data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA PUMU NA MATIBABU YAKE[ BRONCHIAL ASTHMA] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA PUMU NA MATIBABU YAKE[ BRONCHIAL ASTHMA]

                                                                      

pumu ni nini?                                       
huu ni ugonjwa wa njia ya hewa usioambukizwa ambao huambatana na dalili za shida ya kifua kama kushindwa kupumua, kukohoa, kubanwa na kifua na kushindwa kutoa hewa ambayo imevutwa ndani. mgonjwa wa pumu huweza kuvuta hewa ndani lakini hana uwezo wa kuitoa nje kirahisi. kwa maelezo mengine pumu ni aleji inayotokea kwenye mapafu, tumezoea kuona aleji za ngozi tu...

kuna aina mbili za pumu

 1. pumu inayoanzia utotoni ; aina hii ya pumu huanzia utotoni, pumu hii hurithiwa kwenye ukoo, mgonjwa anakua na aleji na vitu fulani kama chakula na mafuta au pafyumu, lakini pia anapata shida zaidi kipindi cha kiangazi ambapo kuna vumbi nyingi, pumu hii hushambulia na kupoa mara kwa mara.
 2. pumu ya ukubwani; aina hii ya pumu hupata watu wazima ambao hawana historia ya ugonjwa huu kwenye koo zao, hawana aleji na kitu chochotena aina hii hushambulia muda wote na mbaya sana kipindi cha baridi kali.
watu walioko kwenye hatari ya kupata pumu

jinsia; 
pumu huwapata sana wavulana mara mbili zaidi kuliko wasichana lakini pia wasichana wengi huipata baada ya kuvunja ungo au baada ya miaka 40.

umri
pumu huwapata watoto wadogo sana na watu wazee sana

rangi
pumu hushambulia watu wa jamii zote yaani weusi na weupe kwa hali moja.

kazi 
pumu hushambulia sana wakulima, wapaka rangi, na wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza plastiki kutokana na harufu na uchafu wanaovuta kwenye shughuli zao.

chanzo cha pumu ni nini?
mpaka leo wataalamu hawafahamu chanzo kikuu ni nini lakini kuna mahusiano makubwa kati ya ugonjwa wa pumu na koo fulani[genetics] au hewa chafu ya mazingira.


shambulio la pumu linakuwaje?
kwa hali ya kawaida mgonjwa wa pumu huwezi kumgundua kama haumfahamu lakini pale anapoguswa na kitu ambacho kinaamsha pumu yake mfano pafyumu, vumbi, moshi au majani ndio shambulio huanza.
pafyumu, vumbi, moshi au chanzo chochote husababisha kinga ya mwili kumwaga maji  ya kamasi kwenye mfumo wa hewa na kubana njia ya koo la hewa na kumfanya mtu ashindwe kupumua. hali hii hutokea ghafla sana na kama mgonjwa asipopata msaada basi anaweza kupoteza maisha.

dalili za ugonjwa wa pumu..
kukohoa sana na kutoa makohozi hasa wakati wa usiku na kushindwa kulala[kikohozi hakina damu]
kushindwa kupumua
kifua kubana
kushindwa kufanya mazoezi

dalili hatari za ugonjwa wa pumu
kushindwa kuongea
kuchanganyikiwa
presha kushuka sana
kupoteza fahamu.
mapigo ya moyo kuongezeka sana au kupungua sana.

vipimo ambavyo hufanywa kuangalia asthma.
x ray kuangalia kifua[chest x ray]
makohozi kuhakikisha sio kifua kikuu[sputum]
kipimo cha damu kuangalia kama kuna aleji ya pumu[full blood picture]

matibabu ya pumu
ugonjwa wa pumu hauponi...., na hapa ndipo waganga wa kienyeji na tiba asili wanapokua waongo...kinachotakiwa na kufuata utaratibu wa kutumia dawa pale unapohitajika kutumia na kujiepusha na vyanzo vya pumu kuamka au kushambulia.
dawa zinazotolewa hospitali ni salbutamol, hydrocortisone, aminopylline na mgonjwa akizidiwa sana hupewa hewa ya oksijeni na antibiotics akiwa hospitali. kumbuka aminopylline na salbutamol hupanua njia ya hewa na ni nzuri kipindi cha shambulio lakini hydrocortisone huzuia mashambulio yajayo hivyo sio muhimu sana wakati wa shambulio.

angalizo; mgonjwa wowote wa pumu anatakiwa atembee na salbutamol inhalor yaani ile ya kuvuta kwa mdomo muda wote hata akienda kuoga kwani pumu huweza kuamka na kushambulia muda wowote na bila ile mgonjwa anaweza asifike hospitali kabla hajapoteza maisha.

madhumuni ya matibabu ya pumu ni nini?
kuondoa dalili za pumu
kuzuia mashambulio ya pumu
kumfanya mtu aishi maisha ya kawaida kama wengine
kuzuia madhara ya dawa za pumu
kuzuia vifo vya pumu.

elimu kwa mgonjwa;
ili mgonjwa pumu aweze kuishi kwa muda mrefu na salama natakiwa afahamu mambo yafuatayo..
 • pumu haiponi; kama sasa hivi kuna mtu anakudanganya kwamba ana dawa ya ungonjwa huu basi anataka kula pesa zako, wewe fuata ushauri wa madaktari wako na utaishi muda mrefu kama wengine.
 • mgonjwa anatakiwa aufahamu ugonjwa wa pumu kiundani kama nilivyoeleza kwenye makala hii.
 • hakuna chakula maalumu sana kwa wagonjwa hawa lakini kuna virutubisho unaweza kutumia kuzuia mashambulio ya mara kwa mara.[ukihitaji tuwasiliane]
 • mgonjwa anaruhusiwa kufanya shughuli zote lakini afahamu vyanzo vinavyosababisha pumu yake imshambulie mfano vumbi na kadhalika.
jinsi ya kuzuia mashambulio ya pumu
 • kaa mbali na wanyama kama mbwa, paka, farasi na kadhalika kwani manyoya yao ni hatari kwako
 • usitumie mto wa kulalia wenye manyoya au pamba.
 • usitumie dawa ambayo hairuhusiwi kwa wagonjwa wa pumu mfano aspirini, propanol na atenolol
 • tambua vyakula ambavyo una aleji na achana navyo navyo kisha achana navyo.
 • jiupushe na kemikali za viwandani zenye harufu kali mfano pafyumu
 • epuka mazoezi makali au mazoezi kwenye hewa chafu.
 • usivute sigara
 • epuka maua na majani yake hivyo vunga madirisha ya chumba chako na hakikisha ni kisafi muda wote.
 • ukitaka kufanya mazoezi usianze ghafla fanya mazoezi ya taratibu kwanza yaani 'warm up' kisha fanya mazoezi zaidi pia tumia salbutamol inhelor kabla ya kuanza mazoezi ili kuapanua njia ya hewa.
mwisho wa ugonjwa wa pumu
kiujumla ugonjwa wa pumu ukitibiwa vizuri na kufuata masharti hauna shida lakini usipofuata masharti basi siku zako za kuishi zinahesabika kwani ugonjwa huu huweza kushambulia mara moja na kuua.kumbuka pumu ya kuzaliwa nayo inasumbua sana kipindi cha kiangazi na ile ya ukubwani kipindi cha baridi.
                                                         STAY ALIVE
                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                        MAWASILIANO 0653095635/0769846183
0 maoni:

Chapisha Maoni