data:post.body Februari 2016 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

ZIFAHAMU HATUA ZA KUKUBALIANA NA UKWELI UNAPOKUTWA UMEATHIRIKA NA VIRUSI VYA UKIMWI.

                                                                           
watu wanaopata maambukizi ya ukimwi ni binadamu na ndugu zetu kabisa, lakini kwasababu ni
wachache  kwenye jamii ukilinganisha na watu wote basi jamii imekua ikiwatenga sana hata kuwakashifu kwenye mitandao ya kijamii bila kujua kwamba kuna watu wanaumizwa sana na kauli hizo. nikiwa kama daktari nimefanya kazi sana na kuongea na waathirika wengi wa virusi vya ukimwi na kujua hisia zao kwa undani sana na leo navyoandiaka hapa najua maumivu ya watu hawa vizuri sana.
mtu anapopata majibu mabaya ya virusi vya ukimwi huumia sana sana na hupitia hatua zifuatazo za kisaikolojia.
kukataa ukweli; hakuna ambaye hua anakubali kwamba majibu ni ya kwake kwa mala ya kwanza na wengi huhisi labda vipimo vimekosewa, majibu yamechanganywa au kipimo kimeharibika na kuisha muda wake.hii hali inaweza kua nzuri mwanzoni na kukupa muda wa kujipanga lakini ni hatari baadae kwani unaweza kushindwa kuchukua hatua mapema na kudhoofu kiafya.
kupata hasira sana; hatua ya pili ni kuchukia sana na kujuta kwanini walishiriki ngono zembe, kumlaumu mme au mke wako hasa kama ulikua mwaminifu kwake na hata kuanza kutaka kujua ni nani amewaambukiza kama huna mpenzi maalumu. hii ni htari sana kiafya na huweza kufanya mtu achukue maamuzi hatari ya kuua mtu.
kutafuta suluhu; kipindi hiki mtu huanza kuulizia kwamaba ataishi miaka mingapi na kuanza kufuatilia kwenye mitandao au habari kama kuna dawa yeyote ya kutibu huu ugonjwa kabisa. kipindi hiki mgonjwa huweza kukutana na matapeli na kumdanganya sana kwamba uwezekano wa kupona upo wakati sio kweli.
mgandamizo wa mawazo; hii ni hatua ya nne ambayo mgonjwa hua na mawazo mengi sana na hupenda kujitenga na kutulia peke yake, kufuatilia maisha baada ya kifo hata kuokoka kwa baadhi ya watu. hii ni moja ya hatua mbaya sana kwani mgonjwa huweza kujiua kama asipopata ushauri wa kutosha.
kukubalina na ukweli; hii ni hatua ya mwisho ambayo mgonjwa hukubaliana na ukweli kwamba yeye na muathirika na swala la kifo halimtishi tena kwania anajua hatakufa peke yake kwani mwisho wa siku binadamu wote njia ni moja na kuna ambao hawana virusi ila watamtangulia, ni hatua nzuri sana.
hatua hizo nimezitaja haraka lakini hatua moja huweza kuchukua hata miezi sita mpaka mwaka mmoja na wala haziendi haraka haraka kama inavyofikirika, hivyo kama wewe unayesoama hapa umeathirika na virusi au kuna ndugu unamfahamua ameathirika basi hatua zifuatazo zitamsaidia kukubaliana na ukweli haraka na kuishai maisha ya kawaida.
ongea na mtu wako wa karibu sana kuhusu ugonjwa wako; mara nyingi waathirika hawataki jamii ijue kwamba wanaumwa na watu wengi yaaani ndugu na marafiki sio waaminifu sana na wanaweza kuvujisha siri zao, hivyo unaweza kuongea na daktari wako kuhusu ugonjwa wako na akakupa matumaini mapya.
jiunge na kikundi cha waathirika;ongea na daktari wako akuonyeshe kikundi cha waathirika wa ukimwi ili uweze kufahamiana nao na wakupe uzoefu wao kuhusu ugonjwa na hii itakupa picha mpya kwamba matumaini ya kuishi yapo kwani utakutana na vijana wenzako au wazee wenzako ambao wanaishi kwa amani kabisa.lakini pia ukipata kikundi cha watsapp au facebook cha waathirika wenzako tanzania au dunia nzima basi jiunge nacho na kitakujenga sana.
jishughulishe na shughuli za kukuondolea mawazo; jiunge na mazoezi, katembee na rafiki zako, kua bize na mambo muhimu ya kimaisha na epuka kukaa peke yako kwa muda mrefu.
pata usingizi wa kutosha; hakikisha unalala masaa nane mpaka tisa kwa usiku mmoja hii itaufanya ubongo upumzike na kuamka na nguvu mpya kesho yake.
usinywe pombe sana; pombe ni mbaya sana kwani ukizitumia kipindi hiki ndio zitakufanya uumie sana kwa mawazo na kila pombe zikiisha uanakumbuka hali ni ileile lakini pia pombe huweza kushusha sana kinga ya mwili na kukudhoofisha zaidi.
onana na mtaalamu wa ushauri; hawa wataalamu wapo wengi sana na wanajua jinsi ya kupambana na maumivu ya kisaikolojia hivyo ukionanan nao watakupa mwanga mpya wa maisha na utajiona mpya kabisa duniani.tatizo kwa nchi zetu hatuwatumii sana kwani tunahisi maumivu ya hisia sio muhimu.
tumia dawa za kupunguza mgandamzo wa mawazo; kama unajiona huwezi kuvumilia maumivu makali ya mwili sababu ya ugonjwa ulipata basi  hospitali na maduka ya madawa kuna dawa maalumu kwa ajili ya watu kama wewe. dawa hizi zitakupoza na kukupunguzia mawazo kwa kiasi kikubwa sana mfano amitriptyline.
kula vizuri na tumia virutubisho; huu sio muda wa kula kama zamani, kula mlo kamili ulinde mwili wako na magonjwa lakini pia kuna virutubisho vingi kwa sasa vya kampuni mbalimbali za nje na ndani ya nchi ambavyo vitakusaidia sana kujenga mwili wako usishambuliwe na magonjwa nyemelezi.[nitafute kama unahitaji virutubisho hivi nikuunganishe na wahusika]
mwisho;kuugua ukimwi sio wa maisha na kabala yako kuna watu wengi yaani watu wazima na watoto amabao wameshaugua ugonjwa huu na wanaishi maisha kawaida kabisa, kuna magonjwa mengi sana yanayoua haraka kuliko ukimwi, lakini nikupe matumaini pia madaktari hawalali usiku na mchana kutafuta dawa hii na tunaamini ipo siku itapatikana na watu wote watakua wazima tena.kama ukoma uliosumbua tangu kipindi cha yesu ulipata dawa.ukimwi ambao una miaka hamsini na kidogo utakosaje dawa? muda si mrefu nitawakutanisha waaathirika kwenye group za watsapp ili wapate matumaini mapya.
                                                       STAY ALIVE 
    
                                   MAWASILIANO 0653095635/0769846183        
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO  


HIZI NDIO DAWA ZA HOSPITALINI ZINAZOUA NGUVU ZA KIUME....

                                                                   

dawa zote zinazopatikana mahospitalini na maduka ya madawa zinaletwa kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali, japokua baadhi ya dawa hizo huambatana na madhara madogo na makubwa kwenye mwili wa binadamu. madhara madogo madogo huweza kua kichefuchefu,kizunguzungu, kutapika, kuharisha na kadhalika. na madhara makubwa huweza kua kansa, madonda ya tumbo, ugumba, kuishiwa nguvu za kiume na kadhalika. leo ntaenda kuongelea dawa za hospitalini ambazo zinhusika sana kuua nguvu za kiume na kama una tatizo hili uziepuke mara moja.
dawa za kutibu presha; kuna dawa nyingi sana za kutibu presha na hufanya kazi kwa njia tofauti tofauti yaani ikishindwa hii unapewa nyingine na zifuatazo ni baadhi ambazo huua nguvu za kiume. mfano  Hydrochlorothiazide, Hydropres, Inderide, Moduretic, Oretic, Lotensin, Chlorthalidone (Hygroton),Triamterene (Maxide, Dyazide),Furosemide (Lasix),Bumetanide(Bumex),Guanfacine (Tenex),Methyldopa (Aldomet),Clonidine (Catapres),Verapamil(Calan, Isoptin, Verelan)Nifedipine (Adalat, Procardia),Hydralazine (Apresoline),Captopril (Capoten),Enalapril (Vasotec),Metoprolol (Lopressor),Propranolol(Inderal),Labetalol(Normodyne),Atenolol (Tenormin),Phenoxybenzamine (Dibenzyline),Spironolactone (Aldactone).
dawa za kutibu kifafa, msongo wa mawazo na wasiwasi; hizi hupewa kwa wagonjwa wenye msongo wa mawazo na kifafa. mara nyingi huleta uzingizi na kumfanya mtu aapate nafuu lakini pia dawa hizo hupunguza nguvu za kiume.mfano Fluoxetine (Prozac),Tranylcypromine (Parnate),Sertraline (Zoloft)Isocarboxazid(Marplan),Amitriptyline (Elavil),Amoxipine (Asendin),Clomipramine (Anafranil)Desipramine (Norpramin),Nortriptyline (Pamelor),Phenelzine (Nardil),Buspirone(Buspar),Chlordiazepoxide (Librium),Clorazepate (Tranxene),Diazepam (Valium)
Doxepin (Sinequan),Imipramine (Tofranil),Lorazepam (Ativan),Oxazepam (Serax),Phenytoin (Dilantin).
dawa za kutibu matatizo ya aleji; hizi ni dawa amazo mara nyingi hutumika kutibu mafua, miwasho, kutetemeka mwili,kuzuia kutapiaka na kadhalika lakini huua nguvu za kiume taratinu mfano Dimehydrinate (Dramamine), Diphenhydramine (Benadryl), Hydroxyzine (Vistaril), Meclizine (Antivert), Promethazine (Phenergan).
dawa za maumivu; hizi ni dawa ambazo hutumika kutibu maumivu makali ya mwili kama jointi, mgongo, miguu na kadhalika lakini bahati mbaya huacha sehemu nyeti katika halia ambayo sio nzuri mfano Naproxen (Anaprox, Naprelan, Naprosyn) na Indomethacin (Indocin).
dawa za kutibu madonda ya tumbo; hutumika na watu wengi sana kuponya na kuondoa maumivu makali yanayosababishwa na madonda ya tumbo lakini huacha madhara hayo.mfano cimetidineNizatidine (Axid), ranitidine (Zantac).
dawa za kutibu tezi dume; pamoja ya kua tezi dume hutibiwa moja kwa moja kwa upasuaji lakini kuna dawa ambazo mgonjwa anapewa kabla ya kufikia hatu ya kupasua na pia dawa hizi humpunguzia makali ya ugonjwa.mfano flutamide(Eulexin), leuprolide (Lupron)
dawa za kutibu kansa; dawa hizi hazipatikani madukani kabisa, na hutolewa kwenye hospitali maalumu kama  ocean road,  dar es laam kupunguza makali ya ugonjwa wa kansa. mfano wa dawa hizo ni  Flutamide (Eulexin), Leuprolide (Lupron).
dawa za moyo; hizi ni dawa amabazo hutumika kutibu watu wenye matatizo ya moyo.. mara nyingi dawa hii hupewa kwa watu ambao mioyo yao haisukumi damu vizuri.mfano norpace.
mwisho; kama una tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na unaatumia baadhi ya dawa hizi, basi ongea na daktari wako anayekutibu akubadilishie dawa. ni hatari kufanya maamuzi mwenyewe bila kumshirikisha daktari. nguvu za kiume ni nzuri lakini maisha ni matamu zaidi.
                                                           STAY ALIVE
                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 
                                               0653095635/0769846183