data:post.body Mei 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

MAMBO KUMI MUHIMU KUZINGATIA ILI KUISHI MAISHA MAREFU NA YENYE AFYA.....

                                                               
ni ndoto ya kila binadamu kuishi maisha marefu na yenye afya, kimsingi hakuna binadamu angependa kuishi maisha mafupi na yenye afya mbovu lakini kulingana na asili ya dunia yetu kuna changamoto nyingi sana za magonjwa na ajali ambazo zimepunguza urefu wa maisha wa binadamu wengi.vipo vyanzo vya vichache vifo ambavyo kimsingi haviepukiki lakini vyanzo vingi vinaweza kuepukika na kuongeza urefu wa maisha yako hapa duniani. yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kuishi maisha marefu.
acha ulevi; unywaji wa pombe kupita kiasi una madhara makubwa kwa binadamu. madhara ya kifedha yaani kufilisika na na madhara ya kiafya. pombe ina haribu maini kwa kiasi kikubwa sana na baadae heleta kansa ya ini ambayo imeua vijana wengi wadogo.kama unapenda pombe basi kunywa kiasi kidogo na nyakati maalumu na haitakudhuru. lakini pia wasichana wengi wamejikuta wakifanya ngono mpaka na watu ambao hawakuwategemea sababu ya ulevi.
acha ngono zembe; tabia ya kufanya ngono na wanawake tofauti bila kinga haitakufikisha mbali, ukimwi umeua vijana wengi sana na sio rahisi kujua kwani hua ni siri ya familia siku ya mazishi na kama huwezi kutumia kondom basi tafuta mpenzi mmoja muaminifu na utulie naye.utafiti unaonyesha wanawake wmeathirika sana na ukimwi, pamoja na sababu zingine za kitaalamu lakini hofu yao ya mimba ni kubwa sana kuliko ukimwi.
kula vizuri; hakikisha kabla hujala chakula chochote unatafakari kama kina faida yeyote kwenye mwili wako, ulaji wa vyakula ambavyo havina faida mwilini kama pipi, biscuit, soda, na jamii zake vitakuua na kansa siku za usoni lakini pia unene ambao kimsingi huletwa na kula sana utakuletea magonjwa hatari kama kisukari na magonjwa mengine ya moyo.
tumia vyombo vya moto kwa uangalifu; matumizi ya vitu kama gari na pikipiki yanahitaji umakini mkubwa sana hasa ukiwepo barabarani, vijana wengi wadogo wameuawa na vyombo hivi.epuka kuendesha gari umelewa, epuka mwendo mkali, vaa helmet wakati wa kuendesha pikipiki, vunga mkanda wewe dereva au abiria na usikubali kubebwa kwenye gari au pikipiki na mtu ambaye hathamini maisha yake.usione aibu kumwambia dereva apunguze mwendo kwani umemlipa na ameshika maisha yako. na wewe usiyejua kuvitumia kajifunze kwanza chuoni ndio uanze kuvitumia.
shiriki mazoezi; magonjwa ambayo sio ya kuambukizwa kama kisukari, ugonjwa wa moyo, na presha husababishwa sana na maisha ya uvivu. binadamu anatakiwa afanye mazoezi angalau nusu saa kwa siku. visingizio kwamba uko bize sana ni dalili ya kukosa vipaumbele na nidhamu kwenye maisha yako.hizo hela unazotafuta usiku na mchana usipokua na afya bora utakufa uziache.
epuka ugomvi usio na maana; mimi nafahamu watu waliopigwa ngumi moja  tu wakafa hapohapo. mwili wa binadamu ni mlaini sana. kuna sehemu ambazo zikipigwa unakufa hapohapo. jitahidi kua mtu wa kusuluhisha zaidi kuliko kukunja ngumi.watu wote waliouawa kwa kuchoma visu au kupigwa mawe walikufa kwenye mazingira haya.kama umejifunza kupigana basi pigana pale unapokua umeshambuliwa ili kujilinda sio kuanzisha ugomvi makusudi.
usivute sigara; sigara ni moja ya starehe ambayo haina faida yeyote kwenye mwili wa binadamu, huharibu seli za kwenye mapafu na baadae huleta kansa ya mapafu.unaeza ukasema mbona fulani kavuta mapak leo hajafa. kila mtu ana kinga yake ya mwili amabyo ni tofauti na mwingine lakini pia hakuna anayechoka kuishi...huyo unayemuona anatamba, siku akiambiwa sigara ndio iko inamuua hata kama ana miaka 90 atasikitika sana.
usijihusishe na madawa ya kulevya; madawa ya kulevya hayatakuua hapohapo lakini yatakuondoa kwenye mkondo wa maisha ya mafanikio. utadharaulika na kila mtu, utakua huwezi kufanya kazi, muda mwingi utawaza kuiba ili upate madawa mengine ya kutumia.rafiki yangu mmoja mwaka 2004 alivuta bangi kwa kama miezi sita tu akawa kichaa na hajapona mpaka leo pamoja na kupelekwa hospitali nyingi za vichaa.unaweza ukaona jinsi amegeuka mzigo kwa ndugu zake.
jiupushe na uvunjaji wa sheria za nchi makusudi; tabia za wizi, dili za kihalifu, uuzaji wa magendo au kumuibia muajiri wako ii ufanikiwe haraka hua hazina muda mrefu sana maishani. yaani huwezi ukawa mjanja maisha yako yote kwani ipo siku utakamatwa tu.lepo hii kijana au mtu mzima ukihukumiwa miaka 30 basi maisha yako yameishia hapo na huenda ukafia gerezani. matajiri wote duniani wlianza miaka mingi iliyopita. jifunze kua mvumilivu.
waheshimu wazazi wako; ukisoma biblia kitabu cha kutoka 20;12 biblia inasema 'waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kua nyingi katika nchi upewayo na bwana mungu wako' sio kuwaheshimu kwa kuwapa shikamoo kila asubuhi bali kwa kufuata maelekezo na ushauri wao kwani wao wameishi miaka mingi sana duniani na wameona mengi.
                                  tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                      STAY ALIVE

                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                  MAWASILIANO; 0653095635/0769846183

HIZI NDIO SABABU 10 KWANINI WATU WENGI SANA MWAKA HUU WAMEJIUNGA NA KAMPUNI YA AFYA NA UREMBO YA FOREVER LIVING.

                                                                       
                                                         
forever living ni nini?
hii ni kampuni ya kimarekani ambayo inajishughulisha na kuudha bidhaa za ubora kabisa za afya na urembo ambazo zinatengenezwa na mmea wa zamani sana na maarufu duniani kwa jina la aloe vera na wanasambaza bidhaa zao kwa njia ya mtandao[bila kujitangaza kwenye radio,tv au gazeti ila kupitia watu], nalazimika kusema ni bora sana kwani nimekua nikizitumia bidhaa zao  kwa wagonjwa wangu na wateja wangu wengi kwa mafanikio makubwa sana.

kampuni hii ya afya kwa sasa inapatikana kwenye zaidi ya nchi 157 duniani. dunia nzima ina nchi 195[taiwani bado haihesabiki kama nchi zingekua nchi 196]. kwa hiyo kampuni hii imebakiza nchi chache sana imalize dunia nzima. unaweza kua umeshasikia mabaya mengi kuhusu hii kampuni lakini ukashindwa kujiuliza swali moja. je kama kampuni hii ni utapeli au freemason mbona haipati hasara na kufungwa lakini inazidi kupanuka kila siku? kwa mfano hapa tanzania office kuu ya kwanza mwaka 2007 ilikua dar lakini leo zipo dodoma, arusha, mwanza na mbeya na kampuni inazidi kuongeza ofisi zaidi mikoa mingine.

ni moja ya kampuni pekee ambazo zinatambulika na board nyingi za ubora duniani ikiwemo bodi ngumu zaidi kutambua bidhaa duniani ya kiisalam kwa jina la halal.bahati mbaya watu wengi wanadhani ukiingia huko lazima ufanye biashara, hapana... unaweza kuingia ili uweze kununua moja kwa moja kwenye kampuni kwa matumizi yako binafsi na bei ya chini  au ukajiunga kwa ajili ya
kutumia na kushirikisha wengine kwa kuwauzia na baadhi waingie kwenye timu yako ili upate faida...hivyo chaguo ni lako.hebu tuzione faida ya kua mmoja wa wanakampuni hii.

afya na kuishi maisha marefu; dunia ya sasa ina magonjwa zaidi ya 10000 ambayo yanua zaidi ya watu milion 50 kila mwaka na magonjwa mengine bado yanaendelea kulipuka, magonjwa haya yamesababishwa hasa na ulaji mbovu yaani kula vyakula vingi vya kiwandani ambavyo kwa sasa haviepukiki, vyakula vilivyokaangwa sana kama chips, maandazi, sambusa,chapati, piza na kadhalika.., moshi wa viwandani na sigara, unywaji wa pombe, magonjwa ya kuambukizwa kama ukimwi na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.mambo haya yote yanaingiza sumu nyingi kwenye mwili wa binadamu na kuzaa kansa za aina mbalimbali.utafiti wa mwisho nchini marekani unakadiriwa kila kati ya watu watano mmoja ana kansa.sasa kampuni hii ina bidhaa nzuri za kuondoa sumu mwilini, kupungua uzito, kupunguza makali ya kisukari, pumu,presha,kujaza mwili kwa mazoezi,kuongeza nguvu za kiume,magonjwa ya moyo, presha, kansa, kuongeza cd4 kwa wagonjwa wa ukimwi na zingine nyingi.hivyo kwa kutumia bidhaa hizi unaweza kuishi maisha marefu wewe na familia yako.mimi binafsi nimeshuhudia zikisaidia watu wengi akiwemo baba yangu mzazi ambaye alisumbuliwa na kansa na kisukari.
                                                                     
faida za urembo; katika mambo ambayo yameshika dunia ya sasa ni urembo na kupendeza, japokua kuna watu wametumia nafasi hii kuuza bidhaa zenye kemikali nyingi ambazo zimeharibu ngozi na kuua watu wengi kwa kansa. leo hii ukienda hospital ya kansa ya taifa ocean road kuana wanawake wengi utawakuta pale wanakata roho baada ya kuugu sana.kampuni hii ina bidhaa zote za urembo ambazo zimetengenezwa kiasili kwa aloe vera na ubora wa hali ya juu. zikiwemo make ups, mafuta ya ngozi, lipsticks, perfum, deodorant, dawa za meno ambazo hazina floride[floride huleta kansa kwa binadamu], sabuni,mafuta ya nywele, kuondoa michirizi ya unene na michirizi inayosabaishwa na kujichubua, scrub za uso ambazo zinatumika na watu kwanzia marekani na dunia nzima kwa ujumla.bidhaa hizi huuzwa kwa bei ya chini sana kwa watu ambao wamejiunga na kununua moja kwa moja kwenye kampuni.

safari za nje ya nchi; unaweza kua umefanikiwa sana kwenye ajira yako kwa kupata mshahara mkubwa, umefanikiwa kwenye biashara zako lakini hujawahi kuvuka tanzania na kama umeenda sana hujavuka east afrika yaani kenya, uganda, tanzania, burundi na rwanda. wenzetu wazungu wanaamini sana kwenye kusafiri kuiona dunia ndio maana baadhi yao wameshapanda mlima kilimanjaro ila wewe mzawa hujawahi hata kuuona kwa macho yako.lakini shida sio pesa. shida ni kwamba leo hii ukisema uende nje utaanzia wapi? mfano unataka kwenda mrekani lazima uwe na sababu ya mzingi sana ili upate viza. lakini ukiwa na kampuni hii, kila mwaka inapeleka watu wake kutembelea sehemu mbili duniani. angalia labda wazazi wako wana pesa ila wanashindwa kutoka nje sababu hawajui watafikia wapi, je unataka ue kama wao?..miaka ya hivi karibuni watu wamekwenda mexico na marekani...mwaka huu ni south afrika na ugiriki. mwakani ni barcelona.hivi ukiingia leo baada ya miaka kumi utakua hujamaliza dunia tu? sasa unaweza ukasafiri kwa gharama zako au kwa gharama zao kama ukikidhi vigezo vyao vya kibiashara.
                                                       

kupata muda wa ziada wa kupumzika na familia; kuna watua ambao wana kazi nzuri sana lakini ukimuuliza mara ya mwisho kukaa na familia yako ilikua lini hajui kwani yeye ni wa kuamka saa 10 usiku na kurudi saa sita usiku. ndugu hayo sio maisha tuliyopangwa tuishi duniani. kama ukijiunga na ukafanya kazi kwa juhudi kuna kipindi itafika utaona hauna haja ya kuendelea na ajira yako kwani unaweza kua umetengeneza timu kubwa  ya watu ambao unafanya nao biashara kupitia timu hii, ambapo hata ukilazwa hospitali mwaka mmoja bado pesa pesa zinaendelea kungia kwenye akaunti yako vitu ambavyo havipatikani kwa ajira binafsi au kujiaajiri mwenyewe.
                                                   
   
urithi kwa familia na watoto; kama umejiunga kufanya biashara au umejiunga kutumia bidhaa haijalishi, kitu cha kujua ni kwamba hata ukifa leo watoto wako na familia yako watendeleza ulipoishi na kuendelea kufaidika ndio maana inaitwa forever living. biashara nyingi za kiafrika hufa mara moja baba anapofariki hata pensheni ambazo watu hupewa baada ya kustaafu huisha na kuacha watu wakiteseka. forever inakupa urithi mkubwa wa familia yako na vizazi vijavyo.
                                                             
kustaafu mapema; kawaida serikali na kampumi nyingi muda wa kustaafu ni miaka 60 lakini kiukweli hakuna anayependa kustaafu akiwa amechoka kiasi hicho lakini ukiwa na kampuni hii na ukajituma inavyotakiwa kabla ya kufikisha miaka 40 utakua umetulia ndani na familia yako na kazi yako kubwa itakua ni kusafiri huku na kule.hapa tanzania kuna watu wapata zaidi ya million 30 kwa mwezi huku wakilipwa zaidi ya millioni 600 kila mwaka kama wana hisa wa kampuni hii.wengi wao hawana hata miaka 30 lakini wengi wetu leo tumekaa ndani tukisubiri pensheni ya milion 50 au 100 baada ya kufanya kazi miaka 40 na wengine tumemealiza vyuo tumekaa ndani na vyeti tunasubiri ajira.                                    

mendeleo yako binafsi ya kifikra; kampuni hii inafundisha mambo mengi sana ukiachana na pesa, afya na urembo. inakufundiisha kujiamini, kuongea mbele za watu wengi, kutokua muoga na kua na msimamo wa maisha yako. ni moja ya kampuni pekee za ambayo inatoa mafundisho mengi kuhusu shughuli inazozifanya kiasi kwamba ukifuatilia mafundisho hayo utagundua umebadilika sana kwenye mtazamo wa maisha yako.
                                                           
inakupa nafasi ya kufanya biashara ya kimataifa; ni ndoto za watu wengi kupanuka kibiashara duniani...mfumo wa kampuni hii kama nilivyosema mwanzoni ni mtandao yaani wewe unatumia bidha huku unashirikisha  watu wengine amabao wataingia kwa jina lako kutumia bidhaa na kushirikisha wengine au kuuza bidhaa na wewe utalipwa maisha yako yote kwa hao walioingia chini yako na vizazi  vyao vyote. sasa katika hizo nchi 157 ambazo kampuni imefika unaweza kuingiza mtu huko. yaani kama wewe ni mtanzania unaweza kumuingiza muhindi au mwarabu na akaaifanya akiwa huko kwao au mtanzania unayemfahamu anaishi nje ya nchi na akaifanya huko huku akiwa chini yako. kama wewe ni mtanzania labda mwanafunzi au unafanya kazi nje unaweza ukaifanya huko huko na kuongeza timu yako huko na ndani ya nchi.kitu ambacho sio rahisi kufanya kwa biashara zetu za kawaida.
                                                           
uhuru wa kifedha; uhuru wa kifedha ni uwezo wa kuishi hata miaka kumi ijayo bila kufanya kazi yeyote ila na kuendelea kuishi kama kawaida. ajira zetu nyingi pesa hukoma pale unapoacha kufanya kazi tofauti na kampuni hii ambayo itakufanya uache kuamka saa 11 kuwahi kazini bali utakua unaamka unawaza leo niende wapi nikapumzike kwani umeshakua mtu huru.
                                                             
kugusa maisha ya wengine; kampuni hii inakupa nafasi ya kugusa maisha ya watu wengine kwa njia mbalimabali... kwa kuwapa msaada ndugu na familia wa kifedha, kuwashirikisha bidhaa bora za afya na kuwaondolea maumivu yao ya magonjwa hata kuwasaidia wazazi wako kwa wale wanafunzi ambao wazazi wao wanateseka sana kuwalipia ada na gharama zingine wakiwa vyuoni.
                                                     
mwisho; mwanzoni nilisema kwamba mtu anweza kuingia kama mtumiaji au mfanyabiashara... sasa hapo kwenye biashara, kama zilivyobiashara nyingine lazima uwe na nidhamu ya biashara lakini ukumbuke kwamba hakuna biashara ya kuanza leo na kutajirika kesho yaani lazima uipe muda lakini hii pia ndio kampuni pekee ambayo itakushika mkono kukuelekeza pakwenda tofauti na biashara zingine zote duniani ambapo ukifungua duka karibu na mwenzako ni vita. hayo yote niliyotaja juu sio hadithi ni mambo ya kweli na watu walioguswa na kampuni hiyo ikiwemo mimi ni mifano inayoishi...huko mtaani ukienda kuulizia utakutana na watu wa aina tatu.

  1. walioshindwa; hawa watakwambia mabaya yote ya biashara hii lakini ukiwauliza je ni biashara hii pekee ndio watu wanashindwa? huko mtaani kwako huoni fremu kila siku anaingia mtu mpya? aliyeuepo kaenda wapi? huu ni mfano kwamba hakuna biashara rahisi duniani.
  2. wasiojua kuhusu forever; hawa nao wamesikia juu juu tu na watakudanganya zaidi.
  3. waliofanya na kufanikiwa; kama umeamua kujikita na unataka ushauri basi watafute hawa watakusaidia sana.
kwanini forever na sio kampuni nyingine?
imekua ikifanya kazi kwa zaidi ya miaka 35 sasa, ni kampuni ya kwanza kwa ubora na ulimaji wa bidhaa za aloe vera duniani, haina madeni, iko nchi nyingi zaidi duniani na imegusa maisha ya watu wengi.

unajiunga vipi?
kujiunga kama mtumiaji gharama ni shilingi laki mbili na nusu tu na hapo utachagua bidhaa zote unazohitaji kulingana na bei hiyo..... kujiunga kama mfanyabiashara gharama ni milioni moja ambapo unaweza kuzitoa kwa awamu hata nne ndani ya miezi miwili na pesa utakayotoa utapewa bidhaa ya thamani ile.kifupi hakuna kingilio.hela utakayotoa ni ya kuchukua bidhaa zako.mtu yeyote, na mkoa wowote anaweza kuingia na kampuni ikawa inamtumia bidhaa anazotaka huko alipo na akaanza maisha ya furaha ya kutumia bidhaa hizi na kuwashirikisha wengine.


kwanini kuna watu baadhi waliongia upande wa biashara wanashindwa?

  • kutohudhuria semina; biashara ya mtandao ni aina mpya ya biashara kabisa na unatakiwa uendelee kufundishwa jinsi ya kuifanya angalau mara moja kwa wiki. jinsi ya kuuza, jinsi ya kupata watu wapya na jinsi ya kukabiliana na changamoto...ukijiunga kama mfanyabiashara afu ukakaa ndani itakushinda.
  • kutaka mafanikio ya haraka; kuna watu hutaka mafanikio ya haraka ambayo hata kwenye biashara zingine hayapo hivyo ipe angalau mwaka mmoja na ukiona huwezi basi endelea kua kama mteja uboreshe afya yako lakini sio ufanye mwezi mmoja useme haiwezekani.
  • kukatishwa tamaa; huko mtaani utakutana na vikwazo vingi kutoka kwa ndugu na jamaa lakini cha kushangaza baadhi yao wanazitumia bidhaa hizi lakini hawataki tu ufanye hiyo biashara...hao watakuondoa barabarani.
  • kutoipa muda biashara yako kwa siku; mara nyingi wanaoifanya biashara hii hua wapo kazini au au hawana kazi kabisa, sasa unatakiwa uipe muda wa masaa mawili kila siku kuangalia biashara inaendaje na kufanya kazi na sio kuifanya pale unapoona umepata muda.kutoipa muda kila siku itakushinda na swala la kukosa muda sio la ubize ila swala la kushindwa kuweka vipaumbele.kama una mpenzi anakwambia yuko bize na hana muda wa kuonana na wewe basi wewe sio kipaumbele chake.
  • kuaminishwa kwamba bidhaa ni ghali sana; duniani hakuna kitu ambacho ni ghali sana ni swala la kipaumbele tu. katika maisha ya kawaida ukitaka mchele wa 2000 upo, 3000 upo, mpaka 5000 kwa kilo upo.kinachofanya mtu anunue ni pale anapoeleweshwa kuhusu ubora wa bidhaa husika. mchele wa 5000 hautachwa kuuzwa eti kwasababu upo wa 2000..lakini pia duniani watu wanaoona gharama za bidhaa ni wale wazima tu ila ukikutwa kitandani na kansa hakuna bidhaa ghali ambayo hutanunua kama pesa unazo ili iokoe maisha yako sasa usisubiri ufike huko. vitabu vitakatifu vinasema umepewa baraka na laana uchague mwenyewe...kazi ni kwako.....
                                             tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                 STAY ALIVE....

                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                MAWASILIANO 0653095635/0769846183                                                             
HAYA NDIO MAGONJWA 4 YA KUAMBUKIZWA,, MUHIMU KUPIMA KABLA YA KUANZISHA MAHUSIANO MAPYA.

                                                         
mara nyingi wapenzi wapya hua wanatumia kondomu mara kwa mara kwa uaminifu lakini wanapokua kwenye mahusiano kwa muda mrefu hujikuta wanaacha kutumia condom na kuisahau kabisa. kumbuka hapa ndipo watu wengi wanaambukizwa magonjwa ya ajabu hasa kama hawakupima mwanzo wa mahusiano lakini sio hivyo tu maambukizi huendelea kama mmoja wao sio mwaminifu ndio maana utafiti unaonyesha wanandoa wanaongoza kwa ugonjwa wa virusi vya ukimwi kwani baada ya ndoa kondomu hua ni mwiko kwao.sasa leo naenda kuongelea magonjwa hatari sana ambayo ni vizuri kupima baada ya kuanzisha mahusiano mapya ila hata siku ikitokea kinga imesahaulika basi huenda uko salama kama mpenzi wako ni mwaminifu.

ugonjwa wa kaswende; kitaalamu kama syphilis, huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya watu wengi bila wao kujifahamu.ugonjwa huu amabao huambukizwa kwa njia ya ngono  huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi sehemu ambapo wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri. kidonda hicho hupona, ,upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea. ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya ndani. mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu kua kichaa.kuna vichaa wengi sana mtaani sababu ya huu ugonjwa.

ugonjwa wa hepatitis b; ugonjwa huu ni hatari na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya ngono na kugusana kwa dmu au majimaji ya mwili  kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu kuliko kupata ukimwi. ugonjwa huu hushambulia maini na kuacha makovu. mgonjwa hupata macho ya njano, homa, maumivu ya kichwa na kadhalika.ugonjwa hii mwishoni hupelekea kansa ya ini ambayo inaua ndani ya miezi sita.

ugonjwa wa ukimwi; huu ni ugonjwa unaofahamika kwani unatangazwa sana hasa kwenye vituo vya radio, tv, magazeti na sehemu mbalimbali. ugonjwa huu uligundulika karne ya 20 na mpaka sasa umeshaua watu wengi sana na zaidi ya 95% ya wagonjwa waliambukizwa kwa kushiriki ngono bila kinga.ni ugonjwa amabao hauna tiba wala kinga na mpaka sasa kulingana na data za shirika la afya duniani watu million 50 duniani kote wanasumbuliwa na ugonjwa huu.lakini bado kuana watu wengi wana uupuza wakati wa kuanzisha mahuasiano wakiamini macho yao kwamba huyu hawezi kua nao.

ugonjwa wa gonorea; huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unashambulia jinsia zote yaani wanaume na wanawake, mara nyingi mwanaume hawezi kujificha na ugonjwa huu kwani dalili za ugonjwa huo kama kutoka na usaa kwenye njia ya kukojolea zitamuumbua lakini kwa wananwake ugonjwa huu huweza kukaa kimya na mwana mke hujikuta akisambaza ugonjwa huo bila kujua. mwishoni ugonjwa huu hushambulia kizazi na kusababisha ugumba.

mwisho; sio vipimo vyote vilivyotajwa hapo juu vinapatikana kirahisi sehemu zote lakini hata kama havipatikani vyote basi ni muhumu upime baadhi ya ambavyo vinapatikana kwenye eneo unaloishi ili kuikinga afya yako na kuwakinga uwapendao.
                              tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                      STAY ALIVE
                              DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                              MAWASILIANO O653095635/0769846183


HIKI NDIO CHANZO NA MATIBABU YA HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE.

                                                                                                     
                                                 
watu wengi hua wanafikiri kwamba uke wa mwanamke hauna harufu kabisa kitu ambacho sio kweli, sehemu yeyote ya mwili iliyojificha hua ina harufu fulani, mfano kwapa, chini ya matiti, katikati ya makalio na kadhalika lakini harufu hiyo hua ya kawaida lakini huweza kua kali kama kuna magonjwa fulani...
hivyo uke wa mwanamke pia una harufu fulani ambayo kitaalamu ni ya kawaida lakini kuna vitu fulani ambavyo huweza kusababisha ile harufu kua kali sana kiasi kwamba hata mtu akipita karibu yake atasikia harufu hiyo. watoto wa kike ambao wanavunja ungo kwa mara ya kwanza hasa shule za msingi wanakua hawajui usafi wa sehemu zao za siri hivyo kutoa harufu mbaya.
wanawake wengi waliolewa na wakishazaa wanajisahau sana na kua bize na mambo mengi ya uleaji wa mtoto na kujiacha wakitoa harufu ya mwili kwa kisingizio cha kua bize na mtoto huku wa kisahau hiyo ni sumu ya ndoa kwani haki ya mume haiondolewi na mtoto. vifuatavyo ni vyanzo vikuu vya harufu sehemu za siri...

magonjwa ya zinaa; magonjwa mbalimbali ya zinaa huleta harufu kali kulingana na aina ya ugonjwa mfano ugonjwa wa gono ambao hutoa uchafu wa njano, ugonjwa wa fangasi ambao hutoa uchafu mweupe, na ugonjwa wa trichomoniasis amabo mgonjwa hutoa uchafu wa rangi ya kijani wenye harufu kali sana.magonjwa yote haya huambukizwa kwa ngono zembe.

jasho la mwili; tabia ya baadhi ya wasichana kuto kuoga kila siku hasa sehemu zenye baridi kali hufanya bakteria kubadilisha maji maji yote ya mwili na jasho kua harufu kali sana.watu wanene sana hutokwa na harufu kali zaidi sababu ya kutokwa jasho jingi na kulihifadhi mwilini.

mabadiliko ya homoni za uzazi;kipindi cha hedhi na kipindi ambapo yai linashuka mwanamke hua na harufu ambayo sio ya kawaida lakini pia kipindi cha uzee yaani zaidi ya miaka 50 homoni za uzazi hupungua sana kiasi kwamba ulinzi wa sehemu za siri kutokana na asidi ya mwili hupungua sana na kusababisha harufu.watu hawa wakipewa oestrogen cream harufu huobdoka.

vyakula unavyotumia;  baadhi ya vyakula huweza kubadilisha harufu ya jasho maji maji yanayotoka sehemu za siri. mfano baadhi ya pombe za kienyeji, vitunguu, pilipili na samaki huchangia mabadiliko ya harufu za sehemu za mwili na sehemu siri hivyo kama wewe una tatizo hilo ni vizuri kuepuka yakula hivyo.

kusafisha uke na sabuni; kawaida uke wa mwanamke unatakiwa usafishwe kwa ndani kwa kutumia maji tu. sasa matumizi ya sabuni na mafuta au kemikali fulani kusafisha huua bakteria fulania ambao kazi yao ni kuzuia maambukizi kutokwa kwa wadudu wengine ambao sio wazuri kwa mwili.

uchafu wa mwili; tabia za kurudia nguo za ndani ni hatari kwani huleta mkusanyiko wa bakteria wengi ambao huweza kua hatari kwa uke wa mwanamke hivyo kwa hali ya kawaida mwanamke anatakiwa avae angalau chupi moja kila siku bila kuirudia kabla ya kuifua.

mwisho;matibabu ya hali hii hutegemea sana chanzo husika cha harufu mfano kama ni ugonjwa wa zinaa utapewa matibabu hospitalini kulinganan na ugonjwa husika.
kupunguza uzito na kuvaa nguo ambazo hazibani sana ni muhimu kwani husaidia kupunguza jasho jingi linalobaki mwilini.
kumbuka harufu mbaya ni hatari kwa jamii na mahusiano yako kwani unaweza ukaachwa na mpenzi wako kama huzingatii hili au ukamfanya hata kutoka nje ya ndoa kama umeolewa. kwa maelezo zaidi bofya hayo maneno ya kijani hapo chini.
                          tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                   
                                                              STAY ALIVE
                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                         MAWASILIANO; 0653095635/0769846183UKIONA HIZI DALILI SITA UJUE MIMBA YAKO IMEHARIBIKA....

                                                           
kuna sababu nyingi sana zinazoweza kuharibu mimba ya mama ikiwemo ugonjwa wa malaria, kaswende, kazi nyingi, magonjwa ya zinaa, u.t.i dawa fulani fulani mfano albendazole, misoprostol, metronidazole na kadhalika. lkiujumla sababu nyingi ambazo zinasababisha mimba kutoka huweza kuzuilika kwa kwenda kliniki mapema yaani pale tu unapohisi una mimba hata kama ni wiki mbili na kufuata ushauri wa wataalamu. sasa kuna wanawake wengi mimba zo huharibika na wao hushindwa kugundua mapema na matokeo yake anakaa na mtoto mfu hata miezi kadhaa bila kujua hivyo leo ntaongelea dalili za kuharibika kwa mimba kama ifuatavyo.

kutokwa na damu nyingi sehemu za siri; hii ni dalili kwamba mimba imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza akufunguka sasa ukienda hospitali utakuta majibu mawili kwamba mtoto ameshafia tumboni au bado hajafa. lakini kama imeshatoka damu nyingi mtoto huyu atakufa tu.

mtoto kuacha kucheza tumboni; kwa kawaida mtoto huanza kucheza wiki ya 18 mpaka 20 kwa wanawake ambao hawajawahi kubeba mimba na wiki ya 16 mpaka 20 kwa wanawake ambao wamehsawahi kuzaa sasa ikitokea mtoto ameshawahi kucheza na sasa hachezi tena au muda huo umepitiliza na bado kimya kuna uwezekano mkubwa ameshafariki.

kupotea kwa dalili za ujauzito; mara nyingi mtu akipata ujauzito anakua na dalili nyingi kama kichefuchefu, kukosa hamu ya kula, kutapika sana na kubadilika sana tabia sasa zile dalili zote za mimba zikisimama ghafla basi ujue mimba imeharibika.

kuacha kuongezeka kwa mimba; tunategemea mimba kuendelea kua kubwa kulingana na umri unavyozidi kwenda mbele sasa kama mimba mara ya mwisho ilikua na miezi mitatu na leo ina miezi sita au mitano lakini iko haijabadilika ukubwa ujue mimba imeharibika.

maumivu makali ya tumbo; maumivu makali ya tumbo hasa kwa mimba kubwa sana au mimba ndogo sana kuna uwezekano mkubwa kondo imeanza kujiondoa kwenye kizazi kwa mimba kubwa au mimba ndogo imeshindwa kuendelea kukua. hii inaweza kua dalili kwamba mimba imeharibika.

kutoka kwa vipande vya nyama sehemu za siri; vipande vya nyama huashiria kwamba kuna mtoto anakua ameharibika tayari tumboni na mama kama huyu anatakiwa asafishwe kuondoa masalio yaliyobaki ili mama asiweze kupata madhara zaidi.

mwisho; kama nilivyosema mwanzoni mimba nyingi zinazoharibika hasa kwa nchi zetu za kiafrika hua kuna uzembe wa watu kutaka kujitibu wenyewe, kutokwenda kliniki mapema na kutofuata ushauri wa kitaalamu. kwa maelezo zaidi bonyeza hayo maneno ya kijani kwa ushauri zaidi.
                                tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

ZIFAHAMU NJIA 10 MUHIMU ZA KUACHANA NA TABIA ZA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE.

                                                                 
                 
moja ya makala zangu zilizopita niliwahi kuzungumzia madhara ya kufanya ngono kinyume na maumbile yaani ushoga lakini baadae pia niliongelea kwanini kuna ongezeko kubwa la watu wa aina hii...nimekua nikipoke simu kadhaa za waathirika ambao waliniomba sana niongelee njia za kuachana na mchezo huo kwani wengi wao wamenasa huko na wameshindwa kujiokoa.unaweza kua umejihusisha na tabia hii kwa muda mrefu lakini labda hutaki kuendelea na unataka uishi kama watu wengine, bado una nafasi kubwa kwani kuacha leo ni afadhali kuliko kuendelea kwani madhara ya kuendelea ni makubwa zaidi. lakini kuingiliwa kinyume na maumbile sio kwa mashoga tu kuna idadi kubwa ya wanawake pia wametumbukia kwenye dimbwi hili la kuingiliwa kinyume na maumbile kwa dhana ya kuongezeka makalio, kuamini ni raha zaidi au kuridhisha wanaume zao bila kujua madhara yake.zifuatazo ni njia muhimu za kuachana na tabia za ushoga au kuingiliwa kinyume na maumbile.
amua kutoka moyoni kuacha; hii ni hatua kubwa sana ya msingi katika chochote unachotaka kufanya...ili ufanikishe chochote lazima uamue kutoka moyoni na uwe tayari kupambana kwa gharama yeyote. unaweza kua kila siku unasema leo ni mwisho ila kwa sababu maneno yako yanatoka mdomoni ndio maana umekwama.
kaa mbali na marafiki ambao wanakufanya uwe hivyo; mara nyingi ukiwa shoga au ukiwa unashirika mapenzi ya kinyume na maumbile utakutana na watu wa aina yako ambao watakusapoti na kukufanya uone uko sahihi kisha utahisi dunia nzima ina kuonea wivu kumbe inakuonea huruma.kama unataka kuacha kaa mbali na watu hawa.
achana na mpenzi wako wa sasa; kama wewe ni shoga ambaye unaingiliwa kinyume na maumbile na umeamua kuishi kama wanaume wengine basi achana na mpenzi wako ili uanze maisha mapya na kama wewe ni msichana ambaye una mpenzi mwenye tabia ya kukuingilia basi kaa naye chini umwambie kuhusu nia yako  kuacha na kama hataki kuelewa achana naye.
tafuta marafiki wapya; tafuta marafiki wapya ambao hawakujui kabisa kwani hawa watajua wewe ni mwanaume kama wanaume wenzao na wataishi na wewe kama mwanaume mwenzao na hii itakua chachu ya wewe kujiona kidume na kuanza kufanya mambo ya kiume.
kumbuka madhara yake kila ukitaka kujihusisha; wewe hukuumbwa ili uingiliwe kinyume na maumbile, kuna madhara makubwa kama kansa ya mkundu, kuharibika kwa njia ya kujisaidia haja kubwa, kuishiwa nguvu za kiume, kushindwa kujiamini,maambukizi ya ukimwi, kutengwa na jamii na nyingine nyingi.kwanini uendelee kua mtumwa wa mwili wao mwenyewe? chukua hatua.
tafuta mpenzi mpya; kama umeachana na mpenzi wako wa zamani na unataka kurudi kwenye maisha ya mwanzo basi ni vizuri kutafuta mpenzi mpya ambaye hajui lolote kuhusu wewe ili uanze naye maisha ya kawaida.kama wewe ni mwanaume tafuta msichana na kama wewe msichana tafuta mwanaume mwingine muelewa.
achana na imani potofu; kuna wanaume hudai hawawezi kutembea na wanawake kwasababu wanavutiwa na wanaume wenzao au mwanamke anavutiwa na mwanamke mwenzake kimapenzi. huyo sio wewe. hayo ni mawazo tu kwenye akili yako ambayo umeamua kuyafuata.ukiyapuuzia na kujihusisha kimapenzi na jinsia tofauti mawazo hayo yatakwisha.
hama maeneo unayoishi kwa sasa; kama wewe ni shoga na mtaa mzima unajua hivyo ni ngumu sana kwa jamii kuamini kama umeamua kubadili maisha yako kwani utaendelea kubezwa hata ukionesha wazi kwamba wewe ni mtu mpya. hama mtaa uende sehemu nyingine ambayo utapata heshima kama wanaume wengine na uanze maisha mapya.
jihusishe na mazoezi; mazoezi yana nguvu sana kwenye mwili wa binadamu...yana uwezo wa kubadilisha kila kitu ambacho si cha kawaida kikawa cha kawaida. kuna kemikali nzuri ambazo huzunguka mwilini mtu akifanya mazoezi na kukufanya kushinda addiction zote duniani.
pata ushauri na matibabu; nenda hospitali na onana na mshauri wa mambo ya afya na hapa atakupa ushauri mzuri sana lakini pia onana na daktari na uombe kufanya vipimo vyote kuangalia kama kuna ungonjwa wowote umeupata kutokana na maisha yako ya zamani.kwa maelezo zaidi soma hapa
                                  tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                         STAY ALIVE
                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183

SOMA HAPA UJUE CHANZO NA MATIBABU YA UGONJWA WA BUSHA.

                                                                   
                                                           
busha ni nini?                             
huu ni uvimbe kwenye korodani ambao unasababishwa na kujaa kwa maji kwenye moja ya sehemu zinazounda korodani kitaalamu kama tunica vaginalis..busha hutokea pale maji yanayotengenezwa kwenye korodani kua mengi sana kuliko yale yanayo ondolewa.
busha huweza kutokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa lakini mara nyingi hupotea baada ya muda mfupi tu, kama ukiona halipotei  kwa mtoto wako ni vizuri kuonana na daktari.

chanzo cha busha ni nini?
kuna aina kuu nne za vyanzo vya busha kama ifuatavyo.

idiopathic; hii ni busha inayotokea tu bila hata kujua chanzo ni nini.
kuumia; busha huweza kutokea sababu ya kuumia kwa kupigwa na kitu kwenye korodani au kuanguka na kuumiza sehemu hizo.
uvimbe; uvimbe kama wa kansa huweza kusababisha busha.
magonjwa; ugonjwa unao ambukizwa na mbu kitaalamu kama filariasisis huleta busha na aina hii ya mbu hupatikana mwambao wa bahari na ndio maana wagonjwa ni wengi sana huko.

dalili za busha..
ugonjwa huu huanza kwa kuvimba taratibu kwa korodani na baadae kua kubwa sana, hakuna maumivu yeyote ambayo mgonjwa anayapata isipokua uvimbe ukiwa mkubwa sana mgonjwa huathirika kisaikolojia kwa kutengwa au kuchekwa na jamii.

vipimo;
ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa kuangaliwa tu na daktari mzoefu lakini pia anaweza kupiga picha kuhakikisha sio ugonjwa mwingine unaosababisha kuvimba kwa korodani.

matibabu;
hapa ndio waganga wengi wa kienyeji wanapodanganya watu,...ugonjwa huu ukiupata lazima upasuliwe kuondoa hayo maji na kuzuia chanzo cha tatizo na hakuna dawa yeyote ya kupaka, kunywa au kuchanja ambayo inaweza kutibu hili tatizo.
uparesheni yake ni rahisi sana na ukienda mapema wakai bado uvimbe ni mdogo ndio rahisi zaidi.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                 

                                                     STAY ALIVE
                                DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183