data:post.body YAFAHAMU MADHARA HATARI KUMI YA KUVUTA SHISHA KWENYE MWILI WA BINADAMU. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

YAFAHAMU MADHARA HATARI KUMI YA KUVUTA SHISHA KWENYE MWILI WA BINADAMU.

                                                                         
                               
shisha ni nini?
shisha ni tumbaku iliyochanganywa na fleva za harufu ya kuvutia kama matunda aina mbalimbali, vannila au chocolate. shisha inavutwa kwenye aina fulani ya mtambo ambao unakua umetengenezwa kwa ajili ya hiyo kazi kama picha inavyoonesha hapo juu.
shisha inapatikana sana maeneo ya starehe nje na ndani ya nchi na imejizolea umaarufu mkubwa sana hasa kwa vijana. bahati mbaya kuna vijana wengi hutumia shisha lakini hawavuti sigara huku wakidhani shisha ni kitu kingine kabisa tofauti na sigara. lakini leo napenda kuwaambia shisha ni zaidi ya sigara na madhara yake ni makubwa zaidi ya yale ya sigara.hivi karibuni serikali ya tanzania imepiga marufuku matumizi ya shisha lakini ikapingwa na vijana wengi ambao wengi wao huvuta kwa kuiga na kutaka kuonekana wa kisasa bila kujua madhara yake kiafya.hebu leo tujifunze madhara ya shisha kama ifuatavyo.

kansa za aina mbalimbali; shisha inavutwa tofauti kidogo na sigara...yaani inavutwa mara nyingi kwa muda mfupi, huvutwa ndani zaidi ya mapafu na kwa kutumika muda mrefu yaani zaidi ya saa moja tofauti na sigara ambayo inavutwa dakika tano na kuisha.. lakini pia tofauti na sigara ambayo inasababisha kansa ya mapafu tu mara nyingi shisha inaleta kansa mbalimbali ikiwemo za figo, koo, mapafu, kibofu cha mkojo, ubongo na damu kwa wakati mmoja.shisha ina mnyanganyiko wa kemikali nzito ambazo kitaalamu zimethibitika kusababisha kansa.utafiti unaonyesha kuvuta shisha kwa saa moja ni sawasawa na kutumia sigara 100 mpaka 200.

mazoea au addiction; shisha ina tumbaku kama sigara za kawaida, ina kemikali inayoitwa kitaalamu kama nicotine ambayo mwili ukiizoea basi unaitaka mara kwa mara.ukizoea shisha hutaweza kuacha kirahisi na hata siku ukisafiri sehemu ambayo haipo basi utalazimika kuvuta sigara ili kukidhi haja ya mwili. hivyo mvuta shisha ataishia kua mvuta sigara.

kusambaza magonjwa; mara nyingi shisha inatumika na watu zaidi ya mmoja, wakati mwingine hata wasio fahamiana. kama ule mpira usipooshwa vizuri basi magonjwa kama kifua kikuu na pneumonia ya fangasi huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine lakini hata ikioshwa vizuri basi kuchangia na mgonjwa wakati huo huo huweza kuleta maambukizi.bacteria wa madonda ya tumbo kitaalamu kama helocobactor pylori huweza kuambukizwa pia.

madhara kwa mtoto wa tumboni; uvutaji wa shisha kwa mama wajawazito kama ilivyo kwenye uvutaji wa sigara husababisha madhara makubwa kwa mtoto, ikiwemo kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo sana au kuzaa mtoto asiye na baadhi ya viungo kama mikono au miguu. kitalaamu tunanita tetatorogenic effect.

magonjwa ya kinywa; mkusanyiko wa kemikali ya nicotine kwenye damu, mate, na mdomoni husababisha magonjwa ya meno na fidhi ambayo huharibu sana meno na kumfanya mtu abaki bila meno ya kutosha.

magonjwa ya moyo; shisha huharibu mishipa ya damu na kuifanya iwe myembamba sana kupitisha damu hivyo husababisha presha kupanda na shambulio la moyo kitaalamu kama heart attack...

kuharibika kwa ubongo; kemikali ya nicotine na compound zingine zinazopatikana kwenye shisha huweza kuzuia damu kufika vizuri kwenye ubongo, hali hii husababisha kiharusi..ugonjwa ambao huanza na dalili za kushindwa kuongea na kupoteza nguvu za nusu ya mwili wa binadamu.

humaliza nguvu za kiume; kemikali za kwenye shisha pia huweza kuziba damu ambayo inaenda kwenye sehemu za siri. hii huua nguvu za kiume kabisa kwa watumiaji wanaume.

ugumba; mirija inayopitisha mayai ya ya mwanamke kitaalamu kama fallopian tubes huzibwa na kemikali ya nicotine na kusababisha mbegu za mwanaume kushindwa kulifikia yai la mwanamke.

huleta makunyazi ya ngozi; mkusanyiko mkubwa wa kemikali ya nicotine kwenye ngozi, mate, damu na kila aina ya maji ya mwili humfanya mtumiaji aonekane mzee kuliko umri wake halisi kitu ambacho watu wengi hawakipendelei..

mwisho;madhara yaliyotajwa hapo juu ni baadhi tu ya madhara ambayo yamegundulika mpaka sasa na huenda kuna mengine ambayo watafiti bado hawajayagundua.usivute shisha kufufurahisha marafiki zako, usivute kwasababu umelewa, usivute kwasababu unataka kuonekana mjanja, na usivute sababu una msongo wa mawazo.kumbuka kila mvutaji ana kinga ya mwili tofauti na mwenzake na kila mtu ataingia kwenye jeneza lake mwenyewe lakini pia taifa haliko tayari kupoteza nguvu kazi ya vijana. vijana amkeni mfanye kazi..
                                          tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                                                                                      STAY ALIVE
                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                      MAWASILIANO 0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni