data:post.body Agosti 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIO NJIA NANE ZA KUMKAGUA MGONJWA WAKO AU MTU YEYOTE KAMA AMEFARIKI KWELI.

                                                                     
kumekua na ripoti nyingi na matukio ambayo inatokea mtu anazikwa kabla hajafa, hasa sehemu za vijijini sana ambapo hakuna madaktari au wahudumu wa afya. kwa sheria za tanzania, mgonjwa akifia hospitali basi dakatari ndio anaruhusiwa kukagua na kuhakikisha kweli mgonjwa huyu amefariki kabla ya kwenda kuzikwa. elimu hii ya kujua kama mgonjwa bado yuko hai au amekufa ni vizuri ikatolewa kwa watu wote ili kuepusha matukio hayo ya kuzika watu walio poteza fahamu tu wakidhani ni wafu.zifuatazo ni dalili hizo...

kusima kwa mfumo wa upumuaji; muangalie mtu kifuani kisha kua makini, kwa mtu aliyepoteza fahamu utaona kifua kinapanda na kushuka lakini kwa mtu mfu utaona kifua kimetulia kabisa na hakuna dalili za kupumua hata kwa mbali.

kusimama kwa mapigo ya moyo; haya unaweza kuyasikia kwa kutumia kifaa maaluma kwa jina la stethoscope lakini kwa mtu wa kawaida ambaye sio mtaalamu basi weka sikio lako upande wa kushoto mwa kifua cha mtu  na kama husikiii mapigo ya moyo huyu mtu ni mfu.
                                                                 
                                       

msukumo wa damu; hii kitaalamu inaitwa pulse rate,kwa kutumia vidole vyako viwili vya mkono wako kandamiza kidogo sehemu ya mkono ambapo kuna kidole gumba. kwa kawaida utahisi damu inapita na inasukuma vidole vyako na kama husikii kabisa basi huyo ni mfu.pia unaweza kuweka vidole shingoni kama wafanyavyo askari mara nyingi kukagua kifo.
                                             

angalia jicho; jicho lina duara mbili nyeusi, moja ni kubwa na nyingine ndogo kabisa kitaalamu tunaita pupil. kwa hali ya kawaida pupil ukipiga tochi ghafla nasinyaa na ukitoa tochi inapanuka kawaida. sasa kwa mfu hautaona hayo mabadiliko lakini pia pupil yake itakua imepanuka kuliko kawaida.angalia tofauti kwenye picha hizi mbili.


kukakamaa sana; kutokana na kusimama kwa kazi ya mishipa ya fahamu, mfu hukakamaa sana muda tu baada ya kufa na usipowahi kumnyosha basi anaweza asirudi kwenye hali ya kawaida.
                                                     

kuwa wa baridi; inategemea na muda wa kifo lakini mara nyingi masaa nane baada ya kifo mtu huanza kuwa wa baridi sana kuliko kawaida hasa miguuni kutokana na kupotea kwa joto la kawaida la kiumbe hai.

kuanza kutoa harufu kali; vitu laini sana kwenye mwili wa binadamu kama ubongo na utumbo huanza kuoza haraka mtu anapokufa, hivyo harufu kuotekea sehemu zote zenye mashimo kama pua, mdomo, na sehemu za siri huanza kutoka.

kutosikia maumivu kabisa; mfinye sana mgonjwa miguuni au mkononi au sehemu yeyote yenye nyama lakini hautaona ushirikiano wowote.

mwisho; kuna njia zingine za kujua kifo ambazo zinatumia vifaa maalumu na zingine huwezi kuzielewa kama wewe sio daktari, lakini ukiona dalili zote hizo kwa mgonjwa kwa uhakika basi unaweza kusema amefariki japokua ni vizuri kumuita na daktari ahakikishe ila kama ni kijijini sana basi mnaweza kuzika.unaweza kubonyeza maneno ya kijani kwa maelezo zaidi na kupitia blog yangu ya kingereza.
                                      tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                                      
                                                       STAY ALIVE
                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                MAWAASILIANO;     0653095635/0769846183
     

HIZI NDIO SABABU KUMI KWANINI WANAUME HUFA MAPEMA KULIKO WANAWAKE.

                                                           
               
ukifanya utafiti wako binafsi utagundua bibi wako wengi duniani kuliko babu lakini pia wanaume kwa kila umri ni wachache kuliko wanawake...unaweza ukadhani labda wanawake wanazaliwa wengi lakini hiyo sio hoja kuu. wanaume wanazaliwa wachache kuliko wanaume ni kweli lakini hufa mapema kuliko wanawake na kuwafanya waonekane wachache zaidi duniani. kuna tafiti nyingi zimefanyika lakini haya ni baadhi ya majibu yaliyopatikana.

wanaume huhatarisha sana maisha yao; ubongo wa mbele wa binadamu unaotufanya tufikiri, tusome na kutoa hukumu unakua taratibu sana kwa wanaume kuliko wanawake, hii inawafanya katika ile hali ya utoto kufanya vitu vya hatari mno bila kuogopa.watoto wa kiume ni wasumbufu na hawasikii.kukimbiza baiskeli, kuogelea na kujaribu kila kitu..wakishakua kidogo wanaume huanza kunywa pombe kali sana, kuvuta sigara, bangi na madawa ya kulevya na kuanza kuugua magonjwa ya kutisha.

wanaume wana miili mikubwa kuliko wanawake; kitaalmu katika biolojia viumbe vyote vyenye miili mikubwa hufa haraka kuliko vile vyenye miili midogo hii ni kwasababu ya mifumo inayofanya kazi kuendesha miili hii kuchoka mapema katika maisha lakini pia hatarini kushambuliwa na magonjwa au ajari mbalimbali.

wanaume wanafanya kazi hatarishi zaidi; majeshi yote duniani, machimbo yote ya madini na viwanda vikubwa huwatumia wanaume kwani wana nguvu sana na wana uwezo wa kuvumilia hali ngumu. kazi hizo ni hatari sana kwa maisha ya binadamu.

hali ya kujiamini sana; sio rahisi mwanaume kukubali kushindwa kupigwa na mtu fulani na mara chache sana mwanaume anaweza akaugua na kwenda hospitali, wengi hujikausha na kwenda hali ikiwa mbaya kabisa.

wanaume wanajiua sana kuliko wanawake; wanawake utawasikia wanasema tu kwamba ipo siku ntajiua lakini mwisho wa siku hawafanyi hivyo. lakini mwanume ukimsikia anataka kujiua toa taarifa mapema apate msaasa kwani atajiua kweli.

dunia haiwajali sana; kesi za wanaume kupigwa na wake zao sio muhimu sana kwenye jamii lakini wapo waliopigwa mpaka kufa, lakini pia kwenye matatizo yeyote ya magonjwa ya kulipuka au ajari basi watoto na wanawake ndio hupewa kipaumbele. historia inaonyesha wakati meli ya titanic inazama zaidi ya  miaka 100 iliyopita wanawake na watoto ndio waliokolewa sana.

wana msongo sana wa mawazo; dunia nzima inajua wanaume ndio wanaohusika kwa malezi ya familia yaani gharama za kuendesha familia. leo hii hata kama baba na mama wanafanya kazi basi ikitokea watoto wamelala njaa basi atalaumiwa mwanaume lakini pia migogoro ya mke wake na mama yake mzazi au dada zake inamuweke sehemu ngumu sana achague nani amuache nani. hii huweza kuleta magonjwa ya moyo na presha na kumletea kifo mapema.

wanaume ni wagomvi sana; huenda sababu ya wingi wa homoni ya testosterone kwenye damu zao, wanaume wanapigana sana kuliko wanawake na hii huwaweka kwenye hatari ya kuchomwa visu au risasi na kufa.

ni walengwa wa matukio yote hatari; ukitaka kuvamia sehemu yeyote kama jeshi au mashambulio ya kigaidi lazima ujue wanaume wako wangapi na hao ndio ukiwaua utafanikiwa kuchukua hiyo sehemu na bila hivyo haitawezekana.

wanakosa matibabu mazuri; sera za afya za nchi nyingi zinawalenga wanawake zaidi kuliko wanaume ndio maana utasikia matibabu kwa wanawake na watoto bure lakini wapo wanaume wengi wasio na uwezo wa kugharamia hizo gharama na hufia majumbani kwao.bofya kijani hapa kwenye blog yetu ya kingereza kwa elimu zaidi.
                       
                                           tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                             STAY ALIVE

                                      DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                       MAWASILIANO 0653095635/0769846183
















HIZI NDIO SABABU 8 ZA KUKOSA HAMU YA KULA KWA WATOTO NA MATIBABU YAKE.

                                                                     
                                                     
watoto wengi husumbua sana kula kipindi  fulani cha maisha yao, japokua wapo ambao sio wasumbufu kula. kuishiwa hamu ya kula kuna vyanzo vingi ambavyo mzazi anatakiwa avichunguze kwa mtoto wake badala ya kufoka au kumanza kumpa dawa mbalimbali. kutokula huku ni hatari kwa mtoto kwani huweza kua chanzo cha magonjwa nyemelezi kwa mtoto. zifuatazo ni sababu kumi kwanini mtoto anapoteza hamu ya kula.

ukuaji wa taratibu; mwaka wa mtoto hua anakua kwa kasi sana hivyo hamu yake ya kula hua nzuri kwasababu mwili unahitaji virutubishoi vingi kwa ajili ya ukuaji lakini akifika mwaka mmoja kwenda wa pili ukuaji unapungua kasi hivyo kula kidogo kipindi hiki ni hali ya kawaida kabisa.

magonjwa; ugonjwa wowote atakao upata mtoto huchangia kukosa kwake hamu ya kula hivyo kama mtoto ana mafua, kikohozi, malaria na kadhalika basi tegemea hamu yake ya kula kua chini sana.

msongo wa mawazo;kama walivyo watu wazima watoto pia hupata mawazo sana kama kuna changamoto zinawakabiri kwenye maisha yao na wakati mwingine mzazi ndio chanzo cha matatizo hayo mfano kutoa adhabu kali akifanya kosa, kumfokea na kumtukana mbele za watu, kumnyima haki zake za msingi kama hela ya kula shule na mguo za kuvaa au kifo cha mzazi au mlezi.

matumizi ya dawa fulani fulani; kama mtoto wako kuna dawa anameza basi zinaweza kumfanya akose hamu ya kula mfano dawa nyingi za kuua bakteria au antibiotics hupunguza  hamu ya kula.

upungufu wa damu; hii ni hatari sana kwa watoto kwani inaweza kufanya mtoto ashindwe kukua na kua na maendeleo mabovu darasani hivyo ni muhimu pia kupima damu ya mtoto kuona kama ana upungufu wa damu au vipi.

minyoo; minyoo mbalimbali ya tumbo hushambulia kuta za tumbo, huleta kichefuchefu, na kuharisha na hali hii huweza kuchangia sana kuondoka kwa hamu ya kula.

choo ngumu sana; kama choo inatoka ngumu sana maana yake kuna vyakula vingi havitoki tumboni hivyo mtoto hawezi kula.

ukosefu wa madini muhimu mwilini; baadhi ya madini kama vitamin b, vitamin c na kadhalika ni muhimu sana kwa ajili ya kuongeza hamu ya kula. ukosefu wa madini hayo huweza kuondoa hamu ya kula.


                                                     matibabu

  • hakuna matibabu ya moja kwa moja ya kukosa hamu ya kula kwa watoto ila kikubwa cha kuzingatia ni kutibu chanzo husika cha kukosekana kwa hamu ya kula.
  • usimtukane au kumchukiza mtoto wakati wa kula kwani utamfanya ashindwe kula kabisa na kama una kesi naye subiri amalize kula.
  • weka ratiba yako vizuri ili upakue wakati mtoto ana njaa sio kula tu sababu muda umefika.
  • kama mtoto anataka kudokoa chakula jikoni kabla ya muda wa kula muache tu ale itamsaidia.
  • muache mtoto akacheze na wenzake huko nje, usipende sana ashinde ndania anacheza gemu za kompyuta kwani hazimjengi. michezo na wtoto wenzake inamjenga na kuleta njaa kali.
  • usimlazimishe kumaliza chakula kama amebakiza, henda hana njaa..unaweza kumwambia kifunike akimalizie baadae.
  • pika chakula anachopenda, usiwe mvivu kupika mara mbili mbili...watoto wengi hawapendi ugali basi ikipidi wape wali muda wote na nyinyi muendelee na ugali wenu. waongezee nyama, samaki,maharage, mboga za majani na matunda.
  • mpe virutubisho vya hamu ya kula, vipo vya aina mbalimbali na vizuri na vimesaidia wengi ambao walikua wamekata tamaa kwa watoto wao.tunaweza kuwasiliana ukihitaji.
  •                                              
mwisho; katika harakati za wazazi kutaka watoto wale basi wamejikuta wakiharibu watoto kwa kuwafanya wawe wanenene sana, kuwapa vyakula ambavyo sio muhimu kwa mwili kama soda, biskuti,chocolate, chips na kadhalika na kusahau matunda na mboga za majani. hivyo hakikisha mtoto wako hanenepi sana kwani anakua kwenye hatari ya magonjwa ya moyo na kisukari.
                                         tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                            STAY ALIVE
                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                       MAWASILIANO 0653095635/0769846183

FAHAMU CHANZO CHA UZITO MDOGO AU WEMBAMBA SANA NA MATIBABU YAKE...

                                                                   
                                                           
japokua dunia ya sasa inakabiliwa na tatizo kubwa la watu kua wanene sana lakini kuna changamoto ya watu ambao ni wembamba sana kiasi kwamba wembamba wao ni hatari kiafya. tafiti zinaonyesha kwamba ukiwa mwembamba sana una hatari ya kufa mapema kwa 100% lakini ukiwa mnene sana una hatari ya kufa mapema kwa 50% hivyo unaweza kuona kwamba wembamba sana ni hatari kuliko unene sana.

uzito mdogo maana yake nini? 
kua chini ya 18.5 kwa vipimo vya body mass index ambavyo vinapatikana kwa kuchukua uzito wako kwa kilogram na kugawanya kwa [ urefu wako zidisha mara mbili kwa kipimo cha mita]. mfano una kilo 75 urefu wa 1.75m unachukua 75 gawanya kwa[1.75x1.75] jibu ni 24.4 huyu yuko kwenye uzito sahihi. lakini  ukizidi body mass index ya 25 umezidi unene na chini ya 18 umezidi wembamba.
tatizo la kua na uzito mdogo linawaathiri wanawake zaidi na huwatesa sana kisaikolojia kwani wengi wao hutamani kua na miili mzuri kama wenzao.

chanzo ni nini?
kuna sababu mbalimbali zinaweza kuchangia mtu kua na uzito mdogo au mwembamba sana kama ifuatavyo.

matatizo ya kushindwa kula; tatizo la kutokua na hamu ya kula, hofu ya kunenepa sana iwapo utakula sana hii inawasumbua sana wasichana wanaopenda mambo ya urembo, matatizo ya kisaikolojia huchangia sana mtu kua mwembamba kitaalamu tunaita anorexia nervosa.

matatizo ya mfumo wa homoni; kuna ugonjwa unaitwa hyperthroidism, huu ni ugonjwa ambao unafanya mwili kufanya mambo yake kwa haraka sana huanza na dalili za kuharisha, kula sana, kutokwa sana jasho, kusikia joto sana na kadhalika. halii hii hupunguza uzito sana na mtu hawezi kuongezeka uzito bila kutibiwa ugonjwa huu.

magonjwa ya utumbo wa chakula; kuna magonjwa ya utumbo yanayoweza kusababisha mtu kushindwa kula aina fulani ya vyakula au kuharisha kila anapokucha chakula fulani. hii hupunguza sana uzito mfano tropical sprue.

ugonjwa wa kisukari; kua na ugonjwa wa kisukari ambayo haitibiwi vizuri humaliza hifadhi yote ya vyakula mwilini na kufanya watu wawe wembamba sana.

kurithi; kuna baadhi ya koo watu ni wembamba tu kwanzia bibi mpaka wajukuu, japokua wembamba huu sio hatari lakini ukiwa chini ya vipimo nilivyotaja basi ni hatari.

ugonjwa wa saratani; magonjwa yote ya saratani hutumia kiasi kikubwa cha chakula na kumfanya mtu apungue uzito sana.

baadhi ya magonjwa ya kuambukizwa; magonjwa kama ukimwi na kifua kikuu huudhoofisha mwili sana na kumuacha na uzito mdogo sana.

nini madhara ya uzito mdogo?
uzito mdogo husababisha magonjwa ya akili, kushusha kinga ya mwili na kuugua mara kwa mara, kukosa hedhi, ugumba, kuwa na mifupa milaini inayovunjika kirahisi na kadhalika.

kitu gani ufanye kuengezeka uzito?
kimsingi kanuni ya kuongezeak uzito ni ndogo ya kula sana kuliko kazi unazofanya, unaweza kunywa soda nyingi, sukari nyingi, na vyakula vyovyote vya haraka[fast foods] lakini hio sio njia nzuri ya kuongeza uzito kwani vyakula hivyo huambatana na magonjwa hatari ya mwili kama kisukari na magonjwa ya moyo lakini pia unaweza ukapata unene mbaya. njia nzuri ni kufuata yafuatayo.

kula vyakula vingi; changanya vyakula vya aina mbalimbali na ule angalau mara tatu kwa siku na ushibe. vyakula vya protini kama nyama, mayai, samaki, maziwa, karanga na kadhalika, vyakula vya wanga kama ugali,wali, viazi,mihogo, na kadhalika, vyakula vya mafuta kama mafuta ya siagi, alizeti,korie na kadhalika. jitahidi ule mara tatu au mara nne ya chakula unachokila sasa hivi.
protini ni muhimu sana kwani yenyewe ndio inayojenga misuli ya mwili hivyo ni vizuri kula kwa wingi.

fanya mazoezi ya kubeba chuma; nenda gym uanze mazoezi ya kubeba chuma kwani mazoezi haya yatazuia kuongezeka uzito kwa mafuta na kukupa ongezeko la uzito la misuli na kua na mwili mzuri. mazoezi ya chuma ni kwa jinsia zote.

tibu ugonjwa kama upo; kama unahisi kuna ugonjwa wowote unaokusumbua hakikisha umetibiwa na kupona au unapata matibabu yake hata kama hautibiki kabisa basi angalau tumia dawa za kupoza mfano kisukari au ukimwi, usipotibu chanzo cha ugonjwa unao kupunguza uzito huweza nenepa kwa njia yeyote ile.

usinywe maji kabla ya kula; tabia hii itakufanya ujaze tumbo na maji na kukufanyaushindwe kula chakula cha kutosha.

kula mara kwa mara; usijibanie kula kabisa, kila ukipata nafasi we kula tu, ikibidi kula hata muda wa kwenda kulala kwani inasaidia sana kuongezeka uzito.

kunywa maziwa mengi; ukipata kiu ya maji kunywa maziwa kwanza kama yapo afu ndio unywe maji kwani maziwa yana protini muhimu kwa ajili ya kuongeza uzito.

jaribu virutubisho maalumu kwa ajili ya kuongeza uzito; kuna virutubisho vingi vimetengezwa maalumu kwa ajili ya kazi hii, ambavyo vinauzwa na kampuni mbalimbali. vitutubisho hivi vinakuwa na protini na madini mengi kuliko chakula cha kawaida na ukivitumia unaongezeka uzito ndani ya muda mfupi sana.unaweza kuwasiliana na sisi ukivihitaji.
                                               
tumia sahani kubwa wakati wa kula; sahani kubwa itakufanya upakue chakula kingi sana na kukupa nafasi ya kula sana tofauti na kutumia sahani ndogo ambayo hukubana kula.

pata usingizi wa kutosha; usingizi ni muhimu sana kwa ukuaji wa misuli ya binadamu.

kula mboga za majani na matunda mwisho wa mlo; mboga za majani  na matunda hupunguza uzito hivyo ukila mwanzoni zijaza nafasi tumboni na kumaliza nafasi ya vyakula vingine.

acha ulevi wa pombe na sigara; tabia hizi hupunguza sana lishe ya mwili na kumfanya mtu ashindwe kuongezeka uzito.

mwisho; shughuli ya kuongeza uzito sio rahisi kama jinsi shughuli ya kupunguza uzito...uzito unaongezeka taratibu ndani ya muda fulani na ukiamua kuongezeka uzito unatakiwa ujipe angalau miezi mitatu kwenda mbele kulingana na kilo unazotaka kuongeza na ili kupata moyo wa kuendelea basi  pima uzito angalau kila wiki kuona maendeleo.
                               tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                        STAY ALIVE
                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                     MAWASILIANO 0653095635/0769846183







HII NDIO MIDA SAHIHI YA KULA CHAKULA ILI UWE NA AFYA BORA.

                                                         
ulaji wa chakula una tofautiana sana kulingana na jamii husika, lakini ulaji huo ndio unao amua jamii fulani iwe na afya nzuri au mbaya..mfano nchi bara la asia wana mfumo mzuri wa kula ndio maana wengi wao ni wembamba na wana afya nzuri lakini nchi za ulaya mfumo wao wa kula si mzuri na sisi tunawaiga wao na kuumia zaidi..leo ntaenda kuongelea muda mzuri wa kula kwanzia asubuhi mpaka jioni na sababu zake.

chakula cha asubuhi, saa 1 mpaka saa 2 asubuhi na sio zaidi ya saa 4; hichi ni chakula kinacholiwa cha kwanza kabla ya kuanza shughuli yeyote kila siku, kimsingi chakula hiki kinatakiwa kiwe kingi kuliko milo yote ya siku nzima kwani muda huu watu wengi huenda kwenye shughuli nzito za siku nzima. lakini ni tofauti kwenye jamii zetu kwani watu hula kidogo sana asubuhi. kukosa kabisa chakula hiki huharibu ubongo na kumfanya mtu ashindwe kufikiria vizuri akiwa kazini..
                                                                   

chakula cha mchana, saa 6 mpaka saa 8 mchana na sio zaidi ya saa 9; chakula hiki hutakiwa kuliwa ndani ya masaa hayo ili kuweka kiasi cha sukari mwilini katika hali nzuri bila kupungua, kula zaidi ya hapo njaa hua kali, tindikali huanza kuunguza kuta za tumbo na kumfanya mtu ashindwe kufanya kazi kwa ufanisi.chakula hiki kinatakiwa kipungue kidogo kulinganisha na kile cha asubuhi.
                                                                 

chakula cha usiku, saa 12 mpaka saa 3 usiku na sio zaidi ya saa 4 usiku; hiki na chakula ambacho kinaliwa jioni. kinatakiwa kiwe kidogo sana kuliko milo yote kwani muda huu ni muda wa kwenda kulala na ukila chakula kingi hakifanyi kazi zaidi ya kubadilishwa na mwili kua mafuta.ikiwezekana kula matunda tu na mboga za majani.chakula cha usiku ndio chakula kinacholeta vitambi na unene kwa watu wengi na kushindwa kupata usingizi mzuri.
                                                           

mwisho; ukiaangalia mfumo nilioandika hapo juu ni tofauti kabisa na jinsi watu wanavyokula afrika kwa ujumla yaani watu huanza na chakula kidogo asubuhi na kushindilia usiku wakati wa kwenda kulala kitu ambacho sio sahihi hata kidogo. kumbuka maji ya kunywa yanatakiwa yatumike nusu saa kabla au baada ya kula lakini kama unapunguza uzito kunywa maji mengi kabla ya kula ili ule tumbo lijae uweze kula chakula kidogo.lakini pia jitahidi kula mchanganyiko wa vyakula vyote kila mlo yaani mchanganyiko wa wanga, protini, mboga za majani, matunda, na maji mengi, isipokua usiku tu ambapo unaweza kula matunda na kulala.
                                                       
                                                 tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                               STAY ALIVE
                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                    MAWASILIANO; 0653095635/0769846183


UFAHAMU UGONJWA WA PUMU NA MATIBABU YAKE[ BRONCHIAL ASTHMA]

                                                                      

pumu ni nini?                                       
huu ni ugonjwa wa njia ya hewa usioambukizwa ambao huambatana na dalili za shida ya kifua kama kushindwa kupumua, kukohoa, kubanwa na kifua na kushindwa kutoa hewa ambayo imevutwa ndani. mgonjwa wa pumu huweza kuvuta hewa ndani lakini hana uwezo wa kuitoa nje kirahisi. kwa maelezo mengine pumu ni aleji inayotokea kwenye mapafu, tumezoea kuona aleji za ngozi tu...

kuna aina mbili za pumu

  1. pumu inayoanzia utotoni ; aina hii ya pumu huanzia utotoni, pumu hii hurithiwa kwenye ukoo, mgonjwa anakua na aleji na vitu fulani kama chakula na mafuta au pafyumu, lakini pia anapata shida zaidi kipindi cha kiangazi ambapo kuna vumbi nyingi, pumu hii hushambulia na kupoa mara kwa mara.
  2. pumu ya ukubwani; aina hii ya pumu hupata watu wazima ambao hawana historia ya ugonjwa huu kwenye koo zao, hawana aleji na kitu chochotena aina hii hushambulia muda wote na mbaya sana kipindi cha baridi kali.
watu walioko kwenye hatari ya kupata pumu

jinsia; 
pumu huwapata sana wavulana mara mbili zaidi kuliko wasichana lakini pia wasichana wengi huipata baada ya kuvunja ungo au baada ya miaka 40.

umri
pumu huwapata watoto wadogo sana na watu wazee sana

rangi
pumu hushambulia watu wa jamii zote yaani weusi na weupe kwa hali moja.

kazi 
pumu hushambulia sana wakulima, wapaka rangi, na wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza plastiki kutokana na harufu na uchafu wanaovuta kwenye shughuli zao.

chanzo cha pumu ni nini?
mpaka leo wataalamu hawafahamu chanzo kikuu ni nini lakini kuna mahusiano makubwa kati ya ugonjwa wa pumu na koo fulani[genetics] au hewa chafu ya mazingira.


shambulio la pumu linakuwaje?
kwa hali ya kawaida mgonjwa wa pumu huwezi kumgundua kama haumfahamu lakini pale anapoguswa na kitu ambacho kinaamsha pumu yake mfano pafyumu, vumbi, moshi au majani ndio shambulio huanza.
pafyumu, vumbi, moshi au chanzo chochote husababisha kinga ya mwili kumwaga maji  ya kamasi kwenye mfumo wa hewa na kubana njia ya koo la hewa na kumfanya mtu ashindwe kupumua. hali hii hutokea ghafla sana na kama mgonjwa asipopata msaada basi anaweza kupoteza maisha.

dalili za ugonjwa wa pumu..
kukohoa sana na kutoa makohozi hasa wakati wa usiku na kushindwa kulala[kikohozi hakina damu]
kushindwa kupumua
kifua kubana
kushindwa kufanya mazoezi

dalili hatari za ugonjwa wa pumu
kushindwa kuongea
kuchanganyikiwa
presha kushuka sana
kupoteza fahamu.
mapigo ya moyo kuongezeka sana au kupungua sana.

vipimo ambavyo hufanywa kuangalia asthma.
x ray kuangalia kifua[chest x ray]
makohozi kuhakikisha sio kifua kikuu[sputum]
kipimo cha damu kuangalia kama kuna aleji ya pumu[full blood picture]

matibabu ya pumu
ugonjwa wa pumu hauponi...., na hapa ndipo waganga wa kienyeji na tiba asili wanapokua waongo...kinachotakiwa na kufuata utaratibu wa kutumia dawa pale unapohitajika kutumia na kujiepusha na vyanzo vya pumu kuamka au kushambulia.
dawa zinazotolewa hospitali ni salbutamol, hydrocortisone, aminopylline na mgonjwa akizidiwa sana hupewa hewa ya oksijeni na antibiotics akiwa hospitali. kumbuka aminopylline na salbutamol hupanua njia ya hewa na ni nzuri kipindi cha shambulio lakini hydrocortisone huzuia mashambulio yajayo hivyo sio muhimu sana wakati wa shambulio.

angalizo; mgonjwa wowote wa pumu anatakiwa atembee na salbutamol inhalor yaani ile ya kuvuta kwa mdomo muda wote hata akienda kuoga kwani pumu huweza kuamka na kushambulia muda wowote na bila ile mgonjwa anaweza asifike hospitali kabla hajapoteza maisha.

madhumuni ya matibabu ya pumu ni nini?
kuondoa dalili za pumu
kuzuia mashambulio ya pumu
kumfanya mtu aishi maisha ya kawaida kama wengine
kuzuia madhara ya dawa za pumu
kuzuia vifo vya pumu.

elimu kwa mgonjwa;
ili mgonjwa pumu aweze kuishi kwa muda mrefu na salama natakiwa afahamu mambo yafuatayo..
  • pumu haiponi; kama sasa hivi kuna mtu anakudanganya kwamba ana dawa ya ungonjwa huu basi anataka kula pesa zako, wewe fuata ushauri wa madaktari wako na utaishi muda mrefu kama wengine.
  • mgonjwa anatakiwa aufahamu ugonjwa wa pumu kiundani kama nilivyoeleza kwenye makala hii.
  • hakuna chakula maalumu sana kwa wagonjwa hawa lakini kuna virutubisho unaweza kutumia kuzuia mashambulio ya mara kwa mara.[ukihitaji tuwasiliane]
  • mgonjwa anaruhusiwa kufanya shughuli zote lakini afahamu vyanzo vinavyosababisha pumu yake imshambulie mfano vumbi na kadhalika.
jinsi ya kuzuia mashambulio ya pumu
  • kaa mbali na wanyama kama mbwa, paka, farasi na kadhalika kwani manyoya yao ni hatari kwako
  • usitumie mto wa kulalia wenye manyoya au pamba.
  • usitumie dawa ambayo hairuhusiwi kwa wagonjwa wa pumu mfano aspirini, propanol na atenolol
  • tambua vyakula ambavyo una aleji na achana navyo navyo kisha achana navyo.
  • jiupushe na kemikali za viwandani zenye harufu kali mfano pafyumu
  • epuka mazoezi makali au mazoezi kwenye hewa chafu.
  • usivute sigara
  • epuka maua na majani yake hivyo vunga madirisha ya chumba chako na hakikisha ni kisafi muda wote.
  • ukitaka kufanya mazoezi usianze ghafla fanya mazoezi ya taratibu kwanza yaani 'warm up' kisha fanya mazoezi zaidi pia tumia salbutamol inhelor kabla ya kuanza mazoezi ili kuapanua njia ya hewa.
mwisho wa ugonjwa wa pumu
kiujumla ugonjwa wa pumu ukitibiwa vizuri na kufuata masharti hauna shida lakini usipofuata masharti basi siku zako za kuishi zinahesabika kwani ugonjwa huu huweza kushambulia mara moja na kuua.kumbuka pumu ya kuzaliwa nayo inasumbua sana kipindi cha kiangazi na ile ya ukubwani kipindi cha baridi.
                                                         STAY ALIVE
                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                        MAWASILIANO 0653095635/0769846183








ZIFAHAMU NJIA TANO ZA KUTABIRI JINSIA YA MTOTO KABLA HAJAZALIWA...

                                                               
                                                               
jinsia ya mtoto inaweza isiwe muhimu sana kwa mzazi fulani lakini kuna baadhi ya jamii za watu ambao swala la jinsia ni muhimu sana na hufarijika sana wanapopata jinsia fulani japokua hii inaweza kua changamoto kwani mzazi fulani anaweza kutoa mimba akiambiwa mtoto wako ni jinsia fulani. baadhi ya sheria za nchi haziruhusu vipimo vya kutaja jinsia ya mtoto ili kuepusha uwezekano wa kutoa mimba au kumchukia mtoto hata kabla hajazaliwa.huko india inasemekana wanawake ndio wanatoa mahali kwa wanaume hivyo wazazi hawapendi watoto wengi wa kike kwani ni hasara lakini pia hata kwenye jamii zetu baba bila kupata dume haridhiki.kuna njia kadhaa za kuweza kutambua jinsia ya mtoto, baadhi ni uhakika yaani asilimia mia moja na zingine uhakika wake ni kama asilimia themanini kulingana na sababu fulani fulani.zifuatazo ni njia hizo.

kipimo cha picha ya utrasound; hichi ni kipimo kinachotumia mfumo maalumu wa kuangalia ndani ya tumbo la uzazi na kutuma taarifa zake kwenye kioo cha mashine hiyo. kikitumika na mtaalamu mzuri kinasoma jinsia ya mtoto kwa zaidi ya asilimia mia moja.utafiti unaonyesha mimba zinazopimwa kwanzia wiki ya 18 kwenda mbele zinatoa majibu ya uhakika kabisa.
                                                 
maji ya ndani ya kizazi cha mtoto; hii kitaalamu inaitwa amniocentesis and chorionic villus sampling ni kipimo ambacho maji ya mama ya nadani ya kizazi yanachukuliwa na kwenda kupimwa. kipimo hicho hakigundui jinsia tu bali hata magonjwa ya kurithi kama siko seli au ugonjwa ambao unaweza kua umempata mtoto tumboni.
                                                       
uzito wa mtoto; utafiti unaonyesha watoto wa kiume huzaliwa wakubwa na wazito sana ukilinganisha na watoto wa kike hivyo ukiona mimba yako ni kubwa sana kuliko kawaida kuna uwezekano mkubwa wa kuzaa mtoto wa kiume na mimba ndogo mara nyingi huleta watoto wa kike.
                                                 
kichefuchefu na kutapika; baadhi ya tafiti zimeonyesha mama anayebeba mtoto wa kike hua anasumbuliwa sana na tatizo la kichefuchefu na kutapika kulilo yule anayebeba mtoto wa kiume, kitaalamu mtoto wa kike hua na homoni kama za mama akiwa bado tumboni huenda ikawa ndio chanzo cha dalili hizi.              
       
   
mapigo ya moyo ya mtoto; kwa kutumia kifaa cha mkononi kitaalamu kama fetoscope nesi au daktari anaweza kutambua mapigo ya moyo ya mtoto aliyeko tumboni. tafiti zinaonyesha katika kipindi cha mimba na mama akiwa hana shida yeyote au haumwi ugonjwa wowote mapigo ya moyo ya mtoto  wa kike ni zaidi ya 140 kwa dakika wakati wa kiume ni chini kidogo ya 140.
                                                       
mwisho; tafiti hizo zinaweza zisiwe asilimia mia moja kulingana na sababu mbali mbali kwa mfano mapigo ya moyo ya mtoto huweza kwenda mbio sana kama mama anaumwa au tumbo linaweza kua kubwa sana sababu ya unene wa mto binafsi lakini zimeonyesha uhalisia kwa asilimia kubwa huku kipimo cha picha ya utrasound na maji ya uzazi vikiwa vya uhakika kabisa.sijaandika makala hii ili utoe mimba kwa sababu zako binafsi. sheria inakuona.unaweza pitia na kusoma blog yangu ya kingereza hapa kwa kubonyeja haya maandishi ya kijani.                        

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                               
                                               STAY ALIVE
                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                           MAWASILIANO 0653095635/0769846183