data:post.body Septemba 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIVI NDIVYO KISONONO KINAVYOSABABISHA UGUMBA KWA WANAWAKE NA WANAUME.[GONORRHEA]

                                                                             
kisonono ni nini?
kisonono ni ugonjwa wa njia ya uzazi kwa wananawake na wanaume ambao mara nyingi huambatana na kutokwa na usaa sehemu za siri.kisonono kinafahamika kama classical sti kwani iliinza kabla hata ya kuanza kwa ugonjwa wa ukimwi.

kisonono ni moja ya vyanzo vikuu vya utasa na ugumba kwa wanawake na wanaume na umeonyesha kupunguza sana idadi ya uzazi kwa jamii nyingi duniani.
ugojwa wa kisonono husababishwa na bacteria kwa jina la kitaalamu kama naisseria gonorhoea, bacteria hawa hawawezi kupita kwenye ngozi ya kawaida kama ya mkono au mguu na hupendelea ngozi laini kama ya uke, ngozi ya ndani ya kichwa cha uume, ngozi ya mkundu, ngozi ya macho na ngozi ya ndani ya mdomo.
ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya kufanya ngono lakini pia watoto huweza kuambukizwa wakati wa kuzaliwa kutoka kwa mama mwenye kisonono.
hatari ya mambukizi baada ya ngono ni asilimia 20 mpaka 35 kwa wanaume na asilimia 60 mpaka 90 kwa wanawake.
dalili za ugonjwa huu huanza siku ya 2 mpka siku ya kumi baada ya kufanya ngono.

dalili za ugonjwa wa kisonono kwa wanaume.
  • kuwaashwa ndani ya njia ya njia ya mkojo
  • maumivu makali wakati wa kukojoa.kutokwa na usaa kwenye uume
  • kukojoa mara kwa mara na kushindwa kuzuia mkojo
  • kutoa mkojo wenye damu
  • mgonjwa asipotibiwa usaa huanza kupungua au kuisha kabisa lakini ugonjwa unakua umehamia ndani na hii ni hatari zaid.
dalili za kisonono kwa wanawake
asilimia 50 mpaka 80 ya wanawake hawana dalili kabisa na ndio maana ugonjwa huu unaweza kumfanya mwanamke akawa mgumba .
wakati mwingine usaha huweza kutokea kwenye mlango wa uzazi bila kuonekana nje
wanawake wengi hugundua walikua na ugonjwa huu baada ya kupata madhara yake kuonekana kama kushindwa kupata mtoto.

madhara ya kisonono wa wanaume
  • njia ya mkojo kuziba
  • majipu ndani ya njia ya mkojo
  • mkojo kujaa ndani ya kibofu
  • utasa na kushindwa kuzaa

madhara ya kisonono kwa wanawake.
  • ugumba
  • magonjwa ya njia za uzazi.
  • mimba kutungwa nje ya kizazi.

vipimo vinavyotumika..
usaha unaotoka huchukuliwa kwenye uume wanaume na ndani ya uke wa mwanamke na kupimwa maabara kuhakikisha kuwepo kwa ugonjwa huu.

matibabu
dawa mbalimbali zinaweza kutibu kisonono lakini kwa muongozo wa sasa wa wizara ya afya mchanganyiko wa dozi ya doxycline na ciprofloxacin kwa muda wa siku saba hutumiaka zaidi. kwa mama mjamzito au kwa ambaye ameshindwa kupona kwa dawa nilizotaja hapo juu sindano moja ya cefriaxon 250mg inatosha kabisa kumaliza ugonjwa huu.dawa za ciproflaxin na doxycline ni marufuku kwa wajawazito.

sababu za kushindwa kupona kwa wagonjwa wengi wa kisonono
  • kutoa dawa kidogo ukilinganisha na uzito wa mgonjwa
  • kutoa dawa za kisonono wakati ni ugonjwa mwingine unaofanana.
  • baadhi ya dawa kushindwa nguvu na bakteria wa kisonono
  • kutomtibu mpenzi husika wa mgonjwa na kusababisha maambukizi mapya.
  • kutomaliza dozi

jinsi ya kuzuia ugonjwa wa kisonono
  • kutoshiriki tendo la ngono kabisa
  • kuvaa condom kwa uhakika
  • epuka kua na wapenzi wengi
  • mpenzi wa mgonjwa lazima atibiwe hata kama hana dalili
  • kua na mpenzi mmoja muaminifu...

  •                     tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
  •                              


                                     STAY ALIVE

             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                        0653095635/0769846183

UFAHAMU UGONJWA WA FANGASI ZA SEHEMU ZA SIRI NA MATIBABU YAKE.[CANDIDIASIS]

                                                                       
                             
ugonjwa wa fangasi za sehemu za siri husababishwa na aina ya wadudu wa fangasi kwa jina la candida albicans.
fangasi za uke hupenda kuwashambulia wanawake ambao wako kwenye umri wa kubeba mimba lakini pia sababu yeyote inayosababisha kinga kushuka huachangia mashambulio ya mara kwa mara ya ugonjwa huu mfano mlo mbovu, ugonjwa wa kisukari, kansa na ukimwi, ujauzito matumizi ya mda mrefu wa dawa antibiotic na dawa za steroid yaani jamii ya predinisolone na hydrocortsisone.
ugonjwa huu hauambukizwi kwa njia ya ngono na maambukizi kwa mwanamke haimaanishi kwamba mwanaume lazima atibiwe au maambukizi kwa mwaume haimaanishi mwanamke lazima atibiwe kama ilivyo kwenye magonjwa ya zinaa.
mara nyingi mgonjwa anayeugua mara kwa mara fangasi hata kama sio za uke ni dalili kwamba kinga imeshuka hasa kwenye ugonjwa wa ukimwi.

                                                 dalili za fangasi za sehemu za siri

  • miwasho ya sehemu za uke.
  • kutokwa uchafu wa rangi ya maziwa ukiwa haina harufu kabisa au harufu ya mkate kwenye uke.
  • sehemu za uke kuvimba na kua nyekundu.
  • maumivu ya kuungua wakati wa kukojoa kwa wanawake.
  • maumivu wakati la tendo la ndoa kwa wanawake.
  • kwa wanaume, wekundu na wakati mwingine kutokwa na uchafu kidogo kwenye uume.
                                            vipimo vinavyofanyika

        mara nyingi daktari huweza kuutambua ugonjwa huu kwa dalili tu bila kupima lakini wakati mwingine kiasi cha uchafu unaotoka hupimwa kuhakikisha hakuna ugonjwa mwingine wa zinaa ulioambatana na fangasi.
vipimo kwa kutumia darubini huonyesha fangasi kwa mgonjwa.

                                                      matibabu
  •  cotrimazole vidonge, chomeka kwenye uke kidonge kimoja cha 100mg mara moja wakati wa kulala kwa siku saba.
  • cotrimazole ya kupaka 1%, paka asubuhi na jioni kwa siku 7 mpaka 14.
  • grusiofulvin vidonge vya kumeza kimoja kila siku kwa wiki mbili na  kama dawa hizo zikishindwa meza flucunazole kidonge kimoja kila siku kwa siku 14.
                                                    jinsi ya kuzuia
  • acha sehemu za siri safi na kavu muda wote yaani epuka kuvaa nguo za ndani kabla hazijakauka.
  • epuka sabuni kali za sehemu ya siri, marashi ya kwenye uke na kuingiza vidole mara kwa mara kuosha uke.
  • badilisha tampoon mara kwa mara.
  • vaa nguo za ndani zilizotengenezwa na pamba na sio nailoni.
  • kama una kisukari hakikisha sukari yako iko vizuri na kama una virusi vya ukimwi basi meza dawa na kufuata masharti yote ili kinga yako isishuke.
  • kula mlo kamili yaani wanga, protini, matunda na mboga za majani kuweka kinga vizuri.
                                                      STAY ALIVE

                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183
   
                                                    

SABABU KUMI ZA KUISHIWA AU KUKAUKIWA MAZIWA KABISA KWA MAMA ANAYENYONYESHA

                                                                     
nimekua nikipata malalamiko mengi kwa akina mama wanaojifungua kwamba matiti yao yanatoa maziwa kidogo au hayatoi kabisa. hii imewafanya kushindwa kunyonyesha au kuingia gharama kubwa kuwanunulia maziwa ya lactogen fomula dukani au kutumia maziwa ya ngombe. lakini pia tukumbuke kwamba maziwa ya mama hua hayana mbadala kabisa yaani virutubisho vinavyopatikana kwenye maziwa yale havipatikani popote hivyo kama una shida ya kutoa maziwa basi tumia maziwa mbadala huku ukitafuta suluhisho la maziwa yako.vifuatavyo ni vyanzo vya vya kushindwa kutoa maziwa.

matumizi ya dawa za uzazi wa mpango; wanawake wengi hutumia njia hizi baada ya kujifungua bila shida yeyote lakini kuna baadhi yao njia hizi huingilia mfumo wao wa  kutoa maziwa hasa zikitumika kabla mtoto hajafikisha miezi sita. hii husababishwa na kuongezeka kwa homoni za uzazi yaani progesterone na oestrogen ambazo hushusha homoni ya kutoa maziwa yaani prolactin hormone.kama umekumbwa na hali hii basi acha mara moja njia hiyo na utumie njia zingine kama kondom,kalenda au njia nyingine isiyotumia dawa.

matatizo ya kimaumbile; baadhi ya wanawake matiti yao hayakukamilika wakati wamakua yaani yanakua na upungufu wa vitu muhimu vinavyohifadhi maziwa kwenye matiti kitaalamu kama grandular tissues hii hufanya maziwa yatoke kwa shida sana.mama anashauriwa akamue maziwa wakati wa kunyonyesha na mara nyingi mtoto wa pili mpaka watatu wakizaliwa matiti haya yanakua yameshazoea hivyo hayasumbui tena kutoa maziwa.

upasuaji wa matiti; kama mama ameshawahi kupasuliwa matiti yake kwa shida yeyote labda majipu, ajari, upasuaji wa kuongeza au kupunguza matiti basi kwa namna moja au nyingine hii inaweza kuharibu mfumo wake wa matiti kupitisha maziwa na kujikuta hatoi maziwa ya kutosha.ukiwa na shida hii utahitaji kutumia maziwa mbadala kwa mtoto.

matumizi ya dawa; wakati wa kunyonyesha mama anaweza kuugua na  kutumia dawa fulani fulani ili apone ugonjwa alionao lakini kuna  baadhi ya dawa ni hatari kwani hushusha kiwango cha maziwa. mfano dawa za kama bromocriptine,methergine,pseudoephredine.

matatizo ya homoni za uzazi; matatizo ya homoni kua juu sana au kua chini sana yanaweza kusababishwa na magonjwa ya ovari, kisukari na kadhalika. pia magonjwa yeyote ya homoni yanayochelewesha mtu kupata mimba huweza kuzuia maziwa pia. ni vizuri ukaonana na daktari kupima kiwango cha homoni na kupata matibabu.

kutonyonyesha usiku; wakati wa usiku homoni inayohusika na kutengeneza maziwa yaani prolactin hutengenezwa kwa kiwango cha juu sana lakini pia ili mtoto alale usiku mzima bila kusumbua lazima anyonye vizuri usiku.kutonyonyesha usiku hupunguza homoni hii na kumfanya mama atoe maziwa kidogo sana siku inayofuata.

kutonyonyesha vya kutosha; kawaida mama anatakiwa anyonyeshe angalau mara kumi ndani ya masaa 24, sasa mwili hutengeneza maziwa unapohisi matiti hayana kitu na kama mwili ukihisi matiti yana maziwa muda mwingi basi unajua maziwa hayahitajiki sana na kuanza kupunguza kiasi cha kutoa maziwa.

kutokula vizuri;maziwa anayotoa mama yanatengenezwa na chakula anachokula wala sio miujiza fulani hivyo kipindi hiki mama anatakiwa ale mlo kamili yaani matunda, protini ya kutosha, wanga, mboga za majan na maji mengi i na ikiwezekana atumie virutubisho vinavyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kuongeza maziwa.

matumizi ya vyakula mbadala;  miezi sita baada ya kuzaliwa mtoto anatakiwa anyonye tu bila kupewa kitu chochote, kuna watu hua wanawapa maji wakidai eti watoto walisikia kiu sio kweli.sasa kuanza kumchanganyia maziwa ya ngombe na yale ya dukani kutamfanya anyonye kidogo kwako na mwili utapunguza kiasi cha maziwa yako...hivyo siku ukikosa mbadala utajikuta huna maziwa kabisa.

mtoto kushindwa kunyonya; kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba maziwa yakitoka mengi na mwili unatengeneza mengi zaidi na kama mtoto hanyonyi vizuri basi na maziwa hutoka kidogo zaidi.hali hii inaweza kusababishwa na dawa ya usingizi ambayo alipewa mama wakati wa kupasuliwa ambayo huamuathiri mtoto pia, au matatizo ya kuzaliwa nayo kama tongue tie[ulimi kushikwa chini ya mdomo, hii inaweza kurekebishwa na daktari] au mtoto kuugua.

                                                  STAY ALIVE
                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                           0653095635/0769846183



HIZI NDIO DAWA 10 AMBAZO HAZITAKIWI KUMEZWA NA MAMA ANAYENYONYESHA MTOTO.

                                                                           
baada ya kujifungua akina mama wengi huendelea kunyonyesha mpaka miaka miwili, japokua wengine hunyonyesha chini ya hapo inategemea na mtazamo wa mtu. lakini kitaalamu mtoto anayenyonya kwa miaka miwili hua anakua vizuri na kua na uwezo sana wa kiakili..kipindi cha kunyonyesha mama anaweza kuugua au kutumia dawa fulani fulani kwa ajili yake. baadhi ya dawa hazitakiwi kutumika kwa mama kipindi hichi kwani zinaweza kumuathiri sana mtoto na kuharibu ukuaji wake..hebu tuzione dawa hizo..

chloramphenicol; hii ni antibayotiki, ni dawa inayotumika kuua bacteria ambao wanashambulia mwili. kwa hapa tanzania dawa hii mara nyingi hutumika kutibu ugonjwa wa typhodi.dawa hii husababisha ugonjwa unaitwa grays syndrome yaani mtoto hubadilika rangi na kua rangi ya gray lakini pia huonyesha dalili kama kutapika, tumbo kuvimba, kukosa hamu ya kula, kushuka kwa joto na presha kushuka.lakini pia dawa hii huzuia utengenezaji wa damu kutoka kwenye mifupa[aplastic anaemia].tatizo hili la damu likishaanza hakuna dawa inayoweza kumponya mtoto huyu.

dawa ya mseto ya malaria; dawa hii hutumika kutibu malaria lakini hua inapita kwenye maziwa na kuingia kwa mtoto. kama una mtoto mwenye chini ya kilo tano usimeze dawa hii kwani ikiingia kwa mtoto hawezi kuitoa nje lakini kama mtoto wako ana zaidi ya kilo tano unaweza kutumia.

vidonge vya uzazi wa mpango; hizi ni dawa ambazo hua zina homoni za oestrogen na progesterone matumizi yake husababisha kiwangi kikubwa sana cha homoni hizi mwilini na kuzuia mimba. lakini dawa hizi hupingana na homoni ya prolactin ambayo ni muhimu kwa kutoa maziwa.hivyo matumizi ya dawa hizi kwa mama mwenye mtoto chini ya miezi sita hupunguza maziwa kwa kiasi kikubwa.

aspirin; aspirin ni dawa ya maumivu lakini pia hulainisha damu na kuifanya kua nyepesi sana hii ni hatari kwa mtoto kwani anaweza kuvuja damu mpaka kufa lakini pia husabibisha ugonjwa unaitwa reyes syndrome ambao huambatana na kuvimba maini na kichwa.

dawa za cancer; kuna dawa aina mbali mbali za kansa ambazo mara nyingi huu seli za kansa au kuzuia zisikue.kwa jinsi zinavyofanya kazi hupunguza kinga ya mwili ya mgonjwa pia hupita kwenye maziwa ya mama na kushusha kinga ya mtoto na kumfanya aharishe.

ergotamine; hii ni dawa inayotumika kutibu maumivu makali ya kichwa kitaalamu kama migraine headache, mara nyingi huchangwanya na kemikali ya caffeine kufanya kazi vizuri. matumizi yake hupunguza utengenezaji wa maziwa ya mama na huweza kuleta degedege kwa mtoto.

adrogens; hizi ni hormone ambazo zinapatikana kwenye mwili wa binadamu lakini pia zinatengenezwa kiwandani kutolewa kwa watu ambao wana upungufu wa homoni hizi.kwenye mwili wa mwanamke homoni hizi hubadilika na kuwa oestrogen yaani homoni ya uzazi.sasa matumizi ya dawa hizi hupunguza kiasi cha maziwa kwa mama.

metformin; hizi ni dawa za kisukari, hupewa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari lakini dawa hizi zina uwezo wa kupita kwenye maziwa na kushusha sukari kwa mtoto..hii ni hatari sana na huweza kuua.

lithium; hii ni dawa inayotumika kwa wagonjwa wa akili, mama ambaye pia ana ugonjwa wa akili anaweza kupata mimba pia au mama aliyekua mzima anaweza kupata ugonjwa wa akili baada ya kuzaa. dawa hii hubadilisha mapigo ya moyo ya mtoto na kuyapeleka tofauti.

 iodine; hupewa kwa watu wenye kiwango kidogo sana cha iodine mwilini lakini pia inapatikana kwenye chumvi.matumizi makubwa ya iodine husababisha kuvimba kwa goita na kiwango kidogo cha homoni za thyroid kwenye mwili wa binadamu.

mwisho; kuna dawa nyingine nyingi huenda sijazitaja hapo lakini hizo ni baadhi ambazo zinapatikana kwa wingi. katika kipindi hicho cha unyonyeshaji basi ni vizuri kuongea na doctor kabla ya kumeza dawa yeyote.
                                               tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                              STAY ALIVE
                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                    0653095635/0769846183

JINSI YA KUTOA MIMBA KITAALAMU KUOKOA MAISHA YA MAMA.

                                                                 
 
makala hii imeandikwa kwa ajili ya elimu kwa watu wanaosomea fani za afya na watanzania wanaoishi nchi ambazo kutoa mimba sio kosa kisheria.nchini tanzania kutoa mimba ni kosa na adhabu yake ni kali. sheria ya tanzania inaruhusu kutoa mimba zilizoharibika au kutoa mimba pale unapoona kwamba mimba ile ni hatari kwa maisha ya mama na kazi hii hufanyika na daktari.
kuna njia mbalimbali zimekua zikitumiwa na watu wengi ambao sio wataalamu kutoa mimba ambazo hazitambuliki kitaalamu na zimeua watu wengi.njia zifuatazo hutumika....

  1. manual vacuum aspiration; hii ni njia ya kuharibu mimba iliyoharibika au mimba iliyo hai, vifaa vinavyotumika hapa hupatikana hospitali tu. lakini pia kifaa hiki hutakiwa kutoa mimba yenye wiki 3 mpaka wiki 7...chini ya umri huo wa mimba au juu ya umri huo kifaa hicho hakitafanya kazi vizuri.

jinsi ya kutumia; muweke mgonjwa wako kwenye position nzuri kitaalamu kama lithotomy position, mpe dawa ya maumivu au usingizi, safisha uke wake kwa kutumia vifaa maalumu ikiwemo gozi au pamba na ant septic, taratibu ingiza speculum ukeni mpaka uone cervix vizuri, chukua manual vacuum aspirator ivute ili kujaza vacuum ndani ya mashine hiyo kisha ingiza taratibu ndani ya mfuko wa uzazi kupitia cervix huku ukizungusha huku na huku kwa angalau dakika moja....hapo utaona damu inaingia ndani ya aspirator yako, ukiona hivyo toa na umwage kwenye dishi la maji, rudisha tena uendelee kuvuta mpaka uone damu imeisha kabisa..baada ya hapo mtoe mama pale avae pedi kisha apelekwe akapumzike na aandikiwe antibiotic na dawa za maumivu mfano doxycline  za siku tano na panadol za siku tatu. epuka dawa za jamii ya diclofenac yaani nsaids kwani huweza kusababisha damu kutoka nyingi.
faida za njia hii
  • mimba hutoka ndani ya dakika tano za kazi..
  • hakuna mdhara makubwa ya kutisha.
changamoto ya njia hii;
  • maumivu makali wakati baada ya mimba kutoka
  • kazi hii hufanyika na daktari tu au mwanafunzi wa udaktari chini ya usimamizi.
  • haiwezi kutoa mimba kuba zaidi ya wiki saba.
                                                     
dilatation and curratage; hii procedure ni maalumu kwa ajili ya kuondoa mabaki kwenye mji wa mimba, kama baada ya mimba kuharibika au mabaki ya kondo la mtoto baada ya kujifungua lakini pia hutumika kutoa mimba ya  kama ifuatavyo.
muweke mama kwenye position kama nilivyotaja juu, unaweza kumchoma sindano ya maumivu au dawa ya usingizi kwani maumivu ya hapa ni makali kidogo..safisha sehemu zake za siri ili uiingize uchafu wa nje huko ndani ya mfuko wa uzazi, ingiza speculum taratibu mpaka uone cervix au mlango wa uzazi, chukua kifaa kinaitwa teneculum uishike cervix na kifaa hicho ili isicheze, chukua dilator kulingana na ukubwa wa mlango wa cervix kisha tanua mpaka upate nafasi ya kutosha, ingiza currete kisha anza kukwangua na kama una kuna nazi... endelea kuondoa mabonge ya damu na nyama mpaka uone povu la damu ndio ujue umemaliza kila kitu.
faida za njia hii..
  • huweza kuharibu mimba kubwa kuliko njia ya kwanza
  • huchukua muda mfupi kama mimba ni ndogo
changamoto ya njia hii
  • unaweza kukwangua mfuko wa ndani kabisa unaoshika mtoto[endometrium] na kusabisha ugumba wa moja kwa moja.
  • unaweza kutoboa mfuko wa uzazi na kusababisha mwanamke akatoka damu mpaka kufa na matibabu ya ajali hii ni upasuaji tu.[watu wengi wamekufa sababu ya hii]
  • lazima afanye daktari au daktari mwanafunzi chini ya usimamizi.
                                                       
njia ya vidonge; njia salama kabisa ya kutoa mimba nzima au iliyoharibika hata ikiwa na miezi tisa lakini njia hii sio nzuri sana kwenye mimba chini ya wiki nne.inafanya kazi vizuri zaidi kwanzia mwezi mmoja mpaka miezi tisa. vidonge vinavyotumika kutoa mimba haviuzwi reja reja hasa kwa nchi ambazo haziruhusu kutoa mimba kama tanzania lakini kwa nchi kama china au marekani vidonge hivi hupatikana madukani na mtu anaweza kujitoa mimba akiwa nyumbani tu lakini kwa mimba kubwa iliyofia tumboni inabidi aende akawekewe hospitali chini ya usimammizi. 
vidonge hivi kwa jina la cytotec, kitaalamu ni kwamba mimba kubwa zaidi inakua sensitive sana yaani inatolewa kirahisi na dawa hizi kuliko mimba ndogo hivyo mimba chini ya miezi mitatu inatumia vidonge vingi zaidi kuliko mimba ya zaidi ya miezi mitatu na zaidi.
jinsi ya kutumia
kupitia mdomoni; kama mimba ina miezi mitatu kushuka chini weka vidonge vinne vyenye micogram 200 kwa kila kimoja chini ya ulimi kila baada ya masaa matatu mpaka umalize dozi tatu yaani vidonge 12.kama mimba ina miezi mitatu kwenda juu weka vidonge viwili vivo hivo. baada ya muda damu ya mabonge itaanza kutoka, kisha anza dawa za antibiotic na zile za maumivu. mara nyingi damu huendelea kutoka kidogo kidogo mpaka wiki tatu wakati mwingine lakini ukiona inatoka nyingi sana kama ya kujaza pedi moja ndani ya saa moja kimbia hospitali haraka.
kupitia uke; kama mimba ina miezi mitatu kushuka chini weka vidonge vinne  kwenye uke kisha weka vingine baada ya saa 12, wakati unaweka dozi ya pili mara nyingi utakuta damu imeshaanza kutoka.[kumbuka wakati unaweka lala chali viingize mpaka usikie umegusa mwisho wa uke kisha viache hapo, pumzika anangalau saa moja, ikiwezekana viweke wakati wa kwenda kulala usiku ili visidondoke] kama mimba ina miezi mitatu kupanda juu weka viwili kisha viwili baada ya saa 12.kumbuka antibiotiki na dawa za maumivu..
faida za njia hii; 
  • mtu anaweza kutoa mimba mwenyewe akiwa nyumbani kwake na hii ni kawaida kwa nchi zilizoendelea.
  • sio rahisi kupata ugumba au kutokwa na damu mpaka kifo hasa ukizingatia masharti hayo rahisi.
changamoto za njia hii
  • maumivu makali wakati mimba inatoka hasa mimba kubwa.
  • madhara madogo madogo kama kuharisha sana.
  • dawa hizi hazipatikani kirahisi japokua hutumika pia kutibu madonda ya tumbo lakini unapewa na dakatri ikithibitika kweli una madonda ya tumbo.
                                                             
dalili za hatari baada ya kutoa mimba; 
  • kutokwa na harufu kali muda baada ya mimba kutoka.
  • maumivu makali sana yasioisha baada ya mimba kutoka
  • homa kali sana.
  • kutokwa na damu nyingi  sana ya kujaza pedi moja kwa saa moja...,ukiona dalili hizi wahi hospitali.
je ukitumia vidonge vichache mimba inaweza kutoka?
kuna watu hua wanatumia njia za vidonge tofauti na nilivyoelekeza kwa kuweka viwili au kimoja  ukeni na kumeza viwili au wanavyojua wao lakini mimba ikitoka kwa njia hizi hua inakua ni bahati tu lakini pia mara nyingi hua haitoki yote yaani kuna mambonge ya damu au mabaki ya kichanga yatabaki ndani na kukuletea matatizo ya uzazi baadae.

inakuaje mtu anatumia dawa hizi na mimba haitoki?

  • mimba inaweza isitoke kwasababu dawa zilizotumika ni feki kama unavyofahamu kwamba 50% ya bidhaa zinazoingia nchini kwetu ni feki na dawa orijino ni ngumu kidogo kuzipata lakini kwa wanao ishi nje ya nchi zilizoendelea sio tatizo.
  • kutumia dawa pungufu na zilizoelekezwa.
  • kutofuata maelekezo ya muda na masaa ya kutumia dawa hizo.
  • uhakika wa vidonge 97% hivyo asilimia tatu ya watu watakaotumia wanaweza wasifanikiwe hivyo kuhitaji njia zingine.
  • njia ya kujiwekea ukeni ni changamoto kwani watu wengi huweka sehemu ambayo sio sahihi.
ukishatoa mimba unaweza kurudia kipimo baada ya muda gani?
kumbuka mimba ikishatoka kile kipimo cha mimba kinaendelea kusoma mistari miwili mpaka baada ya wiki tatu mpaka mwezi. kwanini?  kipimo kile kinasoma homoni ambazo zinaitwa kitaalamu kama human chorionic gonadotrophin hormone ambazo hupungua taratibu sana baada ya mimba kutoka. hivyo ukitoa mimba leo na damu ikatoka ukaenda kupima bado itakua inasoma mistari miwili, hivyo kama unataka uhakika kapime kipimo cha picha maarufu kama utrasound.

angalizo: ukishamaliza kutumia njia zozote kati ya hizo zilizotajwa hapo juu ni lazima kutumia dawa za antibayotiki kuzuia infection au kuoza kwa sehemu za uzazi, mfano doxycycline kidonge kimoja kutwa mara mbili kwa siku tano mpaka saba na dawa za maumivu kama paracetamol.



mwisho; nitoe onyo kama nilivyosema mwanzo, kutoa mimba ni kosa kisheria nchini kwetu,,, makala hii ni maalumu kwa watu waishio nje ya nchi na madaktari wanafunzi ambao waliniomba sana niwaandikie lakini pia kwa wanaotaka kufahamu tu lakini sio kuzitumia..
                                    
                                       

                                                                      STAY ALIVE

                                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0769846183/0653095635




UFAHAMU UGONJWA WA U.T.I NA MATIBABU YAKE..[URINARY TRACT INFECTIONS]

                                                                    

ugonjwa wa uti ni nini?
huu ni ugonjwa ambao unashambulia njia ya mfumo wa mkojo, ni kifupi cha neno urinary tract infections..ugonjwa huu unashambulia 1% mpaka asilimia 3% ya ya watoto wa shule ya msingi lakini unazidi kuwashambulia zaidi wanavyozidi kukua kiumri kutokana na kushiriki sana tendo la ndoa.
ugonjwa huu hushambulia sana wanawake wenye miaka 20 mpaka 50 na mara chache sana mwanaume wa chini ya miaka 50 anaweza kushambuliwa na ugonjwa huu.kumbuka ugonjwa huu haumbukizwi kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke ila ngono huchangia bacteria kushambulia njia ya mkojo ya mwanamke. hivyo ukiugua wewe haimaanishi na mwenzako atibiwe labda kama imegundulika kuna ugonjwa wa zinaa umeambatana.

                         mambo yanayochangia mtu kuugua ugonjwa huu.
jinsia; wasichana wanaugua sana ugonjwa huu kwa sababu ya ufupi wa mrija wao wa kutoa mkojo{urethra], mrija huu ni mrefu sana kwa wanaume kiasi kwamba sio rahisi kwa bacteria kusafiri na kufika wa mrija na kushambulia.
lakini pia umbali mfupi kati ya uke na mkundu kwa wanawake, hii inaweza kusababisha bacteria kuhama kirahisi kutoka kwenye mkundu na kushambulia njia ya mkojo hasa kwa wanawake wanaochamba na maji kutoka nyuma kwenda mbele.
magonjwa ya zinaa na magonjwa ya tezi dume pia huweza kuchangia kuugua kwa ugonjwa huu kwa wanaume.

ujauzito; asilimia 2 mpaka 8 ya wanawake wajawazito huugua ugonjwa wa u.t.i kwa sababu ya kutanuka kwa mrija wa mkojo na kusabisha kutuama kwa mkojo ndani ya mirija hiyo.

kuziba kwa njia ya mkojo; kuziba kwa aina yeyote ya njia ya mkojo huweza kusababisha ugonjwa huu. mara nyingi husababishwa na magionjwa ya zinaa.

magonjwa ya mishipa ya fahamu; magonjwa yeyote yanayoathiri mishipa ya fahamu na na kusababishwa mkojo kushindwa kutoka kawaida husababisha ugonjwa wa u.t.i

bacteria; hawa kitaalamu wanaitwa e.coli, asilimia 80% ya wagonjwa u.t.i hushambuliwa na bacteri a huyu.

kurithi; kuna ushahidi kua ugonjwa huu unaweza kuathiri familia fulani fulani kutokana na matatizo yao binafsi ya kimaumbile.

kushuka kwa kinga ya mwili sababu ya magonjwa au chakula kibovu.

                                        dalili za ugonjwa ya u.t.i
ugonjwa huu una dalili mbalimbali kutokana na viungo ambavyo vimeathirika kama ni kibofu cha mkojo, figo, au mirija ya mkojo kama ifuatavyo..

  • maumivu wakati wa kukojoa..
  • homa 
  • kuumwa tumbo
  • kutapika na kuharisha
  • kukojoa mara kwa mara na hisia za kutaka kujikojolea ukichelewa chooni.
  • maumivu ya misuli 
  • kujikojolea kitandani hasa kwa watoto
                                                   vipimo vya u.t.i
  • urinalysis; hichi ni kipimo kinachopatikana hospitali nyingi nchini, hutumia kitu kama njiti kitaalamu kwa hiyo kazi[dip stick]. kuonekana kwa damu au seli nyeupe za damu kwenye mkojo ni kiashiria cha ugonjwa huu.
  •   urine for sediments; hii ni njia ya kutumia kiasi kidogo cha mkojo na kupima kwenye darubini kuangalia damu na seli za usaha ambazo ndio uhakiki wa u.t.i
  • kipimo cha utrasound scan; wakati mwingine kama mgonjwa ana dalili za kushambuliwa kwa figo kipimo hiki hutumika kuangalia ni kwa kiasi gani figo zimeharibika.
                                                               
                                                         matibabu
matibabu ya uti hutegemea hali ya mgonjwa na majibu yatakavyoonyesha, kama hali ni ya kawaida mgonjwa hupewa vidonge na kama hali ni mbaya sana mgonjwa huchomwa sindano.
vidonge hivyo ni kama cotrimoxazole, ciprofloxacin, lomefloxacin, na kadhalika na sindano ni kama gentamycin, cefriaxon na ampicilin..
dozi ya mgonjwa hutegemea umri na uzito wake lakini pia kwa mama wajawazito usimeze dawa yeyote ambayo hujapewa na daktari kwani baadhi ya dawa tajwa hapo juu sio nzuri kwa mama. dawa salama kwa mama mjamzito mwenye uti ni amoxycillin, ampicilin na cefriaxon.
mara nyingi wanaume huchanganya kati ya uti na kisonono, kwa kawaida kama mwanaume una uti hakuna uchafu mweupe unaotoka sehemu za siri lakini pia kama mwanaume ana uti dawa ya kumeza ya kuanzia ni doxycline kimoja kutwa mara mbili kwa muda wa siku saba na kama mtu ana tatizo la tezi dume yaani prostitis dozi hii hongezeka mpaka siku 14 mpaka 21.
kumbuka kunywa maji mengi sana wakati unaumwa hii husaidia kusafisha figo na kupona haraka.


                                              jinsi ya kuzuia ugonjwa huu..
  •  hakikisha choo unachotumia ni kisafi, kwa wanawake mwaga maji kabla ya kukojoa kisha mwaga maji baada ya kukojoa mara nyingi ile kuchuchumaa kukojoa mkojo hugusa choo kwa presha kubwa  na kukurudia kwenye sehemu za siri.
  • baada ya kujisaidia choo kubwa chamba kutokea mbele kurudi nyuma ili usihamishe bacteria wa mkunduni kwenda kwenye uke.
  • tumia dawa ya kuzuia uti kwa watu ambao inawapata mara kwa mara. mfano kama umegundua kila ukishiriki ngono unaugua basi meza dawa za kuzuia ugonjwa kuanza kila baada ya kushiriki kwa siku kwa dozi ya siku moja tu kwa dawa nilizotaja hapo juu.. mfano cotrimoxazole vidonge viwili tu kwa siku. wajawazito na wanaume wanapata sana ugonjwa huu mfululizo nao wanashauriwa kutumia dawa pia. wajawazito watumie amoxyline au ampicilin mbili kila siku. wanaume watumie doxycline mbili kwa siku.
  • kakojoe haraka unapobanwa na mkojo na hakikisha umekojoa mkojo wote
  • kakojoe mara tu baada ya kushiriki tendo la ndoa.
  • usitumia sabuni zenye kemikali sana kusafisha sehemu zako za siri.
  • usivae nguo zianazobana sana au chupi za kutengenezwa na nailon, tumia chupi za pamba.
mwisho; ni ngumu sana kwa mwanaume kuugua uti na ukimuona anaumwa ni vizuri kuhakukisha kweli kama sio ugonjwa wa zinaa kwa kuminya uume na kuangalia kama kuna uchafu mweupe unatoka. kama uchafu upo hiyo sio uti bali ugonjwa wa zinaa. ugonjwa huu ukipuuziwa muda mrefu huwea kuua figo kabisa.
                                           tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                          
                                                    STAY ALIVE

                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                     0653095635/0769846183

                                                 



HAYA NDIO MAMBO KUMI YA KUZINGATIA KABLA YA KUAMUA KUINGIA KWENYE NDOA.[SAIKOLOJIA]

                                                                   
utafiti uliofanyika nchini marekani umebaini kwa kila ndoa mia moja  zinazofungwa, hamsini zinavunjika..hali hii pia hapa africa ni mbaya sana japokua hakuna tafiti zilizofanyika kuangalia hali halisi ikoje. kumekua kuna makosa mengi sana yanafanyika kabla ya kuoa au kuolewa, yaani watu hufikiria sana jinsi gani watakua na furaha siku ya harusi bila kufikiria itakuaje baada ya harusi. watu hawaangalii hali halisi ikoje na kupofushwa na yale mapenzi motomoto bila kujua kwamba ni ya muda tu  na ipo siku mapenzi  yatapoa na macho yako yatafunguka kuona ukweli.kikristo ndoa ni pingu ya watu wawili ambayo ukiingia hutakiwi kutoka huko mpaka kifo chako hata kwa waislam na imani zingine ambazo zinaruhusu mke zaidi ya mmoja usipokua makini wake zako wote wanne watakushinda.ndoa ina changmoto nyingi sana lakini baadhi ya changamoto watu huziona kabla ya ndoa na kuingia nazo kwenye ndoa bila kujua huo ndio utakua msiba wa maisha yao.yafuatayo ni mambo ya msingi sana yakuzingatia kabla ya kuingia huko.

mapenzi iwe sababu kuu ya ndoa; kuna watu wengi sana wameingia kwenye ndoa bila kuzingatia hili... watu wameingia sababu ya kufuata mali[hasa wanawake], sababu ya presha za familia zao, sababu ya upweke, sababu ya kuona umri umeenda sana, sababu ya kuridhisha watu fulani, sababu kwamba na wao waonekane wameoa au kuolewa, kwasababu alizaa na muhusika na kadhalika ....kumbuka kama unayemuoa au kuolewa nafsi yako haijaridhika naye utaishi kwa mateso maisha yako yote.hutaweza kushiriki tendo la ndoa kwa amani na wala hutaweza kuonyesha mapenzi kwa aina yeyote ile hata ukijalizimisha utashtukiwa tu.

zingatia swala la imani za kidini; swala hili unaweza kuliona dogo kabla ya ndoa au ukaliona kubwa lakini ukalifumbia macho kwasababu umependa lakini kumbuka ndoa haziunganishi watu wawili tu, ndoa huunganisha familia mbili.utafiti umeonyesha kutoelewana kabisa kwa familia za imani tofauti zikikutanishwa na ndoa.mfano mkristo kumuoa muislam. kama unaona familia ya muhusika haijaridhika na iko tayari kukutenga au kumtenga mwenzako basi achana na hiyo ndoa kwani itakupa msongo wa mawazo maisha yako yote na siku watoto wakizaliwa ugomvi ndio utakua mkali zaidi kwani kila familia itataka mtoto afuate imani yao.kuepusha hili tafuta mwenye imani kama yako au upate baraka za familia zote kabla ya ndoa na muelewane kuhusu imani za watoto.kumbuka familia bora ni ile inayosali kwa pamoja.

zingatia swala la ugomvi; kama mtarajiwa wako ameshaanza kukupiga makofi sasa hivi basi ujue baada ya ndoa itakua mapanga na rungu. mtu alizeyezoea kupiga hataacha kukupiga kamwe hata akisema atabadilia usimsikilize kwani muda wa kubadilika ni kabla ya ndoa.kuna watu wengi sana wameuawa sababu ya vipigo ndani ya ndoa.

zingatia swala la heshima; hii ni muhimu sana hasa kwa wanaume... wewe ndio unaenda kua baba wa familia hivyo kimsingi kauli ya mwisho inatakiwa itoke kwako. usioe mwanamke ambaye huwezi kumkemea kufanya kitu fulani kwani ataitesa nafsi yako mpaka utakapokufa.kama huwezi kumwambia usifanye hiki akakusikiliza basi huyo hakufai.

zingatia swala la uchumi; uko tayari kuhudumia familia kwa uchumi wako? utakayefunga nae ndoa ndiye atakaye amua kama mtakua matajiri au masikini. je unaweza kumiliki mtu ambaye hawezi kujishughulisha kwa lolote? swala la kusoma au kua na kazi sio muhimu sana kwani kuna mfano wa watu wengi ambao sio wasomi lakini wana maisha mazuri na kama kasoma hana kazi huenda atapata siku moja.kama mwenzio haonyeshi dalili ya kujituma kutafuta pesa, sio mchumi yaani kila siku mnalazimika kula hotelini na wakati jiko mnalo, ana imani wewe ndio kila kitu basi kimbia mbali. hali ya dunia kiuchumi ni mbaya sana kuna uwezekano hata ukiugua muda mrefu au ukifa watoto watakufa na njaa kwani mwenzio anakutegemea wewe.tafuta muhangaikaji kama wewe au angalau jaribu kumbadilisha kama akibadilika sawa.

zingatia swala la watoto wa nje; lazima iwekwe wazi watoto waliozaliwa nje wataishi vipi kama familia.swala hili ni changamoto sana hasa kwa mwanaume mwenye watoto, mara nyingi wanaume hua hawajali sana kuishi watoto ambao sio wao lakini wanawake wanaweza kuwapa hata sumu watoto wa mume.kama huwezi kuvumilia na kuhudumia watoto ambao sio wako basi achana na hiyo ndoa.uliyezaa nae ni kikwazo kikubwa sana kwa mwenza wako wa sasa. kaa mbali na huduma zake zote za kifedha au mawasiliano naye yeyote. anaweza kua na haki ya kuona mtoto, ni vizuri ukampa ratiba za shule awe anenda kumuona huko lakini walimu wasimruhusu kuondoka naye.lakini kikubwa ni kwamba kama huna moyo wa chuma basi usijaribu ndoa hii.

zingatia swala la magonjwa ya kurithi; kama familia zenu zina magonjwa yanayofanana na ya kurithi mfano albino, siko seli, kifafa, magonjwa ya akili, na kadhalika basi nendeni mkapime kujua kama kuna uwezekano wa nyinyi kuzaa watoto wa aina hiyo.japokua baadhi ya vipimo hapa kwetu havipo.ikithibitika kuna uwezekano wa kuwazaa basi achana na hiyo ndoa usije kuleta viumbe duniani ambavyo vitateseka sana na wewe utateseka sana kuwahudumia.

zingatia mahusiano yaliyopita; ni vizuri kujua mahusiano yaliyopita yaliisha vipi yaani watu waliachana kweli au kuna sababu ambazo ziko nje ya uwezo wao ziliwafanya waachane lakini bado wanapendana.mfano umbali kutoka kwa mpenzi wa zamani, yeye aliachwa lakini bado anampenda, mpenzi kutokua tayari kuoa au kuolewa kwasababu za kiuchumi au sababu zake binafsi au familia kumkataa.fuatilia kama kama wana mawasiliano na uhakikishe mapenzi yaliisha na wewe ndio unayependwa kwa sasa lakini bila hivyo utaendela kusaidiwa na kuna mifano hai mpaka leo yaani vikao vya harusi vinaendelea lakini mtu bado anatembea na mtu wake wa zamani.

zingatia tabia za mwenza wako; binadamu tuna tabia mbalimbali na kila mtu kuna jinsi anazitafsiri tabia hizo kwa upande wake mwenyewe.kama kuna tabia yeyote ambayo binafsi huipendi kwa mwenza wako mfano ulevi, umalaya, hapendi, hajui na hataki kupika, kwenda disco, kuvaa nguo za ajabu, uchafu,kutokwenda kuabudu, matusi, hasira za ajabu, na ameshindwa kuiacha tabia hiyo kabla ya ndoa basi achana nae na sio kwamba hataolewa au kuoa lakini waaachie watu wanaoweza kumvumilia.wewe unaweza kua hupendi kitu hiki ila mwingine haoni kama ni tatizo.

kua mvumilivu;hili ndio swala kubwa ambalo linafanya ndoa za wazee wetu ziweze kudumu mpaka leo, kama wewe unaona kuna matatizo yatakuja ukiingia kwenye ndoa au tayari umeshaingia huko na umejikuta tayari umekabwa silaha ya uvumilivu ndio ambayo unatakiwa uwe nayo sasa hivi. hata kama ukiingia kwenye ndoa na mtu ambaye hana dosari yeyote lakini kuna changamoto za hapa na pale lazima zitatokea na inabidi uzivumilie.

mwisho; mambo niliyotaja hapo juu kuna uwezekano unayaona kwenye nahusiano yako tayari lakini unashindwa kufanya maamuzi magumu sababu una mapenzi makubwa juu ya huyo mwanaume au mwanamke. muda kwa kufanya maamuzi ni sasa kama huamini waulize walioingia tayari na sasa wanajuta.
                                         tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                         

                                                       STAY ALIVE
                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                            0653095635/0769846183[TUMA MESEJI TAFADHARI]

                                                           

FAHAMU AINA TANO ZA SUMU YA NYOKA NA MATIBABU YAKE....

                                                                        
                             
SUMU YA NYOKA NI IPI?
hii ni sumu ambayo inatolewa na nyoka wakati wa kung'ata mtu, asilimia kubwa ya nyoka ambao wapo kwenye mazingira yetu hua hawana sumu yaani kimsingi ukiona mtu ameng'atwa na nyoka leo afu kesho ndio akaenda hospitali baada ya mguu kuvimba basi ujue nyoka yule haukua na sumu. nyoka wenye sumu kama cobra na black mamba huua ndani ya dakika 20 baada ya kumng'ata mtu.hivyo ukingatwa na uko umbali wa mwendo  dakika 20 kutoka hospitali ujue utakufa tu.

aina za sumu ya nyoka..
cytotoxin poison; hii hushambulia seli za juu za mwili na kuziharibu au kuleta kidonda.

haemotoxin; hii husababisha damu iwe nyepesi sana na kuanza kuvuja ndani kwa ndani au damu kushindwa kuganda kama inamwagika kutoka kwenye kidonda, sumu husababisha sehemu muhimu za mwili kukosa damu na kufa kwa muhusika.

neurotoxins; hii aina ya sumu ambayo hushambulia mishipa ya fahamu, mgonjwa akiingiliwa na sumu hii hawezi kufanya chochote, hata kutikisa kidole hawezi na hufariki baada ya muda mfupi.

cardiotoxins; sumu hii hushambulia moyo wa binadamu na kuulazimisha kusimama hivyo kuleta kifo cha ghafla.

myotoxins; sumu hii hushambulia misuli yote ya binadamu na kuiharibu.

dalili baada ya kuumwa na nyoka...
  • maumivu makali sehemu iliyoshambuliwa.
  • ganzi.
  • kuvimba sehemu husika.
  • kidonda.
  • kuvuja kwa damu[isipozuiliwa huweza kuua.

mishipa ya fahamu; nyoka huyu huweza kutoa sumu kali kwenye mishipa ya fahamu ambayo husimamisha shughuli ya upumuaji na kuua kabla ya matibabu. kabla ya kufa mgonjwa huanza na dalili za kushindwa kuona, kushindwa kupumua vizuri, ganzi na kushindwa kusema.

misuli; nyoka kama rusells vipers, nyoka wa baharini na cobra huweza kuharibu misuli kabisa na kuifanya isambae kwenye mishipa ya damu hivyo kusababisha kufa kwa figo mara moja.

damu; aina ya nyoka kwa jina la boomsling huzuia damu kuganda na kuifanya iwe laini sana, mgonjwa huvuja damu ndani kwa ndani au nje mpaka kifo.

macho; nyoka aina ya cobra hurusha sumu yake moja kwa moja kwenye macho ya binadmu na kuyaharibu au kuleta upofu kiabisa.

huduma ya kwanza..
  • hakikisha mgonjwa anapumua hata kama ni kidogo
  • angalia kama kuna damu inavuja sehemu
  • hakikisha anapaata hewa ya kutosha, asizungukwe na watu.
  • mgonjwa asitembee kwani atasambaza sumu mwilini yaani abebwe palepale.
  • usifunge kamba kwenye mguu kwani imeonekana haizuii chochote zaidi ya kuharibu kiungo husika.
  • usichanje na wembe au kunyonya na kutema sumu kwani utaharibu mishipa ya damu
  • usiweke barafu kwani hakuanushahidi kwamba inasaidia.
  • piga simu kuomba msaada ili mgonjwa apelekwe hospitali.
  • usiweke pombe kwani huongeza ukubwa wa mishipa ya damu na kusambaza sumu zaidi.
  • kama nyoka amekufa nenda naye hospitali daktari amuone ili ajue kama ana sumu au hana sumu.


matibabu ya hospitalini..
kulingana na hali ya mgonjwa hupewa vifuatavyo...
  • huongezewa maji mwilini, hii husaidi kuongeza presha ya damu na kupunguza sumu.
  • hupewa dawa za kuua bacteria[antibiotics]
  • huchomwa sindano ya tetenasi
  • hupewa dawa za maumivu.
  • hushauriwa asiwe na wasiwaasi.
  • kidonda huoshwa na maji mengi na kuondoa jino la nyoka kama lipo.
  • mgonjwa atapewa dawa ya kuondoa sumu mwilini kama ikithibitika nyoka alikua na sumu ambayo inaitwa kitaalamu kama polyvalent antisera kama nyoka hana sumu mgonjwa hatapewa dawa hii.
  • dawa ya kuondoa sumu  hutakiwa utolewe ndani ya dakika 20 kama sio hivyo mgonjwa atafariki.               tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
  •                               
                                                                      STAY ALIVE

                                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 MAWASILIANO; 0653095635/0769846183