data:post.body FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA MAUMIVU MAKALI YA MGONGO. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA MAUMIVU MAKALI YA MGONGO.

                                                                     
maumivu ya mgongo ni moja ya sababu kuu kwanini watu huenda hospitali kuonana na daktari lakini pia ni moja ya vyanzo vikuu vya ulemavu duniani. utafiti unaonyesha kila mtu hupata maumivu ya mgongo angalau mara moja kwenye kipindi cha maisha yake.
maumivu ya mgongo yanaweza kua ya kawaida ua makali sana kupindukia, mimi nimeshudia watu wanaoshindwa kutembea kabisa sababu ya maumivu ya mgongo.
maumivu ya mgongo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu yaani maumivu ya juu ya mgongo, katikati na chini ya mgongo.
sasa maumivu ya mgongo huweza kuja ghafla sababu ya kuanguaka au kubeba kitu kizito lakini pia huweza kuanza taratibu sababu ya magonjwa fulani fulani yanayoshambulia mifupa, nyama au mishipa ya fahamu ya mgongo..bahati nzuri kuna njia mbalimbali rahisi za kuzuia na kutibu maumivu ya mgongo kwa njia za asili tu ukiwa nyumbani japokua kuna hali zingine zinazohitaji upasuaji hali ikiwa mbaya kabisa.
zifuatazo ndio sababu kuu za maumivu ya mgongo.
matatizo ya misuli ya mgongo; ubebaji wa vitu vizito sana huweza kuchangia kuvutika na kuuma sana kwa misuli hii lakini pia mazoea ya kukaa umepinda mgongo kwenye kiti huweza kuleta hali hii.
kuvimba au kuvunjika kwa pingili za mgongo; mgongoni kuna pingili ambazo zipo kama disc, katikati ya pingili hizo kuna nafasi ambayo huachwa ili mishipa ya fahamu ipite kupeleka taarifa mwilini.bahati mbaya matatizo ya uzito sana,ajali na baadhi ya magonjwa husababisha ile nafasi kubanwa na hivyo kufinya mishipa ya fahamu. hali hii huleta maumivu makali sana ambayo husambaa mpaka sehemu zingine kama miguuni, kichwani  tumboni na mikononi kulingana na pingili ipi imekandamiza mishipa ya fahamu.ubebaji wa mizito mikubwa huweza kusababisha kukatika au kuchomoka ghafla kwa pingili ya mgongo kutoka kwenye mstari wake.
baridi yabisi[arthritis]; huu ni ugonjwa wa mifupa ya binadamu ambao unaweza kusababishwa na mashambulio ya bakteria, kuisha kwa mifupa sababu ya umri au matatizo ya mwili kujishambulia wenyewe.[autoimmunity]
kupinda kwa mgongo; kuna hali mbalimbali zinaweza kusababisha mtu akapinda mgongo kama kuzaliwa na kibyongo, kulala na mto[kawaida binadamu anatakiwa alale amenyooka kwenye godoro gumu], mazoea mabaya ya kutembea au kukaa huku umepinda mgongo au maumivu ya tumbo ya muda mrefu yanayofanya ujipinde muda wote kujipooza.
kupungua kwa uzito wa mifupa;  mifupa huweza kupungua uzito kitaalamu kama bone density, hii husababishwa na umri mkubwa, ukosefu wa madini ya calcium mwilini na upungufu wa homoni mwili ambazo pia husaidia uimara wa mifupa hasa kwa wanawake.

nani wako kwenye hatari ya maumivu ya mgongo?
kila mtu yuko kwenye hatari ya kupata maumivu ya mgongo hata watoto  lakini pia kuna sababu mbalimbali ambzo zinaweza kuchangia kikundi fulani cha watu kuugua hali hizi kama ifuatavyo
umri; maumivu huanza kadri umri unavyozidi kwenda mbele yaani kwanzia mika 30 au 40 kwenda mbele, watu hawa husumbuliwa sana na maumivu ya mgongo.
kutofanya mazoezi; hii hufanya misuli ya mgongoni kulegea sana na kua chanzo cha kukandamiza pingili za mgongoni.
uzito uliopitiliza; binadamu na kama mfano wa gari..., gari inayotakiwa kubeba kilo 1000 ikipewa kilo 2000 inaweza kufanya kazi lakini itachoka mapema sana. kuna watu wengi sana wanene ambao kulingana na urefu wao wanatakiwa wawe na kilo kama 60 lakini wana kilo 100. huyu mtu hana tofauti na mtu anayebeba na kutembea na ndoo mbili za lita 20 kila siku.maumivu ya mgongo ni lazima.
magonjwa; baadhi ya magonjwa kama kansa na baridi yabisi husababisha maumivu ya mifupa.
uvutaji wa sigara; husababisha virutubisho muhimu kutofikia mifupa na kusababisha mtu kua na hatari ya maumivu ya mgongo.
kubeba uzito vibaya; unaweza kua unabeba uzito unaolingana na wewe lakini ukitumia sana mgongo badala ya miguu kubeba uzito basi utaleta maumivu.

vipimo vinavyofanyika mahospitalini
kwa hapa nchini kwetu vipimo mbalimbali vinatumika kuangalia chanzo cha tatizo lakini vipimo vifuatavyo hutumika zaidi.
X RAY; hii ni mionzi inayopigwa kwenye mwili wa binadamu kuonyesha picha ya tatizo husika, kama baridi yabisi na mfupa uliovunjika.
MRI NA CT SCAN; hizi hutoa picha ambazo x ray haiwezi kuona kama mishipa ya damu, nyama zinazouma, mishipa ya fahamu inayoumwa na kadhalika. kwa tanzania hupatikana hospitali kubwa tu.
VIPIMO VYA DAMU; hivi huweza kupimwa kuangalia kama kuna ugonjwa wowote wa bacteria unashambulia mwili ili uweze kutibiwa.

matibabu 
maumivu ya mgongo mara nyingi huweza kupona yenyewe au kwa kununua dawa za maumivu na kumeza mwenyewe lakini pia wakati mwingine hali ikiwa mbaya mgonjwa hulazimika kwenda hospitali kutibiwa.
matibabu hutegemea na chanzo cha maumivu husika hivyo daktari anaweza kufanya yafuatayo
dawa za maumivu; kuna dawa nyingi sana za maumivu ambazo ni kali na zingine za kawaida na hapa utapata dawa kulingana na ukali wa maumivu yako mfano diclopa, diclofenac, ibuprofen, meloxicam,peroxicam na kadhalika.
dawa za kulegeza misuli; maumivu yanayosababishwa na kukaza kwa misuli huponywa vizuri na dawa za kulegeza misuli kama diezepam na kadhalika.
dawa za maumivu za kupaka; zipo dawa nzuri sana za kupaka maeneo yanayouma ili kupunguza maumivu na hufanya kazi haraka.mfano fastum au ketoprofen cream.
dawa kali za narcotics; hizi ni dawa za maumivu zenye nguvu sana na hutolewa chini ya usimamizi wa daktari, zinaondoa maumivu kwa 100% zikitumika. mfano morphine
dawa za msongo wa mawazo; dawa hizi hutumika kwa watu wenye maumivu makali ya mgongo ya kudumu hasa yale ya muda mrefu lakini husababisha usingizi mara nyingi mfano amitriptyline
sindano; kama maumivu yakikataa kupona na yanaenda mpaka miguuni kuisha daktari anaweza kuchoma sindano kitaalamu kama ant inflamatory katikati pingili za mgongo.husaidia sana kupunguza matatizo ya mishipa ya fahamu.

matibabu yasiyohusiana na dawa
pamoja na matumizi ya dawa lakini kuna mambo muhimu sana kuzingatia ili kupona kabisa kama ifuatavyo.
elimu ya vyanzo vya maumivu; hakikisha unajiepusha na chanzo cha maumivu yako kama ukikitambua mfano kubeba uzito kubwa,kulala na mto kitandani,[kawaida binadamua anatakiwa alale akiwa amenyooka kabisa], unene, na kadhalika lakini pia kula chakula bora chenye kila kitu kama matunda, mboga za majani, protini, wanga na vitamini.
                                                           
mazoezi; hii inaitwa kitaalamu kama physiotherapy, haya ni mazoezi ya kitaalamu ambayo unafanyiwa na mtaalamu wa afya ya physiotherapy au mtu yeyote wa afya anayejua jinsi ya kuyafanya. mazoezi haya yanasaidia sana kupata nafuu kwani huweza kurudisha kila kiungo kwenye sehemu yake ya zamani hasa matatizo ya pingili za mgongo. mimi binafsi nimewasaidia watu wengi sana kwa mazoezi haya.mafuta maalumu hupakwa mgongoni na mtalamu hutumia mikono yake kurekebisha sehemu zenye matatizo kwa kutengeneza joto ambalo hupitisha damu ya kutosha kwenye misuli, mifupa na mishipa ya fahamu ambavyo mara nyingi huuma sana kwa kukosa damu ya kutosha, lakini pia mtaalamu hukuelekeza mazoezi ya kufanya nyumbani kulingana na tatizo lako.physiotherapy  ni moja ya njia pekee ambazo huafanya maumivu yasirudi tena.
upasuaji; kuna baadhi ya wagonjwa hufika hospitali wakiwa na hali ambazo haziwezi tena kusaidiwa kwa mazoezi wala dawa hivyo upasuaji maalumu hufanyika kuzipanua pingili au disc za mgongoni kurudi katika hali yake ya kawaida.
mwisho; chukua hatua sasa kama unasumbuliwa na tatizo hili kwani huambatana na changamoto nyingi kama kuishiwa nguvu za kiume, kushindwa kufanya kazi, kushindwa kutembea na kuathirika kiasaikolojia.
unaweza pitia blog yetu ya kingereza hapa kwa elimu zaidi ya afya zaidi
                          tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                         
                                                          
                                                                   STAY ALIVE
                                            DR.KALEGEMYE HINYUYE MLONDO
                                           MAWASILIANO 0653095635/0769846183

Maoni 1 :