Home »
» ZIFAHAMU SABABU 8 ZINAZOWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUZAA KWA UPASUAJI.
ZIFAHAMU SABABU 8 ZINAZOWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUZAA KWA UPASUAJI.
mwaka 320 kabla ya kristo, mama aliyemzaa mfalme bisindura wa india alikunywa sumu bahati mbaya akafa akiwa anakaribia kusukuma mtoto na daktari aliyekuepo akasema lazima mtoto aishi, basi akampasua mama na kutoa mtoto haraka. kabla ya hapo mama yeyote aliyeshindwa kuzaa kwa njia ya kawaida ilikua lazima afe. lakini pia historia inasema mfalme wa roma ambaye alikua anaitwa cisar alizaliwa kwa upasuaji huo na ndio chanzo cha upasuaji huo kupewa la mfalme huyo kitaalamu kama cesarian section.
basi kwanzia miaka hiyo upasuaji huo ukazidi kufanyiwa marekebisho na mpaka leo hii mama akifanyiwa upasuaji huu huishi yeye na mtoto wake tofauti na zamani ambapo mama ilikua lazima afe.labda na wewe umekua ukisikia akina mama wanafanyiwa upasuaji lakini hujui kwanini.... hivyo leo ntaenda kuongelea vyanzo vikuu muhimu ambavyo vinachangi mwanamke kupasuliwa kama ifuatavyo.
mtoto mkubwa sana; mtoto akishazidi kilo nne tumboni mwa mama basi uwezekano wa yeye kutoka kwa njia ya kawaida unakua haupo hivyo maandalizi hufanyika mapema na wakati mwingine watu hawasumbuki hata kujaribisha kwa njia ya kawaida bali hupelekwa chumba cha upasuaji moja kwa moja.
mapacha walioungana; hawa hawawezi kutoka kupitia njia ya kawaida hata iweje na hakuna njia ya kuwaachanisha wakiwa tumboni hivyo hali hii hulazimisha upasuaji kwa gharama yeyote.
mtoto kulala vibaya; kawaida mtoto anatakiwa alale kwa urefu yaani kichwa kikiangalia sehemu ya njia ya kutokea[vertical lie] lakini wakati mwingine mtoto huweza kulala tofauti yaani kulala kwa upana[horizontal lie] au kutanguliza matako badala ya kichwa. hali hizi kwa mwanamke ambaye anajifungua kwa mara ya kwanza upasuaji ni lazima.
kichwa kikubwa; kujaa kwa maji kwenye kichwa cha mtoto kitaalamu kama hydrocephulus hufanya kichwa kiwe kikubwa kuliko kawaida hivyo kupelekea mtoto kushindwa kupita njia ya kawaida.
kutoka vibaya;kawaida mtoto anatakiwa atangulize kisogo wakati anatoka afu ndio kichwa kizima kitoke kisha shingo na mwili mzima lakini wakati mwingine hujaribu kutoka kwa kutanguliza uso kitaalamu kama face presentation na kulazimisha upasuaji.
nyonga nyembamba; kuna wanawake ambao nyonga zao ni nyembamba sana kiasi kwamba haziwezi kupitisha mtoto au zinafanana na zile za kiume[male pelvis] wanawake hawa huweza kugunduliwa mapema hata kabla uchungu haujaanza.hawa wahawezi kuzaa kawaida maisha yao yote kwani kuna mifupa inayozuia mfano ischial spine. mara nyingi wanawake wenye urefu chini ya sentimita 150 huwa hivi.
uvimbe kwenye kizazi; kuna uvimbe hutokea kwenye kizazi kitaalamu kama uterine mayoma, mara nyingi kwa wanawake zaidi ya miaka 30..vimbe hizi huzuia shughuli nzima ya mtoto kutoka kwa kumuwekea vikwazo. hali hii hulazimisha upasuaji tu.
kifafa cha mimba; hii ni hali ambayo mama hupata presha kubwa ya damu kipindi cha kujifungua ambayo huambatana na degedege kali ambazo humfanya mama apoteze fahamu.hali hii hulazimisha mama kupata
kovu la upasuaji ambalo halijakomaa; kawaida mwanamke akifanyiwa upasuaji hutakiwa kukaa miaka mitatu kabla ya kubeba mimba nyingine, ikitokea akabeba mimba kabla ya muda huo basi hataruhusiwa kusubiri uchungu kwani uchungu unaweza kupasua kizazi.
mwisho; vifo vingi vya akina mama husababishwa na kutokugundua mapema kama mwanamke husika anatakiwa azae kwa upasuaji au kwa njia ya kawaida. ni vizuri kuhudhuria clinic mara kwa mara ili kuepusha vifo hivi ambavyo vinazuilika.
STAY ALIVE....
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183[tuma meseji tafadhari]
angalizo; kwanzia sasa, ushauri wowote kutoka kwa daktari, wa matatizo binafsi kwa njia ya simu utatozwa shilingi 5000, ushauri kwa kufika ofisini kwetu gongo la mboto dar es laam utatozwa shilingi 10000.malipo hayo yatafanywa kwa namba hizo hapo juu.karibuni sana...
0 maoni:
Chapisha Maoni