data:post.body Juni 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIO FAIDA KUMI ZA KIAFYA ZA KUFUNGA KULA.

                                                              

kufunga kula ni nini?                                      
hii ni hali ya kuacha kula na kunywa kwa masaa kadhaa, kwanzia masaa 12 mpaka 24 bila kula chochote kabisa.mara nyingi kidini watu wanafunga mwezi mzima mfululizo au siku 40 mfululizo huku wakila usiku tu lakini kuna njia nyingine ya kufunga ambayo watu wanafunga kwa kuruka ruka, yaani ukifunga leo, kesho haufungi.
watu wengi hufikiri watu wanaofunga kula wanapata faida za kidini tu, au wanafunga kwa sababu za kidini tu. hicho sio kweli kabisa kwani kufunga kula kuna faida nyingi sana kiafya..  kwa ujumla watu wanaofunga mfulululizo au kurukaruka wanapata faida zifuatazo...

kufunga hupungua uzito; mwili hutumia wanga kama chanzo kikuu cha nguvu mwilini, pale unapufunga mwili unakosa wanga wa kutosha na hivyo mwili huanza kuchoma mafuta ya mwili ili kutengeneza nguvu. hii ina faida sana kwani huweza kutoa uzito na kitambi ambacho mara nyingi ndio chanzo kikuu cha magonjwa yasiyioambukizwa kama kisukari na magonjwa ya moyo.kumbuka ukifunga ikifika jioni kula mlo uleule unaokula siku ambazo haufungi, ukila zaidi kulipa kisasi haitakusaidia.

kufunga huongeza kinga ya mwili; mwili unapochukua chakula tumboni na kukimeng'enya kupata nguvu basi kuna mzunguko maalumu unatumika na mwisho kuna vitu vinaitwa free radicals ambavyo hutolewa kama mabaki.vitu hivi huweza kushambulia mwili na kuleta magonjwa kama kansa na magonjwa ya moyo.unapofunga hali hii hupungua kasi.

kufunga hulinda ubongo; unapofunga mwili hutengeneza homoni moja kitaalamu kama brain derived neutrophic factor ambayo huulinda afya ya ubongo pamoja na magonjwa ambayo hubadili muuonekano wa ubongo mfano parkinston disease.

kufunga huondoa harara na chunusi za ngozi; kufunga huondoa sumu mwilini na kusafisha viungo muhimu vya mwili kama ngozi,maini, figo na mfumo wa chakula. kipindi hiki magonjwa yote yasababishwayo na sumu huondoka na pia chunusi na mapele yatokanayo na mafuta ya mwili husafishwa,

kufunga husaidia tabia kubadilisha tabia yako ya kula; waafrika wengi tuna tabia ya kula milo mikubwa mitatu kwa siku ambayo kiafya haitakiwi, tunatakiwa tule milo midogo hata minne au mitano kwa siku.sasa ulaji huu mkubwa husababisha unene. sasa ukainza kula mara moja kwa siku unapunguza kiasi cha chakula na tumbo hua na tabia ya kujikunja na kua dogo kama likila kidogo kwa muda mrefu kitu ambacho kitakufanya uzoee kula kidogo.

kufunga hupunguza hatari ya kupata kisukari; ulaji wa kila siku huichosha kongosho ambayo kazi yake ni kuvunja sukari mwilini. sasa kufunga huipumzisha kongosho na kuifanya ifanye kazi nzuri zaidi siku ukila tena.

kufunga huongeza uwezo wa tumbo kumen'genya chakula; unapofunga unalipumzisha tumbo ambalo limekua likifanya kazi kila siku tangu ulipozaliwa.tumbo hupata muda wa kujiandaa na chakula kingine unapofunga.hebu fikiri nyama tu hukaa masaa 20 tumboni. je wewe umekuala nyama mara ngapi? hii hupelekea kansa za utumbo mkubwa.

kufunga hufanya mtu aweze kuishi muda mrefu; utafiti unaonyesha tabia ya ulaji wa nchi za mashariki kama japan ambazo huambatana na kufunga watu huishi miaka mingi kuliko nchi za magharibi kama marekani ambako watu hula kila siku na kunenepa sana.

kufunga huongeza uwezo wa akili kufanya kazi; kikawaida binadamu hua na uwezo mkubwa sana tumbo likiwa wazi kuliko akiwa amekuala...hebu fikiria kama umeshawahi kua mwanafunzi.vipindi vyote vya asubuhi watu hua makini sana lakini wakishakula mchana wote huanza kusinzia.wagunduzi wengi wakisayansi waligundua usiku sana wakiwa bila kitu tumboni.

kufunga hufanya mtu achelewe kuzeeka; mara nyingi uzee husababishwa na mwili kuanza kuchoka hasa upande wa umeng'enyaji wa chakula. na siku zote watu wanaokula sana hunenepa na kuanza kuonekana wazee tangu wakiwa wadogo. lakini ufungaji wa kula husaidia kua mwembamba na kuonekana kijana siku zote.

                                                      STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183
                                             

HIZI NDIO FAIDA KUMI ZA KIAFYA ZA KUFUNGA KULA ZITAKAZO KUSHANGAZA..

                                 
 kufunga ni nini?                           
hii ni hali ya kuacha kula na kunywa kwa masaa kadhaa, kwanzia masaa 12 mpaka 24 bila kula chochote kabisa.mara nyingi kidini watu wanafunga mwezi mzima mfululizo au siku 40 mfululizo huku wakila usiku tu lakini kuna njia nyingine ya kufunga ambayo watu wanafunga kwa kuruka ruka, yaani ukifunga leo, kesho haufungi.
watu wengi hufikiri watu wanaofunga kula wanapata faida za kidini tu, au wanafunga kwa sababu za kidini tu. hicho sio kweli kabisa kwani kufunga kula kuna faida nyingi sana kiafya. kama wewe unataka kufunga ili ufaidike zaidi, baada ya fungo za kidini basi anza kufunga kwa kuruka siku moja moja amgalau mara mbili au mara tatu kwa wiki, unaweza kutokula kabisa au ukanywa maji tu. lakini kwa ujumla watu wanaofunga mfulululizo au kurukaruka wanapata faida zifuatazo...

kufunga hupungua uzito; mwili hutumia wanga kama chanzo kikuu cha nguvu mwilini, pale unapufunga mwili unakosa wanga wa kutosha na hivyo mwili huanza kuchoma mafuta ya mwili ili kutengeneza nguvu. hii ina faida sana kwani huweza kutoa uzito na kitambi ambacho mara nyingi ndio chanzo kikuu cha magonjwa yasiyioambukizwa kama kisukari na magonjwa ya moyo.kumbuka ukifunga ikifika jioni kula mlo uleule unaokula siku ambazo haufungi, ukila zaidi kulipa kisasi haitakusaidia.

kufunga huongeza kinga ya mwili; mwili unapochukua chakula tumboni na kukimeng'enya kupata nguvu basi kuna mzunguko maalumu unatumika na mwisho kuna vitu vinaitwa free radicals ambavyo hutolewa kama mabaki.vitu hivi huweza kushambulia mwili na kuleta magonjwa.unapofunga hali hii hupungua kasi.

kufunga hulinda ubongo; unapofunga mwili hutengeneza homoni moja kitaalamu kama brain derived neutrophic factor ambayo huulinda afya ya ubongo pamoja na magonjwa ambayo hubadili muuonekano wa ubongo mfano parkiston disease.

kufunga huondoa harara na chunusi za ngozi; kufunga huondoa sumu mwilini na kusafisha viungo muhimu vya mwili kama ngozi,maini, figo na mfumo wa chakula. kipindi hiki magonjwa yote yasababishwayo na sumu huondoka na pia chunusi na mapele yatokanayo na mafuta ya mwili husafishwa,

kufunga husaidia tabia kubadilisha yako ya kula; waafrika wengi tuna tabia ya kula milo mikubwa mitatu kwa siku ambayo kiafya haitakiwi, tunatakiwa tule milo midogo hata minne au mitano kwa siku.sasa ulaji huu mkubwa husababisha unene. sasa ukainza kula mara moja kwa siku unapunguza kiasi cha chakula na tumbo hua na tabia ya kujikunja na kua dogo kama likila kidogo kwa muda mrefu kitu ambacho kitakufanya uzoee kula kidogo.

kufunga hupunguza hatari ya kupata kisukari; ulaji wa kila siku huichosha kongosho ambayo kazi yake ni kuvunja sukari mwilini. sasa kufunga huipumzisha kongosho na kuifanya ifanye kazi nzuri zaidi siku ukila tena.

kufunga huongeza uwezo wa tumbo kumen'genya chakula; unapofunga unalipumzisha tumbo ambalo limekua likifanya kazi kila siku tangu ulipozaliwa.tumbo hupata muda wa kujiandaa na chakula kingine unapofunga.hebu fikiri nyama tu hukaa masaa 20 tumboni. je wewe umekuala nyama mara ngapi? hii hupelekea kansa za utumbo mkubwa.

kufunga hufanya mtu aweze kuishi muda mrefu; utafiti unaonyesha tabia ya ulaji wa nchi za mashariki kama japan ambazo huambatana na kufunga watu huishi miaka mingi kuliko nchi za magharibi kama marekani ambako watu hula kila siku na kunenepa sana.

kufunga huongeza uwezo wa akili kufanya kazi; kikawaida binadamu hua na uwezo mkubwa sana tumbo likiwa wazi kuliko akiwa amekuala...hebu fikiria kama umeshawahi kua mwanafunzi.vipindi vyote vya asubuhi watu hua makini sana lakini wakishakula mchana wote huanza kusinzia.wagunduzi wengi wakisayansi waligundua usiku sana wakiwa bila kitu tumboni.

kufunga hufanya mtu achelewe kuzeeka; mara nyingi uzee husababishwa na mwili kuanza kuchoka hasa upande wa umeng'enyaji wa chakula. na siku zote watu wanaokula sana hunenepa na kuanza kuonekana wazee tangu wakiwa wadogo. lakini ufungaji wa kula husaidia kua mwembamba na kuonekana kijana siku zote.

mwisho; nawatakia afya njema na mfungo mwema waislamu wote duniani katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani.

                                                      STAY ALIVE
                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183
                                             

FAHAMU JINSI YA KUKABILIANA NA MAUMIVU YA KIFO CHA MPENDWA WAKO....

                                                                 
kifo ni hali ya kawaida katika safari ya mwanadamu hapa duniani, tangu dunia imeanza mabilioni ya watu wameshafukiwa kwenye hii ardhi yetu. kimsingi kila baaada ya miaka 100 kizazi kinabadilika kwa maana nyingine baada ya miaka 100 kwanzia leo sisi wote tutakua wafu na kutakua kuna watu wapya kabisa.pamoja na historia fupi hiyo ya kifo bado hakuna mwanadamu ambaye amekizoea kifo kwani kila anayekufa kibinadamu hatutamuona tena. huu ni ukweli mchungu ambao mpaka leo hii binadamu tumeshindwa kuumeza.hata kama kuna maisha baada ya haya kama vitabu vitakatifu vinavyosema bado uwezekano wa kuonana ni mdogo kutokana na masharti magumu ya kuona pepo kama inavyosemwa.hivyo kama wewe ni mzima leo una wazazi na wote wawili lazima ujue ipo siku watafariki na itabidi ukabaliane na ukweli.
kumpoteza mpendwa wako huambatana na maumivu makali sana ambayo hayaponi kirahisi na kwasababu kila binadamu yuko tofauti basi pengo lake haliwezi kuzibika kabisa.kuna watu walichanganyikiwa, kuugua hata kujiua baada ya kuwapoteza ndugu zao. hatuwezi kuwalaumu lakini kila mtu ana njia yake ya kupokea habari mbaya.leo hii naenda kuzungumzia mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kuendelea na maisha yako baada ya kifo cha mpendwa wako.

ziachie hisia zako; usijibane kulia, unyesha hisia zako zote kipindi cha msiba  na baada ya msiba, kwani kulia sana hupunguza uchungu moyoni.kwa hiyo kama una maneneo ya kuomboleza au una uchungu mwingi..ongea maneneo hayo na ulie kadri uwezavyo.kumbuka kwamba hisia ni zako na sio kosa kuzionyesha.

acha hatua za maombolezo zipite;mwandishi elizabeth kubler kwenye kitabu chake cha ''on death and dying'' alielezea hatua tano za majonzi ambazo kila mtu anazipitia baada ya kifo cha mpendwa wake kama ifuatavyo.

  • denial/kukataa; hii ni hatua ya kwanza kabisa ambapo ukipewa habari hizo hautaamini kabisa na utabaki na ganzi ya muda fulani ukihisi labda ni utani au wamekosea kutoa habari.
  • anger/hasira; baada ya muda utagundua ni kweli, utapata hasira sana na kuanza kulaumu watu unaohisi wamehusika. labda kumlaumu dokta kwa kushindwa kumtibu mgonjwa wako, kumlaumu marehemu kwa kukuacha hata kumlaumu mungu.
  • bargaining/kubembeleza; katika hatua hii mtu huanza kuongea na mungu au nguvu za giza labda kwenye maombi au kuongea mwenyewe akiomba ikiwezekana huyo mtu arudishiwe uhai. watu wengine wamefikia mpaka kwenda kwa waganga wa kienyeji wakiamini wafu wao wamerogwa.
  • mgandamizo wa mawazo; hichi kipindi cha msongo mkubwa wa mawazo ambapo mfiwa anakua ametulia sana huku akihisi maumivu makali sana moyoni mwake na mfiwa asipoangaliwa kipindi hiki anaweza kujiua pia.
  • acceptance; hii hali ya mwisho kabisa ya hatua hizi ambapo mtu hukubali ukweli kwamba nimeshampoteza mtu na maisha huanza kuendelea kama kawaida, ni hatua ambayo inapatikana baada ya muda kadhaa kulingana na majonzi ya mtu.
omba msaada; usikae peke yako, ongea na ndugu jamaa na marafiki na wao watakupa moyo sana kulingana na uzoefu wao kwenye swala hilo pia unaweza ukamuona mtaalamu wa ushauri akausaidia jinsi ya kuendelea na maisha yako.

kaa mbali na kumbukumbu za marehemu kwa muda; kama ulikua karibu sana na marehemu kama mke, mume au mtoto basi kusanya vitu vyake vyote uweke sehemu moja usivione kwa kipindi hiki kigumu lakini pia unaweza ukachukua likizo ukasafiri kidogo kwenda maeneo mapya ambayo hukuwahi kwenda na mtu huyo na kama ulikua unaishi naye kwenye nyumba fulani ya kupanga basi unaweza kuhama kabisa eneo hilo kupoteza kumbukumbu.

jipe muda; mambo yote niliyoyataja hapo juu hata ukiyafanya kwa siku mbili bado maumivu makali yatakuepo, unatakiwa kujua kwamba maumivu haya yanataka muda... wazungu wanasema time heals everything. kuna watu kama wewe ambao wameshapoteza watu muhimu sana kama wewe lakini baada ya muda fulani walizoea.
                                               

mwisho; maisha na zawadi kutoka kwa mungu, tumia muda mwingi kuwaonyesha upendo watu wote unaowapenda na usiowapenda kwani siku za kuishi ni chache sana kuliko unavyofikiri na baada ya kifo familia  na rafiki watakumbuka upendo na muda uliotumia ukiwa nao kuliko pesa ambazo unatumia muda mwingi kuzitafuta..

                                                    STAY ALIVE

                           DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                         0653095635/0769846183


HIZI NDIO AINA KUMI ZA DAWA AMBAZO HAZIPATANI NA POMBE KABISA.....

                                                       
       
kumekua na kesi mbalimbali za vifo sababu ya watu kumeza dawa kisha kujisahau na kunywa pombe.hii ni changamoto kubwa sana kwenye sekta ya afya..kawaida dawa yeyote anayopewa binadamu kutibu kitu fulani ni sumu na ikichanganywa na baadhi ya kemikali kama pombe huweza kudhuru na kuua kabisa hivyo leo naenda kuzungumzia dawa kadhaa amabazo ukiona umezimeza usiguse pombe kabisa.
dawa za kutibu bacteria[antibiotics]; hizi ni dawa ambazo hutumika mara kwa mara kwenye jamii kutibu magonjwa mbalimbali kama vidonda, kikohozi, kifua kikuu, madonda ya tumbo na kadhalika.matumizi ya dawa hizi na pombe huweza kuua. mfano fragile. isoniazid,grisiofulvin. lakini pia  na baadhi ya dawa za malaria kama quinine na dawa za ya mseto ya malaria ni hatari zikitumika na pombe.

dawa za kuzuia damu kuganda[ant cougulant]; kuna dawa amabazo hupewa kwa wajawazito mara nyingi kulainisha damu ili isigande....sasa matumizi ya pombe hufanya dawa hizi kushindwa kufanya kazi na kusabisha damu kuganda hivyo kuziba mishipa ya damu ana kuleta kifo..mfano warfin

dawa ya kupunguza mgandamizo wa mawazo[ant depressant]; pombe huingilia kazi ya dawa izi na kufanya dawa hizo ziongezeke kwenye damu kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyopangwa. hii humfanya mgonjwa alegee sana mfano amitriptyline.

dawa za kutibu kisukari[ant diabetic]; dawa za kisukari hutengenezwa kwa ajili ya kushusha kiasi kikubwa cha sukari mwilini, sasa matumizi ya dawa hizi na pombe husababisha hali moja kitaalamu kama lactic acidosis... dalili ya hali hii ni maumivu ya misuli,tumbo kuuma na kusikia usingizi.hali hii isipodhibitiwa hospitali huua.mfano metformin vidonge.

dawa za mafua na aleji;[ant histamine]hizi dawa hutolewa kutibu mafua, miwasho ya ngozi na kikohozi lakini dawa hizi pia husababisha usingizi na uchovu kila zikitumika.pombe huongeza uzingizi huu na uchovu mara duvu na kufanya mtu ashindwe kazi. mfano promethazine maarufu kama fenigani  na chlropherinamine maleate maarufu kama piriton.

dawa za magonjwa ya akili; dawa za akili kama chlopromazine hutolewa kwa wagonjwa wa akili kupunguza dalili a magonjwa haya kwa kuwapa usingizi...sasa matumizi ya pombe huongeza usingizi huu maradufu na kuwafanya washindwe kupumua hivyo huweza kuleta kifo.

dawa za kutibu madonda ya tumbo; mara nyingi madonda hutibiwi na mchahnganyiko wa dawa tatu kitaalamu kama triple therapy, sasa moja ya mchanganyiko huo kama cimetidine, metronidazole,scenidazole au tinidazole hazitakiwi kuchanganywa na pombe kabisa sababu ya madhara ambayo zimeonyesha.

dawa za moyo; hichi ni kikundi kikubwa cha dawa ambacho hutumika kutibu matatizo ya moyo. matumizi ya dawa hizi wakati mwingine huingilia mfumo wa kazi wa mwili na kusababisha kizunguzungu na kuanguka wakati wa kusimama mfano methyldopa, hydralazine na isosorbine mononitrate na dinitrate lakini pia matumizi ya pombe hupunguza uwezo wa dawa ya presha kitaalamu kama propanalol na kuzuia uwezo wake wa kufanya kazi.

dawa za maumivu makali;kuna dawa za maumivu kali sana ambazo hutolewa kwa wagonjwa wenye maumivu makali kama ya kansa, uzazi na maumivu ya ajali. pombe huongeza wingi wa dawa hizi kwenye mfumo wa damu na kusababisha overdose yaani dawa kua nyingi mwilini pale inapomezwa na pombe hata kama ulimeza dozo sahihi.mfano morphine,pethidine, codeine,meperidine...hali hii huleta kifo mara nyingi kwani wasanii wakubwa kama michael jackson na prince waliuawa na hali hizi.

dawa za usingizi; dawa za usingizi kama valium hutumika kwa wagonjwa wenye kushindwa kupata usingizi na wakati mwingine kwenye chumba cha upasuaji. dawa hizi huleta usingizi mkali...matumizi ya dawa hizi na pombe huongeza usingizi huu, hupunguza mapigo ya moyo, hupunguza uwezo wa kupumua, kupoteza fahamu na kifo lakini pia dawa za kifafa kama phenytoin  hupunguzwa uwezo wake na pombe na kushindwa kuzuia uwezo wake wa kuzuia degedege za kifafa.

mwisho;kutaja dawa hizi haimaanishi kwamba dawa zote ambazo sijataja hapa zinafaa kunywa na pombe, hapana..kuna dawa bado zinafanyiwa utafiti kama zina madhara zikitumika na pombe lakini pia ni vizuri kujenga tabia ya kutokunywa pombe kabisa kama uko kwenye dozi ya ugonjwa wowote na hata kama una ugonjwa ambao unataka kumeza vidonge maisha yote kama kisukari, presha, ukimwi, kifafa na kadhalika basi ni vizuri ukaacha pombe kabisa.

                                                      STAY ALIVE
                              DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                             MAWASILIANO 0653095635/0769846183[tuma meseji tafadhari]

      angalizo; kwanzia sasa, ushauri  kutoka kwa daktari wa matatizo binafsi kwa njia ya simu utatozwa shilingi 5000, ushauri kwa kufika ofisini kwetu gongo la mboto dar es laam utatozwa shilingi 10000.karibuni sana...
                                   
                                                 

HIZI NDIO NJIA KUMI BORA ZA KUPATA SIX PACKS ZA TUMBONI.

                                                                     
wanaume wengi na wananawake wachache hutamani kupata six packs tumboni katika kipindi fulani cha maisha yao lakini sio rahisi kupata six packs kwani inahitaji nidhamu ya hali ya juu. maana kwamba ukizipata leo sio rahisi na kuzitunza. lakini pia swala la six packs sio mazoezi tu ila kuna mambo mengine ambayo unatakiwa kuzingatia ambayo wafanya mazoezi wengi hawafahamu na hawajui. kitaalamu misuli ya six packs inaitwa rectus abnominis ambayo hukaa chini ya mafuta ya tumbo hivyo ili kupata six packs lazima mafuta hayo uhakikishe unayaondoa kwanza..sasa leo ntaenda kuzungumzia njia hizo muhimu.

kula vizuri; neno kula vizuri ni pana sana yaani linahusisha ulaji wa chakula angalau mara nne mpaka tano kwa siku kwa kaisi kidogo na sio kula milo mizito mitatu kama ilivyozoeleka ili kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta[metabolism].pia  kula vyakula jamii ya protini amabavyo hujenga misuli mfano nyama, samaki, mayai, maziwa, karanga, dagaa na etc na sio kula wanga mwingi ambao kimsingi huleta mafuta mwilini kama ugali, viazi, mihogo, wali, maandazi, chapati, keki na jamii zote za vyakula hivi.sio kwamba usile kabisa wanga ila kula kwa kiasi kidogo sana.sahani hapo chini ni mfano wa kiasi cha kula kwa sahani moja yaani mboga na matunda mengi na wali au ugali kidogo.

                                                             
kunywa maji mengi; angalau lita tatu kwa siku kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta na kuondoa sumu nyingi mwilini.lakini pia kunywa maji hayo kabla ya kula mlo wowote angalau nusu lita au lita kabla ya kula ili kujaza tumbo kwanza ili usishawishike kula chakula kingi.

                                                                 
pata usingizi wa kutosha; tafiti zinaonyesha watu wanaolala muda mfupi sana husumbua mfumo wao wa homoni kufanya kazi na matokeo yake watu hawa hujikuta wanakula sana kuliko kawaida na hii huongeza mafuta na kitambi.
                                                           
epuka msongo wa mawazo; katika maisha ya kawaida msongo wa mawazo ni kawaida lakini kuna njia mbalimbali za kupambana na msongo wa mawazo hasa kwa kutatua chanzo husika cha msongo huo. kwani msongo wa mawazo huwafanya watu wengine wale sana japokua kuna wengine hula kidogo sana wakiwa na msongo wa mawazo.
                                                                   
fanya mazoezi; ni muhimu kufanya mazoezi ili kuondoa mafuta na kuikaza misuli ya tumbo..mtu anaweza kutoa kitambi kwa kujinyima kula lakini hawezi kupati six packs kwani zinahitaji kukazwa na na mazoezi.unatakiwa kufanya ya ujumla kama kukimbia, kuendesha baiskeli, kuogelea na kuruka kamba pia mazoezi ya maalumu ya tumbo kama roller na sit ups..kwenda gym ni vizuri zaidi kwani utapata moyo ukifanya mazoezi na watu wengine tofauti na kufanya peke yako.
                                             
       
beba chuma au push ups; watu wanaofanya mazoezi haya huwa na misuli mingi ambayo inaongeza kasi ya kuchoma mafuta mwilini kuliko watu wanene wenye mafuta mengi ambapo kasi yao ya kuchoma mafuta hua ni ndogo.
                                                             
usinywe pombe; unywaji wa pombe hupunguza sana kasi ya uchomaji wa mafuta ya mwili ndio maana ukiwachunguza wanywaji wa pombe sana hua hawakosi vitambi kwani hata wakila chakula kidogo mwili unakibakiza na kukifanya mafuta.
                                                                 
 
usinywe soda; soda moja ina kama vijiko 10 vya sukari, kiasi ambacho ni kikubwa sana kwa matumizi a kawaida ya binadamu. sukari hiyo hubadilishwa kua mafuta na kuongeza uzito mwingine na kitambi. jaribu kutumia juice za kutengenezwa kwa mikono na hakikisha sukari yake ni ya kawaida kwani hata juisi za viwandani zina sukari nyingi sana.
                                                               
kula mboga za majani na matunda kwa wingi; hizi zina kiasi kidogo sana cha mafuta kiasi kwamba hata zikiliwa kwa kiasi kikubwa hua hazina shida, lakini pia zinasafisha sumu mwilini na na kuongeza kasi ya mmeng'enyo wa chakula huku zikizuia kupata choo ngumu.
                                       
tumia virutubisho vya kujenga misuli; kuna virutubisho mbalimbali kitaalamu kama protein shakes ambavyo vimetengenezwa maalumu kwa kazi hii huaidia sana kujenga misuli ya tumboni na sehemu zingine za mwili kwa ujumla, huufanya mwili uwe na umbo zuri na kusaidia kukata six packs za tumboni.kama ukihitaji tuwasiliane, zinapatikana kwa 50000 kwa nusu kilo na matokeo bomba kabisa.       


STAY ALIVE

DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

MAWASILIANO 0653095635/0769846183