data:post.body HIZI NDIO FAIDA KUMI ZA KIAFYA ZA KUFUNGA KULA ZITAKAZO KUSHANGAZA.. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO FAIDA KUMI ZA KIAFYA ZA KUFUNGA KULA ZITAKAZO KUSHANGAZA..

                                 
 kufunga ni nini?                           
hii ni hali ya kuacha kula na kunywa kwa masaa kadhaa, kwanzia masaa 12 mpaka 24 bila kula chochote kabisa.mara nyingi kidini watu wanafunga mwezi mzima mfululizo au siku 40 mfululizo huku wakila usiku tu lakini kuna njia nyingine ya kufunga ambayo watu wanafunga kwa kuruka ruka, yaani ukifunga leo, kesho haufungi.
watu wengi hufikiri watu wanaofunga kula wanapata faida za kidini tu, au wanafunga kwa sababu za kidini tu. hicho sio kweli kabisa kwani kufunga kula kuna faida nyingi sana kiafya. kama wewe unataka kufunga ili ufaidike zaidi, baada ya fungo za kidini basi anza kufunga kwa kuruka siku moja moja amgalau mara mbili au mara tatu kwa wiki, unaweza kutokula kabisa au ukanywa maji tu. lakini kwa ujumla watu wanaofunga mfulululizo au kurukaruka wanapata faida zifuatazo...

kufunga hupungua uzito; mwili hutumia wanga kama chanzo kikuu cha nguvu mwilini, pale unapufunga mwili unakosa wanga wa kutosha na hivyo mwili huanza kuchoma mafuta ya mwili ili kutengeneza nguvu. hii ina faida sana kwani huweza kutoa uzito na kitambi ambacho mara nyingi ndio chanzo kikuu cha magonjwa yasiyioambukizwa kama kisukari na magonjwa ya moyo.kumbuka ukifunga ikifika jioni kula mlo uleule unaokula siku ambazo haufungi, ukila zaidi kulipa kisasi haitakusaidia.

kufunga huongeza kinga ya mwili; mwili unapochukua chakula tumboni na kukimeng'enya kupata nguvu basi kuna mzunguko maalumu unatumika na mwisho kuna vitu vinaitwa free radicals ambavyo hutolewa kama mabaki.vitu hivi huweza kushambulia mwili na kuleta magonjwa.unapofunga hali hii hupungua kasi.

kufunga hulinda ubongo; unapofunga mwili hutengeneza homoni moja kitaalamu kama brain derived neutrophic factor ambayo huulinda afya ya ubongo pamoja na magonjwa ambayo hubadili muuonekano wa ubongo mfano parkiston disease.

kufunga huondoa harara na chunusi za ngozi; kufunga huondoa sumu mwilini na kusafisha viungo muhimu vya mwili kama ngozi,maini, figo na mfumo wa chakula. kipindi hiki magonjwa yote yasababishwayo na sumu huondoka na pia chunusi na mapele yatokanayo na mafuta ya mwili husafishwa,

kufunga husaidia tabia kubadilisha yako ya kula; waafrika wengi tuna tabia ya kula milo mikubwa mitatu kwa siku ambayo kiafya haitakiwi, tunatakiwa tule milo midogo hata minne au mitano kwa siku.sasa ulaji huu mkubwa husababisha unene. sasa ukainza kula mara moja kwa siku unapunguza kiasi cha chakula na tumbo hua na tabia ya kujikunja na kua dogo kama likila kidogo kwa muda mrefu kitu ambacho kitakufanya uzoee kula kidogo.

kufunga hupunguza hatari ya kupata kisukari; ulaji wa kila siku huichosha kongosho ambayo kazi yake ni kuvunja sukari mwilini. sasa kufunga huipumzisha kongosho na kuifanya ifanye kazi nzuri zaidi siku ukila tena.

kufunga huongeza uwezo wa tumbo kumen'genya chakula; unapofunga unalipumzisha tumbo ambalo limekua likifanya kazi kila siku tangu ulipozaliwa.tumbo hupata muda wa kujiandaa na chakula kingine unapofunga.hebu fikiri nyama tu hukaa masaa 20 tumboni. je wewe umekuala nyama mara ngapi? hii hupelekea kansa za utumbo mkubwa.

kufunga hufanya mtu aweze kuishi muda mrefu; utafiti unaonyesha tabia ya ulaji wa nchi za mashariki kama japan ambazo huambatana na kufunga watu huishi miaka mingi kuliko nchi za magharibi kama marekani ambako watu hula kila siku na kunenepa sana.

kufunga huongeza uwezo wa akili kufanya kazi; kikawaida binadamu hua na uwezo mkubwa sana tumbo likiwa wazi kuliko akiwa amekuala...hebu fikiria kama umeshawahi kua mwanafunzi.vipindi vyote vya asubuhi watu hua makini sana lakini wakishakula mchana wote huanza kusinzia.wagunduzi wengi wakisayansi waligundua usiku sana wakiwa bila kitu tumboni.

kufunga hufanya mtu achelewe kuzeeka; mara nyingi uzee husababishwa na mwili kuanza kuchoka hasa upande wa umeng'enyaji wa chakula. na siku zote watu wanaokula sana hunenepa na kuanza kuonekana wazee tangu wakiwa wadogo. lakini ufungaji wa kula husaidia kua mwembamba na kuonekana kijana siku zote.

mwisho; nawatakia afya njema na mfungo mwema waislamu wote duniani katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani.

                                                      STAY ALIVE
                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183
                                             









0 maoni:

Chapisha Maoni