data:post.body Julai 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

YAFAHAMU MADHARA YA KUNYWA POMBE KIPINDI CHA UJAUZITO

                                                                 
kipindi cha ujauzito kwa mama ni kipindi muhimu sana ambacho kwa wakati huu mama hatakiwi atumie kitu chochote cha kujitibu bila ushauri wa daktari kwani kinaweza kudhuru mtoto lakini pia kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho mama hatakiwi kunywa kileo chochote kile unachokifahamu. sio bia, sio spirit, wala mvinyo au wine. wanawake wengi wa siku hizi hubeba mimba bila kufahamu kwamba wana mimba na huja kugundua baada ya mwezi mmoja au miwili baada ya kumshindilia mtoto pombe za kutosha.tabia hii ina madhara makubwa sana kwa mama na mtoto kama ifuatavyo...

mtoto kua na umbo la ajabu; mtoto huweza kuzaliwa na kichwa kidogo, uso kama bapa na macho madogo sana. dalili hizi huweza kuanza kuonekana katika umri wa miaka 2 na mara nyingi mtoto hua tofauti na wenzake.
                                                     
kuchelewa kukua; pombe huingilia mfumo wa ukuaji na kumchelewesha mtoto kufanya baadhi ya mambo kama kutambaa, kutembea, kuongea na kadhalika. ukimuangalia mtoto mwenye umri kama huo huo ataonekana mkubwa kuliko huyu anayetumia pombe.

kushindwa kujifunza; mara nyingi watoto hawa hua wabovu sana darasani na kushindwa kuelewa vitu kama watoto wengine..mata nyingi mzazi huishia kulalamika na kumshangaa mtoto na kumuona mzembe bila kujua chanzo ni yeye...

kuchelewa kula kwa mtoto; kawaida mtoto anatakiwa anywe maziwa tu kwa muda wa miezi sita, tena maziwa ya mama baada ya hapo aanze kula chakula. mtoto aliyepata madhara ya pombe hushindwa kunyonya na kuchukua muda mrefu sana kuanza kula.

matatizo ya viungo; siku hizi kuna picha zinatumwa sana mitandaoni zikionyesha mtoto kazaliwa bila mikono, miguu au kaunganikana kichwa na pacha mwenzake. hizo sio bahati mbaya kama watu wanavyodhani ila hayo ni madhara ya vitu ikiwemo pombe.

kuharibika kwa ujauzito;pombe inaweza kuingilia mfumo wa homoni za mwanamke au kufungua mlango wa uzazi na kusababisha kuharibika kwa mimba, mimba huweza kuharibika ghafla au taratibu kulingana na aina ya pombe.

kuzaa kabla ya muda; kwenye mimba kubwa pombe inaweza kusababisha kuanza kwa uchungu kabla ya muda na kumzaa mtoto ambaye hajakomaa maarufu kama kabichi.

mwisho; hakuna kipindi ambacho ni salama kunywa pombe kipindi cha ujauzito, kama hauhitaji mtoto kwa sasa tumia vizuizi vya mimba lakini kama unakunywa pombe na kufanya ngono bila kinga utajikuta una mimba ambayo imeshaathirika na pombe tayari na ukipata mimba acha pombe kabisa.


                                                           STAY ALIVE
                                     DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                      MAWASILIANO; 0653095635/0769846183






HIZI NDIO FAIDA 15 ZA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA....

                                                                       
tendo la ndoa tangu uumbaji lililengwa kati ya mwanaume na mwanamke waliofunga ndoa, sasa hivi dunia imebadilika sana kiasi kwamba tendo hili sio lazima kuliita la ndoa tena. watu wengi wamekua wakishiriki tendo la ndoa bila kujua faida zake.lakini tendo la ndoa lina faida nyingi sana kiafya na kisaikolojia. hivyo kama wewe una mke, mchumba au mpenzi halafu kila siku unampa sababu za kutoshiriki basi huenda hujui faida zake. hebu tuzisome kama ifuatavyo..

huondoa msongo wa mawazo; kipindi cha tendo la ndoa mwili hutoa hormone inayoitwa kitaalamu kama endophirn ambayo huleta furaha.kila aliyeshiriki tendo la ndoa atakua shahidi kama una msongo wa mawazo sana ukaenda kufanya tendo hili utajikuta unajisikia vizuri sana,

hupunguza presha ya damu; wakati wa tendo la ndoa damu inapita kwa kasi sana kwenye mishipa ya damu na kuondoa vikwazo kama mafuta, lehemu na kunyoosha mishipa iliyosinyaa.utafiti unaonyesha tendo la ndo hushusha presha ya chini kitaalamu kama diastolic pressure.

huongeza kinga ya mwili; askari wa mwili kwa jina immunoglubin hutolewa na mwili kupambana na magonjwa wakati wa tendo la ndoa, kama huamini basi shiriki tendo la ndoa ukiwa na mafua na baadae utashindwa kuelewa mafua yameenda wapi.

huimarisha mahusiano; kuna homoni ya furaha na uzazi inaitwa oxytocin homoni, homoni hii hutengenezwa na mwili kipind cha tendo la ndoa.kama umekaa kwenye mahuasiano muda mrefu utagundua kwamba ikitokea umegombana na mpenzi wako halafu mkafanya tendo la ndoa basi ugomvi unaisha bila hata kuongelea swala lililowagombanisha.

hupunguza uwezekano wa kupata kansa ya tezi dume; utafiti uliofanyika nchini australia uligundua kwamba wanaume wanaoshiriki tendo la ndoa angalaua mara 21 kwa mwezi wako kwenye hatari ndogo sana ya kupata kansa ya tezi dume kuliko wale wasioshiriki hivyo kama mpenzi au mke wako hakupi ushirikiano basi atakuletea kansa.

husaidia kupata hedhi kwa wakati; tendo la ndoa huweka homone za uzazi kitaalamu kama oestrogen na progesterone kwenye kiwango sawa. hii husaidia kupata siku zako kwa wakati na bila maumivu.kimsingi tendo la ndoa husaidia sana kuliko vidonge vya uzazi ambavyo humezwa na watu ambao hawaoni siku zao.

huleta usingizi wa kutosha; hii haihitaji ubishi au ushahidi mara nyingi baada ya kushiriki tendo la ndoa hata kama ni mchana kila mtu hupata uchovu fulani na kujikuta unapitiwa na usingizi kwa muda mrefu.

ni sehemu ya mazoezi;tendo la ndoa lina faida zote ambazo mtu anayefanya mazoezi anazipata ikiwemo kupungua uzito, kua na afya bora hata kuondoa kitambi kwani wakati wa tendo la ndoa mapigo ya moyo huongezeka, kasi ya upumuaji hua juu na kua sawa na mtu wa mazoezi.

hukufanya uishi muda mrefu; moja ya sababu kuu zinazofanya watu wafe mapema ni kukosa furaha ya maisha, na kua na afya ambayo sio nzuri.watu wanaoshiriki tendo la ndoa wanapata faida za kua na afya bora na furaha.

huongeza nguvu za kiume na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa; watu wengi wenye umri zaidi ya miaka 40 huanza kupungukiwa nguvu za kiume. hii ni sababu ya damu kidogo ambayo inafika kwenye uume. tendo la ndoa mara kwa mara hupeleka damu nyingi kwenye uume na kukufanya ue na uume imara na wenye nguvu.

hukufanya uonekane mdogo kiumri; tendo la ndoa mara kwa mara hukufanya mwili uwe bize kumwaga homoni mbalimbali mwilini ambazo humfanya mtu aonekane mdogo kwa miaka kumi ukilinganisha na umri wake halisi.

huimarisha afya ya moyo; tendo la ndoa huchoma mafuta ambayo ni sumu kwa moyo, mafuta mengi huweza kuziba mishipa ya moyo na kusababisha shambulio la moyo kitaalamu kama heart attack.

huongeza nguvu ya misuli ya nyonga; katika umri fulani mkubwa wanawake hupata matatizo ya kushindwa kuzuia mkojo sababu ya kuzaa mara kwa mara. kipindi cha tendo la ndoa wakati mwanamke anafika kileleni uke wake unabana sana na kufanya misuli yake ya nyonga kua na nguvu.

hupunguza maumivu; utafiti uliofanywa na madaktari bingwa wa mifupa umegundua kwamba wagonjwa wa baridi yabisi au athritis ambao wanashiriki tendo la ndoa mara kwa mara hawasumbuliwi sana na maumivu kama hao wasio shiriki.

mwisho; wanawake wengi sana walioko kwenye mahusiano au waliolewa hua ni wanakua na sababu nyingi sana za kutoshiriki tendo la ndoa. hii ni moja ya vyanzo vikuu vya wanaume kutoka nje ya ndoa kwani kitaalamu mwanume muda wote ana hamu ya kushiriki tendo la ndoa sasa unapo muwekea vikwazo basi kwenda nje ni lazima.sasa kabla hujaweka vikwazo basi kumbuka faida hizi.

                                                             STAY ALIVE
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                    MAWASILIANO 0653095635/0769846183                                                       



HIZI NDIO NJIA SITA ZA KUACHANA NA UVUTAJI WA SHISHA....

                                                               
hivi karibuni serikali ya tanzania ilipiga marufuku matumizi ya shisha nchi nzima, makala iliyopita nilizungumzia madhara makuu ya kiafya yanayosababishwa na shisha. kama hukuiona makala ile soma hii hapa YAFAHAMU MADHARA HATARI KUMI YA KUVUTA SHISHA KWEN.......moja ya madhara niliyosema ilikua ni addiction yaani kua mteja na kushindwa kuacha au kukimbilia kwenye sigara kama mbadala.kwa kulijua hilo leo nimekuja na makala ya kumsaidia mtumiaji ambaye huenda kwa sasa anahangaika kuzoea kuikosa shisha. zifuatazo ni mbinu muhimu za kuachana na shisha....

amua kutoka moyoni; huu ni wimbo wangu wa kila siku wa watu wote ambao wanatamani kuacha au kufanya kitu fulani. ili ufanikiwe katika chochote unachotaka kukifanya basi hakikisha una nidhamu na wala sio serikali inakulazimisha bali wewe mwenyewe umeona madhara yake na unataka kuacha.

jihusishe na mazoezi;ukifanya mazoezi kuna homoni inatengenezwa kitaalamu initwa endorphin, homoni hii hupunguza maumivu ya mwili na kuondoa uteja au addiction ya kitu chochote ambacho umekizoea na kushindwa kuacha lakini pia hata kama ukikosa muda wa mazoezi basi kua bize na kazi zako unazofanya kama ni za nyumbani au ofisini na zitakupa nafasi ya kusahau kuhusu shisha.

omba msaada;waambie ndugu na jamaa zako kwamba umeamua kuacha uvutaji wa shisha ili wakupe moyo, lakini pia unaweza ukaomba msaada wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa afya kwani kwa sasa kila hospitali tanzania ina mshauri mmoja au unaweza ukawasiliana na sisi ukafika ofisini kwetu hapa dar es laam kwa ushauri zaidi na kama uko mkoani unaweza ukapata ushauri kwa njia ya simu. kuna njia nyingine ya kuingia mtandaoni na kutafuta makundi kwenye mitandao ya kijamii kama forum za watu ambao wanataka kuacha uvutaji wa shisha kama wewe ili upate mawazo mengine na kupeana moyo.

ondoa vishawishi vya kuvuta shisha; usiache kwenda kwenye sherehe au starehe lakini ukiona muda wa kuvuta shisha umefika basi ondoka au toka nje upate hewa safi, epukana na marafiki wavuta shisha kwa watakushauri kufanya hivo, epuka kukaa peke yako ukiwa huna cha kufanya kwani utashawishika kwenda kuitafuta, epukana na msongo wa mawazo kwani ni kishawishi kikuu pia.

kula vizuri; kula vizuri hakukufanyi uashe shisha tu bali kunakufanya ujisikie vizuri na kuondoa sumu mwilini ambazo zimekua zikisababiswa na uvutaji wako...mfano mboga za majani kama mchicha, spinachi, matembele, majani ya maboga, kisamvu na kadhahalika....matunda kama machungwa, apple, machenza, maembe, matikiti maji na kadhalika....vyakula vya protini kama mayai, maziwa na kadhalika ambavyo vina homoni ya serotonin ambayo kitaalamu hupunguza msongo wa mawazo.

kua mvumilivu; nafahamu sio rahisi kuacha kuvuta shisha...hiyo hali unayoisikia sasa hivi ya kutojisikia vizuri ni ya muda tu na baada ya muda fulani itaisha kabisa na utarudi katika hali yako ya zamani ukiwa na afya bora na uwezo wa kua mchango mkubwa kwenye jamiii.
                         
                                      tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                       STAY ALIVE
                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO  
                                   MAWASILIANO 0653095635/0769846183



YAFAHAMU MADHARA HATARI KUMI YA KUVUTA SHISHA KWENYE MWILI WA BINADAMU.

                                                                         
                               
shisha ni nini?
shisha ni tumbaku iliyochanganywa na fleva za harufu ya kuvutia kama matunda aina mbalimbali, vannila au chocolate. shisha inavutwa kwenye aina fulani ya mtambo ambao unakua umetengenezwa kwa ajili ya hiyo kazi kama picha inavyoonesha hapo juu.
shisha inapatikana sana maeneo ya starehe nje na ndani ya nchi na imejizolea umaarufu mkubwa sana hasa kwa vijana. bahati mbaya kuna vijana wengi hutumia shisha lakini hawavuti sigara huku wakidhani shisha ni kitu kingine kabisa tofauti na sigara. lakini leo napenda kuwaambia shisha ni zaidi ya sigara na madhara yake ni makubwa zaidi ya yale ya sigara.hivi karibuni serikali ya tanzania imepiga marufuku matumizi ya shisha lakini ikapingwa na vijana wengi ambao wengi wao huvuta kwa kuiga na kutaka kuonekana wa kisasa bila kujua madhara yake kiafya.hebu leo tujifunze madhara ya shisha kama ifuatavyo.

kansa za aina mbalimbali; shisha inavutwa tofauti kidogo na sigara...yaani inavutwa mara nyingi kwa muda mfupi, huvutwa ndani zaidi ya mapafu na kwa kutumika muda mrefu yaani zaidi ya saa moja tofauti na sigara ambayo inavutwa dakika tano na kuisha.. lakini pia tofauti na sigara ambayo inasababisha kansa ya mapafu tu mara nyingi shisha inaleta kansa mbalimbali ikiwemo za figo, koo, mapafu, kibofu cha mkojo, ubongo na damu kwa wakati mmoja.shisha ina mnyanganyiko wa kemikali nzito ambazo kitaalamu zimethibitika kusababisha kansa.utafiti unaonyesha kuvuta shisha kwa saa moja ni sawasawa na kutumia sigara 100 mpaka 200.

mazoea au addiction; shisha ina tumbaku kama sigara za kawaida, ina kemikali inayoitwa kitaalamu kama nicotine ambayo mwili ukiizoea basi unaitaka mara kwa mara.ukizoea shisha hutaweza kuacha kirahisi na hata siku ukisafiri sehemu ambayo haipo basi utalazimika kuvuta sigara ili kukidhi haja ya mwili. hivyo mvuta shisha ataishia kua mvuta sigara.

kusambaza magonjwa; mara nyingi shisha inatumika na watu zaidi ya mmoja, wakati mwingine hata wasio fahamiana. kama ule mpira usipooshwa vizuri basi magonjwa kama kifua kikuu na pneumonia ya fangasi huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine lakini hata ikioshwa vizuri basi kuchangia na mgonjwa wakati huo huo huweza kuleta maambukizi.bacteria wa madonda ya tumbo kitaalamu kama helocobactor pylori huweza kuambukizwa pia.

madhara kwa mtoto wa tumboni; uvutaji wa shisha kwa mama wajawazito kama ilivyo kwenye uvutaji wa sigara husababisha madhara makubwa kwa mtoto, ikiwemo kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo sana au kuzaa mtoto asiye na baadhi ya viungo kama mikono au miguu. kitalaamu tunanita tetatorogenic effect.

magonjwa ya kinywa; mkusanyiko wa kemikali ya nicotine kwenye damu, mate, na mdomoni husababisha magonjwa ya meno na fidhi ambayo huharibu sana meno na kumfanya mtu abaki bila meno ya kutosha.

magonjwa ya moyo; shisha huharibu mishipa ya damu na kuifanya iwe myembamba sana kupitisha damu hivyo husababisha presha kupanda na shambulio la moyo kitaalamu kama heart attack...

kuharibika kwa ubongo; kemikali ya nicotine na compound zingine zinazopatikana kwenye shisha huweza kuzuia damu kufika vizuri kwenye ubongo, hali hii husababisha kiharusi..ugonjwa ambao huanza na dalili za kushindwa kuongea na kupoteza nguvu za nusu ya mwili wa binadamu.

humaliza nguvu za kiume; kemikali za kwenye shisha pia huweza kuziba damu ambayo inaenda kwenye sehemu za siri. hii huua nguvu za kiume kabisa kwa watumiaji wanaume.

ugumba; mirija inayopitisha mayai ya ya mwanamke kitaalamu kama fallopian tubes huzibwa na kemikali ya nicotine na kusababisha mbegu za mwanaume kushindwa kulifikia yai la mwanamke.

huleta makunyazi ya ngozi; mkusanyiko mkubwa wa kemikali ya nicotine kwenye ngozi, mate, damu na kila aina ya maji ya mwili humfanya mtumiaji aonekane mzee kuliko umri wake halisi kitu ambacho watu wengi hawakipendelei..

mwisho;madhara yaliyotajwa hapo juu ni baadhi tu ya madhara ambayo yamegundulika mpaka sasa na huenda kuna mengine ambayo watafiti bado hawajayagundua.usivute shisha kufufurahisha marafiki zako, usivute kwasababu umelewa, usivute kwasababu unataka kuonekana mjanja, na usivute sababu una msongo wa mawazo.kumbuka kila mvutaji ana kinga ya mwili tofauti na mwenzake na kila mtu ataingia kwenye jeneza lake mwenyewe lakini pia taifa haliko tayari kupoteza nguvu kazi ya vijana. vijana amkeni mfanye kazi..
                                          tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                                                                                      STAY ALIVE
                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                      MAWASILIANO 0653095635/0769846183





ZIFAHAMU FAIDA 10 ZA POMBE KWENYE MWILI WA BINADAMU....

pombe ni nini?
pombe ni neno ambalo linajumuisha aina zote za vilevi unazozifahamu, pombe za aina mbalimbali zinatengenezwa na kutumika na jamii zote duniani japokua kuna baadhi ya dini haziruhusu pombe. historia ya pombe inaonekana kwanzia zamani sana, kibiblia hata kabla ya kuzaliwa kwa yesu. sasa pombe ina hasara nyingi ambazo kila mtu anazifahamu ikinywea kwa kiasi kikubwa lakini kuna faida zake muhimu iwapo zikinywewa kwa kiasi kinachotakiwa.

kiwango sahihi cha pombe ni kipi kiafya? 
kitaalamu mwanaume mmoja anatakiwa anywe vinywaji viwili vya pombe wakati mwanamke anatakiwa anywe kinywaji kimoja cha pombe. sasa tunaposema kinywaji hatumaanishi chupa pombe ila tunamaanisha kiasi cha pombe na asilimia zake ndani.
kinywaji kimoja ni tunachozungumzia ni kama ifuatavyo...

  • milimita 354 za bia ya kawaida yenye 5% ndio kinywaji kimoja.
  • milimita 147 za wine au mvinyo yenye 12% ndio kinywaji kimoja.
  • milimita 44 za pombe kali kama viroba zenye 40% ndio kinywaji kimoja.
mfano hai tunaweza tukasema mwanaume anatakiwa anywe bia mbili tu kwa siku huku mwanamke anatakiwa anywe moja kama hizo kwa siku..

  • mwanaume anatakiwa kunywa nusu glass ya wine wakati mwanamke anatakiwa anywe robo glass ya  wine kwa siku.
  • mwanaume anatakiwa anywe robo glass ya pombe kali wakati mwanamke anatakiwa anywe theluthi ya pombe kali kwa siku.
  • sasa baada ya kuona kiwango maalumu cha kiafya ambacho mtu anatakiwa kunywa basi hebu tuone faida za kunywa kiasi hicho...
pombe hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo; utafiti ulofanywa na chuo kikuu cha marekani kwa jina la havard umebaini kwamba unywaji wa pombe kwa kiasi huongeza aina fulani ya lehemu nzuri inayoitwa high density lipopoprotein, lehemu hii hulinda moyo lakini pia pombe hulainisha damu na kuifanya iwe nyepesi hivyo kupita kirahisi kwenye mishipa ya damu na kuzuia presha na kiharusi. lakini pia katika hatua fulani ya ugonjwa wa moyo, mgonjwa huandikiwa kutumia pombe aina ya red wine angalau robo au nusu glass kwa siku.

huongeza urefu wa maisha; chuo kikuu cha catholic nchini marekani katika moja ya tafiti zake kiligundua kunywa pombe kiasi huongeza urefu wa maisha kwa asilimia 18 kuliko wale wasiokunywa, pia wakaongeza kwamba kunywa pombe na chakula ni moja ya njia nzuri sana ya kupata faida hii muhimu.

husaidia nguvu za kiume; jarida la jounal of sexual medicine liliandika kwamba wanaume wanaotumia pombe walipungukiwa na tatizo la nguvu za kiume kwa 25% kuliko wasiokunywa...lakini pia watu wanaokunywa pombe ni mashaihidi wa hili kwamba hata muda ule ukiwa umekunywa pombe, hamu inakua juu sana na ukipata mwanamke unafanya vizuri zaidi kuliko ukiwa hujanywa hii ikiwemo pamoja na kuchelewa sana kufika kileleni na kua na uume wenye nguvu sana kuliko kawaida..

hupunguza hatari ya kupata kisukari; unywaji wa pombe kwa kiasi huongeza uwezo wa homoni ya insulini kufanya kazi na hii hupunguza hatari ya kupata ugonjwa hatari wa kisukari, habari hii ilitolewa na kituo cha utafiti huko uholanzi..

hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa akili; utafiti uliofanyika kwa watu 365000 tangu mwaka 1977 na shirika la kimarekani, lligundua kwamba wanywaji wa pombe kwa kiasi kidogo kwa siku hawakuugua magonjwa ya akili uzeeni kwa asilimia 23 ukilinganisha na wale wasiokunywa kabisa.

huzuia hatari ya kupata mawe ya nyongo; ugonjwa huu unaitwa kitaalamu kama gallstones, watafiti katika chuo kikuu cha east ganglia walionyesha kwamba wanywaji wa pombe kidogo hawasumbuliwi na sana na ugonjwa huu kama wasiokunywa kabisa.

pombe ina madini muhimu ya mwili; bia nyingi zina vitamin b nyingi yaani thiamine na riboflavin, lakini pia zina calcium na magnesium nyingi ambayo ni muhimu sana kwa jili ya kazi mbalimbali za mfumo wa mwili wa binadamu.

pombe ni nzuri kwa wanawake zaidi ya miaka 50; baada ya umri wa miaka 50 mwanamke huanza kupata dalili za kupungua kiasi cha homone mwilini kitaalamu kama monopause, utafiti unaonyesha kwamba kemikali ndani ya bia zinaweza fanya kazi ya kuondoa dalili za homoni kidogo mwilini kama joto, mgandamizo wa mawazo na kadhalika.

huongeza kumbukumbu; kama wewe ni mnywaji, mara nyingi ukinywa unaanza kukumbuka mambo ya zamani sana na wakati mwingine kufadhaishwa au kufurahishwa na habari hizo. vivo hivyo ndio uwezo wa kumbukumbu zingine muhimu za kazi na kusoma zinavyoongezeka..

husaidia figo; jarida moja la kimarekani kwa jina la clinical journal of american society liliandika kwamba wanywaji wa pombe kiasi wanapungukiwa hatari ya kupata mawe ya figo kwa asilimia 30 kuliko wale ambao hawanywi, hii ni sababu ya kukojoa sana na kusafisha mafigo..

mwisho; faida hizi hupatikana kwa wale wanaokunywa kama nilivyoelekeza hapo juu, lakini unywaji wa kupitiliza una madhara makubwa sana kiafya..kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                               STAY ALIVE
                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183