data:post.body ZIFAHAMU NJIA 10 MUHIMU ZA KUACHANA NA TABIA ZA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

ZIFAHAMU NJIA 10 MUHIMU ZA KUACHANA NA TABIA ZA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE.

                                                                 
                 
moja ya makala zangu zilizopita niliwahi kuzungumzia madhara ya kufanya ngono kinyume na maumbile yaani ushoga lakini baadae pia niliongelea kwanini kuna ongezeko kubwa la watu wa aina hii...nimekua nikipoke simu kadhaa za waathirika ambao waliniomba sana niongelee njia za kuachana na mchezo huo kwani wengi wao wamenasa huko na wameshindwa kujiokoa.unaweza kua umejihusisha na tabia hii kwa muda mrefu lakini labda hutaki kuendelea na unataka uishi kama watu wengine, bado una nafasi kubwa kwani kuacha leo ni afadhali kuliko kuendelea kwani madhara ya kuendelea ni makubwa zaidi. lakini kuingiliwa kinyume na maumbile sio kwa mashoga tu kuna idadi kubwa ya wanawake pia wametumbukia kwenye dimbwi hili la kuingiliwa kinyume na maumbile kwa dhana ya kuongezeka makalio, kuamini ni raha zaidi au kuridhisha wanaume zao bila kujua madhara yake.zifuatazo ni njia muhimu za kuachana na tabia za ushoga au kuingiliwa kinyume na maumbile.
amua kutoka moyoni kuacha; hii ni hatua kubwa sana ya msingi katika chochote unachotaka kufanya...ili ufanikishe chochote lazima uamue kutoka moyoni na uwe tayari kupambana kwa gharama yeyote. unaweza kua kila siku unasema leo ni mwisho ila kwa sababu maneno yako yanatoka mdomoni ndio maana umekwama.
kaa mbali na marafiki ambao wanakufanya uwe hivyo; mara nyingi ukiwa shoga au ukiwa unashirika mapenzi ya kinyume na maumbile utakutana na watu wa aina yako ambao watakusapoti na kukufanya uone uko sahihi kisha utahisi dunia nzima ina kuonea wivu kumbe inakuonea huruma.kama unataka kuacha kaa mbali na watu hawa.
achana na mpenzi wako wa sasa; kama wewe ni shoga ambaye unaingiliwa kinyume na maumbile na umeamua kuishi kama wanaume wengine basi achana na mpenzi wako ili uanze maisha mapya na kama wewe ni msichana ambaye una mpenzi mwenye tabia ya kukuingilia basi kaa naye chini umwambie kuhusu nia yako  kuacha na kama hataki kuelewa achana naye.
tafuta marafiki wapya; tafuta marafiki wapya ambao hawakujui kabisa kwani hawa watajua wewe ni mwanaume kama wanaume wenzao na wataishi na wewe kama mwanaume mwenzao na hii itakua chachu ya wewe kujiona kidume na kuanza kufanya mambo ya kiume.
kumbuka madhara yake kila ukitaka kujihusisha; wewe hukuumbwa ili uingiliwe kinyume na maumbile, kuna madhara makubwa kama kansa ya mkundu, kuharibika kwa njia ya kujisaidia haja kubwa, kuishiwa nguvu za kiume, kushindwa kujiamini,maambukizi ya ukimwi, kutengwa na jamii na nyingine nyingi.kwanini uendelee kua mtumwa wa mwili wao mwenyewe? chukua hatua.
tafuta mpenzi mpya; kama umeachana na mpenzi wako wa zamani na unataka kurudi kwenye maisha ya mwanzo basi ni vizuri kutafuta mpenzi mpya ambaye hajui lolote kuhusu wewe ili uanze naye maisha ya kawaida.kama wewe ni mwanaume tafuta msichana na kama wewe msichana tafuta mwanaume mwingine muelewa.
achana na imani potofu; kuna wanaume hudai hawawezi kutembea na wanawake kwasababu wanavutiwa na wanaume wenzao au mwanamke anavutiwa na mwanamke mwenzake kimapenzi. huyo sio wewe. hayo ni mawazo tu kwenye akili yako ambayo umeamua kuyafuata.ukiyapuuzia na kujihusisha kimapenzi na jinsia tofauti mawazo hayo yatakwisha.
hama maeneo unayoishi kwa sasa; kama wewe ni shoga na mtaa mzima unajua hivyo ni ngumu sana kwa jamii kuamini kama umeamua kubadili maisha yako kwani utaendelea kubezwa hata ukionesha wazi kwamba wewe ni mtu mpya. hama mtaa uende sehemu nyingine ambayo utapata heshima kama wanaume wengine na uanze maisha mapya.
jihusishe na mazoezi; mazoezi yana nguvu sana kwenye mwili wa binadamu...yana uwezo wa kubadilisha kila kitu ambacho si cha kawaida kikawa cha kawaida. kuna kemikali nzuri ambazo huzunguka mwilini mtu akifanya mazoezi na kukufanya kushinda addiction zote duniani.
pata ushauri na matibabu; nenda hospitali na onana na mshauri wa mambo ya afya na hapa atakupa ushauri mzuri sana lakini pia onana na daktari na uombe kufanya vipimo vyote kuangalia kama kuna ungonjwa wowote umeupata kutokana na maisha yako ya zamani.kwa maelezo zaidi soma hapa
                                  tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                         STAY ALIVE
                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni