katika maisha ya kawaida hasa ya kiafrika kuna mambo mengi sana tunayapuuzia katika malezi, wazazi wakiamini kwamba wao ndio wao na watoto hawajui kitu.inawezekana ni sababu ya tamaduni zetu au sababu ya kutoelimika kuhusu hili lakini katika ukuaji wa mtoto ndio kipindi ambacho kitaamua yeye atakua nani baadae kulingana na mambo ambayo anayaona na kujifunza kwako mzazi au mlezi.miaka ya kifalme watoto wa wafalme walikua wanakua wafalme sio kwasababu wana damu tofauti hapana ila kwasababu wamekua wakiona na kufundishwa mambo ambayo yatawafanya wawe wafalme pia.katika umri mdogo mtoto anajifunza mengi kwa kuangalia tu kwa macho na wala hivyo vitu hatavisahau kabisa kwenye maisha yake. sisi wote tumepitia utoto lakini kuna mambo ambayo tuliyaona na mpaka leo hatujasau.nisiwe na story nyingi...leo nataka nitoe mambo muhimu ambayo ni sumu kwa mzazi au mlezi ambaye anataka mtoto wake akue vizuri.
kudanganya mbele ya mtoto; kila mtu anadanganya, lakini kudanganya mbele ya mtoto wako kitu ambacho na yeye anajua sio kweli basi ujue na yeye unamjenga hivyo na wewe pia atakudanganya sana huku akiamini ni jambo la kawaida.mfano ulishinda umelala ndani jana yake na mtoto alikuona, leo anakuja mtu unamwambia mbele ya mtoto kwamba jana nilikua safari.
kumsema vibaya mzazi mwenzako kwa mtoto;kila mzazi ana mapungufu yake lakini swala la kuwaita na watoto na kuwaambia kwamba mama yenu ni hivi na hivi au baba yenu ni hivi na hivi.kwanza unamshushia heshima yake mbele ya watoto na pia baadhi ya watoto watamchukia maisha yao yote.kumbuka hata wewe una mapungufu lakini mzazi mwenzako hajawaambia watoto.usimseme mwenzako vibaya hata kama mmeachana huwezi jua ya mbele.
kulalamika kuhusu fedha; sisi wote tunafahamu pesa ni ngumu sana lakini uliwazaa hao watoto ukijua kwamba lazima wapate mambo muhimu kama chakula, nguo na mahali pa kulala.swala la kulalamika mbele yao kwamba huna hela ni hatari sana.kwanza linawatia wasiwasi lakini pia watakudharau wakikufananisha na wazazi wengine.katika umri mdogo jitahidi kuwapa vitu muhimu kwa uwezo wako wote hasa kwa upande wa chakula na mavazi.watoto wengi hupenda wali utotoni.usiwanyime haki yao wape tu.hata kama huna uwezo wa gari na vitu vya gharama basi utakumbukwa kwa hilohilo.kuna wazazi wana tabia ya kulalamika sana wakati wa kulipa ada ya shule.kumsomesha ni wajibu wako.unataka nani alipe? katika swala la fedha ni vizuri kuwaelimisha kuhusu fedha na wajifunze kutumia vizuri ila sio kulalamika.
kupigana mbele ya watoto; utafiti unaonyesha kwamba wazazi wengi wanaopiga wake zao au waume zao walishuhudia ugomvi wa wazazi wao huku wakijitamba mbele ya watoto kwamba mama yenu amekosea lazima apigwe. kwanza baadhi ya watoto watakuchukia, wengine watamdharau mzazi anayepigwa na siku wakioa watajua ni halali kupigwa au kupiga.mimi ni mfano hai..sitampiga mke wangu sio kwasababu sina nguvu ila kwasababu sikuwahi kuona mama yangu anapigwa au hata kufokewa mbele yangu.
kua mkali sana kwa watoto; mimi nilipokua mdogo baba yangu alikua mkali sana kiasi kwamba akisafiri tunafurahi kwani mama alikua mpole kwetu, pamoja kwamba mama alikua anatuadhibu tukikosea lakini bado tulimpenda.tulikua tukisikia honi ya gari kwamba baba amekuja tunaenda kulala.kipindi hiko baba hakuona kama ni tatizo lakini tulipokua wakubwa na anataka muda wa kuongea na sisi akashangaa tunamkwepa sana mpaka akawa anauliza shida ni nini? lakini sababu tumekua basi tukampa nafasi tena.
kuongea umbea mbele yao: watoto wako makini sana, unaweza kua unamsema mtu fulani labda ndugu, mwalimu wao au kaka yako mbele yao na wao watadhani ni kawaida watu kusemwa na huenda siku moja muhusika akaja wakarudia maneno yako uliyosema kuhusu yeye mbele yake.
kunywa pombe au kulewa mbele yao; ni akili ya kijinga sana kukataza kitu ambacho unakifanya..watoto wa walevi huishia kua walevi pia kwani huona ile hali ni ya kawaida sana kwenye maisha ya binadamu.hivyo kama unakunywa, kanywe kistaarabu urudi kimya na ukalale na hata harufu wasikusikie nayo.ukiona mtoto anakunywa viroba form one shuleni basi na malezi yanahusika sana.
kuvuta sigara mbele yake; kama nilivyoongelea swala la pombe. kwanza unaharibu mapafu yake kwani ule moshi unamfikia pia lakini pia unatoa taarifa kwamba sigara au bangi haina shida na yeye akipata mtaani avute tu.kuna wazazi wanadiriki hadi kuwatuma watoto wawawashie sigara.
kuvaa vibaya mbele ya mtoto; hii inawaathiri sana wasichana waliozaa mapema wakiwa nyumbani kabla ya kuolewa au kabla ya umri sahihi.wao huhisi kutembea na nguo za ajabu ni kitu cha kawaida au kukata mauno mbele ya mtoto ni sawa tu.kumbuka mtoto wako anaiga kwako na siku akikuletea mimba akiwa na miaka 12 usishangae.wewe kama umezaa hata kama una miaka 16 ujue utu uzima ndio umeanza. ishi kama mzazi na kwa heshima.
kutoa taarifa za mahusiano mbele ya watoto; watoto wanachunguza sana. hii ni hasa kwa wanawake ambao wamezaa tu ila wanaishi bila mume au mwanaume umezaa tu na huishi na mke. tabia ya kuja na wanaume au wanawake tofauti kwenye nyumba huku anawaona ni hatari hata kama humwambii huyo ni nani. mtoto anajua huyu ni mpenzi au rafiki kwa kuwaangalia tu mnavyojikanyaga mbele yake. hii itamfanya aone kua na wanaume wengi au wanawake wengi kwa wakati mmoja ni kawaida na ndio chanzo cha umalaya. ficha mahusiano yako na siku ukipata mtu sahihi wa kukuoa au kuolewa basi mtambulishe kwa mtoto baada ya ndoa au maandalizi ya ndoa yakishaanza.atakuheshimu sana.kumbuka ukiwa malaya huko mtaani watu wanajua na wanamwambia mtoto wako na itamuuma sana.
mwisho;kuna mambo mengi sana ya kua nayo makini sana mbele ya watoto, huu uzungu wa kuangalia video za ajabu za muziki mkiwa pamoja ni mbaya sana.ni kweli ni ngumu sana kuzuia lakini onyesha hupendi na ukiwepo anagalia nao chaneli za maadili tu.lakini pia kua bize sana na simu yako mbele yake kutamfanya awe bize na simu pia utotoni na wakati ni muda wa kusoma.
utafiti unaonyesha watoto wanaokua na mama zao au bibi zao wanaharibikiwa zaidi kuliko wanaokua na baba peke yake.kuna mambo ya ajabu akina wasichana bila kujua hata anakuza mtoto wa jinsia gani na wakati mwingine huishia kupata mtoto shoga ukubwani kwa kumkuza kike mtoto wa kiume.lakini pia upole uliopitiliza kwa watoto wao hata wakirudi saa nne za usiku au wakiwaona kwenye mahusiano kwenye umri mdogo hukaa kimya. wanaume wako serious sana kwenye malezi. baba akiwemo mwisho wa kwenda nyumbani saa 12.hivyo wanawake mjifunze kitu hapa.kwa maelezo zaidi soma hapa
tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183