data:post.body Oktoba 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

JINSI YA KUONGEZA MAKALIO NA HIPS KWA MAZOEZI.

                                                             
  
maumbile ya binadamu yanategemea sana genetics yaani alivyorithi kutoka kwa wazazi wake, lakini pia hutegemea sana chakula anachokula na mazoezi anayofanya.kua na makalio makubwa kwa sasa ni kama fasheni kimuonekano mbele ya jamii lakini pia makalio hayo mtu anaweza kuzaliwa nayo au akafanya jitihada za mazoezi akayapata kama jinsi wanaume wanavyozaliwa na vifua na mikono midogo lakini wanafanya mazoezi mpaka wanakua mabaunsa.
mazoezi haya sio kwa ajili wenye makalio madogo tu hata wale wenye makalio makubwa yanawafaa kwani kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kumfanya mtu mwenye makalio makubwa aanze kua na makalio madogo au yasiyokua na shape nzuri. sababu hizo ni kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu hasa kazi za ofisini, umri unavyobadilika kuna homoni muhimu zinazokufanya ue na shepu nzuri zinapungua lakini pia ukiwa binti mdogo mwili unahifadhi mafuta kwenye makalio lakini unavyozidi kukua mwili unaanza kuhifadhi tumboni na hapo ndio utagundua wanawake wanavyozidi kua wakubwa hata kama hawajazaa lakini wanaanza kuota vitambi na kupungua ukubwa wa makalio.
kwenye nchi zilizoendelea wanawake huyatumia sana mazoezi haya kua na makalio makubwa na yenye shepu nzuri.

je kuna njia nyingine za kuongeza makalio?
kuna njia kama tatu za kuongeza makalio ambazo zinatumika kwa dunia ya sasa...njia ya upasuaji, njia ya dawa na njia ya mazoezi...njia za dawa na mazoezi ni hatari sana kwa afya ya watumiaji kwani zina madhara makubwa sana kiafya na kuna watu wengi sana wameuawa na njia hizi, si hivyo tu njia hizo haziruhusiwi nchini kwetu lakini njia za mazoezi ni salama sana kwani hukujenga kiafya pia.                


ni rahisi kufanikiwa kwa mazoezi?
kufanikiwa inawezekana sana lakini sio rahisi hivyo lazima uwe na bidii ya kufanya mazoezi na kufuata maelekezo yote kama inavyotakiwa. watu wengi hawana nidhamu ya chochote wanachokifanya na hujikuta wanafanya mazoezi kwa wiki mbiki au tatu na kuacha japokua mazoezi sio magumu sana.

kuna mfano hai wa watu wanaofanya mazoezi haya?
nchi zilizoendelea hii ndio moja ya njia kuu za akina dada kujiweka katika shepu nzuri na kuna mifano ya watu maarufu wa nje kwenye muziki na sanaa waliotumia njia hizi kujiweka fiti na kua katika shepu nzuri mfano alicia keys, beyonce, jennifer lopez, angelina julie, mariah carey na wengine wengi ndio maana unakuta mtu kama jennifer lopez kwa sasa anakaribia miaka 50 lakini hajapoteza ukubwa wa makalio yake kama watu wengine.

mafanikio yanachukua muda gani?
ukianza mazoezi angalau ndani ya miezi mitatu mpaka sita utaona mabadiliko makubwa na haimaanishi ukishafanikiwa ndio uache hapana, mazoezi haya yanatakiwa yawe sehemu ya maisha yako kama jinsi kula kulivyo sehemu ya maisha yako. mfano hai ni mwanaumwe mwenye mwili mzuri wa mazoezi lakini akiicha na mwili wake hupotea.

mazoezi yanawafaa akina nani?
mazoezi haya huwafaa wanawake wote wenye makalio makubwa na ambao hawana kwani huyafanya yale makubwa kua katika shepu nzuri na haya madogo kukua na kua katika shepu nzuri bila kujali mabadiliko ya umri.

vipi kuhusu mazoezi ya kubana uke?
uke wa mwanamke huweza kuwa mkubwa zaidi kwa sababu mbalimbali kama kuzaa kawaida au kwa upasuaji, kunenepa sana, umri kua mkubwa, kulala na wanaume wengi na kadhalika. hali hii husababisasha wanawake wa aina hii kushindwa kufika kileleni kwani uume unakua haufiki sehemu husika za mishipa ya fahamu au watahitaji uume mkubwa zaidi kuweza kufika kileleni.
mazoezi haya yaligunduliwa na dr.kegel mwaka 1952 na kuandika ripoti kwamba wanawake waliofanya mazoezi haya waliridhika kirahisi sana kwenye tendo la ndoa kuliko wale wasiofanya na matokeo yalianza kuonekana mwezi mpaka miezi mitatu baada ya kuanza mazoezi.
msuli kitaalamu kwa jina la pubococcygeus musle hufanyishwa mazoezi na faida ya zoezi hili sio kubana uke tu bali husaidia wenye matatizo ya kushindwa kuzuia mkojo hasa baada ya kujifungua.
                                                             
chakula gani kiliwe wakati wa mazoezi?
kuna vyakula maalumu vimeelezewa kwenye kitabu hichi ambavyo ni muhimu sana katika mafanikio ya mazoezi haya yote mawili kwani sio chakula chochote tu kinaweza kukusaidia. mfumo wa sasa wa maisha umewafanya watu wale vibaya na kuota sana vitambi. kumbuka hata kama una makalio makubwa kiasi gani, ukiwa na kitambi shepu yako inaharibika sana.

kitabu hiki kinapatikana vipi?
kitabu hichi kina mchanganyiko wa mazoezi ya kukuza makalio na kubana uke, vyakula vya kutumia kipindi hicho cha mazoezi na jinsi ya kubaki kwenye shepu, kitabu hiki kipo kwa mfumo wa soft copy yaani kinatumwa kwenye email au watsapp na kama ukihitaji cha kawaida unaweza kuprint mwenyewe stationery baada ya kutumiwa. bei ya kila kitabu ni 20000 na pesa hiyo itatumwa kwenye namba itakayowekwa mwisho wa makala hii na unaweza kuwasiliana kwa email yetu hii kalegamyehinyuye@gmail.com

angalizo; mazoezi haya yanataka moyo wa uvumilivu na wengi watakao nunua kitabu hichi watafanya kwa muda mfupi na kuacha japokua mzoezi sio magumu sana ila wengi watajifanya wametingwa na majukumu wakati zoezi ni nusu saa tu kwa siku tena siku 21 kwa mwezi...hivyo kama unaona sio mvumilivu usipoteze fedha zako, nunua kitabu ukiwa umedhamiria kufanikiwa katika hilo.
                                           
                                           STAY ALIVE
                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                      MAWASILIANO 0653095635/0769846183


                                             

UFAHAMU UGONJWA WA MACHO WA KUSHINDWA KUONA MBALI NA MATIBABU YAKE.[MYOPIA]

                                                             
                                                               
ugonjwa wa kushindwa kuona mbali ni moja ya magonjwa ambayo yanawapata watu wengi sana hasa watoto, vijana na wazee.
hakuna chanzo maalumu cha ugonjwa huu lakini watafiti wanahisi kutumia computer muda mrefu au kufanya kazi za kuangalia sehemu ya karibu kunachangia sana shida hii.

dalili za ugonjwa huu ni zipi?
mara nyingi mtu hushindwa kuona mbali akiwa kwenye shughuli zake mbalimbali kama darasani kwa wanao kaa nyuma, akiwa anaendesha gari anaweza kushindwa kusoma alama za barabarani, au kushindwa kuona chochote kilichoko mbali pia.
hali hii sio ya kudharau kwani inaweza kua chanzo cha ajali kwa waendesha magari na pia kushindwa kusoma na kuelewa kwa watoto darasani.

nini husababisha hali hii?
kwa kawaida miale ya mwanga ikiingia kwenye jicho ili mtu aweze kuona vizuri inatakiwa miale hiyo ikutane kwenye sehemu ya jicho kwa jina la retina sasa kwa mgonjwa huyu miale hii hukutana mbele ya jicho, na kumfanya ashindwe kuona kawaida.
                                                   

vipimo hufanyika wapi?
kama una tatizo hili onana na daktari wa macho na atakupima kwa chati maalumu ambayo huwekwa mita sita kutoka kwa mgonjwa, chati hiyo hua na maneno makubwa na madogo na mgonjwa hupewa maksi kulingana na uwezo alioonyesha kwenye kusoma chati hiyo.
                                                             
matibabu
kwa kawaida ukishapata ugonjwa huu hakuna matibabu ya kukuponyesha kabisa lakini utavaa miwani yenye convex lens maisha yako yote lakini unaweza kuvaa pale tu unapohitaji kusoma vitu vya mbali ila kama hauhitaji kusoma vya mbali sio lazima kuvaa.
lakini pia unaweza kutumia virutuisho mbalimbali vya macho ili uweze kuendelea kuyapa macho yako uwezo wa kuona kwa miaka mingi zaidi kwani hali, kumbuka virutubisho hivyo havikufanyi uache kuvaa miwani ila huyapa macho yako uwezo zaidi wa kuona.
                                                                                              


STAY ALIVE

DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183

tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA MAUMIVU MAKALI YA MGONGO.

                                                                     
maumivu ya mgongo ni moja ya sababu kuu kwanini watu huenda hospitali kuonana na daktari lakini pia ni moja ya vyanzo vikuu vya ulemavu duniani. utafiti unaonyesha kila mtu hupata maumivu ya mgongo angalau mara moja kwenye kipindi cha maisha yake.
maumivu ya mgongo yanaweza kua ya kawaida ua makali sana kupindukia, mimi nimeshudia watu wanaoshindwa kutembea kabisa sababu ya maumivu ya mgongo.
maumivu ya mgongo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu yaani maumivu ya juu ya mgongo, katikati na chini ya mgongo.
sasa maumivu ya mgongo huweza kuja ghafla sababu ya kuanguaka au kubeba kitu kizito lakini pia huweza kuanza taratibu sababu ya magonjwa fulani fulani yanayoshambulia mifupa, nyama au mishipa ya fahamu ya mgongo..bahati nzuri kuna njia mbalimbali rahisi za kuzuia na kutibu maumivu ya mgongo kwa njia za asili tu ukiwa nyumbani japokua kuna hali zingine zinazohitaji upasuaji hali ikiwa mbaya kabisa.
zifuatazo ndio sababu kuu za maumivu ya mgongo.
matatizo ya misuli ya mgongo; ubebaji wa vitu vizito sana huweza kuchangia kuvutika na kuuma sana kwa misuli hii lakini pia mazoea ya kukaa umepinda mgongo kwenye kiti huweza kuleta hali hii.
kuvimba au kuvunjika kwa pingili za mgongo; mgongoni kuna pingili ambazo zipo kama disc, katikati ya pingili hizo kuna nafasi ambayo huachwa ili mishipa ya fahamu ipite kupeleka taarifa mwilini.bahati mbaya matatizo ya uzito sana,ajali na baadhi ya magonjwa husababisha ile nafasi kubanwa na hivyo kufinya mishipa ya fahamu. hali hii huleta maumivu makali sana ambayo husambaa mpaka sehemu zingine kama miguuni, kichwani  tumboni na mikononi kulingana na pingili ipi imekandamiza mishipa ya fahamu.ubebaji wa mizito mikubwa huweza kusababisha kukatika au kuchomoka ghafla kwa pingili ya mgongo kutoka kwenye mstari wake.
baridi yabisi[arthritis]; huu ni ugonjwa wa mifupa ya binadamu ambao unaweza kusababishwa na mashambulio ya bakteria, kuisha kwa mifupa sababu ya umri au matatizo ya mwili kujishambulia wenyewe.[autoimmunity]
kupinda kwa mgongo; kuna hali mbalimbali zinaweza kusababisha mtu akapinda mgongo kama kuzaliwa na kibyongo, kulala na mto[kawaida binadamu anatakiwa alale amenyooka kwenye godoro gumu], mazoea mabaya ya kutembea au kukaa huku umepinda mgongo au maumivu ya tumbo ya muda mrefu yanayofanya ujipinde muda wote kujipooza.
kupungua kwa uzito wa mifupa;  mifupa huweza kupungua uzito kitaalamu kama bone density, hii husababishwa na umri mkubwa, ukosefu wa madini ya calcium mwilini na upungufu wa homoni mwili ambazo pia husaidia uimara wa mifupa hasa kwa wanawake.

nani wako kwenye hatari ya maumivu ya mgongo?
kila mtu yuko kwenye hatari ya kupata maumivu ya mgongo hata watoto  lakini pia kuna sababu mbalimbali ambzo zinaweza kuchangia kikundi fulani cha watu kuugua hali hizi kama ifuatavyo
umri; maumivu huanza kadri umri unavyozidi kwenda mbele yaani kwanzia mika 30 au 40 kwenda mbele, watu hawa husumbuliwa sana na maumivu ya mgongo.
kutofanya mazoezi; hii hufanya misuli ya mgongoni kulegea sana na kua chanzo cha kukandamiza pingili za mgongoni.
uzito uliopitiliza; binadamu na kama mfano wa gari..., gari inayotakiwa kubeba kilo 1000 ikipewa kilo 2000 inaweza kufanya kazi lakini itachoka mapema sana. kuna watu wengi sana wanene ambao kulingana na urefu wao wanatakiwa wawe na kilo kama 60 lakini wana kilo 100. huyu mtu hana tofauti na mtu anayebeba na kutembea na ndoo mbili za lita 20 kila siku.maumivu ya mgongo ni lazima.
magonjwa; baadhi ya magonjwa kama kansa na baridi yabisi husababisha maumivu ya mifupa.
uvutaji wa sigara; husababisha virutubisho muhimu kutofikia mifupa na kusababisha mtu kua na hatari ya maumivu ya mgongo.
kubeba uzito vibaya; unaweza kua unabeba uzito unaolingana na wewe lakini ukitumia sana mgongo badala ya miguu kubeba uzito basi utaleta maumivu.

vipimo vinavyofanyika mahospitalini
kwa hapa nchini kwetu vipimo mbalimbali vinatumika kuangalia chanzo cha tatizo lakini vipimo vifuatavyo hutumika zaidi.
X RAY; hii ni mionzi inayopigwa kwenye mwili wa binadamu kuonyesha picha ya tatizo husika, kama baridi yabisi na mfupa uliovunjika.
MRI NA CT SCAN; hizi hutoa picha ambazo x ray haiwezi kuona kama mishipa ya damu, nyama zinazouma, mishipa ya fahamu inayoumwa na kadhalika. kwa tanzania hupatikana hospitali kubwa tu.
VIPIMO VYA DAMU; hivi huweza kupimwa kuangalia kama kuna ugonjwa wowote wa bacteria unashambulia mwili ili uweze kutibiwa.

matibabu 
maumivu ya mgongo mara nyingi huweza kupona yenyewe au kwa kununua dawa za maumivu na kumeza mwenyewe lakini pia wakati mwingine hali ikiwa mbaya mgonjwa hulazimika kwenda hospitali kutibiwa.
matibabu hutegemea na chanzo cha maumivu husika hivyo daktari anaweza kufanya yafuatayo
dawa za maumivu; kuna dawa nyingi sana za maumivu ambazo ni kali na zingine za kawaida na hapa utapata dawa kulingana na ukali wa maumivu yako mfano diclopa, diclofenac, ibuprofen, meloxicam,peroxicam na kadhalika.
dawa za kulegeza misuli; maumivu yanayosababishwa na kukaza kwa misuli huponywa vizuri na dawa za kulegeza misuli kama diezepam na kadhalika.
dawa za maumivu za kupaka; zipo dawa nzuri sana za kupaka maeneo yanayouma ili kupunguza maumivu na hufanya kazi haraka.mfano fastum au ketoprofen cream.
dawa kali za narcotics; hizi ni dawa za maumivu zenye nguvu sana na hutolewa chini ya usimamizi wa daktari, zinaondoa maumivu kwa 100% zikitumika. mfano morphine
dawa za msongo wa mawazo; dawa hizi hutumika kwa watu wenye maumivu makali ya mgongo ya kudumu hasa yale ya muda mrefu lakini husababisha usingizi mara nyingi mfano amitriptyline
sindano; kama maumivu yakikataa kupona na yanaenda mpaka miguuni kuisha daktari anaweza kuchoma sindano kitaalamu kama ant inflamatory katikati pingili za mgongo.husaidia sana kupunguza matatizo ya mishipa ya fahamu.

matibabu yasiyohusiana na dawa
pamoja na matumizi ya dawa lakini kuna mambo muhimu sana kuzingatia ili kupona kabisa kama ifuatavyo.
elimu ya vyanzo vya maumivu; hakikisha unajiepusha na chanzo cha maumivu yako kama ukikitambua mfano kubeba uzito kubwa,kulala na mto kitandani,[kawaida binadamua anatakiwa alale akiwa amenyooka kabisa], unene, na kadhalika lakini pia kula chakula bora chenye kila kitu kama matunda, mboga za majani, protini, wanga na vitamini.
                                                           
mazoezi; hii inaitwa kitaalamu kama physiotherapy, haya ni mazoezi ya kitaalamu ambayo unafanyiwa na mtaalamu wa afya ya physiotherapy au mtu yeyote wa afya anayejua jinsi ya kuyafanya. mazoezi haya yanasaidia sana kupata nafuu kwani huweza kurudisha kila kiungo kwenye sehemu yake ya zamani hasa matatizo ya pingili za mgongo. mimi binafsi nimewasaidia watu wengi sana kwa mazoezi haya.mafuta maalumu hupakwa mgongoni na mtalamu hutumia mikono yake kurekebisha sehemu zenye matatizo kwa kutengeneza joto ambalo hupitisha damu ya kutosha kwenye misuli, mifupa na mishipa ya fahamu ambavyo mara nyingi huuma sana kwa kukosa damu ya kutosha, lakini pia mtaalamu hukuelekeza mazoezi ya kufanya nyumbani kulingana na tatizo lako.physiotherapy  ni moja ya njia pekee ambazo huafanya maumivu yasirudi tena.
upasuaji; kuna baadhi ya wagonjwa hufika hospitali wakiwa na hali ambazo haziwezi tena kusaidiwa kwa mazoezi wala dawa hivyo upasuaji maalumu hufanyika kuzipanua pingili au disc za mgongoni kurudi katika hali yake ya kawaida.
mwisho; chukua hatua sasa kama unasumbuliwa na tatizo hili kwani huambatana na changamoto nyingi kama kuishiwa nguvu za kiume, kushindwa kufanya kazi, kushindwa kutembea na kuathirika kiasaikolojia.
unaweza pitia blog yetu ya kingereza hapa kwa elimu zaidi ya afya zaidi
                          tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                         
                                                          
                                                                   STAY ALIVE
                                            DR.KALEGEMYE HINYUYE MLONDO
                                           MAWASILIANO 0653095635/0769846183

UFAHAMU UGONJWA WA KASWENDE NA MATIBABU YAKE. [SYPHILIS ]

                                                                  

kaswende ni nini?
huu ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa kutoka kwa njia ya ngono au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.
utafiti unaonyesha kwamba asilimia 2 mpaka 20 ya akina mama wanaoenda kupimwa kipindi cha ujauzito hukutwa na kaswende lakini pia ugonjwa huu umetapakaa sana maeneo ya mijini ukilinganisha na vijijini.

jinsi ugonjwa unavyosambaa.
  • husambaa kwa zinaa kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke
  • husambaa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.
  • mgonjwa mwenye vidonda anaweza kuambukiza mtu kwa kumkumbatia tu.
  • kugusa vidonda vya mgonjwa kwa bahati mbaya.

dalili za kaswende
  • kidonda kisichokua na maumivu hutokea baada ya siku 10 mpaka 90 baada ya kupata maambukizi, kidonda hicho hakina maumivu na hukaa siku chache na kupotea bila matibabu. kidonda hiki hutokea pale wadudu walipoingilia yaani huweza kua kwenye uume,uke, mdomoni, kwenye maziwa na kadhalika.
  • upele hutokea baada ya miezi sita na kusambaa sehemu za uke, kwenye mkundu, mikononi, miguuni, kifuani, mgongoni na hata usoni. upele huu hauwashi na kipindi hichi mgonjwa anakua hatari sana kwani huweza kuambukiza mtu kwa kumkumbatia au kumshika tu.
  • baada ya mwaka mpaka miaka kumi ugonjwa huu huingia ndani ya mwili na kushambulia mishipa ya fahamu na ubongo.mgonjwa huanza kuonyesha dalili za ugonjwa wa akili na wakati mwingine mtu hua kichaa kabisa.
vipimo vya maabara kugundua kasendwe
kipimo maalumu kitaalamu kama rapid plasma reign, kipimo hiki huweza kugundua ugonjwa wiki ya 6 mpaka 8 baada ya kuambukizwa.

matibabu
sindano maarufu kama pena du au benzathine penicilin huchomwa kwa kiasi cha 2.mu yaani 1.2m.u kwa kila tako. sindano hiyo huchomwa mara moja kwa kaswende inayoanza au mara moja kwa wiki moja kwa muda wa wiki tatu.
kwa wagonjwa wenye allergy na penicilin kuna dawa kama doxycline ambayo hutumika lakini pia kwa sasa kuna dawa nyingi mpya sokoni ambazo huweza kutumika pia mfano cefriaxon.

madhara ya kaswende
  • ugonjwa huu unaongoza kwa kusababisha kuharibika kwa mimba kuliko magonjwa mengine yoote ya zinaa, ni vizuri kwa mama kupima ugonjwa huu kabla ya kuamua kubeba mimba.
  • ugonjwa huu hauzuiliki hata kwa kondom kwani una uwezo wa kupita hata kwenye ngozi isiyo na michubuko......unaweza kusoma blog yetu ya kingereza hapa.

SECRETS OF GOOD HEALTH,SCHOOL OF MEDICINE AND MEDICAL DISCOVERIES.


                                                   STAY ALIVE
                                  KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183


                                                                   
                                                   

UFAHAMU UGONJWA WA ZINAA WA PANGUSA NA MATIBABU YAKE..[CHANCROID]

                                                             

pangusa ni nini?
huu ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa kwa njia ya ngono, huambukizwa na bakteria anayefahamika kitaalamu kama haimophilus ducrey.
bacteria huweza kupita kwenye ngozi laini kama ya uke kirahisi bila hata kuwepo kwa michubuko.
wanawake huweza kuhifadhi bacteria hawa bila kuonyesha dalili yeyote na kuwaambukiza waanaume wengi zaidi.
ugonjwa huu huleta vidonda vikubwa sana kwenye sehemu za siri na kusababisha kulika kwa sehemu hizo, huweza kuzimaliza kabisa sehemu za siri kama matibabu yasipopatikana.
ugonjwa huu hupatikana kwenye sehemu za joto na wagonjwa wengi ni wanawake wanaojiuza hasa sehemu za mijini.
ugonjwa huu hurahisisha zaidi maambukizi ya virusi kwa ukimwi kwa waathirika wa ugonjwa huu.
baada ya kuambukizwa mgonjwa huchukua siku 3 mpaka 14 kuanza kuonyesha dalili.

dalili za ugonjwa wa wa pangusa..
baada ya maambukizi vipele hutokea kisha huchimbika na kutoa vidonda vikubwa ambavyo husambaa pande mbalimbali za sehemu za siri na kuchimba mashimo ya vidonda.
vidonda hivi hua na maumivu makali na hutoa damu pale vinapoguswa.
hali hua mbaya zaidi kwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi.
             
vipimo vinavyofanyika
daktari mzoefu anaweza akagundua ugonjwa huu bila vipimo vyovyote lakini kwa uhakika zaidi majimaji yanayotoka sehemu za siri huchukuliwa na kupimwa maabara.

matibabu
vidonda vinatakiwa viweke visafi, vioshwe na sabuni mara kwa mara
dawa zinazotumika kutibu shida hii ni kama cotrimoxazole, ciproflaxin na erythromycin.

jinsi ya kuzuia
matumizi ya kondom kwa usahihi.
kua na mpenzi mmoja muaminifu.
usishiriki ngono kabisa kama huwezi kutumia kondomu.
epuka wapenzi wengi.
                                                tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                               

                                                      STAY ALIVE
                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183


UFAHAMU UGONJWA WA ZINAA WA TRICHONOMIASIS NA MATIBABU YAKE....

                                                                

ugonjwa wa trichomoniasis ni upi?
huu ni ugonjwa wa zinaa unaoshambulia sehemu za siri kwa jina la trichonomiasis na husababiswa na aina ya protozoa kwa jina la trichomona vaginalis.
huu ni ugonjwa unaoshambualia angalau 10% ya wanawake wote kwenye kipindi chote cha maisha yao,
maambukizi ni kwa njia ngono kati ya mwanaume na mwanamke lakini pia kuchangia nguo za ndani au mataulo kunaweza kuambukiza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
ugonjwa huu huweza kuambukiza watu wa jinsia zote lakini unawaathiri sana wanawake na mgonjwa asipotibiwa anaweza kuishi na ugonjwa huo kwa siku miaka kadhaa.
baada ya kuambukizwa ugonjwa huu, huchukua siku 5 mpaka 28 kuanza kuonyesha dalili zake waziwazi.

dalili za ugonjwa wa trichomoniasis
kuwashwa sana sehemu za siri
kuchubuka sehemu ya juu ya uke na mlango wa uzazi
maumivu wakati wa kukojoa
maumivu wakati wa tendo la ndoa
maumivu makali ya tumbo la chini
kutokwa uchafu wa kijani na njano wenye harufu kali kama ya kitu kilicho oza.
kwa wanaume ugonjwa huu mara nyingi hauna dalili lakini mara chache sana wanaweza kupata maumivu wakati wa kukojoa

vipimo
daktari mzoefu anaweza kuujua ugonjwa huu bila vipimo vyovyote lakini pia kwa upande wa maabara uchafu unaotoka huchukuliwa na kupimwa kwa darubini...

matibabu
metronidazole au kwa jina lingine fragile 2g kwa wakati mmoja [vidonge kumi] au 400mg[vidonge viwili] kutwa mara tatu kwa siku tano.
tinidazole 2g kwa wakati mmoja
scenidazole 2g kwa wakati mmoja.
kumbuka dawa hizi hazipatani na pombe kabisa hivyo usitumie pombe ukitumia dawa hizi.

jinsi ya kuzuia
tumia kondom kila tendo na kwa usahihi
achana na ngono kama huwezi kondom
kua na mpenzi mmoja muaminifu
epuka kua na wapenzi wengi
epuka kuchangia chupi, taulo au nguo yeyote ya ndani.
                                                                         
                                                     STAY ALIVE
                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                 MAWASILIANO 0653095635/0769846183