data:post.body HIZI NDIO SABABU 8 ZA KUKOSA HAMU YA KULA KWA WATOTO NA MATIBABU YAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO SABABU 8 ZA KUKOSA HAMU YA KULA KWA WATOTO NA MATIBABU YAKE.

                                                                     
                                                     
watoto wengi husumbua sana kula kipindi  fulani cha maisha yao, japokua wapo ambao sio wasumbufu kula. kuishiwa hamu ya kula kuna vyanzo vingi ambavyo mzazi anatakiwa avichunguze kwa mtoto wake badala ya kufoka au kumanza kumpa dawa mbalimbali. kutokula huku ni hatari kwa mtoto kwani huweza kua chanzo cha magonjwa nyemelezi kwa mtoto. zifuatazo ni sababu kumi kwanini mtoto anapoteza hamu ya kula.

ukuaji wa taratibu; mwaka wa mtoto hua anakua kwa kasi sana hivyo hamu yake ya kula hua nzuri kwasababu mwili unahitaji virutubishoi vingi kwa ajili ya ukuaji lakini akifika mwaka mmoja kwenda wa pili ukuaji unapungua kasi hivyo kula kidogo kipindi hiki ni hali ya kawaida kabisa.

magonjwa; ugonjwa wowote atakao upata mtoto huchangia kukosa kwake hamu ya kula hivyo kama mtoto ana mafua, kikohozi, malaria na kadhalika basi tegemea hamu yake ya kula kua chini sana.

msongo wa mawazo;kama walivyo watu wazima watoto pia hupata mawazo sana kama kuna changamoto zinawakabiri kwenye maisha yao na wakati mwingine mzazi ndio chanzo cha matatizo hayo mfano kutoa adhabu kali akifanya kosa, kumfokea na kumtukana mbele za watu, kumnyima haki zake za msingi kama hela ya kula shule na mguo za kuvaa au kifo cha mzazi au mlezi.

matumizi ya dawa fulani fulani; kama mtoto wako kuna dawa anameza basi zinaweza kumfanya akose hamu ya kula mfano dawa nyingi za kuua bakteria au antibiotics hupunguza  hamu ya kula.

upungufu wa damu; hii ni hatari sana kwa watoto kwani inaweza kufanya mtoto ashindwe kukua na kua na maendeleo mabovu darasani hivyo ni muhimu pia kupima damu ya mtoto kuona kama ana upungufu wa damu au vipi.

minyoo; minyoo mbalimbali ya tumbo hushambulia kuta za tumbo, huleta kichefuchefu, na kuharisha na hali hii huweza kuchangia sana kuondoka kwa hamu ya kula.

choo ngumu sana; kama choo inatoka ngumu sana maana yake kuna vyakula vingi havitoki tumboni hivyo mtoto hawezi kula.

ukosefu wa madini muhimu mwilini; baadhi ya madini kama vitamin b, vitamin c na kadhalika ni muhimu sana kwa ajili ya kuongeza hamu ya kula. ukosefu wa madini hayo huweza kuondoa hamu ya kula.


                                                     matibabu

  • hakuna matibabu ya moja kwa moja ya kukosa hamu ya kula kwa watoto ila kikubwa cha kuzingatia ni kutibu chanzo husika cha kukosekana kwa hamu ya kula.
  • usimtukane au kumchukiza mtoto wakati wa kula kwani utamfanya ashindwe kula kabisa na kama una kesi naye subiri amalize kula.
  • weka ratiba yako vizuri ili upakue wakati mtoto ana njaa sio kula tu sababu muda umefika.
  • kama mtoto anataka kudokoa chakula jikoni kabla ya muda wa kula muache tu ale itamsaidia.
  • muache mtoto akacheze na wenzake huko nje, usipende sana ashinde ndania anacheza gemu za kompyuta kwani hazimjengi. michezo na wtoto wenzake inamjenga na kuleta njaa kali.
  • usimlazimishe kumaliza chakula kama amebakiza, henda hana njaa..unaweza kumwambia kifunike akimalizie baadae.
  • pika chakula anachopenda, usiwe mvivu kupika mara mbili mbili...watoto wengi hawapendi ugali basi ikipidi wape wali muda wote na nyinyi muendelee na ugali wenu. waongezee nyama, samaki,maharage, mboga za majani na matunda.
  • mpe virutubisho vya hamu ya kula, vipo vya aina mbalimbali na vizuri na vimesaidia wengi ambao walikua wamekata tamaa kwa watoto wao.tunaweza kuwasiliana ukihitaji.
  •                                              
mwisho; katika harakati za wazazi kutaka watoto wale basi wamejikuta wakiharibu watoto kwa kuwafanya wawe wanenene sana, kuwapa vyakula ambavyo sio muhimu kwa mwili kama soda, biskuti,chocolate, chips na kadhalika na kusahau matunda na mboga za majani. hivyo hakikisha mtoto wako hanenepi sana kwani anakua kwenye hatari ya magonjwa ya moyo na kisukari.
                                         tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                            STAY ALIVE
                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                       MAWASILIANO 0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni