data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA MACHO WA KUSHINDWA KUONA MBALI NA MATIBABU YAKE.[MYOPIA] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA MACHO WA KUSHINDWA KUONA MBALI NA MATIBABU YAKE.[MYOPIA]

                                                             
                                                               
ugonjwa wa kushindwa kuona mbali ni moja ya magonjwa ambayo yanawapata watu wengi sana hasa watoto, vijana na wazee.
hakuna chanzo maalumu cha ugonjwa huu lakini watafiti wanahisi kutumia computer muda mrefu au kufanya kazi za kuangalia sehemu ya karibu kunachangia sana shida hii.

dalili za ugonjwa huu ni zipi?
mara nyingi mtu hushindwa kuona mbali akiwa kwenye shughuli zake mbalimbali kama darasani kwa wanao kaa nyuma, akiwa anaendesha gari anaweza kushindwa kusoma alama za barabarani, au kushindwa kuona chochote kilichoko mbali pia.
hali hii sio ya kudharau kwani inaweza kua chanzo cha ajali kwa waendesha magari na pia kushindwa kusoma na kuelewa kwa watoto darasani.

nini husababisha hali hii?
kwa kawaida miale ya mwanga ikiingia kwenye jicho ili mtu aweze kuona vizuri inatakiwa miale hiyo ikutane kwenye sehemu ya jicho kwa jina la retina sasa kwa mgonjwa huyu miale hii hukutana mbele ya jicho, na kumfanya ashindwe kuona kawaida.
                                                   

vipimo hufanyika wapi?
kama una tatizo hili onana na daktari wa macho na atakupima kwa chati maalumu ambayo huwekwa mita sita kutoka kwa mgonjwa, chati hiyo hua na maneno makubwa na madogo na mgonjwa hupewa maksi kulingana na uwezo alioonyesha kwenye kusoma chati hiyo.
                                                             
matibabu
kwa kawaida ukishapata ugonjwa huu hakuna matibabu ya kukuponyesha kabisa lakini utavaa miwani yenye convex lens maisha yako yote lakini unaweza kuvaa pale tu unapohitaji kusoma vitu vya mbali ila kama hauhitaji kusoma vya mbali sio lazima kuvaa.
lakini pia unaweza kutumia virutuisho mbalimbali vya macho ili uweze kuendelea kuyapa macho yako uwezo wa kuona kwa miaka mingi zaidi kwani hali, kumbuka virutubisho hivyo havikufanyi uache kuvaa miwani ila huyapa macho yako uwezo zaidi wa kuona.
                                                                                              


STAY ALIVE

DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183

tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

0 maoni:

Chapisha Maoni