data:post.body ZIFAHAMU HATUA ZA KUKUBALIANA NA UKWELI UNAPOKUTWA UMEATHIRIKA NA VIRUSI VYA UKIMWI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

ZIFAHAMU HATUA ZA KUKUBALIANA NA UKWELI UNAPOKUTWA UMEATHIRIKA NA VIRUSI VYA UKIMWI.

                                                                           
watu wanaopata maambukizi ya ukimwi ni binadamu na ndugu zetu kabisa, lakini kwasababu ni
wachache  kwenye jamii ukilinganisha na watu wote basi jamii imekua ikiwatenga sana hata kuwakashifu kwenye mitandao ya kijamii bila kujua kwamba kuna watu wanaumizwa sana na kauli hizo. nikiwa kama daktari nimefanya kazi sana na kuongea na waathirika wengi wa virusi vya ukimwi na kujua hisia zao kwa undani sana na leo navyoandiaka hapa najua maumivu ya watu hawa vizuri sana.
mtu anapopata majibu mabaya ya virusi vya ukimwi huumia sana sana na hupitia hatua zifuatazo za kisaikolojia.
kukataa ukweli; hakuna ambaye hua anakubali kwamba majibu ni ya kwake kwa mala ya kwanza na wengi huhisi labda vipimo vimekosewa, majibu yamechanganywa au kipimo kimeharibika na kuisha muda wake.hii hali inaweza kua nzuri mwanzoni na kukupa muda wa kujipanga lakini ni hatari baadae kwani unaweza kushindwa kuchukua hatua mapema na kudhoofu kiafya.
kupata hasira sana; hatua ya pili ni kuchukia sana na kujuta kwanini walishiriki ngono zembe, kumlaumu mme au mke wako hasa kama ulikua mwaminifu kwake na hata kuanza kutaka kujua ni nani amewaambukiza kama huna mpenzi maalumu. hii ni htari sana kiafya na huweza kufanya mtu achukue maamuzi hatari ya kuua mtu.
kutafuta suluhu; kipindi hiki mtu huanza kuulizia kwamaba ataishi miaka mingapi na kuanza kufuatilia kwenye mitandao au habari kama kuna dawa yeyote ya kutibu huu ugonjwa kabisa. kipindi hiki mgonjwa huweza kukutana na matapeli na kumdanganya sana kwamba uwezekano wa kupona upo wakati sio kweli.
mgandamizo wa mawazo; hii ni hatua ya nne ambayo mgonjwa hua na mawazo mengi sana na hupenda kujitenga na kutulia peke yake, kufuatilia maisha baada ya kifo hata kuokoka kwa baadhi ya watu. hii ni moja ya hatua mbaya sana kwani mgonjwa huweza kujiua kama asipopata ushauri wa kutosha.
kukubalina na ukweli; hii ni hatua ya mwisho ambayo mgonjwa hukubaliana na ukweli kwamba yeye na muathirika na swala la kifo halimtishi tena kwania anajua hatakufa peke yake kwani mwisho wa siku binadamu wote njia ni moja na kuna ambao hawana virusi ila watamtangulia, ni hatua nzuri sana.
hatua hizo nimezitaja haraka lakini hatua moja huweza kuchukua hata miezi sita mpaka mwaka mmoja na wala haziendi haraka haraka kama inavyofikirika, hivyo kama wewe unayesoama hapa umeathirika na virusi au kuna ndugu unamfahamua ameathirika basi hatua zifuatazo zitamsaidia kukubaliana na ukweli haraka na kuishai maisha ya kawaida.
ongea na mtu wako wa karibu sana kuhusu ugonjwa wako; mara nyingi waathirika hawataki jamii ijue kwamba wanaumwa na watu wengi yaaani ndugu na marafiki sio waaminifu sana na wanaweza kuvujisha siri zao, hivyo unaweza kuongea na daktari wako kuhusu ugonjwa wako na akakupa matumaini mapya.
jiunge na kikundi cha waathirika;ongea na daktari wako akuonyeshe kikundi cha waathirika wa ukimwi ili uweze kufahamiana nao na wakupe uzoefu wao kuhusu ugonjwa na hii itakupa picha mpya kwamba matumaini ya kuishi yapo kwani utakutana na vijana wenzako au wazee wenzako ambao wanaishi kwa amani kabisa.lakini pia ukipata kikundi cha watsapp au facebook cha waathirika wenzako tanzania au dunia nzima basi jiunge nacho na kitakujenga sana.
jishughulishe na shughuli za kukuondolea mawazo; jiunge na mazoezi, katembee na rafiki zako, kua bize na mambo muhimu ya kimaisha na epuka kukaa peke yako kwa muda mrefu.
pata usingizi wa kutosha; hakikisha unalala masaa nane mpaka tisa kwa usiku mmoja hii itaufanya ubongo upumzike na kuamka na nguvu mpya kesho yake.
usinywe pombe sana; pombe ni mbaya sana kwani ukizitumia kipindi hiki ndio zitakufanya uumie sana kwa mawazo na kila pombe zikiisha uanakumbuka hali ni ileile lakini pia pombe huweza kushusha sana kinga ya mwili na kukudhoofisha zaidi.
onana na mtaalamu wa ushauri; hawa wataalamu wapo wengi sana na wanajua jinsi ya kupambana na maumivu ya kisaikolojia hivyo ukionanan nao watakupa mwanga mpya wa maisha na utajiona mpya kabisa duniani.tatizo kwa nchi zetu hatuwatumii sana kwani tunahisi maumivu ya hisia sio muhimu.
tumia dawa za kupunguza mgandamzo wa mawazo; kama unajiona huwezi kuvumilia maumivu makali ya mwili sababu ya ugonjwa ulipata basi  hospitali na maduka ya madawa kuna dawa maalumu kwa ajili ya watu kama wewe. dawa hizi zitakupoza na kukupunguzia mawazo kwa kiasi kikubwa sana mfano amitriptyline.
kula vizuri na tumia virutubisho; huu sio muda wa kula kama zamani, kula mlo kamili ulinde mwili wako na magonjwa lakini pia kuna virutubisho vingi kwa sasa vya kampuni mbalimbali za nje na ndani ya nchi ambavyo vitakusaidia sana kujenga mwili wako usishambuliwe na magonjwa nyemelezi.[nitafute kama unahitaji virutubisho hivi nikuunganishe na wahusika]
mwisho;kuugua ukimwi sio wa maisha na kabala yako kuna watu wengi yaani watu wazima na watoto amabao wameshaugua ugonjwa huu na wanaishi maisha kawaida kabisa, kuna magonjwa mengi sana yanayoua haraka kuliko ukimwi, lakini nikupe matumaini pia madaktari hawalali usiku na mchana kutafuta dawa hii na tunaamini ipo siku itapatikana na watu wote watakua wazima tena.kama ukoma uliosumbua tangu kipindi cha yesu ulipata dawa.ukimwi ambao una miaka hamsini na kidogo utakosaje dawa? muda si mrefu nitawakutanisha waaathirika kwenye group za watsapp ili wapate matumaini mapya.
                                                       STAY ALIVE 
    
                                   MAWASILIANO 0653095635/0769846183        
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO  


0 maoni:

Chapisha Maoni