitakapokua sawa kuna uhakika wa mafanikio zaidi ya asilimia tisini na mgonjwa ataanza kutembea mwenyewe au kwa kusaidiwa kwa mazoezi ndani ya mwezi mmoja"
"sasa hivi tunaleta tumaini kwa watu wengi ambao wamekua wakiangushwa na mfumo wa kimagharibi wa matibabu'
"hatutaki uongo tena kwani medicine ya sasa ina uwezo wa kucheza na chembe chembe za uhai yaani genes na kuzibadilisha" alizungumza daktari huyu wakati akiongea na kipindi cha newsbeat huko ungereza.
unaweza tembelea pia blog yetu ya kingereza hapa www.secretsofgoodhealth258.blogspot.com

                                                             STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183


HIZI NDIO SEHEMU 10 ZENYE MSISIMKO MKALI ZAIDI KWENYE MWILI WA MWANAMKE....

                                                     
                                                                 
kila mwanaume anapenda kua fundi wa tendo la ndoa akiwa faragha na mke au mchumba wake lakini bahati mbaya sana hakuna kanuni maalumu ya kumsisimua mwanamke kwani kila mwanamke ana eneo lake ambalo likiguswa anakua taabani hivyo ni wajibu wa mwanaume kulitafuta na kuligundua eneo hilo.
mazoea ya kufanya mambo yaleyale kila siku kwa muda mrefu hufanya tendo hilo la ndoa lianze kua baya na huenda ikawa chanzo  cha mtu kuchepuka kutafuta ladha zingine.
kitaalamu katika sayansi ya binadamu kuna maeneo kadhaa ambayo wanawake wote wakiguswa hupata msisimko mkali lakini msisimko hutafautiana kutokana na mwanamke husika kama ifuatavyo.
kichwani; juu ya kichwa cha binadamu kuna mishipa mingi ya damu na ile ya fahamu hivyo maeneo  haya yakishikwa homoni kama oxytocin na serotoinin huachiwa mwilini na kuleta msisimko mkubwa.
jinsi ya kufanya; mshike kwanzia nyuma ya sikio kisha ingiza vidole katikati ya nywele kama unamkuna kichwa bila kutumia nguvu.
sikio; sikio ni sehemu yenye mishipa ya fahamu inayoenda kwenye ubongo, mara nyingi sikio watu hua wanalipuuza sana na kuzani halihusiki lakini naomba nikwambie ni moja ya sehemu inayoweza kumfanya mtu achanganyikiwe.
jinsi ya kufanya; anza kwa kumnong'oneza kwa sauti nzito, kisha libusu sikio lake baada ya hapo unaweza kulamba sehemu ya sikio la nje na baadae kuingiza ulimi ndani ya sikio kabisa. hapa msisimko ni mkali sana na anaweza kukukwepa na kutoa sauti kali ya kimahaba.

ulimi ; ulimi ni sehemu ya mwili ambayo ina mishipa mingi mara mia moja zaidi kuliko ile mishipa ya fahamu ya viganja vyetu. msisimko wa ulimi unasababishwa kumwagika kwa homoni ambazo zinatuletea furaha ya mioyo yetu.
jinsi ya kufanya; busu tu  inatosha kusisimua ulimi wa mtu wako, bahati mbaya kuna watu hawajui kubusu. ukiwa unabusu mtu usipanue mdomo mzima kama samaki mfu... fungua mdomo wako kidogo kisha nyonya lips za juu wakati mtu wako ananyonya za chini na hii ndio busu linavotakiwa kua.
shingo; hii ni sehemu ya mwili yenye ngozi laini sana ambayo inasisimka hata kwa kuipumulia tu na pua. ni moja ya sehemu nzuri sana kunyonya, kulamba na kubusu.
jinsi ya kufanya; ukiwa umemkumbatia mtu wako basi busu upande wa kulia au wa kushoto wa shingo huku ukinyonya ngozi la eneo hilo.

chuchu; wanaume wengi wanatumia sehemu hii kama sehemu kuu kumsisimua mwanamke, ni kweli kabisa tafiti zinaonyesha kwamba sehemu ya ubongo ambayo husisimuka chuchu za mwanamke zikiguswa ni sehemu hiyohiyo ambayo inasisimka kinembe na uke vikiguswa. kwa hiyo ni moja ya sehemu muhimu sana.
jinsi ya kufanya; tomasa matiti yote ya mwanamke kwa kutumia mikono yako miwili kisha nyonya chuchu yake taratibu huku kama unaing'ata na kuiachia. badilisaha kwa kuchocha chuchu ya kulia na kushoto.
kiuno au mgongo wa chini; kama umechunguza ni kwamba wanawake wengi husisimka sana wakiguswa viuno vyao ghafla hata wakati wa kukumbatiwa tu. hii ni sababu ya mishipa ya fahamu inayoenda hadi kwenye sehemu zake nyeti hupita huko.
jinsi ya kufanya;tomasa kama unafanya masaji sehemu ya chini kabisa ya kiuno kabla makalio hayajaanza. hii itamfanya arelax sana lakini pia kuongeza damu kwenda sehemu zake nyeti tayari kwa tendo la ndoa.
tumbo; tumbo ni sehemu ambayo watu wengi hawaitilii manani sana lakini misuli ya tumbo imeungana na uke moja kwa moja ndio maana baadhi ya wanawake hufika kileleni kwa kufanya mazoezi ya tumbo kitaalamu kama core exercises..
jinsi ya kufanya; tomasa tumbo lake kwanzia juu kabisa ya tumbo na kwenda tumbo la chini na kisha busu taratibu maeneo mbalimbali ya sehemu ya tumbo na unaweza kumalizia kwa kunyonya kitovu.
katikati ya mapaja; hii ni sehemu yenye msisimuko mkubwa kwenye mwili wa mwanamke, watu wanaondesha magari wanajua siri hii kwani wakimpakia mwanamke wanatumia njia hii kumsisimua kwa kuweka mkono mmoja kwenye mapaja yake.
jinsi ya kufanya; shikashika sehemu za katikati ya mapaja kwanzia magotini kwenda mpaka karibu na uke.unaweza fanya hivyo wakati ukiwa unambusu.
nyayo za miguu; nyayo za miguu zikiguswa hata kwa mtu ambaye sio wa kike zina msisimko sana kama wa kutekenywa hivi na sina msisimko mkubwa kuliko sehemu nyingi nilizotaja.
jinsi ya kufanya; shika nyayo moja ya mguu kisha kwa kutumia viganja viwili tomasa katikati ya mguu kwanzia kwenye kisigino mpaka kwenye vidole.usitumie nguvu nyingi...
kinembe[critoris]; hii ni sehemu ya mwanamke ambayo kazi yake ni kuleta msisimko tu na raha kwa mwanamke..eneo hili lina mishipa mingi sana ya fahamu, ni eneo dogo sana lakini shughuli yake sio ndogo. naweza kusema ndio eneo lenye msisimko mkali kuliko yote niliyotaja hapo juu na likiguswa tu mwanamke analoana kabisa.
jinsi ya kufanya; kidole chako kikubwa cha kinganyani bonyeza na kuachia sehemu hiyo kama mtu anayekagua parachichi pia sugua kwenda chini, juu na pembeni kuangalia muhusika anapenda wapi zaidi pia kama una uhakika na usafi au afya ya muhusika unaweza lamba lwa kuzungusha ulimi sehemu hiyo.
mwisho; sehemu zote nilizotaja hapo juu ni muhimu sana kwa ajili ya kumuandaa mwanamke japokua kila mwanamke anapata msisimko zaidi kutokana na yeye mwenyewe alivyo yaani mwingine shingo linaweza kua na msisimko wa kawaida likiguswa lakini mwingine ikawa  msisimo mkali zaidi...

                                                    STAY ALIVE

                             DR.KALEGaMYE HINYUYE MLONDO
                                        0653095635/0769846183




UFAHAMU UGONJWA WA KUSHINDWA KUSOMA KARIBU NA MATIBABU YAKE.[FARSIGHTED]

                                                           
huu ni ugonjwa wa macho ambao unamfanya mtu aweze kusoma vitu vya mbali lakini hawezi kusoma vitu karibu yake kirahisi kama meseji ya simu au gazeti. ni ugonjwa unaopata vijana[hyperropia] lakini pia watu zaidi ya miaka 40 hupata hali hii na kitaalamu huitwa presybayopia.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
hii hutokea pale miale ya mwanga inapoingia jichoni na kukusanyika nyuma ya retina badala ya kukusanyika kwenye retina yenyewe lakini pia hali hii kwa wazee kiungo kwa jina la pupil ambacho kazi yake ni kuhakikisha mwanga unaoingia ndani ya jicho sio mkubwa wala sio mdogo sana huanza kuchoka na kushindwa kufanya kazi yake.
tafiti pia zinaonyesha hali ya kushindwa kuona karibu hasa kwa vijana wadogo hua inafuata ukoo fulani.

dalili zake ni zipi?
kushindwa kusoma vitu vya karibu kirahisi kama gazeti na simu.
maumivu makali ya kichwa
kutumia nguvu nyingi kusoma maandishi madogo ya karibu.
macho kuchoka na kuwashwa au kuuma pembezoni kwa macho.

vipimo vinavyofanyika
mgonjwa hupimwa na mtaalamu wa macho kwa kutumia picha maalumu kama snellen chart ambayo atatakiwa kusoma maandishi madogo na makubwa akiwa umbali wa mita sita na aweze kuyatambua bila tatizo.

matibabu
mgonjwa akishathibitika na ugonjwa huu matibabu pekee ni matumizi ya miwani ambayo ataivaa maisha yake yote. mgonjwa hupewa miwani yenye convex lens kwa ugonjwa huu.

jinsi ya kuzuia hali hii
ugonjwa huu unaweza kuzuilika kwa watu fulani kwa kufanya yafuatayo...
chunguza macho yako angalau mara mbili kwa mwezi; hii itakusaidia kujua ugonjwa ukiwa ndio kwanza unaanza na kupata matibabu mapema.
kua makini na magonjwa unayoumwa; kama unasumbuliwa na presha au kisukari hakikisha magonjwa haya yanatibiwa vizuri kwani huharibu sana macho.
vaa miwani kwenye jua kali; hii itakusaidia kupunguza miale mikali ya jua ambayo pia huharibu macho.
usivute sigara; sigara inaharibu sana uwezo wa kuona na haina faida yeyote kwenye mwili wa binadamu.
kula vizuri; hakikisha unakula vyakula vyenye vitamin a nyingi au kupata virutubisho vyenye vitamin hizi ili uweze kutunza macho yako.


                                                        STAY ALIVE
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0653095635/0769846183
karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]