data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA KISUKARI NA MATIBABU YAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA KISUKARI NA MATIBABU YAKE.

                                                                               
kabla ya ukoloni utafiti unaonyesha palikua hakuna wagonjwa wa kisukari kwa nchi za kiafrika lakini miaka mingi baada ya ukoloni na kutawaliwa na kupata uhuru wagonjwa waafrika wa kisukari walianza kuonekana. hii ni kwasababu ya mabadiliko ya ulaji wa vyakula na kuingia kwa tamaduni za kizungu ambazo ni tofauti na za kwetu ambzo tamaduni hizi huchangia kwa namna moja au nyungine kuleta ugonjwa huu mfano kutumia gari muda mwingi bila mazoezi, kushinda ofisini umekaa, kuangalia tv na kadhalika.

ugonjwa wa kisukari ni nini?
huu ni ugonjwa ambao huanza kujionyesha kwa kua na sukari nyingi kwenye damu sababu ya kongosho kushindwa kabisa kutengeneza homoni ya insulini au kutengeneza insulini kidogo sana ambayo insulini hii huhusika moja kwa moja kushusha sukari mwilini.
hali hii huleta madhara mbalimbali kwenye viungo vya binadamu na isipo shughulikiwa huweza kuleta kifo cha mapema kabisa.

kuna aina mbili za kisukari
type 1 diabetes; aina ya kisukari ambayo husababishwa na kongosho kushindwa kabisa kutoa insulin mara nyingi hutokea pale ugonjwa fulani unaposhambulia kongosho hilo. hutokea mara nyingi kwa watoto na ni aina ya sukari ambayo huua kirahisi sana.

type 2 diabetes; hii ni aina ya kisukari ambayo hutokea mara nyingi kwa watu wazima zaidi ya miaka 45 na kongosho hapa hutoa insulini kidogo ambayo haitoshi kupunguza sukari mwilini.

        watu wenye hatari ya kuugua kisukari

 • familia au ukoo wenye historia ya kisukari
 • unene na vitambi
 • umri zaidi ya miaka 45
 • historia ya kuugua kisukari cha mimba
 • presha kubwa ya damu
 • lehemu nyingi kwenye damu[cholestrol
 • matumizi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.
 • ulevi wa kupindukia na uvutaji wa sigara.
 • kutofanya mazoezi kabisa.
 • ulaji mkubwa wa nyama hasa nyama nyekundu.


dalili za ugonjwa wa kisukari

 • kukojoa mara kwa mara
 • kupata kiu kikali cha maji mara kwa mara
 • kusikia njaa sana mara kwa mara
 • kupungua uzito hata kama ulikua mnene.
 • kuchelewa kupona kwa vidonda vya kawaida
 • kutoona vizuri
 • kuchoka sana
 • kukojoa mkojo wenye sukari
 • kutoona vizuri


vipimo ambavyo hufanyika
mgonjwa hupimwa damu asubuhi akiwa bado hajala chochote na kama sukari ikionekana ni zaidi ya 7.0g/dl basi ana kisukari au kama akipimwa masaa kadhaa baada ya kula na sukari ikazidi 11g/dl basi huyo ni mgonjwa wa sukari.

matibabu
hapa ndipo watu wengi wamepoteza pesa zao kwa waganga wa kienyeji...ugonjwa huu ukishaanza hauponi hata iweje, kinachofanyika ni kwamba utapewa huduma itakayo kufanya kuondoa dalili za sukari, kuepusha madhara ya sukari kua juu mwilini na wewe kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine.

matibabu ya type 1 diabetes; mgonjwa huyu hana insulini hata kidogo mwilini hivyo atachomwa sindano ya insulin asubuhi na jioni kwa maisha yake yote bila kuacha. ni ngumu kidogo mwanzoni kujichoma mwenyewe lakini baada ya muda fulani unazoea.kumbuka mgonjwa huyu hatumii vidonge  vya kupunguza sukari kabisa.

matibabu ya type 2 diabetes;matibabu ya kwanza kabisa ya mgonjwa huyu ni mazoezi na chakula bora na akifanikisha hili anaweza asitumie dawa kabisa lakini sababu watu wengi hawana nidhamu ya chakula na mazoezi basi watu hawa huanzishiwa vidonge ambavyo husaidi mwili kutengeneza sukari zaidi ili kuipa nguvu ile kidogo inayotengenezwa. wakati mwingine baada ya muda mrefu wagonjwa hawa sukari yao ikishindwa kudhibitiwa na vidonge huhamia kwenye sindano. mfano wa dawa zilizopo ni metformin,gibenclamide, tolazamide na etc

madhara ya ugonjwa wa kisukari
kufa kwa figo; figo inapochuja damu yenye sukari nyingi huchoka mapema na baadae hushindwa kabisa kufanya kazi.

kufa kwa mishipa ya fahamu; sukari nyingi kwenye damu huharibu mishipa ya fahamu na baadae mgonjwa huanza kupata ganzi sana hasa miguuni na huweza kukanyaga vitu vyenye ncha kali bila kusikia maumivu.

upofu; eneo maalumu kwa ajili ya kumfanya binadamu aone kitaalamu kama retina huharibiwa kwa uwepo wa sukari nyingi kwenye damu.

kidonda cha mguu; kitaalamu huitwa diabetic foot, kidonda hichi huanza chenyewe bila maumivu yeyote na mtu anaweza asikione kama kipo chini ya nyayo. hiki ndio chanzo kikuu cha wagonjwa hawa kukatwa miguu kwani kidonda kinaweza kikapanda mpaka juu bila kuonekana.

kiharusi; huu hutokea pale mishiba ya damu inapozibwa kichwani kwa kiasi kikubwa cha mafuta na cholestrol ambavyo vyote huambatana na ugonjwa huu pia.

presha ya damu; ugonjwa huu huongeza uzito[viscosity] wa damu na kuweka vikwazo kwenye mishipa ya damu na kusababisha moyo kutumia nguvu nyingi kusukuma damu na kusababisha presha.

kuishiwa nguvu za kiume; nguvu za kiume zinategemea sana msukumo wa damu kukaa kwenye uume ili kuleta ule ugumu sasa kwenye kisukari hutokea mafuta na cholestrol ambavyo huziba ile mishipa midogoya damu ya kwenye uumenna kusababisha nguvu hizo kuisha kabisa na uume kua mdogo.hili ni tatizo kubwa kwa wagonjwa hawa.
madhara mengine ni kubadilika kwa ngozi na kua nyeusi, magonjwa ya mishipa ya damu na kuharibika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

                                 elimu kwa mgonjwa wa kisukari
 • wagonjwa wengi sana wamekufa kwa kutozingatia masharti na kujifanya wao wanawajua vizuri waganga wa kienyeji. wengine waliacha dawa baada ya kupata vikombe vya babu na kufa baada ya muda. kama wewe unaamini waganga wa kienyeji wana dawa basi hakikisha sukari yako inapimwa kila siku kuona kama kweli inashuka kipindi unatumia dawa hizo. ugonjwa huu hauponi na kama uko kwenye dozi ya kuuponya basi ujue unapoteza muda na pesa zako.
 • hakikisha unafanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku hata ya kutembea tu kwani husaidia sana kuchoma mafuta na kutengeneza insulini mwilini hasa kwa wagonjwa wa type 2
 • nunua mashine ya kupima sukari ya kwako mwenyewe kwani ugonjwa huo ni wako, mwili huo ni wako na ukifa utazikwa peke yako wala sio na daktari au mtu yeyote anayekuuguza hivyo usisubiri kufuatiliwa.hivyo hakikisha unapima sukari yako hata mara nne kwa wiki kujua kama iko sawa na kama ndio mgonjwa mpya pima kila siku kwanza mpaka utakapoona sukari imetulia.
 • kula vizuri;hapa ndio mzizi mkuu wa huu ugonjwa..ukileta uzembe hapa unakufa na nina fahamu watu walioambiwa wakasema kuliko nisile kitu fulani bora nife na walikufa kweli..kula vizuri...narudia kula vizuri.... uepuke vyakula vyenye sukari nyingi kama soda. biskuti, chocolate na  kadhalika.utafiti mpya unaruhusu mgonjwa huyu kula vyakula karibia aina zote ila kwa kiasi kidogo mfano wali kidogo, ndizi kidogo, viazi mviringo kidogo,ugali kidogo, samaki kwa wingi, mboga za majani kwa wingi, matunda ambayo hayana sukari nyingi kwa wingi.nyama sio nzuri kwa wagonjwa hawa. lakini pia unaweza kutumia virutubisho mbalimbali vinavyosaidia kushusha sukari na kusafisha mwili lakini haimaanishi uache dawa.sisi tunavyo virutubisho kwa ajili ya wagonjwa wa kisukari tunaweza kuwasiliana ukapata.
 • ulevi wa kupindukia; unywaji mkubwa wa pombe huua kongosho japokua unywaji  kawaida ni mzuri kwa moyo hivyo epuka ulevi wa kupinduki kwani utakumaliza mapema.
 • hudhuria clinic ya kisukari; huku utajifunza mambo mapya kuhusu kisukari lakini pia daktari anaweza kugundua shida yako mpya ambayo wewe hujaiona na  pia clinic hizi zitakukutanisha na walioishi na kisukari miaka mingi bila kusumbuliwa nacho.
 • mwisho; idadi ya wagonjwa wa kisukari imeongezeka kutoka wato milion 108 mwaka 1980 mpaka watu milion 422 mwaka 2014. mwaka 2016 utafiti mpya unaonyesha katika kila watu 11 mmoja ana kisukari. zaidi ya watu milioni moja na nusu hufa kila mwaka sababu ya ugonjwa huu lakini pia ndio ugonjwa unaoongoza kusababisha upofu, kukatwa miguu,kiharusi, shinikizo la moyo na kuua figo.
 •                                   
                                                        STAY ALIVE       
                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                       0653095635/0769846183

                               
                                           

0 maoni:

Chapisha Maoni